BINTI MDUNGUAJI (61)

SEHEMU YA SITINI NA MOJA

 

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI : huku mlango ukifunguka, “kumekucha” aliongea Eva akijibanza pembeni ya mlango akiwaza namna ya kufanya tukio bila Denis kuona, nyumba nyingine zote zilikuwa na umeme, kasolo yakwao tu, Jackline akatuliza akili akasikiliza kwa umakini, akasikia michacho ya nyayo za watu toka ndani, hapo Jackline akaona bola aingie ndani akawamalize huko huko, pasipo Denis kuona, lakini kabla ajapiga hatua kuingia ndani, ENDELEA ……..
Akasikia sauti za watu wakinong’onezana “mbona unachelewa bwana” ilikuwa sauti ya kike, ambayo ilifwatiwa na sauti ya nyayo za kunyatia, kisha ika sikika switch ya taa ya sebuleni iki to mlio, ikionyesha kuwa imebonyezwa, hapo Jackline Mcheale Nyati akajuwa kuwa kitafwatia kitendo cha gari kushambuliwa, kwa hiyo anatakiwa awai haraka sana, hivyo Jackline au mama France kwa kitendoo cha haraka sana, akiwa na uakika akuna anae mwona kutokana na giza akajivilingisha kwa mtindo wa sarakasi, na kuji toma ndani kisha aka jibanza pembeni ya sofa akizungusha macho yake kwa haraka sana, ndipo alipo ona taswala ya mtu aliesimama karibu na ilipo switch ya taa za sebuleni, hapo akajisemea kimoyo moyo , “karibu kuzimu” wakati anajiandaa kwenda kuchomoa roho ya yule mtu, mala ghafla akasikia switch kubwa ya umeme (main switch) ikitoa sauti ya kuwashwa, ikifwatiwa na mwanga wataa za nje kuwaka, sambamba na sauti ya music, “surprise” hapo Jackline akatulia na kuusikiliza ule music, ulikuwa ni ‘happy born day’ hapo Eva akahisi kunauwezekano wa kuharibu mambo, akatulia kiya akitafuta jinsi ya kuinuka toka mafichoni, “akaskikia minongono mingine, “bado wapo nje ebu washa taa” hapo haraka sana Eva akasimama, toka mafichoni, na taa zika washwa, akajifanya kustuka na kujishika kifuani, hapo Jackline alitazama ndani nakuona watu zaidi ya ishilini ambao walipiiga kelele za kushangilia, ndani ya nyumb mlikuwa mmepambwa kwa taa kama zile za chriss mass, pia yalionekna mabox mengi sana ya zawadi, pamoja vitu vya kuchezea mtoto, huku mezani kukiwa kumetapaa vinywaji mbali mbali, pombe zikiwa nyingi zaidi Jackline usoni akiwa ameachia tabasamu, aliwatazama kwa awamu, watu wengi, wake kwa waume waliojaa ndani ya nyumba yao, huku nyuso zao zikionekana kutawaliwa na furaha iliyo changanyika na ulevi, kati ya watu wale Jackline aliwaona boss wa mume wake Mahadhi na Janeth, ‘mnabahati mngekufa bila hatia’ alijisemea kimoyo moyo Jackline, “he! umeingia saa ngapi?” aliuliza Janet kwa mshanngao huku akimsogelea Jackline, na kumsalimia kwakumkumbati, huku anamwambia, “hongera mwaya umekuza” hapo watuwengine waliopo mle ndani, nao wakasanuka kumshangaa Jackline, maana awakumwona wakati anaingia, Jackline aikumtisha sana maana walionekana tayari wamesha anza kunywa pombe, “engineer yupo wapi?” aliuliza mtu mmoja mwenye hasiri ya kihindi, na wakati huo huo Denis akaingia ndani akiwa amembeba mwanae Fransis, pamoja na mtu alie valia jacket jeusi na mkononi alikuwa amebeba kofia ngumu ya kuendeshea pikipiki “naomba nmiambie kitu kimoja, funguo mmepata wapi?” aliuliza Denis kwa sauti ya mshangao iliyo ambatana na ulevi, hapo Jackiline akakumbuka swala hilo, la kmba watu awa wameingiaje ndani, lakini kikalipuka kicheko, kabla boss wa akina Denis ajajibu, “jiangalie mfukoni” huku kicheko kina endelea, hapo Jackline akamwona Denis akijikagua mifukoni, kisha akaonekana kukumbuka jambo, alafu akaangua chekeo, nikwamba wakati akiongea na boss wake kule ofisini, akimweleza juu ya kuomba luksa akafanye manunuzi ya familia yake, alikuwa ameshika fungu za gari na nyumba mkononi, na kunakipindi aliziweka mezani, hap ndipo boss wake ambae alsha panga kumfanyia surprise Denis ya kumpa hongera ya kupata mchumba na mtoto, akaichukuwa na kuanza mipango ya kumfanya surprise, akiwa julisha wateja wao na marafiki ambao aliwai kuwajulisha azma yake ya kumpongeza kijana huyu, ambae utendaji wake ni mkubwa na mzuri sana, na wao ndio walio mpigia simu Denis, ili kumchelewesha, siku hiyo mambo yaliuwa ni shamla shamla, mpaka saa nane za usiku, ndipo walipo tawanyika na kuelekea makwao, wakitumia magari yao, ambayo mwanzo waliya gesha mbali kidogo, ili kufanikisha surprise yao, kwa Denis na familia yao, kiukweli Jackline alifarijika sana kwa upendo walio uonyesha rafiki zake Denis, ambao licha ya kujumuika nao usiku ule pia wali leta zawadi nyingi sana za kwake na zamtoto Fransis, ambae ata siku zilizo fwata Fransis alikuwa na vitu vingi sana ya kuchezea, vilivyo chania apate marafiki wengi sana toka nyumba za jirani, na kusababisha ata wa mama wajirani nao waanze mazowea madogo madogo na mama France, lakini Jackline alijitaidi kuwakwepa, maana akutaka rafiki kwa mda huu, mpaka amalize kazi yake, japo maneno yaikuwa mengi toka kwa wamama wamtaani, wapo waliosema kuwa mama Frnce anajidai, wengine anajisikia sana, lakini Jackline akujari wala kuya sikiliza maneno hayo, yeye aliendelea na ratiba yake ya kila siku, ambapo asubuhi, baada ya kuandaa chai au supu ya mume wake, na kuakikisha mume wake ameenda kazini, alifanya mazoezi ya nguvu kisha kuanza shuguli za nyumbani kama mama, huku upande wa Denis nae, japo maisha yalikuwa ni yenye amani na furaha, lakini ilimshangaza tabia ya mke wake yakuto kumkubaria swala la kupeleka barua kwa wazazi wake, ili waweze kufunga ndoa, kila siku akimwambia, asiwe na haraka, kiukwei Denis alikuwa na wasi wasi sana juu ya jambo hilo, akiofia kuwa pengine Jackline angebadiri mawazo yake na kuolewa na mtu mwingine, japo alifarijika na tabia ya mke wake huyo, ya upole na unyenyekevu mwingi juu yake, ulio tawaliwa na upendo mkubwa na uaminifu, ukizingatia kuwa alimkuta bikira, na akuoneka kuonyesha dalili yoyote, ya kusaliti penzi lao, ambapo muda mwingi sana mama France alishinda nyumbani pasipo kudhurula, ** huku nako kwa Insp Johnson pamoja na kikundi chake maalumu alicho kiunda, kwaajili ya kumsaka muuwaji wakike anae sadikiwa kuwa ni mtoto wa mzee Nyati, amba mpaka sasa wanachi walikuwa wanafahamu kuwa amesha kufa, huku askari wapelelezi wakizagaa kwenye centre mbali mbali za jiji la dar, kumsaka muuwaji ambae idadi kubwa ya polisi hao, awakuwa wana mfahamu, ndani ya miezi mitatu ya mwanzo mabo yalikuwa ni magumu sana kwa wanchi wanao penda kudhurula usiku, maana licha ya kuzagaa kwa polisi wapelelezi, pia usiku kulikuwa na doria kali sana, ya polisi, hivyo kwa alie onekana na zulula usiku alikuwa na hali mbaya, hapo ange pewa kipigo cha kue;eweka, kisha angeenda kujieleza kituoni, ambako atakama ungekuwa na vielelezo gani, basi ungeachiwa asubuhi, hali hiyo iliyodumu kwa miei mitatu, akuwa na mafanikio yoyote, na hali ilikuwa shwali kabisa, akukuwa na tukio jingine la mauwaji lililo tokea linalo fanana na matukio yanayo, sadikiwa kufanywa na mwanamke hatari, ndani ya miezi mitatu, insp Johnson aliangaika sana kumtafuta Jackline, huku akiangaika kumwuliza baba yake, jambo ambalo alilifanya nchini congo, mwaka 1988, alitumia mbinu nyingi sana, ikiwa pamoja na siku ambayo alikaa na baba yake wakinywa pombe nyingi sana, kiasi cha mzee Masinde kulewa sana, lakini alipo jaribu kumwuliza juu ya swala hilo, lakini mzee Masinde alijibu, kwa mkato “hachana na nahuyo mjinga” Insp ambae alikuwa anania thabiti, ya kumwokoa baba yake, akukata tamaa, alirudi mala kadhaa kwa mzee Soud, ambae safari hii akutaka kutoa ushirikiano kwa insp Johnson, zaidi ya ushauri “kijana unapo mfwatilia mzee Nyati kuwa makini sana” maneno ambayo insp aliyaona ya kinafiki, na kwamba yana lengo la kumtisha na kumkatisha tamaha, insp akiwa na tegeo kwa askari wake aliowaweka kumlinda baba yake pasipo mwenyewe kujuwa, na pc busungu alie kuwa akishinda, maeneo ya mbezi mpaka kibamba, aliendelea uongoza kikundi chake kipya, chenye watu zaidi ya sitini, wenye mafunzo mazuri na silaha za kisasa, pamoja na vazi maalumu la kuzuwia risasi (bullet proof) ambalo walikuwa wakivaa muda wote wakiwa kazini, siku zilisonga, mambo yakwa kimya kabisa, ata baada ya miezi mitatu aliyopewa Insp Johnson kupita, mambo yaliendelea kuwa kimya, licha ya insp kuwa tayari kupokea simu, toka kwa Jackline, huku akitega askari kila kona ya mtaa anao kaa, kule mbezi, akitarajia kumkata Jackline endapo angeingia nyumbani kwake, kuulizia kwanini akutekeleza shariti la wakina mzee Masinde, ujitangaza makosa waliyo fanya miaka hiyo, lakini akaona kimya kabisa, ** mzee Masinde na mwinzie bwana Kaijage waliendelea na maisha yao, huku siku zikizidi kuendelea kusonga, wakiamini kuwa mzee Nyati ameshindwa kuwa kabili kutokana na msakako unaoendelea, hivyo wazee awa walifanya shughuli zao, za kibiashara kama kawaida, shulizao kwakiasi kikubwa azikuwa halali, wakati mzee masinde akeajiri vijana wengine wanne, baada ya wale wanne wa kwanza kupoteza maisha, aliendelea ku fanya biashara zake za kuvusha magendo kwa kutumi ameli yake, huku mala nyingine wakivamia na kupola kwenye meli kubwa, zinazo safirisha mizigo, huku lunten mstaafu Kaijage akindeleza biashara yake ya usafirishaji wanchi kavu, kwa kutumia magari yake makubwa, mna licha ya kusafirisha mizigo kutoa na kupeleka nje ya nchi, pia kama ilivyo kuwa kawaida yake ya kusafirisha meno ya tembo na ngozi za chui, ambavyo vilimwingizia pesa nyingi sana, *** ilsha timia miezi sita toka Jackline aingie Dar es salaam tokea Songea, ilikuwa alahamisi saa mbili usiku, akiwa sebuleni na mume wake wana pata chakula cha jioni, huku wakitazama taharifa ya habari kwenye television ya taifa, ndpo alipo vutiwa na habari moja iliyo kuwa inasomwa, ilikuwa ni habari ya hajari, iliyo toke kongowe mkoani pwani, gari kubwa aina ya scania la mizigo, lililo gongana na bus la abiria, nakusabisha vifo vya watu wengi sana zaidi ya ishirini, huku wengine wote wakiwa maututi hospital ya Tumbi, mkoa wapwani, kitu kilicho vutia kwenye habari hiyo, nikupatikana kwa nyala za serikali kwenye gari hilo la mizigo ambalo, kwa mujibu wa mashuhuda, ndilo lililo sababisha hajari, wakati Jackline na mume wake wanaanglia habari hiyo, waliona ikionyesha tukio la kukamatwa kwa mmili wa gari la mizigo ambalo gari lake limesababisha hajari na kukutwa na pembe za ndovu na ngozi kadha za chui, na kwamba jumatatu anafikishwa mahakamani, “kama na mfahamu huyu mzee” aliongea Jackline akimtazama Denis, “sijuwi kama unamfahamu, huyu tajiri sana anaitwa Kaijage, kumbe dili zake ni noma” aljibu Denis akishangaa kidogo, wakati huo huo simu ya Jackline ikaita Jackline akaitazama simu yake, akaona jina lime andikwa baba, akaipokea na kuweka sikioni, hapo Denis akusikia kitu chochote zaidi ya shikamoo, kisha ikafwata ndiyo ndiyo ndiyo, mwishoni kabisa ikawa sawa, alafu simu ikakatwa, alafu Jackline akasema “kazi imeanza” maneno hayo yali mstua Denis akamtazama mkewake kwa mshangao, itaendelea ……………

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata