BINTI MDUNGUAJI (11)

SEHEMU YA KUMI NA MOJA

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI : ndipo Denis akatafuta sehemu nzuri karibu na bar, akaparki gari, Jackline akamtazama kwa umakini sana, akujuwa yule kijana mlevi anataka kufanya nini, Denis akamgeukia Jackline, ambae alikuwa amekaa seat ya nyuma, huku akiachia tabasamu lake la kilevi, hapo Jackline akaona kuna dalili ya kujeruhi mtu au kuuwa kabisa, maana alihisi kuwa huyu kijana mlevi ameingiwa na tamaa ya kimwili, endelea ……

“vipi.. we! mdada..umesha kula” aliongea Denis kwa sauti kilevi levi, Jackline akashusha pumzi kwanguvu, ni kweli Jackline njaa ilikuwa imemkamata, maana tokea alipo kuwa amekula mchana pale Mapambano bar, Jackline akatabasamu kidogo, na kusababisha vijishimo kujitokeza kwenye mashavu yake, na kufanya sura yake izidi kuwa nzuri, “kweli kaka yangu, nina njaa sana” aliitiakia Jackline, akiendelea kumsoma huyu kijana, ambae aliduwaa kidogo akimkodolea macho usoni, kabla ajafunua kwenye mkebe wagari, yani kwenye dash board, akachomoa noti mbili za elfu kumi, kati ya noti nyingi zilizomo ndani ya kile kikebe, kisha akakirudishia kifuniko chake, kisha akashuka nakuelekea kwenye hile bar iliyopo maeneo hayo maalufu kwa jina la full dose, wadau wengi wanajiuliza kwa nini inaitwa hivyo, ni kwasababu ya mambo yanayo fanyika maali hapo, Denis alipotelea ndani ya bar, akimwacha Jackline ndani ya gari, jackline mle ndani ya gari akapandisha gauni lake na kuchomoa simu, kwenye mfuko wakikaptula chake cha jinsi haraka, na kumpigia baba yake, huku akiangalia kule alipo elekea Denis “baba nime uwa vijana wa tatu, waliokuwa wanajaribu kunibaka” alongea Jackline kwa sauti ya chii yenye tahadhari kubwa, badaa ya baba yake kupokea simu, “je ulionekana namtu yoyote?” aliuliza baba yake na Jackline akamsimulia tukio zima lilivyokuwa, mpaka alipo pata msaada wa huyu kijana mlevi, “ok! sasa kajifiche kwa huyo kijana, ila uwenae makini sana, akikisha agunduwi lolote kuhusu wewe” aliongea baba yake Michael Nyati kwa msisitizo “sawa baba” Jackline alikata simu na kuiweka kwenye kikaptula cha jinsi ndani ya gauni lake chakavu, mle ndani ya gari akiwa amebaki peke yake, Jackline alimtafakari sana huyu kijana mlevi, kuna mambo machache aliya gungua juu ya huyu kijana, la kwanza ni kwamba huyu kijana anapenda sana pombe, pengine kwa kuwa akuwa na familia, au amesababishiwa na kitu ambacho kime mfanya asiwe na familia, la pili nimcheshi sana, la tatu ni mtu mwenye moyo wa kutoa msaada na mwenye huruma sana, sababu alijitolea kumsaidia japo akujuwa ni kwasababu gani alimpatia huo msaada, labda kwa ajili ya matamanio ya kingono, au ni ulevi ndio ulimfanya kutoa msaada bila kujijuwa, na kwa mtu asiye mfahamu, lakini tokea wameingia kwenye gari mpaka hapa walipo, akuonyesha dariri ya kuendekeza ngono, sababu ata naongezi yao yalikuwa ya kawaida tu!, “mh! ngoja tufike, akianza ujinga tu! nayeye atakiona cha moto” aliwaza Jackline, Denis alikuwa ana rudi, huku amebeba mifuko midogo mitatu myeusi ya rambo, akamkabidhi Jackline “yote hii ya kwangu” alishangaa Jackline huku anapokea “ndiyo..kwa..kwa sababu siku kuuliza utakula nini…. nimeeee..amua kubeba ili ujichagulie mwenyewe, utakachokula” alijibu Denis kilevi huku akichomoa kopo moja la bia kwenye katoni lake, na kuifungua kisha aka gugumia mafundo mengi mfurulizo, alafu akaiweka sehemu ya kuwekea vinywaji mle ndani ya gari, kisha anaingiza gia ya kuondokea, na kuliingiza gari barabarani, na kukanyaga mafuta kufwata uelekeo wa kibamba kwa mwendo wa fujo, akimfanya Jackline ashindwe kula, akabaki ameshikilia vifuko vya chakula, ** Mtaa wa manzese Tip Top polisi walikuwa wamezagaa, wakimsaka dada mwenye mabegi, wakati huo huo inspector Johnson alikuwa anaingia akiwa na askari wake kumi na magari mawili, aina ya land lover 110, baada ya kupewa taharifa ya kutokea mauwaji maeneo ya manzese, karibu na eneo yalipotokea mauaji ya mchungaji Chilumba, asubuhi ya siku hiyo, magari yapolisi yalisimama mbele ya mapambano bar and guest house, wale askari wakiwa tayari kimapambano, waliruka na kujipanga kulizunguka lile jengo la bar, huku Insp Johnson akiingia ndani ya ile bar, akikaribishwa na mkuu wa kituo kidogo cha manzese, na kumwongoza moja kwa moja, kwenye chumba ambacho ile miili ya vijana watatu ilikuwa bado hipo chini, insp Johnson aliitazama kwa dakika kadhaa huku akijaribu kutafakari ili na lile, “ina maana aliyo ya fanya haya ni mwanamke?” Insp Elenest alimwuliza mkuu wa kituo, “ni kwa mujibu wa maelezo ya mhudumu wa vyumba, kuwa aliefanya haya ni mwanamke kutoka jijini ambae alikuja hapa tokea jana” alijibu mkuu wakituo, “yupo wapi huyo mhudumu?” aliuliza insp Elenest “yupo huku pamoja na wahudumu wengine, tuliwaifadhi kwenye chumba kimoja” alijibu mkuu wakituo, na hapo ilitolewa amri kuwa aitwe ule mhudumu wa vyumba, aliitwa yule dada mhudumu wa vyumba, alikuja akiwa amevimba usoni huku damu zikiwa zime gandiana sehemu kubwa ya pua na mdomo wake, kutokana na kichwa alichopigwa na Jackline, “awa vijana walikuwa wana fanya nini chumbani kwa mwanamke na mapanga mkononi?” hilo swali alikuwa na jibu kwa huyu manamke, maana alijuwa akisema ukweli na yeye angeozea jela, “sijuwi, mimi niliwaona wanaingia tu! nikajuwa ni wenzake” Insp alimuoji maswali machache yaliyo mfanya agundue kuwa yule dada alichukuwa chumba, jana yake jioni aliandikisha jina la Sikujuwa Saidi, anatokea bagamoyo anaelekea mtwara, akuandika kazi wala namba ya kitamburisho, licha a kunduwa hayo, lakini kuna maswali yalimchanganya sana insp Johnson, kwamba inaonekana hawa vijana walikuwa na nia ya kumzuru huyo mschana, akawazidi nguvu, je? huyo manamke ni nani anauwezo kiasi gani cha kuichinja midume mitatu kama kuku? *** saa nne za usiku, Jackline alikuwa amesha fika nyumbani kwa kijana mlevi, alikaribishwa ndani na mwenyeji wake mlevi, Jackline akiwa pamoja na mizigo yake, akaingia ndani, huku akiitazama ile nyumba kwa umakini sana, walifika na kukaa sebuleni, Jackline alimwona mwenyeji wake akimkaribisha kwa sauti ya kilevi iliyo jaa ukarimu, akaletewa maji ya kunywa na kunawa pamja na soda, kwaajili ya kupata msosi ule alio kujanao, toka full dose, Jackline baada ya kulizika na maandalizi na ukalimu wa mwenyeji wake cha pombe, akaanza kula vyakula vyake kwenye mifuko, chips mayai pamoja na nyama za kuku wa kukaangwa na mishikaki ya ng’ombe, Jackline alikula huku akiendelea kuingalia ile nyumba, kwandani ilikuwa nzuri sana yenye vitu vya thamani na vizuri, alishangaa kuona yule kijana licha ya kuwa mlevi, lakini alikuwa amejijenga vizuri kimaisha, Denis muda wote tokea wameingia humu ndani, alikuwa amekaa kwenye kochi pembeni ya Jackline, akinywa pombe zake alizo zibeba, huku wakimwongelesha mwenyeji wake mambo mawili matatu kuna kipindi wakawa kimya kabisa, Jackline akitafakari machache kichwani kwake, juu ya kazi aliyopewa na baba yake ya kutoa roho za watu sita, mpaka sasa ni mmoja alie mpoteza, lakini kun watu wengine watatu tayari, wamesha msindikiza mchungaji Chilumba, baada ya kuwaza ita kuwaje mpaka anawamaliza hao watano waliobaki, atakuwa amewauwa wangapi, kisha mawazo yake yalirudi kwa huyu kijana mlevi, kwanini licha ya kuishi kwenye nyumba kubwa kama hii lakini haja oa na wakati umri una mruhusu, Jackline akaamua kuvunja ukimya “eti! Kaka, kwanini ujaoa mpaka leo” kimya Jackline akujibwa, akamtazama mwenyeji wake, akamwona akiwa ameegemea kochi amesinzia, sekunde chache baadae akasikia akikoroma, “amepitiwa na usingizi”, Jackline akacheka kidogo, kisha akajisemea “mgeni siku ya kwanza, analala sebuleni” Jackline alitikisa kichwa chake, na kucheka kidogo,
Jakline aliendelea kula mpaka alipo maliza, kisha akatafuta bafu lilipo, alipo lipata akajaribu kufungua maji ya katoka, Jackline akaoga haraka kisha akarudi sebuleni, alimkuta Denis ambae bado akuwa akimjuwa jina mpaka muda ule, akiwa bado amelala vile vile kama alivyo muwacha, alicho fanya ni kulinyanyua lile begi lake dogo jeusi na kutafafuta sehemu nzuri ya kuliifadhi, alizunguka mpaka akafika kwenye store iliyojaa vifaha vya ujenzi, akalihifadhi humo, kisha akaanza kuikagua nyumba nzima kwa ndani, akagundua ilikuwa ni nyumba kubwa ya vyumba vinne, yenye jiko na sehemu zote muhimu kwa nyumba za familia, pia ina milango mitatu ya kutokea nje, alipomaliza akarudi sebuleni, akamkuta mwenyeji wake ametopea kwenye usingizi, akikoroma, Jackline akaenda kwenye kochi moja kubwa, kati ya makochi seti mbili (sofa) ya kisasa ya mle ndani, na kujilaza akimwigiza mwenyeji wake, ** Michael Nyati akiwa na mke wake Anitha au mama Jack, walikuwa bado sebuleni mama Jack akiwa amejilaza kwenye mapaja ya mume wake, macho kwenye tv, wakijaribu kufwatilia habari zilizotokea leo, alipata kusikia tukio la kuuwawa ya askari mstaafu wa jeshi afisa mteule Chilumba, ambae alijulikana kama mchungajiwa kanisa la kilokole, alipata kushuhudia polisi wakitoa taarifa hiyo, waki haidi kumsaka muuwaji mpaka watakapo mtia nguvuni, muda wote Michael alikuwa ametabasamu, “hivi huyu Jack amesha fika huko anakoelekea na huyo kijana mlevi” aliuliza mama Jack, bila kujibu Michael au baba Jack aliinua kitu mfano wa simu kubwa mezani na kuitazama, akabonyeza kidogo, kisha akamwonyesha mke wake “inaonyesha wameshafika, ni maeneo ya kibamba njia panda ya shule,” aliongea baba Jack akirudisha kile kipad mezani, “naimani atamaliza kazi vizuri, japo vikwazo ni vingi sana, maana amewauwa vijana watatu waliojaribu kumbaka” aliongezea baba Jack, mama Jack naye akadakia “tena na huyo aliejifanya kumsaidia ajiangalie, akileta ujinga wamapenzi atapotea” walicheka wote huku Anitha au mama Jack akianza kusinzia ** Asubui na mapema mida ya saa kumi na mbili na nusu, Jack alistushwa na pilika pilika za Denis, akijiandaa kwenda kazini, Jackline akajifanya bado amelala, alikuwa juu ya kochi kama alivyolala jana usiku, akamwona yule kijana mlevi akiwa mevaa vizuri akijilekebisha tai shingoni, wakati akitokea kenye chumba kimoja cha mle ndani, akaiendea friji na kutoa soda moja ya kopo aina ya cola, ni zile alizokuja nazo usiku, akainywa kwa kuigugumia mala mbili mfurulizo, ikawa imekwisha, Jackline akamwona mwenyeji wake akichukua kopo jingine la soda kwenye friji, kisha akachukua makopo mawili ya bia, zile alizobakisha jana mezani, akataka kutoka nje akaonekana kama amekumbuka kitu, hapo Jackline akamwona akiyaweka yale makopo mezani, kisha akaingia kwenye chumba alichotoka mwanzo, akutumia muda mrefu akarudi na shuka mkononi, Jackline alimshuhudia yule kijana mlevi akimfwa pale alipolala, kisha akamfunika na ile shuka, ni kweli kulikuwa na kaubaridi flani, alafu yule kijana akaingiza mkono mfukoni akatoa wallet nakuifungua, akachomoa noti tatu za elfu kumi kumi, na kuziweka mezani, akazikandamizia na kopo moja wapo la bia, kisha akamwona akiinua makopo yake ya soda na bia na kutoka nayo nje, muda mchache akasikia muungurumo wa gari likiondoka, Jackline akafungua macho yake, akabaki amejilaza juu yakochi akitafakari machache, juu ya huyu kijana mlevi, akupatajibu, akajaribu kutafuta usingizi lakini aukuja tena, akaamua kuamka, akakunja shuka nakulipeleka kwenye kile chumba alichoingia yule kijana mlevi wakati akijiandaa, Jakline akakitazama vizuri kile chumba akagunndua kuwa kilechumba ndicho cha mwenyeji wake, japo kilionekana smati kama kilikuwa akitumiki sana, alipotoka mle chumbani akavua lile gauni lake, akabaki na kikaptula cha jinsi na tishert, akaanza mazoezi ya viungo ya kupasha mwili, pia akapiga push up nyingi sana, akamalizia kwa mazoezi ya ngumi aina ya gou jo lou, na Tai kwondo, alipo maliza akaingia bafuni kuoga, alipomaliza akaanza kufanya usafi, nyumba yote, maana ilionyesha kuwa aifanyiwi usafi mala kwa mala, alikagua jikoni akakuta kuna vifaa vyote vyakupikia, ikiwepo jiko la gesi na umeme, pia jiko la mkaa na mkaa wenyewe, masufuria ya kila size, na vingine vingi, *** Michael Nyati alikuwa amesha amka, amekaa mbele ya TV akitazama kipindi cha magazeti, habari kubwa ilikuwa ni, mauwaji yaibuka dar, mchungaji maarufu auwawa, na nyingine ikiwa ni, mauwaji kwenye guest manzese, habari hizo ziliambatana na picha, Michael aliangalia picha za magazeti ambayo yalikuwa kipita pale kwenye TV, huku akisikiliza zile habari zikisomwa kwa kifupi, habari moja ilimvutia sana bwana Michael, iliyosema kuwa viongozi wa dini watoa tamko juu ya mauwaji ya mchungaji Chilumba, habari hii iliambatana na picha ya watu watatu wakiwa wamesimama, alichoweza kuona ni jina la gazeti kisha ile habari ikapita, alitaka kujilidhisha na ukweli wa alichokiona kwenye picha, akaagizia gazeti mjini haraka sana, itaendelea …..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata