BINTI MDUNGUAJI (56)

SEHEMU YA HAMSINI NA SITA

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA TANO : Johnson ambae alikuwa na shahuku ya kuiona sura ya mwanamke huyu, ambae alionekana kuwa na shepu nzuri sana, akinekana kutoka nyuma, macho ya huyo mgeni wakike na insp Johnson yakagongana, mke wa bwana Johnson, ambae alikuwa anasubiri kwa hamu, kuona wawili awa, wakikumbukana, alishuhudia vitu viwili tofauti kwa watu hawa, wakati mume wake akishikwa na mstuko mkubwa sana, lakini yule dada alioneka kutabasamu, “Jackline, umepajuwaje hapa nyumbani kwangu?”aliongea Johnson kwasauti ya kunong’ona, endelea ………..
Iliyo tawaliwa na mshangao, insp alimtazama mke wake kujuwa kama yupo salama, maana akuamini kama mke wake amekaa na kucheka na huyu mwanamke hatari sana, ambae kwake kuuwa ni kitu cha kawaida kabisa, nikama kukata vitunguu jikoni, Johnson akamwona mke wake akiwa anatabasamu bila wasi wasi wowote, “kaka Johnson za masiku” sauti ya Jackline ilimzindua Johnson toka kwenye mshangao, na kugundua kuwa Jackline yupo pale kwa lengo maalumu na hakuitaji mke wake ajuwe yeye ninani, “karibu sana, ni Jackline vile?, kama nina kukumbuka vizuri” aliuliza insp Johnson huku akizuga na tabasamu ambao ata mke wake alijuwa kuwa anazuga, lakini mama Bety aliwaza kuwa pengine watu awa walikuwa ni wapenzi kipindi wapo shule, asa alipozingatia uzuri wa sura na mwili alionao mwanamke huyu, “ndio mimi kaka Johnson, inamaana ulisha anza kuni sahau?” alijibu Jackline Nyati au mama Fransi, huku tabasamu bado limetawala usoni mwake, “karibu sana Jack, siwezi kukusahau dada yangu, karibu ndani tuongee” alisema insp Johnson ambae akili yake nikama ilikuwa imeganda asijuwe afanye nini juu ya huyu mschana, anaemtafuta kwa hudi na uvumba, ambae leo amejileta mwenyewe nyumbani kwake, “hapana kaka Johnson leo sikai sana, ila kwasababu nimesha pajuwa, nitapanga siku yakuja lasmi” kauli hiyo ya Jackline ili mstua sana insp Johnson, akijuwa Jackline anamaanisha nini, aliposema kuwa atakuja lasmi, “ok! kwa hiyo utaongelea hapa hapa?” aliuliza Johnson, akimtazama mke wake, ambae alikuwa ametulia akiwatazama wawili awa wakiongea, “kaka Johnson unaazani mimi mkaaji, yani ungechelewa kidogo tu! usinge nikuta” aliongea Jackline kisha akamtazama mke wa insp, “mama bite wacha mimi niondoke, nita tafuta siku tuongee sana, ila usisahau kumsalimia Bite” aliongea Jackline akimwambia mke wa insp Johnson, ambae aliitikia kwa uchangamfu, lakini bado alkuwa kwenye mshangao, ila akuwa na wasi wasi maana alijuwa mgeni akiondoka ata ambiwa ukweli wote na mume wake, mama Bite aliwashuhudia wawili awa wakitembea pamoja kuizunguka nyumba wakielekea upande wa mbele wa nyumba, ** siku hiyo Denis alikuwa amewai kurudi nyumbani kwake, kibamba njiapanda ya shule, akiwa na Cartoon yake ya bia, “huyu mwanamke asipo rudi mwezi huu namfwata mwenyewe, isijekuwa ameshaolewa huko kwao” aliwaza Denis au baba Frans, akiwa sebuleni kwake anatazama filamu, na kushushia bia, Denis ambae alianza kunywa bia toka mchana mida ya chakula akiwa na rafiki yake Mahadhi, aliwaza mambo mengi sana juu ya mke wake, na mwane, maana ukiachilia mabadiliko mabaya ya nyumba na maisha ya pale nyumbani, pia alikumbuka sana utamu wa kitumbua cha mke wake, “isije kuwa amesha kolezwa na midume mingine huko, amesha nisahau” hayo ni mawaazo yaliyo iumiza akili ya Denis. na kumfanya aendelee kugida ombe kama amepungukiwa akili, ** wakati huo huo mzee Soud Hassan alikuwa nyumbani kwake kigamboni, akifwatilia habari za burudani kwenye television, ya taifa, huku mke wake akiwa nje ya nyumba upande wajikoni, akiongea na rafikizake wa wili, ambao ni wa mama wajirani zake, mzee Soud akiwa hana ili wala lile, mala akasikia mlango wa nyumba yake ukigongwa, pasipo kusikika sauti ya mtu akiita hodi, “karibu, pita ndani” alikaribisha mzee Soud Hassan, brigedia mstaafu wajeshi la ulinzi, huku macho yake yakiwa kwenye television “asante afande” mzee Soud alielekeza macho yake, mlangoni kumtazama alie mwita afande, maana sauti yake aikuwa ngeni masikioni mwake, naam mzee Soud alijikuta akishikwa na mtetemeko wa hali ya juu, ulio sababishwa na uoga, akijuwa leo ndio mwisho wake, “karibu sana bwana Nyati, zasiku nyingi bwana” mzee Soud alisalimia huku akimtazama Michael Nyati, ambae siku zote mzee huyu alikuwa akitambua fika kuwa bado yupo hai, na alijuwa kuw siku kama hii lazima itatokea, na kweli leo bwana Michael alikuwa mbele yake akitabasamu, “asante sana mzee wangu, habari ya kufaidi upepo wa bahari?” alisalimia mzee Nyati huku akikaa kwenye moja ya kochi, kati ya matatu yaliyopo mle ndani ya sebule ya mzee Soud, “salama kabisa bwana Nyati, karibu sana” aliongea mzee Soud huku akitetemeka wazi wazi, na sura ya uoga ikiwa imemtawala, “asante sana mzee wangu, za toka siku ile tuonane Songea” aliongea mzee Nyati akimtazama kwa umakini sana mzee Soud , ana kumwona jinsi alivyo kuwa anatetemeka kwa uoga, kiasi cha yeye kuanza kuona huruma, “kwakweli safi tu! bwana Nyati, lakini mmbona ghafla hivyo?” aliuliza mzee Soud huku akimtazama mzee Nyati kama vile vile anatazama mzimu, “aiwezi kuwa ghafla, nazani ulisha tarajia ujio wangu miezi mingi iliyo pita, sababu unajuwa ulicho kifanya” mzee Nyati aliongea taratibu kwa sauti ya chini, “ni kweli bwana Nyati, lakini sikuwa na maana ya kile alicho kifanya yule kijana mpumbavu” alongea mzee Soud akionyesha kujilahumu kwa kitendo cha kumwelekeza namna atakavyo mpata mzee Nyati, “lakini mzee Soud, unafahamu kuwa sikuzote polisi, na mwalifu, awawezi kupatana, kwanini ukamwelekeza?” aliuliza mzee Nyati, huku akimtazama mzee huyu, ambae alionekana kukata tamaha ya iendelea kuishi, “nililihisi hilo mapema sana, ila kwa maelezo yake ya mwanzo, ndio maana nika mwamini na kumwelekeza pale dukani, kwa yule mschana, nikijuwa kuwa lazima ukisikia ujio wake utajipanga vizuri, sikutaka kumwelekeza nyumbani kwako moja kwamoja, lakini nilimsihi sana asijaribu kufanya jambo lolote la kijinga” alijitetea mzee Soud, “ok! mzee Soud, sina ubaya na wewe, labda unge nieleza alikuambia anafwa nini Songea” aliongea mzee Nyati kwa sauti ya kirafiki kabisa, na mzee Soud akaanza kumsimulia, jinsi kijana huyu alivyo kuja na kumpa wazo la kutaka kukutana na mzee Nyati, kwaajili ya kuangalia nana watakavyo maliza mauwaji kwa njia ya amani, pia akamsimulia jinsi alivyo sikia kilichotokea Songea, kisha mzee Soud akamaliza kwa kumsimulia jinsi walivyo kutana na Johnson miezi sita iliyo pita, pale kivukoni, na kumwonyesha dharau ya hari ya juu, “ina maana huyu kijana Johnson David ni yule mtoto wa meja Masinde?” aliuliza mzee Nyati, kwa mshangao, ** “najuwa unashangaa ujio wangu” aliongea Jackline baada ya kuwa yeye na Johnson, wamesha zunuka nyumba ile na kutembea atuwa kadhaa, kutoka pale nyumbani, “ni kweli Jack, lakini naomba usihidhuru familia yangu tafadhari” aliongea Johnson ambae kiukweli mpaka dakika hii, alikuwa anatamani kama watokee polisi wenzake wakiwa na silaha kali sana, wamzibiti mwanamke huyu, “sheria yangu sito mzuru mke wako wala mwanao, sababu awa usiki, na wewe mwenyewe iwapo utafwata nitakayo kuagiza” aliongea Jackline huku uso wake ukiendlea kuachia tabasamu, kama vile walichokuwa wanaongelea, ni kitu cha kawaida sana, na chakupendeza, “maagizo gani tena?” aliuliza insp kwa shahuku, huku wakisimama, pembeni ya barabara, “ni maagizo mawili tu! bwana Johnson, ila siyo ombi ni lazima ufanye hivyo, najuwa wewe ni mkaidi sana, ata baba kule Songea alikuonya usifanye jambo la kipumbavu wewe ukawa mkaidi” hapo kengere ya tahadhari juu ya utata wakifo cha mzee Nyati ilianza kugonga kichwani kwa insp Johnson, ambae alikuwa ametoa macho akimsikiliza Jackline, “agizo la kwanza kabisa, nakupa miezi mitatu, wafatwe wakina mzee Masinde na mwenzie Mwijage, awaambie kuwa, waende kwenye vyombo vya habari wakatangaze walicho kifanya kule congo mwaka 1988, juu ya askari wao Michael Fransis Nyati” hapo Jackline alitulia kidogo akamtazama Johnson, usoni, akamwona ameduwaa kwa bumbuwazi, “pili usi jaribu kuni tafuta, au kuzuwia mauwaji yatakayotokea endapo melekezo ya kwanza, yatashindikana katika utekelezaji, sababu sito penda uingie katika orodha ya watu watakao uwawa” alisema Jackline, huku akinyosha mkono juu, na kuonyesha ishara ya kuita kitu, “samahani kidogo Jackline, unaweza kuni julisha, ni jambo gani walilifanya wazee hao?” aliulza Johnson akimtazama Jackline, huku akitamani kumkamata hapo hapo, lakini alijuwa kuwa aito kuwa lahisi kumkamata mwanamke huyu, kutokana na uwezo wake mdogo wa kimapigano, dhidi ya huyu mwanamke hatari sana, “Johnson kila mala unaongea na kula na hao wazee, sidhani kama wanashindwa, kukueleza kitu walicho kifanya juu ya mzee Nyati” aliongea Jackline, na wa wakati huo huo lika simama Toyota Lav four pembeni yao, lililo kuwa linaendeshwa na mschana mrembo sana, insp Johnson aliduwaa baada ya kumwona dereva wa lile gari, alikuwa ni Felister, yule mwanamke alie mwelekeza nyumbani kwa mzee Nyati baada ya kufika Songea, “habari yako bwana Vasco” alisalimia Felister na kumfanya Johnson atabasamu kivivu, akijiona ni mjinga kupita kiasi, “safi” aliitikia Johnson, kimkato, na kupotezea, Johnson akamwona Jackline ailingia kwenye gari, ambalo zaidi ya dereva mrembo pia siti ya nyuma, alionekana binti mmoja alie mpakata mtoto wa miezi kama tisa hivi, kabla gari alijaondoka, Jackline aka mtazama insp Johnson, huku akiachia tabasamu, kisha akaongea kwa sauti ya chini, “insp ni miezi mitatu tu!, pia kumbuka kuwa uwezi kunizuwia” hapo kabla Johnson ajasema lolote, akashangaa kuona gari likiondoka, insp ambae alitamani vitu vingi sana, juu ya wale wanawake ikiwa ni kuwakamata na kujuwa kama, mzee Nyati ni mzima au amesha kufa, alisimama akilitazama lile gari likiyoyoma nakutokomea mtaa wapili, hapo insp kama aliezinduka, alirudi nyumbani kwake mbio mbio, akumjari mke wake ambae mda wote, alikuwa anawachungulia dirishani, insp alipitiliza chumbani kwake, na kutoka na funguo ya gari mkononi, pasipo kumwambia chochote mke wake, ambae alisimama akimshngaa, insp Johnson akiwa amevalia bukta yake na tishert alitoka nje ya nyumba yake na kuingia kwenye gari akatoka speed kali sana, kihasi cha kutimua vumbi nyingi sana, ** ilikuwa saa kumi na mbili za jioni, Jackline na Felister wakiwa pamoja nabinti wakazi alie mshika Fransis, waliendelea na safari yao wakiwa ndani ya gari lao Toyota Lav four, kwenye foleni za makongo, wakirudi mwenge, na kufwata bara bara ya ubungo kisha wakakatakulia kuelekea mbezi ya kimara, huku njiani wakikutana na foleni za hapa na pale, njiani waliendelea na story za hapa na pale, “hivi Jack, kwa nini usi mwambie shemeji kama unaenda leo?” aliuliza Felister, wakati wana pita kibanda cha mkaa, na kuingia mbezi mwisho, “nataka nikamfumanie” aliongea Jackline wote wakacheka, “Jackline bwana unajuwa kufumania siyo mchezo, unaweza kuzimia mwenyewe” aliongea Felister, wakati huo alikuwa anaongeza mwendo baada ya kuvuka tuta la kituocha polisi kwa yusuphu, sasa giza liliuwa limesha tanda, ghafla walistuka boda boda moja ikikatiza mbele ya gari lao ikiwa speed, baada ya kuwa over take, na kusababisha Felister astuke na kuyumbisha gari kidogo, ile na kaa sawa, ika chomoka piki piki nyingine, ikitokea bara bara ya zamani, na kuwa ovar take, kisha mwendesha boda boda akafanya kama alivyofanya yule wakwanza, akaichomeka piki piki mbele ya gari lao, akiwepa gari ambalo lilikuwa lina tokea mbele, bahati aikuwepo upande wa dereva wa boda boda, aliguswa na kingo ya mbele ya gari la kina Jackline, na kusababisha akose uelekeo, hapo watu walo kuwepo eneo lile walishuhudia yule deeva wa boda boda akijibwaga chini na kusota mita hamsini juu ya lami, “mungu wanu nimeuwa” Felister alipiga kelele, huku akikanyaga brek na kusimama, naam wakina Jackline wakisaidiwa na mwanga wataa zagari lao, walimwona yule mwendesha boda boda akisota na kugota akiwa ameshaachalama nyingi ya damu kwenye lami, “Felly ebu endesha gari tuondoke” aliongea Jackline uku ana tazama nyuma kwa kutumia kioo cha nyuma cha gari, akaona mwanga mkali wapikipiki zikija kwa speed, huku watu wengi sana, walio peba mawe na vipande vya magongo, tayari kuwa shambulia, wakisogea kwenye eneo la tukio, “Felly endesha gari tuondoke” safari hii jackline aliongea kwa sauti kali, akimwambia Felister ambae alikuwa bado ameduwaa akimtazama yule mwendesha boda boda asiye kuwa na tahadhari na barabara, Jackline akatazama pembei akawaona wananchi wenye hasira kali wakiwa wamesha wakaribia kabisa, akatazama nyuma, akaona zile pikipiki zikiwa zimesha wafikia, “hapa siyo pazuri” alinong’ona Jackline, huku aki shika kiti cha dereva na ku kilaza kwa kutumia kitufe chake, nakumfanya Felister aliekuwa ameduwaa alalie kwa nyuma, kisha Jackline akamvuta Felister kwanguvu, na kumpeleka seat ya nyuma, kisha kama umeme Jackline akaamina kwenye seat ya dereva na kuiingiza gia ya kuendeshea, na kukanyaga mafuta mengi sana, na kusabisha gari liondoke kwa mwendo wa kasi ya hajabu, huku gari likikoswa koswa na mawe, toka kwa wananchi ambao hawa kujuwa sababu ya yule dereva wa pikiki kusukumwa na gari, Jackline aliendesha gari kwa speed akijitaidi kupenya kushoto na kulia wa barabara, akipia magari yaliyo kuwa mbele yake yakienda taratibu, “dada wanakuja” ilisikika sauti ya dada wakazi, hapo Jaackline akatazama kwenye side mirror, akaziona piki piki saba zikija kwa speed, “kazi imeanza mapema sana” alisema Jackline, ambae alipeleka mkono wake kati kati ya seat zambele za gari, na kukigusa kisu chake, kilicho ifaziwa ndani ya kifuko chake, akatabasamu *** baada ya kutoka nyumbani kwake insp Johnson alielekea kigamboni, akiwa na lengo la kwenda kumwona mzee Soud, Johnson ambae akukumbuka kabisa, jinsi alivyo shindwa kuelewana na mzee huyo miezi sita iliyo pita, aliendesha gari kwa speed kali sana, kama vile amechanganyikiwa, insp Johnson aliendesha gari pasipo kuwaza ataanzaje kuongea na mzee Soud, ambae alitokea kumchukia siku za nyuma, pasipo sabau za msingi, insp Johnson aliona kama anachelewa kufika, ilifikia kiasi akaona aa pantone linaenda taratibu, pantone lilifika kwenyeukingo wa bahari upande wa kigamboni, na kusimama, hapo magari yakaanza kutoka taratibu sana, na kuondoka huku yakitengeneza msongamano mdogo wa magari, waki pishana na magari yaliyokuwa yana subiri kuingia kwenye panton, wakati insp Johnson akiwa anatembea taratibu katika msururu wa magari akatazama pembeni, yalipo simama magari yanayo subiri kuvuka, ghafla macho yakamtoka insp, ni baada ya kuwaona watu watatu anao wafahamu, vyema kabisa, wakiwa ndani ya Toyota V8, “aijawai kuwa lahisi” insp Johnson alijikuta akiongea peke yake, huku bado akiwatazama mzee Nyati, mke wa mzee Nyati na kijana Side Tall, ambao walikuwa wakiongea na kucheka kwa furaha, “ameponaje huyu mwanga?” alijiuliza Johnson, huku akiwa aamini macho yake, (jiandae kujuwa mzee Nyati na mke wake waliponaje ndani ya ile nyumba ya udongo) itaendelea ………..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata