
BINTI MDUNGUAJI (33)

SEHEMU YA SELATHINI NA TATU
ILIPOISHIA SEHEMU YA SELATHINI NA MBILI : “naiona kazi yako, vipi hupo salama?” aliuliza mzee Nyati, “nipo salama baba, ni takupigia nikifika nyumbani,” alisema Jackline akiofia kkunaswa maongezi yake na kijana mmoja pembeni yake, alie kuwa anamtaza sana, “samahani dada sijuwi ulijiumiza sehemu, naona kuna madoa ya damu usoni mwako, unge nunua maji unawe kidogo,” aliongea yule kijana, hapo Jackline alistuka na kumtazama yule kijana, ENDELEA ……
“Haaa! kumbe yule muuza bucha alinimwagia damu nyingi sana?” alijifanya kushangaa Jackline, “lakini aijapoteza mwonekano wako mzuri” alioongea yule kijana huku akiachia tabasamu, wakati huo dala dala lilisimama kwenye kituo cha mahakama ya ndizi, hapo Jackline Michael Nyati, akashuka haraka toka kwenye dala dala, kisha akaanza kutembea akitazama huku na huku, akitafuta sehemu ambayo anaweza kujiweka vizuri kwa kuusafisha uso wake, kwanza kabisa akaingia kwenye vibanda vya wauza mitumba na kununua tishert moja, alafu akamuiza yule muuza mitumba, “samahani kaka eti kuna guest house hous maeneo ya karibu na hapa” yule kijana alimtazama kwanza Jacklie huku ameachia tabasamu la kumsuta, akiamini kuwa mwanamke huyu anamiadi na mwanaume flani, “hapo mbele kidogo kuna bar moja kubwa sana, inaguest nzuri sana ina vyumba vizuri sana” hapo Jackline akaaga na kuondoka zake, akielekea upande alioelekezwa na yule muuza mitumba, mpaka alipoona bar moja kubwa sana, ailiyo jaliwa na watu wengi sana, wakipata chakula cha mchana, na wengine wakishushia vinywaji mbali mbali zikiwepo pombe, akachepuka na kuingia ndani ya bar hiyo kisha akaenda moja kwamoja kwenye sehemu ya mapokezi, akaomba apatiwe chumba kimoja chenye bafu ndani yake, kwaa jili ya kujifanyia usafi, ** baada ya kuangaika kwa mda mrefu sana, akiangaika kwenye mitaa ya kaliakoo, sambamba na askari wake, akimtafuta Jackline Nyati, insp Johnson aliamua kurudi kituo kikuu, ambapo alimkuta baba yae akiwa pale anamsubiri, ni kwelimzee huyu akuweza kuinua makalio yake kurudi nyumbani, akiofia usalama wake, Insp Johnson baada ya kukamilisha report yake, aliaga na kuondoka na baba yake wakitumia gari la baba yake huku lie jingine 110 walilokuja nalo wale vijana watatu, liligunduliwa na polisi na kupelekwa kituoni, “baba huu ni wakati wakuweka wazi kila kitu, iliniweze kuokoa maisha yako” aliongea Johnson, baada ya kutoka kituoni pale, “mwanangu kwakweli akuna ukweli wowote uliojificha, sijuwi huyo mtu anatuandama kwanini?” aliongea mzee huyu ambae alioneka bado anania ya kuficha swala hili, “atakama ujuwi chanzo lakini siuna juwa nanani anausika?” aliongea Johnson, “yani muuwaji ndio kitenda wili kikubwa” alongea mzee huyu bila aibu yoyote, “baba sijuwi kwanini una nificha mimi mwanao ambae ndie nawezakukusaidia kuepuka na hili, maana kama msinge mjuwa muuwaji, msinge watuma wale vijana kwenda kumteka yule binti” hapo mzee Masinde akatulia kimya kabisa, akitazamambele ya gari, “kumbuka nilicho kuambia dakika chache kabla ya mwenzio kuuwawa?” aliongea Johnson akionyesha kushikwa na uchungu mkali juu ya baba yake, ambae aliamini kuwa yupo hatarini kupoteza maisha, “Johnson naomba uelewe kama ninavyo kuambia, simjuwi muuwaji na sijuwi anafanya hayo kwa sababu gani?” alisema mzee Masinde kwa hasira, hapo Johnson akakaa kimya kidogo kisha aka ongea kwa sauti ya upole kidogo, “nitajitaidi kuyalinda maisha yako mpaka hapo utakapoona inafaha kunieleza ukweli” ** baada ya kuoga na kubadiri tishert, Jackline alitoka kwenye chumba alicho kodisha, na kutokeza kwenye sehemu ya bar, akitaka kwenda kurudisha funuo a chumba mala akashangaa kuona gari la Denis likipaki kwenye maegesho ya ile bar, “mh! so Denis yule?’ alijiuliza Jackline huku akisogea sehemu nzur ambayo aliamini anaweza kumwona Denis pasipo yeye kumwona, akajisogeza karibu na ukimgo wa ile sehemu iliyo kuwa na watu wengi waendelea kupata chakula na vnywaji, sehemu ambayo ilikuwa karibu kabisa na liliposimama gari la Denis, wakitenganishwa na uzio wa mbao, ulio tengenezwa kwa mtindo wa draft ndogo ndogo, na kufichwa na maua malefu yaliyostawi vyema, akiwa pale amesimama akastuka kumwona akishuka kwenye gari, mwanamke mmoja mwenye shepu ya maana, “ni yule wa juzi, nilijuwa tu huyu mwanamke analake jambo” aliwaza Jackline, huku wivu wa hatari ukiwa ume mkamata, aliona wazi kuwa kuna kila dalili ya kuchomoa roho ya mtu, “karibu dada ni kuhudumie nini?” Jackline alistuliwa na sauti ya muhudumu wakike, hapo Jackline akatazama pembeni yake na kuona kunameza yenye viti vitatu, ambavyo havikuwa vimekaliwa na mtu, “naomba soda” aliongea Jackline huku akitoa fedha na kumpatia yule mhudumu, kisha yeye akaa kwe kiti kimoja kati ya vile vitatu, na kuweka lile begi lake chini karibu kabisa ya miguu yake, huku muda wote macho yake yakiwa kwa Denis na yule mwanamke, ambao aliwaona wakiingia mle ndani nakwenda kukaa meza ya nne toka alipo kaa yeye, mala mhudumu akaleta soda yake, hapo Jackline akiwa amejitanda vizuri ile nguo aliyo iba kule kaliakoo, alikunywa soda yake taratibu akiwa fwatilia Denis na yule mwanamke, ambao walionekana wakiagiza kitu kwa mhudumu, na baada ya mhudumu kuondoka, wakaonekana wakiongea jambo flani, na mwongea ji alikuwa yule mwanamke ambae alikuwa aamsimulia kitu Denis, “samahani dada naweza kukaa hapa” Jackline alistuliwa na sauti nzito ya kiume, akamtazama mwongea alikuwa jamaa moja ambae kimwonekano ni kipande cha mtu kilicho panda hewani, na kutanuka maeneo ya kifua, akionyesha kuwa ni mtu anae jishughulisha na unyanyuwaji wa vitu vizito, Jackline akaona kuwa itakuwa vyema akia na mtu mwingine pale mezani iliasionekane kilahisi, “hapana tatizo kaa tu!” alijibu Jackline , ambae sasa alibadiri mfumo wa utazmaji, maana hakutaka huyu jamaa wa pembeni yake, ajuwe kama kuna watu anawafwatilia, ** baada ya kumfikisha baba yake nyumbani insp Johnson alirudi kituo kikuu kwenda kupata alama za vidole, za muuwaji alie wa uwa wale vijana watatu, ambmae aliamini ndie alie muuwa mzee Mathayo, alipofika pale kituoni alikuta bahadhi ya polisi wakiwa nje ya jengo la kituo wakijadiliana kuhusu tukio lililo tokea leo asubuhi, ni baada ya kuangaika mtaani wakimsaka muuwaji, walieambiwa uwa ni mwanamke, , bila mafanikio yoyote, insp Johnson akiwa na mawazo mengi sana, alipitiliza ndani moja kwa moja, akiwaacha askari wkiwa makundi makundi wakipiga porojo, Johnson akaingia ofisini kwake, na kukuta report ya mtambuzi wa alama ikiwa mezani kwake, akaitazama kwa umakini sana, akagundua kuwa report ile ni tofauti na report za siku za nyuma, hii ilionyeshakuwa marehemu wame uwana wenyewe kwa wenywe, kwa kutumia bastola zilizo kutwa eneo la tukio, “itawezekana vipi?” alijiuliza insp Johnson, “huyu mtu anaonekana, anamafunzo makubwa sana ya kijeshi” alendelea kuwaza Johnson, wakati huo akakumuka jambo, akachukuwa simu yake, na kupiga kwa pc Busungu, aikuchukuwa mda mrefu akapokea, insp Johnson akamwelekeza wakutane nyumbani kwake jioni, akidai kunajambo anataka kumweleza, ** akiwa ajuwi lolote Denis pale coner bar, akinywa bia pamoja na Sablina, ni baada ya kumaliza kula, huku anamsikiliza yule mwanamke tapeli, ambae alikuwa anamsimulia story ya uongo, akidai kuwa, kuna mwanaume ambae alipanga kuoana nae, hivyo kwa kujuwa ndie mmewake mtarajiwa yeye Sablina akauza nyumba yake ya urithi, aliyo achiwa na marehemu mama yake, na fedha akamlkabidhi yule mwanaume, ili afanyie biashara itakayo wasaidia katika maisha yao, sablina alidai kuwa yule jamaa yake alitoroka na zile fedha, na mpaka leo haja mwona tena, “dah! pole sana” alisema Denis, ambae alionekana kuanza kukolea kilevi, huku anaweka chupa tupu ya bia mezani na kufungua nyingine, “sante mbona nilisha sahau maumivu” alisema yule mwanamke, huku akiandika ujumbe kwenye simu yake, ‘naona pombe imesha anza kumlegeza’ akaituma kwa mwanaume wake, ambae alikuwa amekaa meza ya nne toka walipo kaa wao, aikuchuuwa mda mrefu jibu likarudi, ‘poa endelea kumpigisha story, mpaka alegee kisha tumwamishe maana naona hapa kazi itakuwa ngumu’ Sablina alipo maliza kuisoma ile sms akaiweka simu yake mezani, “yani nili hapa kuwa sitopenda tena tena, lakini nashangaa nilipokuona kwa mala ya kwanza nikajikuta natokea kukupenda sana” aliongea Sablina tapeli, huku akijichekesha chekesha, ni kauli iliyo mstua Denis, “mh! ume nipenda, ki vipi?” aliuliza Denis kwa mshangao, “yani ata mimi sielewi, nime tokea kukupenda tu!, unaonekana mstaarabu, mpole, unamoyo wa huruma, na jisikia raha kukaa karibu na wewe, yani natamani kama unge kuwa mume wangu” aliongea Sablina kwa sauti ya uzuni, huku akijidai kujizuwia kulia, kiasi cha kumfanya Denis aingiwe na huruma, lakini moyoni mwake akakili kuwa leo amekutana na kituko cha mwaka,mala Denis akahisi kuwa kuna ujumbe umeingia kwenye simu yake, akachomoa simu yake na kusoma ujumbe toka kwa Jackline, ‘hupo wapi?’ Denis akajibu, ‘nipo coner ya mabibo na pata bia kdogo nirudi nyumbani, vipi ume nimiss?’ kisha akaitumwa kwa mama kijacho, “usijari mungu atakupatia mume mzuri zaidi” aliongea Denis wakati anasubiri jibu toka kwa Jackline, ‘sidhani kama nita mpata kama wewe, kwani unachati na nani?” aliuliza sablina ambae alianza kutilia mashaka juu ya uchezeaji wa simu wa Denis, aikuchukuwa mda mrefu jibu lika rudi, ‘yani nahisi kama naibiwa, maana hapa nilipo chini kunatekenya sana?’ “hahahahaha! nachati na mke wangu” Denis alimjibu Sablina, huku anaandika sms, kurudisha jibu kwa mpenzi wake Jackline, ‘usijari uwezi kuibiwa, nakuja kukuletea dudu, maana najuwa inabidi tumkuze mtoto’ kisha akaituma, maongezi yaliendelea huku vinywaji vina endelea, walitumia mda mrefu sana, wakiongea na kunywa pombe, Denis alioneka kunywa pombe nyingi sana, lakini akuoneka kulewa mpaka, kupitiliza, ndipo Sablina akaomba ushauri kwa bwana wake, kupitia sms, ‘huyu jamaa anaoneka nimzoefu wa pombe sasa tufanyaje?’ jamaa yake akajibu, ‘tutumi plani B, akiinuka wenda chooni tu! nifwate, hapa nilipo kaa’ sablina akajibu ‘sawa’ atimae saa kumi na mbili na nusu, ndipo Denis alipo inuka na kuelekea chooni, akidai kuwa, akitoka chooni wamalizie bia zao waondoke, ile Denis anapotea kwenye mlengo wa choo, Sablina akainuka haraka na kumfwata jamaa yake, ambae alikuwa ame kaa meza ya nne, toka alipo kaa yeye na Denis, alimfikia mwaume wake ambae alikuwa ame kaa pamoja na mwanamke mmoja alie jitanda nguo kichwani na kushindwa kumtambua vizuri, kutokana na ile nguo na giza lililoanza kutanda, “amesema akitoka chooni anamalizia bia tunaondoka, kwa hiyo tunafanyaje?, amaana namwona kama hajalewa vizuri” aliuliza Sablina akiwa ame simama mbele ya meza hile aliyo kalia mwanaume wake, ambae aliingiza mkono kwenye mfuko wake wa suluali na kutoa kichupa kidogo hivi, akamtazama yule mwanamke wa pembeni yake, ambae muda wote alikuwa akichezea simu huku anakunywa soda, akamwona yupo busy na mambo yake, akamgeukia Sablina, nenda ka mwekee hii kwenye bia yake, akinywa kidogo tu! msisitize kuondoka maana akichelewa kuingia kwenye gari ata lala pale pale, itakuwa msala kumbeba” aliongea yule jamaa huku anampa Sablina kile kichupa, sablina akakipokea na kurudi haraka kwenye meza yake akakifungua kile kichupa na kumiminia tonye la maji kwenye chupa ya bia ya Denis, alafu akakifunga ile kichupa na kukiweka kwenye mkoba wake, Denis akiwa ajuwi kinacho tokea, alitoka chooni na kurudi pale alipo mwacha Sablina, ile anakaa tu akapokea ujumbe kwenye simu yake, akaitoa simu yake mfukoni, huku akiinua bia yake na kupiga mafundo mfululizo mkapaalipo kuwa imekwisha, akaiweka chupa tupu mezani na kuufungua ujumbe kwenye simu yake ‘usinywe hiyo bia’ hap Denis aliduwaa, akajaitazama ile chupa mezani, akaiona ikiwa na wenzake kama watatu huku zikicheza cheza kama zipo kwenye bembea, na kuanza kufifi kwa mwanga usoni kwake, kabla aja mwona yule dada akisimama na kumshika mkono kisha kuanza kumpeleka kwenye gari, lakini Dens anahisi miguu yake ina kuwa mizito, kiasi cha kutaka kudoka, mala anaongezeka mwanume mmoja mwenye nguvu, ambae ana mskika kwanguvu na kuzidi kumsogeza kwenye gari lake, hapo Denis anaona giza nene likitanda usoni mwake, macho yake yana shindwa kufumbuka, kina fwata kimya kizito, mala anaanza kisikia sauti ya mvumo wa feni, inayotembea taratibu, akasikia sauti ya music wa taratibu, na sauti za watu wakiongea karibu yake, “kwahiyo shemeji ujajuwa alifikaje hapa?” ilikuwa sauti ya Mahadhi, “yani tena nashukuru aliiweza kufika mpaka hapa, maana ange zidiwa huko mbali sijuwi ingekuwaje” iilikuwa sauti ya Jackline, “daaa! ila shemeji una moyo sana, umeweza kukaa na mtu ambae ajitambui kwa siku tatu” sasa ilikuwa ni sauti ya boss wake, hapo Denis akapata picha kwamba yupo nyumbani kwake na hao ni wakina Mahadhi, akajaribu kufumbua macho, yaka fumbuka, akajikkuta yupo ndani ya chumba chake nyumbani kwake kibamba njia panda ya shule, ameamka jamani, wakwanza kumwona alikuwa Mahadhi, “we mshenz… umefikaje huku bila kuniambia nawakati nilikucha ofisi, au… unampango na mke wangu” aliongea Denis kwa sauti ya uchovu, huku akijaribu kuinuka toka kitandani, kumfwata Mahadhi, ambae akutaka kumwonywsha kabisa mpenzi, itaendelea….

