BINTI MDUNGUAJI (49)

SEHEMU YA AROBAINI NA TISA

ILIPOISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA NANE: tukio jingine ambalo hakuweza kulitambua vizuri, kuna mwanamke mmoja amekimbia na kuacha maiti ya mwanae kitandani, na mbaya zaidi hakuna kumbu kumbu yoyote, iliyo andikwa juu ya mwanake kulazwa chumba hicho ch VIP, pia yule koplo alimkabidhi insp Johnson simu tatu za maremu wote, “ok! naomba vipimo na harama za vidole katika miili ya malehemu” aliongea insp Johnson, ambae alionekana kuchanganyikiwa na tukio hilo ambalo mpaka hapo ni tukio moja, endelea ……
Haraka sana akaitwa mkaguzi wa halama za vidole, ambae aliliport kwa insp Johnson David, akiwa na file mokononi mwake, pamoja na kifuko chenye vichwa kadhaa vya risasi, baada ya kusalimia kijeshi, yule mtaalamu wa ukaguzi wa miili ya malehemu, akaanza kumsomea insp matokeo ya uchunguzi, ambayo yalionyesha kuwa licha ya marehemu hawa wawili yani Amson na Nuru, kuuwawa kwa risasi lakini pia zimekutwa halama za vidole kwenye mwili wa Amson, ni Alama zina zo fanana na zile ambazo zimesha wai kukutwa kwa marehemu Kileo na wengine, “pia afande tumegundua kuwa risasi zilizo tumika ni za siraha aina ya pistor mic gurlily moder 99, toka England, yenye uzingo wa mm 5.5,” hapokwa haraka insp Johnson akavuta kumbu kumbu, juu ya siraha hiyo, ambayo iliingia nchini mwaka 1999, lakini aikuruhusiwa kuuzwa, wala kutumiwa na raia yoyote, akawaida, wala vyombo vya usalama, zaidi ya jeshi la ulinzi , tena kwaajili ya VIP protection, “nandio risasi zilizotumika kwenye tukio la Cosovor Hotel,” mpaka hapo insp alikuwa amesha changanyikiwa, “inawezekanaje?” alijiuliza insp, “inamaana wanausika na huu mkasa?” kiukweli ni maswali yaliyokosa majibu, insp akakumbua kitu, akachukuwa simu ya kwanza ambayo iliwekwa kibadiko cha plast na kuandikwa kijana no 1, ikimaanisha ni Amson, akaingiza namba ya simu ya baba yake, akitegemea ilngetokea jina la baba yake, lakini aikuwa hivyo, akafanya hivyo kwenye simu ya pili, nayo ikawa hivyo hivyo, lakini ya tatu ambayo iliandikwa nesi, ilileta mafanikio kidogo, japo siyo aliyo yategemea, insp alibaada ya kukosa jina la baba yake, akaonelea atazame sehemu za meseji, ni kweli sms yakwanza tu katika simu ya nesi iliandikwa hivi, ‘tayari mtoe tupite’ akatazama mda ilikuwa yapata saa sita za usiku, akaanza kufwatilia sms nyingine, akitazama zilizo tumwa na kupokelewa, aliona sms nyingi zilizo ashilia kuwa kuna mpango ulikuwa unaendelea kati ya nesi na huyo mtu aliekuwa anawasiliana nae, ambae alimsevu kwa jina la, mtoto, maana alikuta sms moja iliyo msisitiza huyo mtu awai hapo hospital, kuwa kuna uwezekano wa kufanikiwa, ndipo insp alipo pata hamu zaidi ya kuipekua ile simu, atimae akaikuta sms iliyo tumwa siku iliyopita, ‘naomba msaada wako kama wakipindi kile, ila safari hii anaitajika mzima kabisa’ kengere ya tahadhari ika gonga kichwani kwa insp akaichukuwa ile namba ya simu iliyo andikwa kwa jina la mtoto, akaiandika kwenye simu yake kisha akaipiga, lakini akashangaa simu moja wapo kati ya alizo zishika ikaanza kuita, akaitazama ni kijana no1, akaikata ya kwake ili apokee kwanza ile, lakini bahati mbaya na ile ikakatika, akaipiga tena, na ile ikaita, hapo insp akatazama namba ya simu iliyo kuwa ina piga kwenye simu a marehemu, akagundua kuwa ni namba yake, kwa hiyo hii namba ni ya simu hii, inamaana aina ubishi kuwa nesi na awa wawili walikuwa na mpango mchafu juu ya kuiba mtoto?” aliongea insp Johnson kisha akamtazama yule dada nesi, ambae alikuwa anatetemeka kwa uoga, “wewe nesi nifwate” aliongea insp huku anainuka na nakutuka nje, akifwatiwa na dada nesi, waliongozana mpaka nje ya jengo, wakasogea pembeni kidogo, sehemu ambayo insp aliiona kuwa ni tulivu, “dada naomba upunguze wasi wasi, nachoitaji ni majibu machache tu ya maswali mepesi nitakayo kuuliza” aliongea insp Johnson na yule nesi akaitikia kwa kichwa akionyesha kuelewa alicho ambiwa na insp Johnson, “unasema uli waona watu wawili wakitoka hapa hospital,” aliuliza imsp Johnson, “ndio niliwaona, tena mala yakwanza yule kijana nilimwona anangea na Nesi” aliongea nesi huyu, huku hali ya uoga bado ime mganda, “je uli mwona dada mjamzito alie letwa usiku?” aliuliza insp akimtazama nesi, kwa umakini kuangalia majibu yake kama ni ya ukweli, “nilimwona na mimi nilishiriki wakati anajifungua” aljibu Nesi, akionyesha kuwa na uakika wa kitu anachoongea, “ok! kuna watu walimleta au alikuja mwenyewe?” aliuliza tena insp akiamini kuwa nesi huyu anampatia majibu ya uakika, ni kweli yule nesi alimweleza jinsi wakina mzee Nyati walivyo mleta, huyo mdada, wakijitambulisha ni wasamalia wema walio mkuta dada huyu anatafuta usafiri wa kujia hospital, na baadae akaja mume wa yule dada, na yeye ndie alie waruhusu waka mwone baada ya kujfungua, ila akika sana akarudi kwenye sehemu yake ya kazi na kumwacha marehemu nesi akiendele kumsimamia ward ile maana ili muusu moja kwamoja, “unaweza kukumbuka hao wasamalia walivaaje” aliuliza insp, hapo yule dada akaonekana kuvuta kumbu kumbu, kisha akaoneka kushindwa kuvuta kumbukumbu sahihi, “kiukweli yule baba kama sikosei, alivalia suti nyeusi, lakini yule mama alivalia nguo iliyotengenezwa kwa kitenge, sina uakika ni kutoka nchi gani, nilivutiwa nacho” aliongea Nesi, huku tayari mda mrefi Insp alikuwa amesha pata jibu, kuwa mzee Nyati ndie aliekuwepo pale Hosptal, usiku ule, na pengine yule mwanae Jackline, ndie aieletwa kujifungua, maana insp alijumlisha na tukio la kuuwawa kwa daktari wa magonjwa ya kina mama, Joseph Ndilane, pia kutokea kwa tukio jingine, siku hiyo hiyo kwenye hospital ya Dr Stellah, ambayo ni maalufu kwa maswala ya uzazi, “ok! Jackline amejifungua, na walitaka kumwibia mtoto, pasipo kumjuwa kuwa ni hatari” aliwaza insp huku anatabasamu, tabasamu lililo fwatiwa na kicheko kikubwa, ** Denis baada ya utoka hospital kwend kupeleka chai na nguo za mke wake, ambazo nyingi zilikuwa ni kanga na vitenge, akaelekea azini kuomba ruksa kwaajili ya kumwangalia na kumhudumia mke wake, alie jifungua, baada ya kupewa mapumziko ya week mbili, Denis akaondoka zake na kwenda kaliakoo, ambakp alifanya manunuzi ya nguo na vifaa vya mtoto, mda wote Denis alionekana kuwa mwenye furaha iliyo pitiliza, Deis akwa kaliakoo akasikia habari ya kutokea kwa mauwaji ya bwana Alex na walinzi wake, pale Cosovor, na pia habari nyingine ni ya kuuwawa nesi jana usiku, hospital ya muhimbili, lakini Denis akaliicukulia kama story ya kawaida ambayo amesha sikia mala nyingi sana, akaendelea na shughuli zake, ** wakati Denis yupo kaliakoo mzee Nyati na mke wake walikuwa Matumaini Hospital, wakijadiliana jambo na mtoto wao, wazo la mama Jackline lilikuwa ni kwamba, Jackline na mwanae France waende Songea, ili mzazi akapate mda wa kupata huduma anzo stahili, kabla ya kulejea kumalizia kazi, ni kweli wakakubarina hivyo, kwamba wakina mzee Nyati waondoke na Jackline, ikapangwa mipango ya jinsi ya kumshawishi Denis akubari swla hilo, ndipo hapo, mzee Nyati alipo piga simu kwa Denis, “hallow baba, hongereni sana, wenzio ametutaalifu kuwa amejifungua salama” aliongea mzee Nyati, kwa namana ile ile ambayo Denis utambua kuwa baba mkwe wake ni mzee fukara wa huko kijijini, “samahani mzee, yani nilitingwa kidogo kuwajulisha, ni kweli amejfungua mtoto wa kiume tume mwita France” aliongea Denis, huku akikumbuka kuwa akuwai kuwajulisha wazee hao juu ya mbinti yao kujifungua, “umemkumbuka babu yenu, safi sana, lakini inabidi huyo ajae haraka sana ili aweze kufanyiwa huduma anazo stahili, maana huko mjini mpo wenyewe tu, alafu ndio mala yake ya kwanza kujifungua” aliongea mzee Nyati, na Denis hakuwa na pingamizi, akapanga kwenda kumjulisha mke wake juu ya safari hiyo muhimu, *** saa sita mchana, insp Johnson aliikuwa njiani anaenda igamboni mji mwema kwa mzee Soud, akiwa na lengo moja tu, kupajuwa nyumbani kwa mzee Nyati, kwa kisingizio cha kwenda kuongea nae, kumbe lengo lake likiwa ni kumvamia na kundi kubwa la askari kisha wammiminie risasi na kumpoteza kabisa, wakidai alijaribu kupambana na polii akiamini ndio utakuwa mwisho wa mauwaji na kwamba baba yake anakuwa ameepuka kifo, wakati anapanga hayo insp Johnson alijuwa fika kuwa lazima atumie hakili nyingi sana kuzunumza na mzee Soud ili akubari kumwelekeza nyumbani kwa mzee Nyati, na kisingizio kikubwa ni kuwa anaenda kuongea nae kutafuta suruhu, itaendelea……..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata