BINTI MDUNGUAJI (44)

SEHEMU YA AROBAINI NA NNE

ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA TATU : ambao wamepoteza maisha miezi kadhaa iliyopita” aliongea Busungu huku akionyesha walaka maalumu unao waruhusu wao kufany mahojiano na mzee huyo, “ok! ila ninaombi moja, naomba nije kesho kituoni, sababu leo sija jiandaa kabisa, pia nina udhuru, nimeitwa kwenye taflija moja, nazani me isikia, ni hii ya kuwasaidia walemavu” aliongea mzee Masinde kwa sauti ya pole iliyokosa matumaini, pasipo kujuwa kuwa huko anakoomba kwenda siyo sehemu salama kwake, ENDELEA………
“kwakweli mzee wangu tukikubari ombi lako, atuto weza kutoa maelezo kwa mkuu wetu” aliongea Pc Pange, wakati huo wote wakitoa viji tabu vidogo, na karamu zao za wino, tayari kuanza mahojiano, huku mzee Masinde akikunja uso kwa hasira, ya kukosa Taflija, iliyo andaliwa na rafiki yake bwana Alex, “ok! ngoja nimtalifu bwana Alex, kuwa snitachelewa kwenda kwenye Taflija” aliongea mzee Masinde, huku akitoa simu yake mfukoni, “utachelewa au uendi kabisa” alijisemea Busungu kimoyo moyo, ** maeneo ya Cosovor Hotel yalikuwa yame tawaliwa na uwingi wa watu, wengi wao wakiwa ni walemavu wa aina mbali mbali, viwete vipofu, walemavu wa mikono, ata wangozipia viziwi, mabubu, na ata wenye tatizo la hakili, eneo hilo lilionekana ku zungukwa na polisi wachache, waiokuwa wame kaa kwenye mlango wa kuingilia, pamoja na vijana wanne waliovalia suti nyeusi wakikagua kila anae ingia ndani, kwa kutumia vifaa maalumu, vya kutambua kitu chochote cha hatari kilicho bebwa na mtu anaepita mahali hapo, kwaajili ya kuingia ndani, wakati huo huo mita mia moja, toka kwenye jengo hilo kubwa sana, palikuwa na bar moja kubwa sana ya Mwenge pub, ambayo usiku huu ilichangamka sana, wakione kana watu wengi wame kaa kwa pea kuzunguka meza zao, zilizopambwa na vinywaji mbali mbali, meza moja wapo walikuwa wamekaa Denis na Jackline, wakiburudika kama Jackline alivyo mwomba Denis amlete mahali hapa, “nimepapenda sana hapa”aliongea Jackline, huku akitazama upande wa Cosovo, ambako wageni waalikwa toka serikalini na sehemu mbali mbali walikuwa wanaingia, na sasa alionekana mkuu wamkoa akishuka toka kwenye gari lake, wakati huo huo akayashuhudia magari mawili yanayo fanana yakiingia maali pale, Jackline akayatazama kwa umakini, akayaona yakisimama, kwa pamoja alafu kwa haraka sana, vijana watatu wakashuka toka kwenye gari la nyuma na kulizunguka gari la mbele, ambalo nalo milango ika funguliwa akashuka mzee mmoja wa makamo, sambamba na waschana wawili warembo sana, akaungana na mkuu wa mkoa, kisha wakaelekea ndani, huku wale vijana wakiwa wamebeba brief case, mikononi mwao, “ndio wanakuja huko ndani, hapa nje salama kabisa, akuna dalili ya uovu” Jackline alistuliwa na sauti iliyo penya masikioni mwake, akainua macho yake na kumtazama kijana mmoja alie valia kikawaida tu! akiongea na simu, “ndio kaka tupo makini, na nina kuakikishia hakuna litakalo tokea kabisa” japo sauti ya music ilikuwa kubwa sana, lakini aliweza kumsikia vizuri yule kijana, ambae alikata samu na kwenda kukaa kwenye meza moja ambayo ilikuwa na kijana mwingine amekaa, Jackline akatoa simu yake na kuandika ujumbe haraka sana, ** mzee Nyati alikuwa ndani ya ukumbi huu wa cosovo, amekaa jirani na mke wake, atua chache toka meza kuu ya wageni lasmi, safu ya pili, upande wa watu wasio na ulemavu, akiwa anaonekana kupendeza sana kwa suti aliyo ivaa, huku make wake akivalia gauni la kitenge na kilemba kikubwa cha kitenge, kichwani mwake, huku kinngine kkiwa kimefungwa kwa chini, yani kuanzia kiunoni, wakiwa wanakunywa soda na maji, ambazo kila mmoja alieingia ndani ya ukumbi huu, alikuwa amepewa, akaitazama simu yake iliyoonyesha kuwa kuna ujumbe umeingia, kweli kulikuwa na ujumbe toka kwa mwanae Jackline, ‘kuwa makini, kuna polisi wengi sana huku nje, wamevalia kiraia’ baada ya kuusoma ujumbe huo, mzee Nyati ambae sasa alikuwa anasikia sauti ya mshereheshaji (MC) akitangaza kuwa watu wasimame kwa ajili ya kumkaribisha mkuu wa mkoa, hapo mzee Nyati akainua brif case yake na kumkabidhi mke wake, huku wanasimama, kisha yeye akarudisha ujumbe kwa mwane Jackline, ‘usiwe na wasi wasi, nilijuwa lazima watakuwepo’ dakika chache baadae, akaingia mkuu wa mkoa akiongozana na mzee Alex, huku wakisindikizwa na sauti kubwa ya music, wakaende moja kwa moja, adi kwenye meza kubwa iliyokuwa mbele ya ukumbi ule mkubwa sana, ikipambwa na vinywaji mbali mbali ksoro pombe, hapo mzee Nyati akajikuta akitabasamu kwa hasira, “Alex, zamu yako” alinong’ona mzee Nyati, ambae sasa alisikia sauti ya MC akiwaomba wake kwaajili ya kuendelea na ratiba, hapo mzee Nyati akamnongoneza mke wake, “subiri kidogo, ratiba ya kutoa msaada” ** kati ya watu waliokuwepo ndani ya ukimbi huo, ni kijana insp Johnson David Masinde, alikuwa amekaa safu ya nyuma kabisa, ya watu wasio na ulemavu, muda wote alikuwa ana angaza macho huku na huko, akiwatazama sana wanawake walio kuwepo ndani ya ukumbi ule, kutazama kama kunakitu chochote kitakacho mpa ishara ya kumtambua muuwaji, ambae alijitaidi sana kuikalili sura yake, wakati huo huo, akiendelea kuwasiliana na askari wake, ambao walikuwa wamezagaa nje, na wachache wakiwemo ndani ya ukumbi huo, ** mda ulizidi kusogea, taflija iliendelea, baada ya hotuba fupi iliyo jaa majigambo, ya mzee Alex, ilifwata hotuba ya mkuu wamkoa, ambae alimwaga sifa nyingi sana, kwa mzee Alex, akimsfia kwa kitendo cha upendo na kujitolea alicho kifanya, cha kujitolea kwa kusaidia jamii ya walemavu, mkuu wamkoa aliendelea kuongea kwa kutoa ahadi ya kumuunga mkono bwa Alex, kwa kumtambua kama mfanya biashara anaejitoa kwajamii, wakati hotuba ya mkuu wamkoa ikiendelea mzee Soud Hassan, mzee ambae alikuwa amekaa safu ya pili na mke wake, safu aliyo kaa mzee Nyati na mke wake, wakiipisha upande, wakati mzee Sou akiwa kushoto mwisho, mzee Nyati alikuwa kati kati kabisa ya safu hii yenye watu selathini, alistuliwa na mke wake, “napenda sana kuvaa vile, lakini kinacho nishinda ni kufunga kilemba, mtindo hule” hapo mzee Soud akatazama kule aliko uwa ametazama mke wake, akamwona mama mmoja ambae nivigumu kumwita mzee, pia isinge wezekana kumwita kijana, akitembea taratibu akikatiza kwenye safu ya mbele, akimfwata mshereheshaji, moja kwa moja na kumnong’oneza jambo flani, kisha akasimama pale pale akimsubiri yule MC ambae alienda kwa mzee Alex alie kuwa amekaa jirani na bwana Mwijage, na kumnong’oneza jambo flani, wakaonekaa kuongea jambo kisha MC akarudi kwa yule mama, na kumnong’oneza jambo wakaonekana kukubaliana jambo lililo mpendeza yule mama, ambae alirudi kwenye meza yake, tukio hilo lilimvutia sana Soud maana Sura ya mama huyu aikuwa ngeni kwake, akukumbuka aliwai kumwona wapi, tuio lile alikumvutia mzee Soud peke yake, pia ata insp Johnson alistushwa kidogo na kuonekana yule mama aienda pale mbele, lakini mwonekano wa yule mama na binti ambae alishawai kukutana nae, uso kwauso, napia anapicha yake ambayo kwasasa ilisha chakaa kidogo, akuendandana na huyu mama kwa umbo, kwaupande wa mzee Soud alipata jibu baada ya dakika chache mbele pale hotuba ya mkuu wamkoa, kikafwatia tangazo toka kwa MC, “wageni wote waalikwa, kuna tukio lakusisimua hapa lina fwata” alisikika MC, “ni tukio la kutoa misaada kwa wenzetu, lakini kabla ya tukio hilo, kuna mdau mmoja mama yetu mpendwa Aneth, yeye na familia yake, ameguswa na tkio hili” hapo ukumbi mzima ukatega sikio kusikia anachotaka kusema MC, “mama Aneth, akiongozana na mume wake wanakuja kutoa kisi cha fedha taslimu, million moja” hapo ukumbi wote ukalipuka kwa shangwe, samba mba na muziki toka kwa DJ, huku macho ya watu wote mle ndani ya ukumbi, wakielekezwa kwa watu wawili, waliosimama na kuelekea mbele ya ukumbi, huku watu walikuwa kwenye meza hiyo, wakisimama kuwa pokea, mzee Soud aliduwaa sana, baada ya kumwona mume wa yule mama, “kimenuka” alinong’ona mzee Soud, baada ya kumtambua Michael Nyati, akiongozana na mke wake kuelekea mbele ya ukumbi walipo kuwa wakina Alex na Mwijage, mzee SOUD aliona msngao wa wazi kabisa usoni kwa Alex na Mwijage, baada ya bwana Michael Nyati na mke wake, kuifikia meza ile ya wagen lasmi, tofauti na mzee Nyati ambae alikuwa ametawaliwa na tabasamu, huku yeye na mke wake wakiwapa mikono ya salamu wazee wale, ambao awakuyaamini macho yao, kwa kumwona Nyati mbele yao, ambae aliwapa mkono mtu mmoja baada ya mwngine kisha kukabidhi kitta cha shilingi million moja kwa mkuu wa mkoa, ikiwa ni mchango wake wa walemavu, kisha wakaelekea kukaa pale walip kuwa wame kaa mwanzo, hapo mzee Soud akabaki ameganda kama sanamu, “wewe vipi, unawafahamu awa watu?, mbona umewashangaa sana?” aliuliza mke wa mzee Soud, kwa sauti ya chini kidogo, zaidi ya kuwafahamu ile safari ya Songea, nilienda kwa huyo bwana” aliongea mzee Soud huku akionekana kuchanganyikiwa, maana alijuwa kuwa bwana Nyati, akwenda pale bule bule, lazima kuna jambo ilinaenda kutokea, wakati mzee Soud anaendelea kuwaza lakufanya, mala akamwona mzee Alex akitoka na kwenda chooni, akisindikizwa na walinzi wake vijana watatu, huku aiacha utaratibu wa kugawa misaada ukianza kwa walemavu, kupanga mstari mmoja, na wengine wasio weza kutembea, wakisindikizwa na wasaidizi wao, na mgawaji akiw ni mkuu wa mkoa, dakika chache baadae Alex akarudi toka chooni akiongozana na walinzi wake, akaa sehemu aliyo kaa sehemu yake, sasa ilisha timia saa tatu kasoro, Jackline alikuwa yupo Mwenge pub na mume wake Denis, leo Jackline aliona mda unachelewa sana, kiasi cha kuanza kumsumbua baba yake kwa sms, za kuulizia kinachoendelea huko ndani, na hii ilitokana na maumivu ya tumbo aliyoanza kuyasikia ghafla, ‘baada ya dakika ishirini anza kuingia ndani’ lilikuwa jibu la baba yake, hapo Jackline, ambae alikuwa ansikia maumivu, ali tulia kwa muda huo alio ambaiwa na baba yake, na ilivyo timia saa tatu na dakika tano, akamtazama mume wake Denis, “Ngoja niende kutafuta dawa ya maumivu, nakuja sasa hivi” aliongea Jackline huku akiinuka, “hapana Jack, wacha nikakutafutie mimi, kwani vipi unajisikia maumivu?” alisema Denis huku akimzuwia Jackline asiinuke, “usijali mume wangu, wacha nitembee kidogo, maana nimekaa sana, mpaka mgongo unaniuma” hapo Denis hakuwa na neno, akamluhusu mke wake aende akanunue hizo dawa, Jackline ambae aliacha pochi yake mezani , akaichukua shilingi elfu moja, na simu yake, kisha akaondoka zake, akiwa ana kitu chochote mkononi, zaidi ya hilo buku, na simu, kabla ajafika mbali akapokea ujumbe toka kwa baba yake, ‘unadakika kumi tu, lazima uwe chooni’ hapo Jackline akujibu chochote, zaidi aliendelea kutembea huku maumivu, ya tumbo yakizidi kuongezeka kila dakika, Jackline Michael Nyati akitumia akili nyingi sana alimkwepa mume wake na kuingia kwenye jengo la cosovo Hotel, akikaguliwa mlangoni kama alikuwa na silaha yoyote, baada ya walinzi kujilizisha kuwa mwanamke huy akuwa na kit chochote cha kudhuru, akaachiwa aingie dani, hapo bila kuchelewa Jackline akaingia kwenye lifti, na kubonyeza namba mbili, lifti ikajifunga na kuanza kupanda juu, mda mfupi alikuwa amesha fika gholofa la pili, ambalo lilitawaliwa na shamla shamla za taflija, yeye akaelekea kwenye vyoo, huku tumbo likizidi kumuuma , maeneo ya chini ya kutofu, na kubana mpaka kwenye kiuno, Jackline Nyati alielekea kwenye mlango wa choo alichoingia jana usiku, bahati nzuri akikuwa na mtu, Jackline akafunua kifuniko cha tank la maji ya kufalashia choo, akakuta kile kimfuko alicho kibandika bado kipo vile vile, kama livyo kiacha jana, akakipachua pale kwenye kifuniko, akaufungua ule mfuko na kutoa bastora, aina ya mic gurlily moder 99, toka England, yenye uzingo wa mm 5.5 , akaingiza tena mkono kwenye ule mfuko, akatoa vimkebe viwili vya risasi, akainua gauni lake na kukipachika komja kwenye chupi yake, pia ile nyingine akaiweka kwenye bastora hiyo, kisha akaingiza tena mkono kwanye mfuko ule na kutoa kiwambo cha kuzuwia sauti, akakifunga kwenye ile bastora, hapo Jackile ambae maumivu ya tumbo yalizidi umbana, na kuhisi mkojo una muuma, akachukuwa simu yake, na kumpigia baba yake, itaendelea…..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!