
SEHEMU YA AROBAINI NA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA NNE: akaingiza tena mkono kwenye ule mfuko, akatoa vimkebe viwili vya risasi, akainua gauni lake na kukipachika komja kwenye chupi yake, pia ile nyingine akaiweka kwenye bastora hiyo, kisha akaingiza tena mkono kwanye mfuko ule na kutoa kiwambo cha kuzuwia sauti, akakifunga kwenye ile bastora, hapo Jackile ambae maumivu ya tumbo yalizidi kubana, na kuhisi mkojo una muuma, akachukuwa simu yake, na kumpigia baba yake, endelea ….
aikuchukuwa mda mrefu simu ika pokelewa, “kaa tayari na mwona anainuka, atakuwa anakuja chooni,” Jackline aliisikia sauti ya baba yake, “sawa baba, ila tumbo lina niuma sana, pengine uchungu ndio umeanza” aliongea Jackline kwa sauti iliyoonyesha kuwa kweli anasikia maumivu, “ok! huyo bwege anakuja fanya kazi, tuwai hospital” baada ya hapo simu ikakatwa, Jackline akaiweka simu ndani ya chhupi yake kama alivyofanya kwenye magazine, (vikebe vya risasi), kisha aka ikock ile bastora, na kuiviligia kwenye mfuko aliokuwa ameifazia silaha hiyo tokea jana, kisha akatoka mle chooni, na kwenda kusimama kwenye mlango mkubwa wa kutokea nje kabisa ya choo cha wanaume, ambao ulikuwa wazi bila kuwajari wanawake wenzie, wachache walio kuwa mle ndani ya choo wakimaliza haja zao, na wengine wakiingia nakutoka, mala akwaona watatu wanne wakiingia upande wa vyoo vya kiume, wakionekana vijana watatu wanao mlinda boss wao, ambao waliwazuwia na kuwaondoa watu wengine kwenye vile vyoo, “hakuna kuingia humu ndani choo, mpaka mheshimiwa atakapo toka” Jackline akatabasamu, tabasamu lililo tawaliwa na maumivu ya tumbo na kiuno, akijuwa kuwa windo lake tayari lipo ndani, hapo Jackline alishuhudia mlinzi mmoja kati ya wale watatu, akigeuza kibao cha open na kusomeka out of oder, kwamba akitumiki kwa mda ule, kisha akaingia ndani ya choo, kujunga na wenzake, kumlinda boss, hapo Jackline akatabasamu tena, huku akihisi maumivu yakiongezeka, kila dakika, ** huku ndani nako, akiwa amesha anza kuamini kuwa hali ilikuwa salama, ndani ya ukumbi hule, insp Johnson, alitulia huku akitazama shughuli za utoaji wa misaada, pia kijana huyu aliendelea kuwasiliana na askari wake, walio mwakikishia kuwa akukuwa na dalili yoyote ya uvunjifu wa amani , pia wakina busungu ambao walimweleza kuwa bado wana mwoji mzee Masinde, ambapo yeye aliaminikuwa kwamuda ule asinge weza tena kuja kwenye Tafija, akawaambia kuwa kwa sasa wanaweza kumwacha, na ndio wakati insp Johnson alipo mwona mzee Alex, akiinuka kwa mala ya pili kuelekea chooni, lakini hakujali akaendelea kutazama ugawaji wa misaada, japo baada ya dakika chahe akamwona yule mzee alie toa shilingi million moja akiongozana na mume wake, wakielekea kule alikoelekea mzww Alex, nadio upande ambao kuna mlano mkubwa wakutokea nje ya ukumbi, akujali sana, maana watu wengi walisha anza kutoka ukumbini, lakini baada ya dakika kama tano hivi, insp Johnson akasikia sauti ya mlio toka kwenye simu yake, ikiashilia kuingia kwa ujumbe mfupi, kwenye simu yake, akaitoa mfukoni na kufungua ujumbe, ulikuwa unatoka kwa mzee Soud, ‘upowapi kijana?’ hapo Johnson, akastuka kidogo, “vipi tena? huyu mzee atakuwa na jambo jipya?” aliwaza Johnson huku ana jibu ujumbe na kuutuma kwa mzee Soud, ‘nipo cosovor kwenye taflija, vipi kuna jipya?’ hapo aikuchukuwa mda mrefu ujumbe wake ukajibiwa, fanya haraka mfwatilie mzee Alex chooni, nimemwona Nyati, anamfwatilia kwa nyuma’ hapo insp Johnson akainuka haraka sana na kuanza kukimbia haraka sana, akiwakosa kosa watu waliozagaa ndani ya ukumbi, huku akibinyeza namba flani kwenye simu, “nifwateni haraka sana, huku chooni” aliongea Johnson, baada tu ya simu kupokelewa, baada ya hapo wakaonekana vijana watatu, wakiinuka kwenye viti vyao na kumkimbilia insp Johnson, ambae sasa alisha fika karibu na mlango wakuingilia vyooni, ambao ulikuwa wazi, wakaingia mala moja, na kusimama kwenye kolido la sehemu hiyo ya vyoo, apakuwa na dalili yoote ya kutokea tukio, ambapo mlango wa upande wakike, ulikuwa wazi, na wanawake wakiingia na kutoka chooni, ila ule mlango wa wanaume, ulikuwa na kibao cha out of oder, insp Johnson aka jaribu kufungua mlango wa choo cha wanaume, ukafunguka, wakaingia ndani, naam Insp Johnson na askari wake, macho yao yakashuhudia miili ya watu wanne, ikiwa emelala sakafuni pasipo kujali hali ya sakafu yenyewe, ambayo kwa sasa ilikuwa imetapakaa damu, iliyo tokea kwenyematundu madogo vichwani mwa watu hawa, “hapana, tuelekee chini haraka sana” aliongea insp Johnson huku akitimua mbio kuifwata lift, akifwatiwa na askari wake, huku akipiga simu kwa askari wake waliopo nje ya jengo hilo la cosovo, “akikisheni atoki mtu yoyote eneo hili, pigiananeni simu, waambieni askari wote wakusanyike hapa haraka” aliongea insp Johnson, wakati wanaisubilia lift ifunguke, ** kumbe basi, dakika tano zilizo pita, Jackline Michael Nyati, akiwa ame banwa na maumivu ya tumbo na kiuno, alifungua haraka sana malango wa choo cha wanaume, na kuurudisha haraka sana, kitendo ambacho akikutegemewa na walinzi wa bwana Alex, ambao walikuwa wana msubiria boss wao aliesimama mbele ya sink la haja ndogo, akikojoa mkojo mrefu, ikiwa ni mala ya pili, ndani ya dakika ishilini, kitu ambacho awakukijuwa ni kwamba, wakati ule bwana Nyati anawasalimia kwa kuwashika mikono pale mbele, ndio mda ambao alitumia kuweka unga mweupe ndani ya kinywaji cha bwana Alex, unga huo ni wa tunda la libonga, (sijuwi kwakiswahili wanaitaje) akichanganya na unga wambegu ya msuku dume, ambayo utumika kama dawa ya pressure ya kupanda, na tabia yake uwa ina kusababishia ukojoe mala kwamala, wakati pressure inashuka, “we Malaya umefwata ni….” Jackline akusubiri yule mlinzi mmoja amalizie kauli yake chafu, alichomoa bastora yake toka kwenye ule mfuko alio uviligia, kisha akainua bastora, na kuwaelekezea, huku akiachia risasi moja kwa mtu mmoja, mpaka anafika nne tayari wote walikuwa wameenda chini, hapo Jackline aka fungua kiwamba sauti cha bastora yake na kuiviligia kwenye mfuko ule ule kisha, akatoka nje ya choo, huku maumivu yakizidi kumbana kisawasawa, kiasi cha kuanza kujishikilia umboni, maeneo ya chini ya kitofu, lakini sasa, ile anatoka tu! akahisi miguu igoma kwenda, kama nyonga imekataa kuruhusu mguu kusogea, wakati huo huo akahis kunamtu anamfwata akachoma bastora yake ilikumtafuna risasi lakini akastuka bastora ikidakwa haraka sana kisha akashikwa mkono kwa nguvu, “tulia mwanangu