
SEHEMU YA SITINI NA SITA
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA TANO : “Denis kumbe wewe ni muongo hen! si umesema gari lako bovu, sasa kile nini?” aliuliza Mahadhi huku akisongea kwenye TV nakuonyesha gari aina ya Toyota Noah lililo kuwa linapisha na na magari ya polisi, yaliyo kuwa yanaingia eneo la tukio, hapo wote mle ndani waka toa macho kulitazama lile gari, “kweli bwana” alisema Boss wa Denis huku wakilikazia macho gari lile, ambalo lilionekana wazi kuwa ni gari la Denis, asa kutokana na stiker moja kwenye kioo cha nyuma iliyo tangaza pombe flani, iliyotengenezwa na kiwanda kimoja cha humu nchini, endelea……..
“nani ameenda nalo mjini wakati gari bovu, napia mama France ajuwi kuendesha, ebu nimpigie simu” aliongea kwa kuchachawa Denis, huku anatoa simu yake mfukoni, nakuanza kutafuta namba ya mke wake, “ebu subiri kwanza” aliongea Mahadhi ambae alikuwa karibu kabisa na Tv, nawote waka tazama kwenye TV, Denis nae akaacha kubonyeza simu yake na kutazama kwenye Tv, “hivi hii namba ni ya gari lako Denis?” aliuliza Denis, wote wakatazama lile gari ambalo kwa sasa lilikuwa linaonekana liktembea taratibu, ukulikipishana n magari ya polisi yaliyo kuwa katika mwendo wa kasi sana, wakasoma namba za usajiri wa gari lile, waka iobna ni T182 C..P, wakati gari la Denis namba ya gari lake ilikuwa ni T 322 A..D, “hapo Denis akashusha pumzi kwangu, sambamba na wenzake, kasili Mahadhi aliegundua utofauti mapema, “dah! unaweza kuingia kwenye matatizo hivi hivi” aliongea Denis ambae alionekana kuondokewa na wasi wasi, “unazani, yani unaingia kwenye mikono ya wababe bila utetezi wowote” aliongea boss, huku wakiendelea kutazama ile habari, iliyo kuwa inaonyeshwa moja kwa moja, ambapo waliona magari ya polisi ya kisimama eneo la jengo la wajasiliamali, na kushusha polisi waliozunguka eneo hilo kwa haraka sana, ** insp Johnso akiwa amechanganyikiwa, maana akuwa na uakika na usalama wa Busungu, alipandisha ngazi kwa mwendo wa mbio, akifwatiwa na polisi watatu mmoja kati yao akiwa na silaha, lakini insp na askari wake walipofika gholofa ya nne wakakutana na mwili wa Busungu ukiwa unetulia chini ya sakafu, akionekana kuwa akiwa na uhai, “kum.. make, tayari” alipayuka Johnson kwa sauti kubwa ya machungu, kisha aka uelekeza uso wake pembeni, na kuanza kulia kimya kimya, wakati huo wale askari wakendelea kulikagua eneo lile, huku wakisikia ving’ora vya magari yapolisi, ikiashilia kuwa polisi wenzao walikuwa wanaingia eneo lile, na dakika tano baadae wakaonekana polisi wengine wakiingia mle ndani, nakufika kule gholofa yajuu, hapo polisi wale wakaendelea na shughuli zote, za ukaguzi wa eneo lile, muda wote insp Johnson alikuwa akitokwa na machozi ya uchungu, ilitumika saa nzima pale wajasiliamali, kuwakagua watu wote waliokuwepo ndani, lakini pamoja na usumbufu manyanyaso kwa watu wle waliopo mle ndani, polisi awakuweza kuambulia chocote, zaidi waliwaacha rahia wema wakinung’unika, kwa usumbufu walio upata, saa sita mchana ndio mda ambao, insp Johnson aliondoka, akimpitia baba yeke ambae alikuwa ameifadhiwa kituo cha polisi, pamoja na wenzake, kw usalama zaidi, akiwa anatumia gari la polisi, baada ya magari yote yaliyo kuwepo eneo la mahakama na kupigwa mawe, yakivunjwa voo na wanachi wenye hasira kali, nakupelekwa kwenye gereji ya polisi, ambapo wenye magari wata yafwata wenyewe kwaajili ya kwenda kuyatengeneza, insp akiwa njiani na baba yake alijitaidi kumweleza baba yake kuwa mtulivu nyumbani, asa kwa kipindi hiki ambacho wanajaribu kutafuta ufumbuzi wa swala hili, insp alijuwa kuwa baba yake asingeweza kueleza juu ya kilicho tokea huko DRC mwaka 1988, lakini alijaribu kumweleza baba yake kuhusu faida ya yeye insp kufahamu swala ilo pengine lingeleta njia ya kumkatama Jackline na baba yake, “tuna weza kutafuta vifungu ambavyo vita igeuza kesi na yeye akaonekana ndie mkorofi, na pia tuka litumia jeshi la ulinzi, kumkata huyu mtu” hapo kidogo mzee Masinde alitabasamu, maana ilimgusa kidogo, “ok! njoo kesho jioni, nikueleze jinsi ilivyo kuwa” kauri hiyo ya mzee Masinde ili mtabasamulisha Johnson, akiamini kuwa mwisho wa matatizo umefika** mzee Nyati na mke wake walikuwa wana kagua jengo moja kubwa sana la kibiashara, pembeni ya mji wa Songea pembei ya bara bara kuu iendayo mikoa yakusini, yani Lindi na Mtwara, wakionekana wenye nyuso za furaha, wakati mzee Nyati kifurahi mwanae ana karibia kuwamaliza maadui zake, mama JACKLINE, alikuwa anafurahia kuwa mwanae anamaliza kazi, naataishi maisha ya kawaida, kama mama, “nazani ili jengo litakuwa mfano kwa mikoa yote ya kusini, na litafaa sana kwa biashara iliyo kusudiwa” aliongea mzee Nyati huku wakiendelea kukagua kagua jengo lile mbalo lilonekana kuwa katika atuwa za mwisho kukamilika, “na yale magari vipi uli yaulizia?” aliuliza Anitha yani mama Jack, “kwani kati naongea na simu wakati tunakuja, ulizani nilikuwa naongea na nani?” aliongea mzee Nyati, kwa mapozi huku akiushika mkono wa mke wake, ambae aliachia tabasamu, “tatizo wewe unapokuwa unaendesha gari mawazo yote yanakuwa kwenye barabara” aliongea tena baba Jack, “ha! mimi nilisikia tu tupo njiani tuna karibia Iringa, sikujuwa kama ndio wao, ok! kwahiyo yapo yote sita?” aliuliza mama Jack, huku wana endelea kutazama jengo hilo kubwa na lakisasa, ambalo lilikuwa lina shambuliwa na fundi kwa fujo za hali ya juu, “yes! kama tulivyo agiza” ** saa tisa jioni insp, baada ya kumpeleka baba yake nyumbani na yeye kwenda kumtazama mke wake wake nyumbani, alirudi ofisini na kugawa majukumu kwa akari wake, ambao walitakiwa kuzunguka jiji zima la dar es salaam, wakiakikisha kuwa msako mkali unaendelea, na kuwa kamata watu wotewakao onekana kuwa awana shughuli za kueleweka, wakati huo kikao kikali kilikuwa kina endelea kwenye ofisi ya mkuu wa jeshi la polisi, akiongea na wakuu wote wa vitengo vya jesho hilo, waki laumiwa kwa tukio lililo tokea mahakama kuu, sikuhiyo mkuu wajeshi hilo alikuwa mkali kweli kweli, maana ilikuwa ni kitendo cha aibu sana, kutokea tukio hilo la mauwaji mbele ya mahakama kuu, wakati hayo yakiendelea, mala mkuu wa jeshi hilo alipigiwa simu toka kwa wazili wa mambo yandani, akimtaka mkuu huyo aripot haraka ikuru, ambapo yeye waziri ameshaitwa na raisi, kwenda kusimangwa juu ya tukio hilo, hapo matumbo yakawaunguruma, kwani walijuwa kuwa kimenuka, na kilicho waumiza vichwa ni kwamba, waliamini mauwaji ya namna hii amesha koma, baada ya kutangaza wamaesha mmaliza askari mtoro wa jeshi la ulinzi, ambae alikuwa anawawinda na kuwa uwa, askari wastaafu wa jeshi hilo, ambao alikuwa nao kwenye kazi maalumu huko nchini congo, mwaka 1988, “sasa huyu nani ambae anaendeleza mauwaji hayo” hilo lilikuwa swali la kila mmoja wao, maana licha ya kupata taalifa kuwa muuwaji ni wakike, na taalifa hizo kusambaa mitaani na kwenye vyombo vya habari, lakini aikuwaingia hakilini mwao, maana ukiachilia nwalifu wakike mwenye uwezo kama huo, pia akuwai kutokea ata askari wake, mwenye uwezo wa namna hii, kwa nchi za afrika, kitu kingine kilicho waumiza vichwa vyao ni kwamba, muuwaji huyo anaesemekana wakike, amekuwa akiwa uwa watu wenye record za ualifu tu!, nambaya zaidi, idadi kubwa ya wanchi wameonekana kumuunga mkono, kwa vitendo anavyo vitenda, mkuu wa polisi aliwaacha wenzake, na kwenda kunana na viongozi wake wa nangzi za juu, ** siku hiyo insp alishinda akiwa mwenye wasi wasi na uzuni mwingi sana, siyo kwasababu Busungu alipoteza maisha, lakini aliuzunika na kuingiwa na wasi wasi mwingi, kwasababu alijuwa kuwa ,uda wowote baba yake anawafwata rafiki zake watano, walio tayari walisha tangulizwa mbele ya haki, insp akujuwa afanye nini kumwokoa baba yake, nambaya zaidi adui yake, alionekana kuwa ni mwenye uwezo mkubwa sana, kuliko jeshi kubwa la polisi, “inabidi niongee na mzee Soud, anisaide kuongea na mzee Nyati, tuilipie zambi waliyo mkosea kwa ghalama yoyote, lakini siyo ya kumwaga damu ta baba yangu” aliwaza insp Johnson akiwa ofisini kwake, hapo hapo akatoa simu yake mfukoni, na kutaka kupiga kwa mzee Soud, lakini wakati anaitazama simu yake, akaoziona missed call nyingi na msseji moja, akazifungua kwanza miseed call, akaona zilitoka kwa Pc Busungu, akauma meno kwa uchungu, huku anafungua messeji nayo ilikuwa inatoka kwa pc Busungu, iliandikwa hivi, ‘Jackline anakuja mjini anatumia gari aina ya Toyota Noah, lenye namba T 182C..P’ hapo insp Johnson aliduwaa, huku akizitaja namba zile za gari, kwa sauti ya chini na yakunong’ona, “T 182C..P” kisha akamalizia kwakicheko cha uchungu, alafu akatulia kwa sekunde kadhaa, “huyu mwanamke mshenzi, ametumia namba za gari langu” aliwaza Johnson, huku tabasamu la uchungu likichanua usoni mwake, “ulikuwa askari mwelevu Busungu” alinong’ona Johnson huku akidondokwa na chizi, “nakuaidi nitamkamata huyu mwanamke” aliaidi Johnson huku akibonyeza namba ya mzee Soud na kuomba kuonana naye jioni ya leo, ** vyombo vya habari nchi nzima vilikuwa vina zungumzia tukio la kushinda kesi na kuuwawa kwa mzee kaijage, na pia kifo cha polisi mpelelezi leo ata redio za kwenye vyombo vya usafiri wa jumuiya, viliacha kupiga mziki na kuweka redio, ilikusikiliza habari hizo, saa kumi na mbili za jioni baada ya kutoka ofisini, Mahadhi alimpeleka Denis nyumbani kwake, sababu Denis leo akwenda na gari lake, wakiwa wana karibia kufika nyumbani wote wawili, kila mmoja aliwaza kimoyo moyo kukuta jambo flani kwenye gari la Denis, maana licha ya kuona namba ni tofaauti, lakini lilifanana kwa kila kitu na lile walilo liona kwenye Tv, likitokea kwenye tukio la pale jengo la wajasiliamali, lakini walipofika pale, walilikuta gari likiwa pale pale alipo liacha Denis, na hapakuwa na harama yoyote ya gari kutoka, ata walipo fungua bonet ili Mahadhi atazame tatizo ni nini, walikuta engine ya baridi kabisa, zaidi ya hapo walikuta France anacheza na watoto wajirani, huku mama yake yupo ndani anaendelea na shughuli zake kama mama, Denis na Mahadhi waligundua kuwa waya mmoja wa bettry ulikuwa ume funguka toka kwenye terminal yake, hivyo kusababisha kushindwa kupeleka umeme kwenye astater motor ili kuwasha gari, japo walishangaa ilichomokaje, lakini awakuwai kufikilia kuwa hiyo ilikuwa ni janja ya Jackline, ambae baada ya kumaliza kazi yake, alirudi haraka nyumbani, na kuliegesha gari kama lilivyo kuwa limeegeshwa jana, kisha akafagia eneo lote la nyumba na kuichomoa ile waya kwenye bettry, kama alivyo fanya jana yake usiku, baada ya kuakikisha wamesha liweka vizuri gari na kuliwasha Mahadi akaaingia ndani kumsalimia shemeji yake, kisha akaondoka zake kurudi nyumbani kwake, akimwacha rafiki yake akiwa na mke wake, ** tokea asubuhi, mzee Soud alikuwa ametulia sebuleni kwake, akfwatilia habari zilizo kuwa zina rushwa kwenye vyombo vya habari, ni inayo muusu mtu anae mfahamu, lutein Kaijage, kuuwawa mbele ya mahaka kuu, wakati akitoka kumaliza kesi yake, ambayo alishinda na kuachiwa huru, “ili nitatizo jingine, lazima masinde upatikane, na ukicheza mtoto wako atapoteza maisha” alijisemea mzee Soud ambae siku zote aliamini kuwa ubishi wa watu awa ndio unao wapoteza wakina mzee Masinde, *** jioni hii kabla yakwenda msibani, insp alielekea nyumbani kwake kubadiri nguo, na kuvaa za kiraia, njia nzima insp alizidi kuumiza kichwa, juu ya kumsaidia baba yake, yote kwa yote aliamini kuwa, kama hiyo kesho baba yake ata mweleza ukweli, basi itakuwa lahisi sana kwa mzee Soud kumsaidia, itaendelea…………..
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU