
BINTI MDUNGUAJI (35)

SEHEMU YA SELATHINI NA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA SELATHINI NA NNE : kisha akampatia yule konda fedha zilizo bakia, dereva kuona kuwa mwenzie amezidiwa na mwanamke akaona labda mwenzie alizidisha dose ya ulevi anao tumia, bola akamsaidie kumwadabisa yule mwanamke, wakati huo abilia wote walikuwa wana shangilia, wakimtazama dereva akijiingiza kwenye mikono hatari, hapo sasa kilicho fwata kilimfanya pc Kess ashuke haraka kwenye gari, endelea…….
Dereva alipo mfikia yule dada, akajaribu kurusha ngumi, lakini akashangaa mkono wake ukidakwa na kubanwa kwanguvu, kama umebanwa na ile spana ya kutengenezea mabomba, huku konda kita akiwa ameachiwa, ana jikagua mdomo wake uliokuwa unavuja damu kwa kukosa meneo, Dereva alijaribu kufurukuta, lakini wapi, alibanwa kwanguvu sana kiasi cha kuhjisimkono wake una waka moto, wakati anasikilizia maumivu ya mkono, alistuka akipigwa ngumi moja mzito sana ya shavu, huku akiachomoka kwenye mkono wa yule mwanamke ambae sasa, aligunduwa kuwa, sio wa mchezo mchezo, kondakota na yeye akaona wakati huu mwenzie anatandikwa na yeye ndio wakati wa kulipiza kipigo kwa huyu mwanamke, akamzungukia kwa nyuma na kurusha teke kwenda kwa yule mwanamke, lakini bahati aikuwa upande wake, maana mguu hule ulikutana na mguu wa mwanamke huyu wa hajabu, ikasikika “paaaa!” kama sauti ya kuvunjika kwa mti mkavu, akiwa ajatambua killicho mkuta mwenzie, Dereva na yeye akarusha ngumi kumpiga mdada wa hatari, lakini ilikuwa siku mbaya kwake, maana mkono wake ulidakwa, na kukutana na ngumi mfululizo za usoni, zilizo sababisha yule Dereva aone giza usoni, na kujibwa ga chini kama kiloba, huku damu nyingi zikimchuruzka sehemu mbali mbali za uso wake, ** insp Johnson alikuwa ofisini kwake akijiandaa kwenda kwa mzee Soud ili kupata ushauri, mala akasikia simu yake ya mkononi ikiita, akaitoa na kuitazama ‘Pc Kessy’ akaipokea, vipi Kessy mgonjwa wako anasemaje?” aliuliza insp Johson mala tu baada ya kupokea simu toka kwa askari huyu, alie omba kwenda kumtama mgonjwa wake hospital ya tumbi uko kibaha, “afande bado sija fika hospital nipohapa kiluvya gogoni” aliongea pc Kessy, kwa sauti ya chini kidogo, “ebu! ongeza sauti kidogo maana kuna kelele sana hapo ulipo” alishauri insp Johnson, “afande hapa nilipo kuna fujo zina tokea, namwona yule mwanamke wasikuile buguruni akiwapiga kondakta na Dereva wake” ahapo Insp Johnson alistuka na kusimama toka kwenye kiti alicho kalia, “una uakkika pc?” aliluza huku anauendea mlango wa ofisi nakutoka nje, nauwakika ni yeye, na mambo anayo yafanya hapa kwakweli kla mtu anashgaa, maana anawapiga awa jamaa, utazani yeye ni askari sita wajeshi la ulinzi” alisisitiza pc Kessy, “ok! nachukuwa askari tunakuja wewe mfwatilie mpaka anapo elekea, tutakuwa tua wasiliana” ** “ndiyo afande fanyeni haraka, mimi sina la kufanya, maana sina silaha yoyote” aliongea Kessy, huku anamtazama yule dada ambae baada ya kumaliza kuwaadhibu wale watukutu wawili, kisha akavuka barabara na kuelekea kwenye kituo cha daladala zinazo rudi kibamba, hapo pc Kessy na yeye akavuka barabara halaka sana na kuwa kwenye kituo hicho cha daladala zinazorudi kibamba, akamkuta yule dada akiwa pale kituoni, alipo litazama lile basi upande wapili wa barabara bado lilikuwa lipo pale pale, lime zungukwa na watu waki washangaa wale watukutu wawili, aikuchukuwa mda mrefu, likaja daladala likitokea kibaha likasimama pale kituoni Kessy akategemea umwona yule mwanamke akipanda haraka, ilinayeye apande lakini aikuwa hivyo alishangaa kumwona yule dada akiliacha lile gari likishusha abilia na kupakiza kisha likaondoka, mala simu yake ikaita Kessy alipoitazama alikuwa ni insp Johnson, “bado hupo nae” lilikuwa swali toka kwa insp Johnson, “ndio” Kessy alijibu kwa kifupi, “swa sisi tupo njiani tuna kuja wewe endelea kumfwatilian na kutupa report,” hapo wakakata simu, pc Kessy akatulia pale kituoni akimfwatilia yule mwanamke, ambae sekunde chache baadae akamwona akipokea simu, “kisha akayanasa maongezi yake, “ndio nimesha pata, ….. ndio nilipitilizwa na gari… ndionasubiri gari la kurudi” sawa nitakujulisha” yule mwanamke alimaliza kuongea na simu, na muda mchache baadae likaja daladala lingine, hapo Kessy akamwona yule dada akipanda haraka ndani ya gari hilo, na yeye akuzubaa akapanda haraka, mala simu yake ikaita,akaipokea, “samahni nitakupigia nikishukakwenye daladala aliongea Kessy, huku gari likiondoka, kuekea kibamba njia panda ya shule, kutoka gogoni mpaka njiapanda ya shule nimweno wa dakika tatumpaka nne kwa gari la habilia, kwa hiyo aikuwachukuwa mda mlefu kufika na gari kusimama, hapo Kesy akamwona yule mwanamke akishuka toka kwenye gari, pamoja na abilia wengine, hapo na yeye akuzubaa akashuka mala moja, na kumtazama yule mwanamke, akamwona akivuka barabara na kuelekea upande wa pili, hapo Kessy akchomoa simu yake huku aksubiri magari matatu yaliyo kuwa yana pita barabarani yapite ili na yeye avuke kumfwata huyu mwanamke, kama alivya agizwa kufanya, Kessy alitumia muda huo kupiga simu kwa insp Johnson, “tumeshkuka kimba njiapanda ya shule mkono wa kushoto kama unaenda kibaha,” aliongea haraka haraka, huku akianza kuvuka bara bara, “sawa tunakuja tupo mbezi, endelea kumfwatilia kwa umakini” alisistiza Johnson, na kukata simu, baada ya kuvuka barabara Kessy alimwona yule mwanamke hatari akii toka kwenye duka moja, ambalo alionekana kama alikuwa ananunu kitu flani, kisha akaingia kwenye moja ya chochoro ya maduka yale, hapo Kessy akatembea haraka na kuifwata ile chochoro, lakini hakuona mtu mbele yake, akatembea mbele kama atuwa hamsini mpalka sitini akizipita nyumba kadhaa, mpaka akatokea kwenye makutano ya chochoro nne, zilizo tenganisha nyumba nne, akashidwa aftwate njia hipi kati ya zile, akakosa ata mtu wa kumwuliza, maana chochoro ilikuwa kimya sana, akachomoa simu yake na kunnza kuongea na isp Johnson, ** “tupo kibamba kwa mangi, vipi bado hupo nae” aliuliza insp Johnson mala tu alipo ipokea simu toka kwa askari wake, afande kwakweli amenipote, katika mazingila ya kutatanisha” kauli hiyo ilimstua sana insp Johnson, sababu alijuwa kuwa muuwaji alisha gunduwa kuwa anafwatiliwa hivyo kinachofwata, “bado ujanipoteza, nipo hapa” kupitia kwenye simu ya askari wake, insp Johnson aliweza kusikia sauti ya mwanamke, ikimdhiaki askari wake, “ “mungu wangu nmekwisha” likuwa nisauti ya kunong’ona iliyo jaa uoga ya askari wake iliyo mfikia masikioni mwake, kupitia kwenye siimu ya pc Kessy ambayo ilikuwa bado aijakatwa, “ongeza mwendo, mwenzetu yupo kwenhatari” alipiga kelele insp Jonson akimwamlisha askari wake aliekaa kwenye kiti cha dereva akitembea speed ya mia themanini, ambayo alitembea nayo toka walivyo toka mjini kituo kikuu, huku askari sita wakiwa wana ning’inia nyuma ya gari hilo aina ya land lover 110, huku wameshikilia vyema silaha zao, zilizo jaa risasi, na sasa gari alikuwa na uwezo wakukimbia zaidi ya hapa, insp Johnson akiwa bado ameiweka simu sikioni, alijaribu kumwita Kessy, “hallow hallow, kessy unanisikia, ebu kimbia mahali hapo haraka” aliongea insp Johnson bila kujibiwa kitu, zaidi alisikia kishido cha kitu kizito kikidondoka chini, kikifwatiwa na mikoromo ya mtu alie kwenye mauivu makali, na arakati za kukata roho, hapo insp akajuwa kuwa amesha poteza askari mwingine, mwili ulimwisha nguvu, akabaki ameganda na simu bado hipo sikioni, “hallow insp wafundishe askari wako namna ya kufwatilia mtu! alafu nakuomba kaambali na hii kesi, wacha nimalizane na watu wangu pasipo kuongeza wasio usika” iinsp aliweza kuisikia sauti ya mwanamke ikisikika kwenye simu yake, ilizihilishakuwa Kessy hayupo duniani, “hallow, ebu tuambie unataka..” insp Jonson akuweza kumalizia maneno yake kwani simu ilikatika, dakika chache baadae waliingia kibamba njia panda na kusimamisha gari lao mbele ya maduka yaliyopo pembeni ya barabara, kisha ikatlwa amri askari wote wasambae kwenye chochoro za yale maduka, kumtafuta mwenzao, ambae hawakutumia mda mrefu kumpatana, wakikuta kisu na simu ya Kessy , waka mchkuwa mwenzao, na kuondoka nae haraka sana, wakiwaacha raia wanashangaa wasijuwe kinacho endelea, ** Jackline Michael Nyati, ambae alikuwa amekosa amani, kutokana na afya ya Denis, baada ya kumaliza kutoa roho ya askari polisi aliekuwa anamfwatilia alirudi barabarani na kujibanza sehemu akiwa tazama polisi wakizunguka eneo alilo fanyia tukio, mda mfupi uliopita, aliwaona wakichukuwa mwili wa mwenzao na kuondoka zzao, ndipo yeye alipo panda boda boda na kueleka nyumbani, baada ya kufika akapiga simu kwa baba ake na kumsimulia, kilicho tokea kuanzia makondakta wa daradara na yule askari polisi, baba yake alimsisitiza kuwa makinisana kwa sasa ikiwezekana apumzike kufanya mauwaji ya aina yoyote, ili kuwa sahaulisha polisi, pia baba yake alimwelekeza namna ya kutengeneza, dawa ya kumnywesha Denis, huku akimtahadharisha kuwa ajiandae kwa matokea ya mikojo, atakayo ikojoa huyu jamaa, ** saa tisa jioni insp Jonson alikuwa yupo kituo kuu cha polisi, akiwa amesimama nje akiwasikia polisi wenzakewapale kituoni wakijadiliana juu ya mauwaji yanayo endela, “unajuwa mimi siamini kama huyo muuwaji ni mwanamke kweli” aliongea askari mmoja alie kuwa zamu ya ulinzi pale kituoni, “sikia kijana kuna mfungwa mmoja hivi, yupo ukonga, anaitwa Majaliwa, uwa anaendaga wizalani kufyeka, yule jamaa ukitazama usowake unaweza kusema alikatwa na mapanga, yani atamdomoi amepoteza bahadhi yameno, uliza sasa kilicho mkuta” aliongea askari polisi mmoja mwenye cheo cha sajenti ambae sikuhiyo alikuwa mkuu wa zamu pale kituo kikuu, “alifanywa nini” aliuliza yule askari, huku wenzie wanne waliokuwa pamoja, wakitega masikio, sambamba na insp Johnson ambae akili yake ilikuwa imeganda, “yule mfungwa alisimulia kuwa, wakati yupo kidato cha pili walijaribu kumbaka binti mmoja, unaambiwa huyo binti ni mzuri sana, yani kwa kipindi hicho huko Songea, akuna mwanamke angeweza kumfikia kwa uzuri, lakini kilicho watokea ni balaha, maana licha ya kuwa watatu lakini walitembezewa kichapo mpaka wakelewa somo, yani siku yapil walienda kuripot wenyewe kitu cha polisi” alisimulia yule askari ambae ata kwa umri alionekana kuwa ni mtu mzima kidogo, ile story ili mvutia Johnson, “huyo mfungwa anweza kuwa na umri gani?” aliuliza insp Johnson, huku ajkisogea eneo la tukio, “mh! n miaka ishilini na nne au natano hivi, maana usoni amepondeka sana, uwezi kukadiria umri wake” alijibu yule askari sajenti, “ok! ilikuwa Songea, unasema huyo mfungwa anaitwa nani?” aliuliza Johnson, kwa umakini sana, ** saa tatu usiku Jackline alishapokea simu toka kwa Mahadhi akiulizia hali ya Denis,akamjib kuwa bado ajisikii vizuri, Jackline aliwaficha hali halisi, ili wasije kutemblea pale nyumbani na kumkuta mwenzao yupo vile, wakati huo Jacline Michael Nyati, alikuwa amesha nadaa ile dawa, aliyo elekezwa na baba yake, alicho kifanya ni kumwamishia Denis chumba cha wagenikisha akatafutakipisi kifupi cha mpra wa kupitishia maji, akamvwesha Denis kwenye dudu yake, kisha ule mpira akauweka kwenye dumu la lita tano, kisha aka mnywesha ile dawa, alafu akaenda kutulia sebleni na kusubiri kwa muda wa lisaa lizima akaenda kutazama lile dumu la lita tano, lilikuwa limejaa mikojo nusu, aka lichukuwa na kwenda kumwaga kisha akarudi na kuliweka tena, kisha akarudi sebuleni, nakumpigia simu mama yake, ilikumweleza matokeo ya dawa inavyoanza kufanya kazi, “endelea kumwangalia, ila akiamka akikisha unampa uji wamoto, na supu” aliongea mama Jackline, lakini wakati wanaagana kunakitu mama Jackline akaonekana kutilia shaka jambo flani, “hivi Jack hupo salama kweli” aliuliza mama Jaackline, “zaidi ya salama, siunajuwa mimi zaidi ya kikosi cha makomadoo” alijibu Jackline kwa kujiamini, “hacha utani mwanangu, atakama ni komadoo sijuwi kitu gani, lakini kumbuka, ukali wote wakiu lakini mbele ya maji uonekana mjinga, namaanisha umeziona sikuzako, maana sielewi jinsi unavyo hema sielewi elewi” hapo Jackline akatulia kidogo na kushusha pumzi kwa nguvu, itaendelea ……..