tuwai hospital” hapo Jackline akainua uso wake kumtazama baba yake usoni, nandipo alipo mwona mama yake pia, ambao walimsaidia Jackline kuingia kwenye lifti na kushukanae chini, wakwa wame mshika huku na huku,“tafadhali janai tupisheni tuna mgonjwa mjamzito” aliongea mama Jackline, kwa sauti ya juu, akiwaambia watu waliokuwa wame tanda mlangoni wakielekea nje, ata walinzi wa mlangoni, sasa walikuwa wame kaa pembeni wakiwapihs awatu wanao toka., maana waliamini kuwa taflija inaelekea ukingoni, ni baada yakuonekana watu wengi wana ondoka zao, nao waka pita bila matatizo yoyote nakuingia kwenye gari la mzee Nyati, Toyota V8, safari ya hospital ikaanza, ** walipo fika pale nje insp na askari wake, wakatanda eneo lote na kuzuwia sehemu zote za kutokea, wakiamini lazima wata mkamata yule mzee alietoa million moja, huku akiwatuma askari watatu waende kule juu waka zuwie watu wasiingie chooni na yeye wemwenyewe insp Johnson akaelekea ukumbini kuwajulisha wakina mkuu wa mkoa na mzee Mwijage, juu ya kifo cha mzee Alex na walinzi wake, ** upande mwingine wa bar ya Mwenge pab, Denis alikaa sanapale akimsubiri mke wake, lakini ikapita nusu saa, bila kumwona Jackline mwanzo akupata wasi wasi, lakini aliingiwa na wasi wasi baada ya dakikatano mbele, alipoona magari ya polisi yakiingia kwa fujo eneo la jirani na pale, yani Cosovo hotel hapo ndipo alipo mkumbuka mke wake, Denis aka chukuwa simu yake na kumpigia mke wake, simmu iliita kidogo, ikapokelewa, “hupo wapi wewe? kumechafuka huku wai tuondoke” aliongea Denis baada ya simu yake kuokelewa, “samahani kaka, huyu dada mwenye hii simu ninani wako?” Denis alikutana na swali, lililo ulizwa na mwanamke mwenye rafudhi ya kicongo kwambali, “ni mke wangu, kwani kuna nini kimetokea?” aliuliza Denis kwa sauti ya mstuko, huku akisimama toka kwenye kiti, “usi stuke kaka, mkeo ameshikwa na uchungu tume msaidia kumkimbiza hospital ya muhimbili” hapo Denis aka onekana akishangaa wazi wazi, huku akichomoka pale mwenge pub, kama chizi akiingia kwenye gari lake na kuondoka kwa mwendo wa speed ya hajabu sana, akishika uelekeo wa morocco, ** “jikaze mama mume wako yupo njiani anakuja” aliongea mama Jack huku akisaidiana na mume wake kumshusha Jackline kwenye gari, ni baada ya kuwa wamesha fika muhimbili hospital, huku Jackline mwenyewe akiendelea kulalamika maumivu ya uchungu, yaliyoongezeka kila dakika, bahati ilikuwa upane wao, maana walipokelewa vizuri na muuguzi wa zamu kishan akapelekwa kwa mkunga wazamu, katika chumba cha kujifunguliwa, baba yake na mama yake wakibak nje ya jengo hilo, “jackline anamoyo wakikatili sana huyu mtoto” alipngea baba Jack, “wewe sindio ulikuwa unataka awe hivyo, ila amenifurahisha sana alikoifadhi simu na zile risasi” aliongea mama Jackline wote wakacheka, na mda huo huo wakaliona gari la Denis lina ingia kwa fujo, nakusimama mbele ya jengo lile walilo kuwepo wao, wakamwona akishuka na kusogea walipo kuwepo wao, huku anatoa simu yake n kupiga, mala mama Jack akaona simu ya Jackline, iliyo kuwa mikononi mwa mama Jackline, ikianza kuita, Denis akaonekana kuutambua mlio wa simu ya mke wake, akamtazama mama Jack, itaendelea …….
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU