BINTI MDUNGUAJI (47)

SEHEMU YA AROBAINI NA SABA

ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA SITA: Jackline ambae alikuwa ameilaza mikono yake iliyo fungwa kwa pingu za minyololo mapajani kwa Denis, akiendela kumwelezea kuwa yeye ni muuwaji na kwanini alifanya hivyo, alitulia kidogo na kumtazama Denis usoni, maana alimwona kama alikuwa anajambo alilotaka kuuliza, “ndio maana huyu mzee alilipia hile ward ya VIP, nayule ness ambae tulisikia amekutwa bafuni amekufa, je ulimuuwa pia?” aliuliza Denis, ambae mpaka hapo alisha anza kumwogopa mke wake, ENDELEA ……
“Ndio nilimuuwa mimi, tena siyo peke yake, alikuwa na watu wengine wawili, nazani unakumbuka alichowafanyia usiku pale mlipo luhusiwa kuja kuniona ndani” aliuliza Jackline akimtazama Denis usoni, nakugundua kuwa, mume wake huyo alikuwa na wasi wasi sana juu yake, “ndio alitudai lushwa, nazani ata wewe ulimsikia” aliongea Denis ambae licha y kuujuwa ukweli kuhusu mke wake kuwa muuaji, lakini alikubari kuwa mke wake aliuwa kwa sababu, “ndio nilisikia kila kitu, sasa kama hilo alitoshi, alitaka ufanya kitu ambacho, kama ange fanikiwa nisinge sahau katika maisha yangu” aliongea Jackline huku anatabasamu, “alifanya nini tena?” aliuliza Denis kwa shahuku, “mume wangu kuwa mpole nikusimulie” ** baada ya wakina Denis na wazazi wa Jackline, kumpatia shilingi elfu kumi, yule nesi alie wazuwia mlangoni, akawa luhusu kuingia ndani ya chumba cha VIP, alicho kuwemo Jackline na mwanae, ambacho kipo kwenye gholofa ya pili, na yule nesi alie waleta akaondoka zake, wakati huo huo akaingia kijana mmoja alie valia koti jeupe, ni doctor, akasimama nje ya chumba kile akiongea jambo na yule nesi alie chukuwa elfu kumi kwa kina Denis, “Denis mme wangu, tume pata mtoto wa kiume, aliongea Jackline akimkumbatia Denis, ambae alionekana kuwa nafuraha kubwa sana, “tuta mwita Fransis, jina la babu yako, pia huyu mzee aliekusaidia na yeye anaitwa ameomba tumwite jina hilo, hapo Jackline akamtazama baba yake, macho yao yaka gongana, mzee Nyati akafinya jicho, “nashukuru sana mume wangu, kwa kunipa kipambele” Jackline pia aliwashukuru wale wazee wawili mtu na mke wake kwa kutumia mdawao kumsaidia, huku moyoni alishukuru uwepo wa wazazi wake katika eneo la tukio, na kumshuhudia mjukuu wao, pasipo Denis kujuwa lolote, juu ya wazee wale, wakati wanaendelea kuongea, Jackline aliweza kuwaona nesi mkorofi na yule doctor, wakisistizana jambo flani huku yule docor wakiume akisistiza mda kwa kuonyesha ishara ya kugusa kwakidole chake, karibu na nyuma ya kiganja chake, kisha yule doctor akaondoka na yule nesi akaingia mle chumbani, “haya jamani mda ume waishia naomba muondoke mama apumzike” aliongea yule mama ambae auwa na sura ya kirafiki na ukarimu, “haya dada nesi tunaondoka zetu, wacha tuagane na mgonjwa” aliongea Denis akionyesha kuwa anahamu ya kuendelea kuongea na mke wake, ila kwa upande wa Jackline akaona kuna ishara ya kuwa na hatari mahali pale, baada ya kuagana na wakina Denis, Jackline akaongea kwa lugha moja ya kificho, “sijuwi kama nitalala vizuri, yaningekuwa na moder 99, ningelala vizuri sana,” “ndio kinywaji gani hicho mke wangu?” aliuliza kwa mshangao Denis, pasipo kujuwa kuwa alie ambaiwa amesha elewa, “hahaha mumewangu kwa vinywaji, siyo kinywaji ni mafuta yay a dawa ya mbu” hapo wote wakacheka sana, kisha wakatoka nje ya chumba huku mama Jackline akiipenyeza bastora kwenye shuka, pamoja na kikasha cha risasi na kiwambo cha kuzuwia sauti, pasipo Denis na yule nesi kuona, wakina Denis waliondoka zao, huku akimwachia simu yake na Jackline akimsisitiza kesho kuwai asubuhi pamoja na chai au uji, na kumwacha yule nesi akiwa amesimama nje ya chumba, kile alichokuwepo Jackline na mwane, Jackline aliiweka vizuri Bastora yake, huku anaendelea kumtazama yule nesi, ambae sasa likuwa ameshika simu yake, akabonyeza ndamba kadhaa kisha akaiweka sikioni, akutimia ata sekunde tano, yule nesi akaongea neo moja tu , “tayari” kisha akakata simu na kuingia kwenye chumba alicho kuwepo Jackline, safari hii aionekana mwenye tabasamu, japo lilikuwa la kulazimisha, “samahani dada japo chumba chako ni VIP, lakini kuna mzazi mwingine analetwa na Doctor, ametoka kujifungua, tunaomba apumzike kidogo hapa, wakati tuna mtafutia kitanda” aliongea yule nesi ambae alionyesha dalili zote za mashaka mashaka, “ok! hakuna tatizo si kwamda tu, maana kitanda chenyewe ni kidogo,” aliongea Jackline huku akizidi kumsoma huyu Nesi, “kitanda siyo tatizo maana mta kaapembeni kidogo watoto mta walaza kitandani, nazani aita dhukuwa nusu saa, kabla ajahama” aliongea yulenesi kisha akatoka nje, hapo Jackline akaichukuwa bastora yake na kupakia kimkebe cha risasi, kisha aka funga bomba la kuzuwia sauti, akaiweka chini ya dogoro, baada ya hapo haraka sana aka nyofoa kiuzi kwenye shuka la hospital na kumfunga mwanae kwenye kidole kimoja cha mguu wa kushoto, ile ana mfunika vizuri mwane alie kuwa amepitiwa na usingizi, akaingia yule nesi, akiwa amebeba kitoto kilicho funikwa mwili mzima, kwa ngu zilizo fanana na zile alizo funikwa france mtoto wa Jackline, akiongozana na binti mmoja alijitanda kanga mwili mzima, “karibu na hongera sana” alisema Jackline huku akiwa meachia tabasamu languvu sana, “asante sana dada” aliongea yule dada, akiachia tabasamu, lakini lilioneka ni la kulazimisha, lililo jaa wasi wasi, yule nesi alimlaza yule mtoto, aliie ingia nae pembeni ya mtoto wa Jackline, kitanda kikipatikana, atakuja doctor kukuchukuwa” aliongea yule nesi na kutoka nje, akiwaacha Jackline na yule dada mwingine wakianza kupiga story, huku watoto wao wakiwa wamelala, Jackline mda wote wamaongezi yao, alijaraibu mkumtazama kwaumakini sana huyu dada ambae aligunduwa kuwa ndani ya kanga chini alivaa suluali ya jinsi, “mh! mzazi jinsi” aliwaza Jackline huku anamtazama yule dada, kisha akamtazama mtoto alikuwa ametulia kimya, huku akaviligishiwa nguo mwilimzima kisi cha kuto kuonekana sura, “eti dada mbona ume mfunika sana huyu mtoto, si atakosa hewa?” aliuliza Jackline, na yule dada akaanza kujiumauma kujibu, lakini hapo hapo akaingia yule nesi, akiwa ameshiaka file mkononi mwake, “Jackline Michael, ndio nani kati yenu?” aliuliza yule nesi akisoma kwenye lile file, “ni mimi hapa” aliitikia Jackline, “ok nifwate” aliongea yule nesi na kuanza kutoka nje, jackline akainuka na kutaka kumbeba mwane, “mwache mtoto apumzike” alisema yule nesi ambae alisha kuwa ametoka nje ya kile chumba na kusimama nje ya mlango, Jackline akamwacha mwane na kumfwata nesi, ambae alielekea moja kwamoja mpaka kwenye meza moja kubwa sana nje y ail;e ward aliyo kuwepo Jackline, wakiwa wanakaribia ile meza wakapisha na yule doctor wakiume, alie onekana mida ile wakina mzee Nyati wakiwa kwenye chumba alichokuwa amelazwa, yule doctor aliwapita kidogo kisha akasimama, “samahani Nesi, naenda kumwamisha yule mzazi, maana tayari tumesha pata kitanda kingine,” aliongea yule doctor, kwa sauti ya unyenyekevu, “swa fanya haraka maana chumba chenyewe tume dandia tu!” aliongea yule nesi, na kumshangaza sana Jackline, kwani yeye anajuwa anae paswa kutumwa ni huyu nesi, na sie yule doctor ambae anaonekana kuto kufahamu nafasi yake yakazi, Jackline akamwona yule Doctor akielekea kule walikotokea wao, lakini akujari sana, akaendelea kumfwata nesi, ambae alienda na kusimama wenye ile meza, inayo tumika kama ofisi katika ile ward, kisha yule nesi akaonekana kufanya jambo flani la makusudi, lakumchelewesha Jackline, maana alianza kushughulisha kwa kupekua mallla huku mala huku, akitumia dakika kumi nzima, mala ikasikika sms kiingia kwenye simu ya nesi, ambae aliusoma ule ujumbe, kisha akamtazama Jackline, “haya dada weka hapa sahihi yako” aliongea yule nesi, akimwonyesha sehemu ya kuweka sahihi, kwenye form moja iliyopokwenye lile file alilokuwa nalo mkononi, alipokuja kumchukuwa Jackline ule chumbani, hapo Jackline akajuwa kuna namna, kwanini asinge mpa awe sahihi kule chumbani, Jackline aliwaza huku anaweka sahihi haraka haraka, kisha akamrudishia peni yake Nesi, “umesha maliza wai ukamtazame mwanao, yupo peke yake” aliongea yule nesi, akijifanya yupo busy na shughuli zake, hapo Jackline akatembea haraka haraka, kuwai chumbani kwake, alipoingia mle ndani ya chumba, Jackline akakutana na mambo tofauti na alivyo yaacha, kwanza kabisa akumkuta yule dada na mwane, pili alikuta mwae ame funikwa mwili mzima tofauti na walivyokuwa amemfunika yeye, akawai na kumfunua yule mtoto, kwanza aikutana na arufu flani kali ya marashi, ambayo akuwai kumpulizia mwanae, akamfunua miguu, akuona ile nyuzi aliyo mfunga kwenye kidole, pia mtoto alikuwa amekakamaa, akionyesha alikuwa amesha fariki mda mrefu uliopita, “mama yangu France kaibiwa” aliongea Jackline, huku akichana shuka na kujifunga kiunoni, mfano wa chupi flani, au kamawalivyo kuwwa wanavaa watu wa zamani, akavaa gauni lake alilikuwa amevaa wakati analetwa hospital, akachukuwa bastora yak echini ya godoro na kuikuki, kisha akaivuligia kwa kipande cha shuka, mwisho akachukuwa simu yake nakutoka nje ya kile chumba, mbio mbio, akaelekea kwenye ile ofisi aliyo mwacha yule nesi, ambae sasa alikuwa anahesabu fungu kubwa la fedha, “wewe unaenda wapi?” aliuliza yule nesi kwa sauti ya kibabeuku akatoka nyuma ya meza kumzuwia, akizani anapitiliza kwenda nje, huk akiziacha zile fedha pamoja na simu mezani, “wala usiwe na wasi wasi, nakuja kwako, nimeibiwa mtoto” aliongea Jackine kwa sauti ambayo usinge zani kuwa anatatizo kama hilo, “weee, unauakika ebu acha kusingizia watu mtoto ulie mkuta kiatandani ndie wakwako” alibwabwaja yule nesi, “dada naongea kwamala ya mwisho, yule doctor na yule dada wapo wapi?” aliongea Jackline safari hii akishindwa kuvumilia na kuonyesha hasira, “we binti unakichaa cha uzazi ngija niwa ite walinzi waku…” aliongea yule nesi huku akichukuwa simu yake toka mezani, alaki akuwai atakumalizia ata maneno yake, kwani alikatinzwa kwa ngumi nzito ya usoni, iliyotuwa katikati yam domo wa yule nesi, na kumrusha nyuma ya meza, kabla yule nesi hajapiga kelele, Jackline akaruja meza na kumuwai yule nesi, ambae alisha juwa kuwa leo ameingia cha kiume, “dada umekosea kuniibia mtoto, aliongea Jackline akiushindilia mguu wake mzima mzima shingoni kwa yule nesi na kubaki amekanyaga hapo hapo, akaichukuwa simu ya yule nesi, ambae alikuwa anaangaika kutafuta pumzi, kutokana na mguu wa Jackline kukita na kushindilia shingoni kwake, Jackline abonyeza simu ya yule nesi akatazama kwenu ukumbi wa sms, akaona iona sms ya mwisho imeandikwa ‘mtoe hapo njiani, sisi tupite’ hapo Jackline akaipiga ile namba, ikaita kidogo tu! na kupokelewa, “ndio tuna tka kwenye jengo ili, vipi kuna ishu?” iliongea sauti ya kiume, hapo Jackline akakata simu, na kumtazama yule nesi, ambae alikuwa anaonyesha ishara ya kuomba samaha, akishindwa kutoa sauti huku macho yame mtoka kweli kweli, “ufai kuishi shetani we” aliongea Jackline na huku akiuinua mguu wake, na kuushusha shingoni kwa yule nesi, nakufwatiwa na mlio wa kuvunjika kwa mti mkavu, ambao ulimfanyanesi yule aanze kutupa tupa miguu kama mtu mwenye ugonjwa wakifafa, huku damu ziki mtoka mdomoni na puani, ulimi na macho yame mtoka, Jackline akaiacha simu ya nesi, na kuondoka maali pale kuelekea chini gholofa ya chini, huku akisikia simu ya nesi ikianza kuita, Jackline wakati anashuka ngazi kwa tahadhari, lile basotra yake aliyo iviligishia shuka ikiwa mkononi, alitazama mlango wa kutokea nje na kuwaona wale watu wawili, yani yule doctor na yule mwanamke wakianza kutembea kuelekea nje kabisa, “washenzi nyie mme kwisha” aliongea Jackline kwa suti ya chini kidogo, itaendelea …….

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata