
SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA MOJA: kiukweli mzee Nyati tokea alipo sikia ujio wa vijana awa waliojifanya ni vijana toka mtwara, wanataka kuonana nayeye, “kwa njia wanayo pitia, ni wazi wameelekezwa na mzee Soud, maana na yeye alifikia kwa Felister, kabla ya kuja Nyumbani kwangu, huyu mzee ameshakuwa tatizo kwangu” ENDELEA ……..
Aliwaza mzee Nyati ambae bado alikuwa ndani ya andaki lake la siri, hapo ata mzee Nyati akajilahumu sana, kwa kuto kuwa na namba ya simu ya mzee Soud, “lakini aina shida wacha tuone mwisho wa hadithi, tutajuwa lengo la huu polisi, kama ni kuniona kwa maongezi au anataka vita” aliwaza mzee Nyati, huku akiendelea kupanga vitu vyake, mle ndani ya andaki, ** “unajuwa nini Busungu, kunakitu kina nishangaza sana” insp Johnson alimwambia Pc Busungu, wakati wanashuka toka kwenye gari na kuingia Polosi lest house, iliyopo bombambili, “nini kina kushangaza afande?” aliuliza Busungu wakisimama nje ya mlango wa jengo kubwa la kuingilia kwenye ukuumbi mkubwa wa mess hiyo ya maafisa wa polisi, “kwa jinsi nilivyo mwona yule mzee, siku ile cosovor hotel, nashangaa kuambiwa kuwa anakaa kijijini” insp Johnson alitowa duku duku lake, “uwezi kujuwa insp, pengine tunaweza kukuta amejenga mtaa mzima wa nyumba za kisasa” aliongea Busungu na wte wakacheka kidogo, “poa tuta ona iyo baadae tukifika huku kijijini” alimalizia insp kisha wakaingia ndani ya jengo hilo kubwa, ** mambo yalikuwa moto kwa nzee Nyati na familia yake, walikaa pamoja na kupanga jinsi watakavyo kabiriana na kuficha ukweli juu yao, mbele ya polisi awa kutoka dar es salaam, yalifanyika maandalizi kwenye nyumba ya udongo, ambayo ata Denis alifikia siku aliyo mleta Jackline na mtoto wao, maandalizi yalikuwa ni makubwa sana ya mazingira na usalama wake yeye mwenyewe mzee Nyati na mke wake watakao kuwemo ndani ya Nyumba ya udongo, mpaka saanane mchana wakawa wamesha maliz, na wakawa tayari kwa kuwasubiri wageni mda wowote, wakiwa wamesha jipanga namna ya kuakikisha usalama wa eneo lile na kuakikisha wale polisi awaleti madhara ** askari stini wa jeshi la polisi walikuwa katika mazoezi makari sana, kwenye kambi moja iliyokuwa ya wapigania uhuru, toka kusini mwa afrika, lililopo ndani ya misitu minene, ya mbuka za wanyama za selous, uliopo wilaya ya namtumbo, km sabini toka Songea mjini, askari hao walifanya mzoezi ya aina mbali mbali, ukiachilia mazoezi ya utimamu wa mwili pia askari awa alifundishwa namna ya kuvamia na kushambulia, walifanya mazoezi hayo usiku na mchana, huku wakisubiri report toka kwa insp Johnson, ** saa kumi jioni, insp Johnson na Pc Busungu, walikakatiza misitu na vichaka vinene wakielekea kule waliko elekezwa na mschana mrembo felister, huku Busungu akiendesha gari aina ya Toyota corolla, walilo kodi wakiofia kutumia lile land rover la polisi upelelezi, wakijuwa kuwa itakuwa lahisi kwa mzee Nyati, kustukia kuwa wao ni polisi, “huku kuzuri sana, yani anamalizwa kimya kimya” aliongea Busungu, kisha wote wakacheka kidogo,”ebu simama kidogo, tumwulize huyo kijana” aliongea Insp Johnson, baada ya kumwona kijana mmojamvupi sana, akipasua kuni kwa kutumia shoka, pembezoni ma barabara, “mambo vipi dogo” alisalimia insp Johnson huku, baada ya busungu kusimamisha gari, “safi tu blaza! shikamoo” alisalimia yule kijana kwa sauti ya uchangamfu, kiasi cha wakina Johnson kuwa na uakika kuwa wataelewana nae vizuri, “poa dogo, naona una andaa kuni” aliongea Johnson huku akishuka na kumsogelea yule kijana, wakagongeana mikono, “si unajuwa tena blaza, bila kufanya hivi hakuna msosi” aliongea yule kijana mchangamfu, “ok! poa dogo, mimi naitwa Danny, mwenzangu unaitwa nani, maana tunaweza kukutana tena, huko mbele mbele” aliongea Johnson akidanga’a jina, huku akiigiza sauti na rafudhi ya kiujana, “naitwa Saidi, au ukitaka uni pate kilahisi kule kijijini, ulizia Side tall (mrefu)” kauli hiyo ya Saidi, iliwafanya busungu na Johnson waangue kicheko, “kwa nini wanakuita mrefu wakati wewe ni mfupi sana?” aliuliza Johnson hwakati huo Busungu nae, alikuwa amesha shuka toka kwenye gari na kusogea walipo simama wakina Johnson, Side Tall alicheka kidogo, kisha akaongea “sababu mimi ni mrefu” hapo Johnson na Busungu walicheka sana, kutokana na kijana huyu kuto kujuwa tafsili ya neno tall, lakini Side alitulia akiwatazama kwa mshagao, “ok! ok! bwana tall, naani wewe ni mwenyeji kodogo maeneo haya, vipi kuna kijiji huku mbele chochote huku mbele?” aliuliza Johnson akimalizia kucheka, “kijiji kipo, tena kikubwa tu, ukiachi majumba yay a hao wazungu upande huu wakulia, upande wa kushoto kuna barabara mbili moja ya kwenda mahilo, na nyingine ya kwenda kwa Nyati” alieleza kijana huyu, ungezani ameulizwa mambo hayo yote, “kwani kwa Nyati nacho nikijiji?” safari hii aliuliza Pc Busungu, “siyo kijiji kama kijiji, sema kuna mzee mmoja hivi anameneo makubwaaaa, amejitenga na wanakijiji enzake, amejenga kijumba chake anakaa yeye na mke wake” aliongea kijana huyu akionyesha zalau na lawama, kw mzee huyo mwenye kujitenga, “mzee huyo anaitwa nani?” aliuliza insp Johnson, “si ndio anaitwa mzee Nyati, yani uanajidai huyo mzee utamwona ameulamba mwenyewe, alafu anakaa kwenye nyumba ya hajabu hajabu” hapo wakatazamana kidogo kisha waka tabasamu, “vipi yule mwanae, yule demu mzuri mzuri” aliuliza busungu, “daaah! huyo demu sija mwona siku za hivi karibuni, nazani atakuwa ameolewa mjini” alieleza Side tall, na baada ya maswali ya hapa na pale, wakina Johnson wakaomba waelekezwe njia ya kufika hapo, side nae hakuwa na kinyongo, aliwaelekeza vyema kabisa mpaka nyumba anayopatikana mzee huyu, alie amua kukaa kwenye nyumba yake huko shambani akijitenga na wana kijiji wenzake, “yani mkipita pale pachani nyumba mtakayo ikuta mbele yenu simamisheni gari ulizeni” alimaliza kuelekeza bwana Side tall, “poa bwana Tall, lakini ni bola ujifunze maaa ya neno kabla ya kulikubari” aliongea bwana Johnson, wakati wana muaga side, wakaingia kwenye gari lao, na kuondoka zao, wakimwacha Side tall, akiwasindikiza kwa macho mpaka walipo potea usawa wa macho yake, side akatabasamu kidogo, “mtajuwa kwanini mimi naitwa mrefu, sababu ninaona mbali sana, bwana Danny” aliongea Side huku akichomoa simu yake toka mfukoni mwake, na kubonyeza namba flani flani, kisha akaipiga, sekunde chache akaanza kuongea haraka haraka, “wanakuja wapo wawili, mmoja amejitambulisha kuwa anaitwa Danny” hapo ikasikika sauti ya mzee Nyati, “ok! sawa aina tatizo, endelea kuwa makini” *** baada ya kumwacha kijana mpasua kuni, wakina Johnson walitembea mwendo wa kilomita moanza kuona jumba kubwa sana mbele yao, lakini baada ya mita miatamo mbele zaidi wakaona kuna barabara nyingine inaingia upande wa kushoto, wakaifwata kama walivyo elekezwa na kija asie juwa maana ya neno tall, safari ya polisi awa wawili iliendelea, huku wakiangala mazingila yote waliyo pitana jinsi ya kupanga majeshi yao wakati wa kumvamia bwana Nyati, dakika kumi baadae walisha ingia ndani ya eneo moja kubwa sana, lenye nyumba moja tu! ya udongo, nje ya nyumba hiyo alionekana mama mmoja kiosha vyombo, karibu na mti mmoja sana wenye kimvuli kikubwa sana, pembeni ya nyumba hiyo, upande wa kulia, walipozidi kusogea karibu, ndipo walipo gundua uwepo wa mzee mmoja wa kiume alietulia kwenye kit cha uvivu, chini ya kimvuli cha mti huo, “watakuwa ni mzee Nyati na mke wake” aliongea Johnson, huku uso wake ukionyesha dalili zote za mshangao, “inashangaza kwakweli, yani mtu alie toa million moja kusaidia walemavu, anaishi porini namana hii” aliongea Busungu kwa sauti ya kung’ona, “tena cha udongo, au mzee soud aliwa fananisha?” yalikuwa ni maswali magumu sana toka kichwani mwa Johnson na mwenzie, ambao walisimamisha gari lao kwenye uwanja wa nyumba hiyo ya udongo, “hoooo! karibuni jamani” alikaribisha mke wa mzee Nyati huku akiacha kuosha vyombo, na kunawa mikono yake, kwa maji masafi, toka kwenye ndoo moja ya bati, iliyo chakaa kidogo, kisha akaingia ndani ya ile nyumba ya udongo, “asante mama asante sana” aliesema insp Johnson, aliekuwa amesha shuka toka kwenye gari, akifwatiwa na Busungu, “hoooo! tumepata Baraka za wageni, karibuni sana vijana” aliwakaribisha mzee Nyati, akionyesha uchangamfu huku akikijiweka vizuri kwenye kiti chake cha uvivu, “asante sana mzee wangu naimani ndie mwenyeji wetu mzee Nyati” aliongea insp Johnson akimsogelea mzee Nyati na kumpa mkono wa salamu, huku macho yake yakijaribu ku mtambua mzee huyu, kama ndie yule alie mwona mala ya mwisho kule cosovo hotel, “uja kosea, na hapa ndio nyumbani kwangu, karibuni sana vijana” dakika chache baadae, mke wa mzee Nyati alitoka akiwa na viti viwili vya mbao, karibuni wakina baba” aliongea mama Jackline akiwakabidhi viti wakina Johnson, nao waka shukuru na kupokea vile viti, kisha wakakaa chini ya kimvuli kikubwa kama mzee Nyati mwenyewe, “karibuni vijana inaonyesha mme tokea mbali sana” aliongea mzee Nyati, akiwatazama kwa zamu vijana awa wawili, “nikweli mzee wangu, sijuwi nianzaje, ila kwa kifupi naitwa Jafari, nime tumwa na mzee Mwijage, nazani unamfahamu vizuri” hapo mzee Nyati pasipo kuonyesha mstuko, kama wakina Johnson walivyo tegemea, akajibu kwa kutikisa kichwa, akionyesha kukubari kwamba anamfahamu Mwijage, hapo insp Johnson aliejitambulisha kwa jina la Jaffari, akamweleza zee Nyati kuwa wazee awa waili wame mtuma kuja kuomba suluhu ya tatizo linalo endelea, na kwamba wapo tayari kurekebisha na kumaliza tofauti zao, ili mauwaji ya kome, “walikueleza kunatatizo gani kati yao na mimi?” aliuliza mzee Nyati huku akiwatazama usoni kwa zamu vijana awa, ambao walitazamana kwa sekunde kazaa kisha wakamtazama mzee Nyati, ambae kimtazamo akuwa na sifa ambazo mzee Soud alimweleza, alionekana mtu wa kawaida kabisa, “hapana awa kunieleza” alijibu Johnson, “unafikilia nini kama nikikuambia kuwa sina tatizo na watu hao?” aliuliza mzee Nyati wakati huo mke wake alikuwa anaendelea kuosha vyombo, “utakuwa unanidanganya, labda mzee bado ujaelewa lengo letu la kuja hapa kwako, ni kuweka mambo sawa, ili amani ipatikane kati yenu” aliongea tena Johnson, “nazani wewe ndie ambae bdo uja elewa, nikuulize kitu kijana?” aliongea mzee Nyati akimtazama Johnson, “bila shaka mzee unaweza kuni uliza” aliongea Johnson ambae alionekana kushangaa aneno ya mzee huyu, “labda nikuulize kuwa ulisha wai kuongelea ugomvi ambao auna sababu yoyote, au chanzo?” aliuliza mzee Nyati na insp akakataa kwa kichwa, “ok! ulisha wai kujiuliza, ni kwa nini mzee Mijage ajakuambia kisa kilicho mpelekea yeye kukutuma kwangu?” swali hilo la mzee Nyati, llimfanya Johnson agundue kuwa, hapa kuwa na suluhu mahali hapa, sababu mzee huyu alikwepa sana kuombwa msamaha, “kiukweli sija wai kujiuliza” alijibu insp “ok! labda ufanye kitu kimoja, nenda kaongee nae, ikiwezekana mpigie simu, akueleze vizuri, pengine ni hisia tu, maana sio kila kosa hadhabu yake ni kifo” aliongea mzee Nyati kwa sauti yenye busara na hekima, iliyo mchukiza Insp ambae alijikaza kisabuni, na kuzuga kwa tabasamu la kinafiki, itaendelea ……..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU