BINTI MDUNGUAJI (32)

SEHEMU YA SELATHINI NA MBILI

ILIPOISHIA SEHEMU YA SELATHINI NA MOJA : alipo maliza akaliweka begi lake begani, nakuanza kushuka ngazi kwa haraka sana, lakini hakufika mbali akawaona vijana watatu wakipandisha ngazi mbio mbio, akajuwa kuwa ni wageni wake, hapo akajuwa uwa anatakiwa kufanya jambo kabla awaja mchelewesha, maana alsha juwa kuwa kuna polisi alishaona uwepo wake kule gholofani, endelea …….
Jackline Michael Nyati akaachia tabasamu lake la kuogofya, huku akitoa begi lake begani na kutoa kibati kimoja kinachotumika kuzuwia mitambo ya silaha yake, (resever cover) akakishika kono wa kulia na begi mkono wa kushoto, kisha akaanza kukimbia kwa kasi ya hajabu kushuka chini, ambako wale vijana watatu walikuwa wana tokea, nao awakuwa mabwege kwani walisha juwa kuwa huyu mwanamke siyo wa mchezo mchezo, wakasimama na kutoa bastora zao, toka mafichoni, na kuanza kuzikoki, tayari kumshambulia mwanamke huyu ambae alikuwa ana washukia kwa speed ya hajabu, lakini walichelewa, maana wakati wana jiandaa kumshambulia, tayari walimwona yule mwanamke ambae kimtazamo ni mrembo na mzuri sana, akiwa ameruka juu kama mwana sarakasi, akiwapita nakutua karibu na mwenzao ambae alikuwa nyuma kabisa kisha akamshindilia kile kibati shingoni, na kusababisha damu zimwagike kwa fujo, kama kuna bomba la maji lime pasuka, huku Jackline akiushika mkono wa yule jamaa ulioshikilia bastora na kugeuka nae kuwa tazama wenzake, kama afanyavyo mwalimu wa shabaha, anae mfundisha mwanafunzi kulenga kwa mala ya kwanza, hapo vijana wawili waliobakia, wakajuwa kuwa wakizubaa wa tapotea maisha, hivyo kitendo bila kuchelewa, waka ekelekeza bastola zao kwa Jackline na kumimina risasi kwa fujo, ambazo zilimwingia yule mwwenzao ambae tayari alikuwa amesha kata roho, ilisikika milindimo ya risasi mfurulizo, zilizo sikika mpaka kwenye gholofa ya pili, ambako wanchi waikuwa wengi wakifanya manunuzi kwenye maduka yaliyopo ndani ya jengo lile, na kusababisha mtafaluku ndani ya jengo lile, watu walikiambia hovyo huku na uku, wakitafuta mlango na ngazi za kutokea mahali pale, wale vijana wawii waliendelea kumwaga risasi bila kukoma, mpaka walipo sikia ‘kacha kacha’ tayari walisha ishiwa risasi, waka mwona Jackline akiwa bado amesimama nyuma ya mwenzao, ambae alikuwa anavuja damu, kama maji kwenye mfuko wa Rambo, ulio dondokea kwenye mti wa miba, na ndipo walipo juwa kuwa zile risasi zilikuwa zina mchakaza mwenzao, na siyo mwanamke walie mkusudia, hapo Jackline akuwapa nafasi ya kujiuliza, akiwa ame mshikilia yule kijana wa kwanza aka fanya kama ana mfundisha kupiga risasi, akawa tandika wale vijana wawili risasi za vichwa, kisha akamwachia yule kijana ambae kwa sasa alikuwa ametobolewa vibaya sana kwa kwa risasi, akadondoka chini, hapo jackiline ambae alikuwa ame chafuka kwa damu bahadhi ya sehemu za mwili wake, aka shuka ngazi kwa kasi ya ajabu, mpaka kwenye golofa ya pili akiungana na wanachi wengine kukimbia, huku akiangalia hhuku nahuku mpaka alipo liona duka la nguo, akatabasamu kidogo “yes” alijisemea Jackline huku akinyoosha mkono na kufuta nguo moja mfano wa kanga nyepesi, ** Denis alikuwa sambamba na Mahadhi, ndani ya ofisi yao wakifanya makadilio ya ramani ya jengo moja kubwa la kisasa walilo li sanifu wenyewe, kwa ajili ya wateja wao toka Nigeria, ambao walikuwa wana taka kutengeza hospital hapa nchini, “Denis kumbe unaishi na mke alafu uniambii kaka?” aliuliza Mahadhi, wakati wanaendelea na kazi yao, Denis akatulia kidogo na kushusha pumzi kwa nguvu, kisha akamtazama rafiki yake Mahadhi, “tena nikuambie kitu kaka?, yani ata leo nimekuambia kwa bahati mbaya tu!” aliongea Denis, kwasauti ambayo ilionyesha akuwa anatania, “haah! Denis inamaana tuna bifu?” aliuliza Mhadhi kwa mshangao, “hatuna bifu, ila nikikuona unamvizia mke wangu, itakuwa zaidi ya bifu” maneno hayo ya Denis, yalimfanya Mahadhi aangue kicheko kikubwa sana, “wecheka tu, maana nakuona jinsi unavyo jifanya bingwa la mademu” aliongea Denis kisha akaendelea na kazi ya kuitathmini ile ramani, “usifanye hivyo Denis, kweli wewe wakini fikilia hivyo?” alilalamika Mahadhi, huku bado anamalizia kicheko chake, “ndio maana sikuhizi uwa unanikimbia” alisema tena Mahadhi, Denis hakujibu kitu, zaidi aliendelea na kazi kimya kimya, huku ikimjia kumbukumbu ya miadi yake na yule dada mwenye shepu ya kuvutia kingono, “yule demu asije akawa najilengesha, maana anajifanya kunijuwa sana” aliwaza Denis, ambae alipania kumficha Mahadhi kuhusu miadi hiyo, maana alisha ambiwa na yule dada kuwa aende peke yake iliaweze kumsimulia kilicho msibu, ** wakati Denis anawaza hayo huku nako, yule dada tapeli Sablina aliuwa anapanga yake, maana mda wote alikuwa anachezea simu yake kuandika ujumbe ujumbe kwenda kwa mwanaume wake, ‘zingatia muda, ili tuwai kumkamua’ aliandika Sablina nakuituma, ‘nimeshafika zamani sana, nipo big braza’ alijibu mwanaume wa Sablina, ‘nikitoka nae, nimlete wapi?’ aliandika Sablina, mlete kona ya mabibo, tena aje na gari lake, ili iwe lahisi kuondoka nalo’ alijibu yule mwanaume, ‘akikataa itakuwaje?’ aliuliza tena Sablina, ‘siyo tabu, utanijulisha sehemu mlipo, nitakuja mala moja’ ** polisi walioekana wakipandisha ngazi mbio mbio, wakipisha na wananchi waliokuwa wanakimbia hovyo, kutoka nje ya jengo hilo la MH Production, polisi wakiongozwa insp Johnson, ambae leo alikuwa makini sana, maana alikumbuka siku ile kule buguruni, Johnson aliofika kwenye ngazi za kupandia ghorofa ya sita akasimama ghafla, huku akionyesha ishara ya kusimama kwa askari wake waliokuwa wanamfwata nyuma, nao wakasimama nakujificha kwenye kiambaza, insp Johnson alioneka amekaza macho yake mbele akitazama juu ya ngazi kadhaa, ambapo aliona miili ya watu watatu wakiwa wame lala kwenye madimbwi ya damu, lakini akukuwa na mtu aliesimama, “ameondoka huyu mshenzi” alisema kwa sauti ya kunong’ona, huku akianza kupandisha ngazi kusogea pale walipo lala wale watu watatu, huku akifwatiwa na askari wenzake, ambao nao walishikwa na mshangao, “ok! akuna kushangaa, nyie watano kagueni eneo hili, na msubiri hapa mpaka waje watu wa alama na michoro, sajenti utabakinao, wapigie simu mala moja watu wa mochoro” alisema Johnson, akionyesha kwa vidole askari watakao bakia, kisha akaondoka nao wale walio bakia, akiwapa maelekezo ya kutawanyika kenye mitaa ya pale kaliakoo, pia Johnson akapiga simu kuomba askari zaidi, waongezeke kumsaka muuwaji, maana Johnson aliamini kuwa, alie wauwa wale vijana ndie alie muuwa mzee Mathayo, na pia wale vijana ni kati ya wale vijana walio uliwa pale Matumaini Dispensal, na nikati ya vijana waliotumia gari la bwana Mathayo kuwatorosha wenzao waliokuwa wameuwawa, kwa hiyo wale vijana walio uwawa pale MH Production, walikuwa wame kuja na wakina mzee Masinde, na inaonekana kuwa walianza kumwona muuwaji mapema, na kuamua kumfwatilia, wakati anaendelea kuangaika kwenye mitaa ya kaliakoo, insp Johnson alikuwa akiwaza na kuwzua jinsi mchezo unavyo kwenda, na kufikilia jinsi atakavyo mlinda baba yake, juu ya kumkamata muuwaji siku ile, insp aliona ni ndoto za mchana, kwani alijuwa wazi kuwa, muuwaji awezi kuwepo eneo lile muda huo, ** taalifa za kuuwawa kwa mwanajeshi mstaafu, aliestaafu miaka mingisana nyuma , akiwa na cheo cha sajenti taji Mathayo, mbele ya kituo kikuu cha polisi, zilitambaa kwa haraka sana, huku Redio na Tv mbali mbali, zilitangaza kama taarifa ya hivi punde, (brecking news), saa sita na robo, mzee Nyati alikuwa mbele ya Tv yake akitazama habari hiyo nyeti aliyo kuwa anaisubiri kwa hamu, kilicho mshangaza ni kukutwa kwa maiti zaidi za vijana watatu, hapo akampigia simu mwanae, ** mida hiyo ndio mida mbayo Denis alimtoroka mahadhi na kishuka chini ya jengo la Mazao lenye gholofa tatu, na kumpigia simu yule mwana mke mwenye msambwanda wa ajabu, kama waliambizana kumbe yule mwanamke nae alikuwa tayari amesha shuka chini ya jengo lao la Kamanga Plaza, lengo lake likiwa ni moja tu, kama Denis ange ghaili kuongea nae, basi yeye angemvizia wakati anaenda kwenye chakula cha mchana kisha ange jifanya amekutana nae kwa bahati mbaya, dakika chache baadae walikuwa ndani ya gari, tuna elekea wapi, aliuliza Sablina, “labda useme wewe, sehemu unayo iona inafaa kukaa” aliongea Denis akiwa ajuwi kuwa mwenzie anawasiliana na mwanaume wake kwaajili ya kumfanyia kitu roho inapenda, ** “za saa hizi baba” alisalimia Jackline, baada ya kupokea simu toka kwa baba yake, Jackline ambae alikuwa ndani ya dala dala litokalo poster, alilopandia mnazi mmoja kituo cha baridi, na sasa walikuwa wana katiza manzese, kuelekea ubungo, akika usingeweza kumjuwa kama ametoka kufanya tukio mida ile ile, kwa jinsi alyo jitanza ile nguo aliyo ikwiba pale dukani, “naiona kazi yako, vipi hupo salama?” aliuliza mzee Nyati, “nipo salama baba, ni takupigia nikifika nyumbani,” alisema Jackline akiofia kkunaswa maongezi yake na kijana mmoja pembeni yake, alie kuwa anamtaza sana, “samahani dada sijuwi ulijiumiza sehemu, naona kuna madoa ya damu usoni mwako, unge nunua maji unawe kidogo,” aliongea yule kijana, hapo Jackline alistuka na kumtazama yule kijana, itaendelea………..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata