
BINTI MDUNGUAJI (68)

SEHEMU YA SITINI NA NANE
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NA SABA: japo kuwa akuwa ameafikiana na mama yake, Johnson aliaidi kufwata kama alivyoagizwa na baba yake, muda huo huo wakasikia muungurumo wa gari nje ya nyumba yao, na baada ya gari kuzimwa ikachukuwa dakika moja kumwona mzee Masinde akiingia ndani, endelea …….
“Hooo! Johnson ulikuja tena” alisema mzee Masinde huku akinyoosha kuingia chumbani kwake, pasipo kusubiri jibu la mwanae, maana alijuwa kuwa, tayari mke wake amesha mfikishia ujumbe mwanae, kuwa akutakiwa kuendelea kumfwatilia Michael Nyati, mzee huyu ambae alisha anza kupata matumaini ya kuendelea kuishi kwa amani, baada ya kukutana na mganga, aliingia chumbani kwake na kukaa huko huko, akikwepa maswali ya mwanae, ambayo aliamini kuwa leo yangekuwa mengi zaidi, mzee Masinde ambae alianza ujilahumu kwa kuto kwenda kwa mganga mapema alikaa, sana ndani ya chumba chake, akitega sikio kusikia mungurumo wa gari la polisi, ambalo leo alikuwa anatumia mwanae, baada ya gari lake pamoja na la yeye mzee Masinde, kupigwa mawe na wananchi wenye hasira kali, yakiwemo gari mengine mengi sana, ya watu mbalimbali, ambapo nusu saa baadae mzee Masinde akasikia mwanae akiaga na kuondoka zake ikifwatia muugurumo wa gari, kisha mke wake nae akaingia chumbani, “nimesha ongea nae, na amekubari, ila kasema ata kutafuta kesho” aliongea mama Johnson, huku akianza kuandaa mabegi yake kwaajili ya safari, ** Jackline akamtazama Denis ambae aliinuka haraka sana na kwenda kui chukuwa simu ya mke wake akaitazam kwenye kioo cha simu hiyo, akaona jina la mpigaji, “baba” akampatia simu Jackline, ambae aliipokea na kuongea neno moja tu! “shikamoo baba” kisha akaonekana kusikiliza simu na kuitikia mala chache, “ndio baba.. ndio baba… sawa ….. lakini hakuna tatizo ……” ilisikia sauti hiyo ya Jackline huku anainuka kitandani akiwa uchi kabisa, na kumwonyesha mume wake ishara ya kuwa anenda sebulenni kunywa maji, kisha huyooooo, Jackline akatoka nje ya cumba chao na kupotelea sebuleni, ** mzee Nyati au baba Jackline alikuwa anaongea na Jackline, akimsimanga kwa kutumia gari la Denis, kwenda kwenye mauwaji, maana mzee Huyu ambaae analifahamu vizuri gari lile aliliona wakati anatazama taalifa ya habari ya saambili,nakugunduwa kuwa ni gari la mkwe wake Denis, ambae amechangia kwa kiasi kikubwa sana kufanikiwa kwa mpango wake wa kulipiza kisasi, japo yeye mwenyewe akuwa anajuwa, Jackline alikili kuwa alifanya kosa, japo alimwakikishia baba yake kuwa akukuwa na tatizo lolote, pia baba Jack alimsisitiza mwanae kusoma hali ya uwanja, kabla ya kummaliza mzee Nyati, pia alimtaka kuwa mtulivu sana hasisababishe mauwaji ya aina yoyote yatakayo fahamika kuwa ameyafanya yeye, ** siku iliyo fwata Johnson baada ya kulipot kazini akaelekea msibani, ambako alikaa mpaka saa tano, muda ambao mwili wa Busungu uliagwa, na kusafilishwa kwenda kwao Dodoma, kisha Johnson akiwa na majonzi mazito alielekea nyumbani kwa baba yake, akizani kuwa atakuwa nyumbani akijificha, zidi ya risasi ya BINTI MDUNGUAJI, lakini akukuta mtu myoyote, mama yake na dada wakaazi tayari walikuwa wamesha safari kuelekea musoma, na baba yake akuwepo nyumbani, ikabidi ampigie simu, ilikujuwa yupo wapi, lakini baada ya simu kupokelewa, Johnson alikutana na maneno ambayo yalizidi kumchemsha kichwa, “Johnson sidhani kama tunakitu cha kuzungumza, zaidi mwanangu kaambali na swala hili, maana lita kupoteza duniani, mzee Nyati namfahamu mwanangu, mimi nitajuwa namna ya kujilinda” kisha mzee huyu akakata simu, baada ya hapo kila Johnson alipojarbu kupiga simu, aliambiwa inatumika, “dah! ameni block” alisema Johnson kwa masikitiko makuwa, kumbe wakati huo, Johnso anaangaika kumsaka baba yake mwenzie alikuwa ndani ya meli yake kilomita ishilini ndani ya bahari, ya hindi tokea pwani ya kilwa, akiongea na vijana wake akiitaji ulinzi zaidi, na kazi ya kumsaka mtu ambae atauchukuwa moyo wake na kwenda kuupeleka kwa mganga, kwakifupi vijana wake walisha wai kufanya kazi kama hizo mala nyingi sana, ikiwa ni matambiko ya kazi yao ya ualamia wanayo ifanya kule baharini, huvyo aikuwa shida kwao kumwelewa boss wao ambae alikuwa anawalipa vizuri sana, hivyo walikubariana kuwa wagawane majukumu, vijana wawili wakaondoka na na mzee Masinde, wakitumia speed bot ambayo ilimleta mzee huyo, wakarudi nchi avu na kuanda safari ya kuelekea dar, ** mkuu wa jeshi la polisi CGP, CHEF General Polis, aliwaita kwamalanyinge wakuuwote wa idara, zilizopo chini ya jeshi la polisi, ni baada ya kwenda ikulu na kukalipiwa vibaya sana na mkuu huyo wa nchi, nakutakiwa kuleta report ya kukamwata kwa muuwaji huyo, na kupatatikana kwa majibu ya vitendo vya kialifu vinavyo endelea nchini, CGP nae alitoa maagizo kwa wakuu wa idara hao, akiwa sisitiza kuwa anaitaji matokea mazuri kwa muda mfupi sana, alieleza kuwa nikitendo cha aibu mtu anae isiwa kuwa ni mwanamke tena mdogo sana, kufanya matukio ambayo yana lifanya jeshi la polisi kuoneka ni wazembe, akitolea mfano tukio la jana mahakani, CGP alisema “inawezakanaje, kwa mtuhumiwa aliepatikana na ushaidi wa wazi kabisa kushida kesi, inaonekana kunawenzetu washilikiana na warifu” aliongea CGP kwasauti ya ukari kidogo, kisha akatulia na kuwatazaa makamanda wake usoni, baadhi wakaonekana kutazama chini, wakijifanya kuandika andika kwenye vijitabu vyao, “maana katika report ya uchunguzi toka morogoro, imeonyesha ndani ya week hiyo moja huyu bwana anaejulikana kwajina la Carles Kijage ambae kwa sasa ni marehemu, alikuwepo mkoani humo akiongozana na gari hilo, ambalo lilikuwa linaendeshwa na dereva huyo huyo aliepata nalo hajari, ambae kwa sasa ni marehemu” aliendelea kuongea CGP akionyesha kuwa amekeleka sana na kitndo kile, haya sasa anakuja mtu form n were anatu saidia kuuwa mwalifu, maana anaona tumeshindwa kazi, sasa naagiza kitafutwe chanzo sahii cha mauwaji haya, na apatikane muuwaji mala moja” ** wakati huo insp Johnson mwenye kuvalia sale za kazi, alikuwa anasimamisha gari lake, nje ya nyumba ya mzee Soud, alipokelewa na watu wengi walijawa na furaha kwenye nyuso zao, wakionyesha kuwa walikuwa na taflija flani, kwani walikuwa wame kaa nje ya nyumba ya brigedia General mstaafu, chini ya vimvuli vya miti iliyo katiwa vizuri nakuonekana kama mapambo katika nyumbahii, kila watu wanne mpaka watano, walionekana kukaa kwenye viti na kuizunguka meza, huku mezani kukionekana vinywaji mbali mbali, kuanzia vinywaji laini, mpaka pombe, sahani za nyama choma, na ndizi za kuchoma zikionekana kwenye sahani juu ya meza hizo, huku alufu ya nyama hizo na ndizi, zikiendelea kusikika zikitokea jikoni nyuma ya nyumba ambako jiko kubwa lilionekana limefunikwa na mapaja ya mbuzi, “karibu mwanangu, karibu sana ujiunge na familia katika kuadhimisha miaka sitini na nne ya baba yenu” alikuwa mke wa mzee Soud ambae ndi alikuwa wakwanza kumwona Johnson, “sante sana mama, shikamoo” alisalimia Johnson, na wakati huo mzee Soud nae alikuwa anasogea pale alipo simama mke wake, na insp Johnson, “hoooo! bwana Masinde, karibu sana” aliongea mzee Soud ambae licha yakuwa leo ilikuwa ni siku muhimu kwake, ambayo akuwai kuwazia kabisa, akiongezewa na tukio la kuuwawa mfanyakazi wake wazamani, katika utumishi wa Jeshi la ulinzi, bwana Charles Kaijage, mzee Soud alionekana wazi kunyongea, ukweli akuwa na furaha kabisa, wakati huo alikuja binti mmoja akiwa na trey lenye grass nne, zenye vinywaji tofauti ndani yake, insp akachukuwa grass ya pombe kari, “asante mzee shikamoo” alssalimia insp kwa sauti kama ya mzee Soud iliyo jaa uzuni, marahaba kijana” aliitikia mzee Soud, kisha aamtazama mke wake, “samahani kidogo wacha sisi tuongee” hapo mke wamzee Soud akaondoka zake akiwaacha wakina mzee Soud na Johnson waki tembea taratibu kuli fwata gari la insp Johnson, grass za vinywaji vyao mkononi, “nimestuka sana kwa kilicho tokea jana” aliongea mzee soud, baada ya kulifikia gari la insp Johnson, na kuzunguka upande wa pili wa gari hilo, “hapo ndio naiona taswila ya baba, akiwa ametandikwa risasi” aliongea Johnson kisha akanywa funda moja la pombe kali kwenye grass, “hapa Johnson, huu sio wakati wa kukata tamaha, bado unayo nafasi ya kumlinda baba yako” aliongea mzee Soud, huku anamshika Johnson begani, “hipi tena mzee wangu?, nimejaribu naaskari sitini, ikawa kazi bule, nimeweka wapelelezi kila kona bado mauwaji yanaendelea, na mbaya zaidi, ata wapelelezi wenyewe nilio wategemea, wana uwawa kizembe kabisa, aliongea Johnson kwa sauti iliyo kata tamaha, “fwata maelezo ya mzee Nyati” aliongea mzee Soud, na Johnson aka inua uso wake kumtazama mzee huyu, “nitawezaje, ikiwa atakuniambia chanzo cha haya yote amekataa, atakubari kwenda kuongea kwenye vyombo vya habari?” aliuliza Johnson kisha akapiga funda moja la pombe kali, “nikuulize kitu Johnson, unazani utajiri wa baba yako nawenzake, unawenzake unaweza kuwa chanzo ya haya yote?” hapo Johnson akatoa macho kwa mshangao wa kiulizo, “hiyo ni kwaasilimia mia moja” alijibu Johnson, mzee Soud akatabasamu, “je uisha wai kujuwa chanzo cha utajiri wa baba yako?” aliuliza mzee Soud, akimtazama Johnson usoni, “yah! nafahamu, ni mchanganyiko wa hakiba ya fedha alizo kuwa analipwa kwa safari za nje, na zile alizolipwa baada ya kuacha kazi” alijibu Johnson kwa kujiamini, mzee Soud akacheka kidogo, kicheko cha mshangao, ambacho kilipingana na maneno ya Johnson, kicheko kilicho mshangaza Johnson, “si unazungumzia fedha alizo weza kuanzishia biashara anzo zifanya hivi sasa?” aliuiza Johnson kwa tahadhari, na mshangao, akijuwa kuwa lipo anlolijuwa mzee Soud, “sikia kijana, kwa miaka ya 1988, brigedia general alie staafu kwa umri, alilipwa laki nne, na kwasafai moja ya nje walilipa elfu themanini, na kwa safi ambazo walisafiri wao, , na ukizingatia walistaafu kabla ya muda, pengine mwenye malipo makubwa alikuwa baba yako kutokana na cheo alicho kuwa nacho hivyo alilipwa si zaidi ya elfu hamsini, wakichanganya mishara yao, ya miaka yote ya utumishi, wasinge weza kufikisha ata millioni mbili, fedha ambayo wenge weza kujenga nyumba yakawaida, au kununua gari moja tu!” Johnson aka duwaa, huku akiuona ukweli unamjia kichwani kwake, “kwahiyo mzee Soud unamaanisha kunakitu walikipata huko congo, nandio kilicho sababisha haya yote, nadio sababu ya wao kuacha kazi mala moja” aliongea Johnson huku akimtazama mzee Soud, na grass ya pombe ikiwa mkononi mwake, imebakia karibia robo tatu nzima, “nasiyo kuacha kazi tu, ila kuibuka majiri wa kutisha” aliongea mzee Soud, kwa kulikoleza swala lile, “inawezekana ikawa ni kitu gani wali kipata huko, na kwanini Nyati, aliwakimbia wenzake?” aliuliza Johnson, akimtega mzee Soud, akizani kuwa mzee huyu anafahamu kila kitu, lakini anamficha, “na kwanini Nyati huyu huyu, alie watoroka wenzake, anataka kuwa uwa?” aliongezea swali mzee Soud, Johnson akaduwaa, maana jibu lililo mjia ni kwamba “pengine alizurumiwa, nandio maana mpaka sasa maisha yake bado ni duni” aliongea Johnson, akivuta swila ya maisha ya mzee Nyati wenye nyumba ya udogo, mzee Soud akacheka kidogo, “umekosea, Nyati hayupo kama unavyo zani, Nyati nitajiri mkubwa sana, naweza kukuambia kuwa utajili wa baba yako pengine unaweza kuingia mala mia na zadi kwa utajiri wa bwana Nyati” aliongea mzee Soud na kumshangaza Johnson, akahisi huyu mzee amechanganyikiwa, lakini akaanza kuvuta picha ya mwonekano wa mke wa Nyati na mazingira ya kule shamba, akaona kuna utofauti mkubwa sana, pia akakumbuka jinsi walivyo toa million mbili kuchangia walemavu, alafu akakumbuka jinsi alivyo mwona Jackline akiwa na gari jingine, na mzee Nyati akiwa na gari jingine la gharama zaidi, hapo Johnson aka tikisa kichwa kukubari, “sasa anataka nini kwa wazee awa?, kama anafedha kiasi hicho?” aliuliza Johnson, “sidhani kama ujaelewa kuwa Nyati anatafuta roho zao tu!” aliongea mzee Soud Hassan akigeuka na kutazama kule waliko jaa watu, waliokuwa wanaendelea kupata vinywaji na nyama choma, akamwona mke wake anakuja na grass nyingine mbili mkononi, zikiwa na vinywaji, moja juice na nyingine pombe kali, Johnson aka igugumia ile pombe kari, mpaka ikaisha yote, kisha huku anakunja sura kwa ukari wa lile pombe, akapokea grass nyingine toka kwa mke wa mzee Soud, ambae baada ya kuwakabidhi vinywaji wawili awa, akaondoka zake, “kwahiyo mzee unanisaidiaje?” aliuliza Johnson, kisha akapeleka grass mdomoni mwake na kugonga funda moja kubwa, “kijana cha kukushauri hapoooo, endelea kumwekea ulinzi wa siri baba yako, huku ukijaribu kumshawishi afwate maelekezo ya Nyati, japo umesha chelewa” wakati huo huo simu ya insp Johnson ikaita, akaitoa mfukoni na kuangalia, “mama yangu, ni CCIDP” alionge Johnson huku anaigugumia ile grass ya pombe kali, na kuimaliza yote, kisha akamkabidhi mzee soud, “tutaonana zee wacha nielekee huko” aiongea Johnson huku anaingia kwenye gari nakupokea simu, huku analiwasha wagari lake, “ndiyo afande …… nipo njiani nakuja afande, nidiyo afande, nimepata bahadi ya mambo yakayo tusaidia katika upelelezi” aliongea Johnson huku akiliondoa gari kwa speed kari sana, kiasi cha watu wote waliokuwa wanashrehekea birth day ya mzee Soud kushangaa, ** saa limoja baadae Johnson alikuwa ndani ya ofisi ya Chif CID Polisi, akita report yake na ushauri, na yeye akipewa jukumu kama lilivyo agizwa na CGP, report ya Johns oleo ilimflahisha sana mkuu huyu wakitengo cha upelelezi, ni baada ya Johnson kueleza mambo mengi sana na njia ya kumnasa muuwaji, Johnso akiwa amewonyesha video iliyo patikana kwe camela za usalama pale wajasiliamari, zilizo mwonyesha mwanamke anae shukiwa kuchukuwa uhai wa Busungu, akiwa natoka kutekeleza mauwaji ya mzee Kijage, pia alitumia nafasi hii kumtambulisha mzee Masinde, kuwa ni mmoja wawatu wanao takiwa kuuwawa, Johnson ambae aliona kuwa hiyo ndiyo njia pekee ya kumwokoa baba yake, akashauri kuwa mzee huyu ambae anakila dalili ya kuwa nimmoja wao awekewe ulinzi mkubwa na mkali, tena wasiri, ambao utasaidia kumkamata kila atakae kuwa anamfwatilia mzee huyu, “ndio maana najivunia sana kuwa na wewe mahali hapa” aliongea mkuu wa upelelezi, ambae alikuwa anamfahamu vyema mzee Masinde, sababu alishawai kukutananae mala kwa mala, na kumsaidia kwenye maswala yake ya kupindisha sheria, “ok! kibari kimetolewa chagua aina na idadi ya askari ambao utaona wafaha kufanya hivyo” aliongea CCIDP, akitegemea kusafisha jina lake baada ya kuanza kuchafuka, ** naikawa hivyo, askari kumi wenye uwezo mkubwa wakimapigani, ambao walitumia gari na nguo za kiraia, kumfwatilia mzee Masinde kila sehemu, wakiwa na silaha aina ya smg, wakihifadhi kwenye magari mawili ya kiraia, waliyo kabidhiwa kwa kazi hiyo, na ndani ya nguo zao za kiraia, walikuwa wanavalia vazi maalumu la kuzuwia risasi, yani bullet proof, walimfwatilia mzee Masinde kila alipoenda, nakila alich fanya, huku wakigunduwa kuwa, mzee huyu anawalinzi, na mala zote alikuwa anapenda kunywa pombe kwenye bar za jirani na nyumbani kwake, akikamata mabinti warembo na kuwasogeza nyumbani kwake, ambako alienda kuwa ingizia dudu, licha ya kunduwa mahovu ya mze huyu, asa ya bishara yake ya uko baharini, lakini walifwata maelekezo yakuwa wasi mkamate mzee huyu juu ya makosa yake, ila wamtazame mtu anae mfwatilia mzee huyu, ndie anaestahili kukamatwa, lakini licha ya siku kuyoyoma hapakuwa na mafanikio wala dalili ya mafanikio, ** nyumbani kwa Denis mambo yalikuwa yanazidi kupamba moto, mapenzi yake na mkewake Jackline ungesema wanakutana leo, siku zote walionyeshana mapenzi moto moto, huku wakianzisha ratiba ya kutoka kila juma moss, huku Denis akizidi kumnunulia mke wake nguo nzuri na mala chache akimshauri kwenda saloon kusuka nywele zake ambazo zilizidi kuwandefu na kupendeza, mtoto wao Johnson alikuwa amebakiza siku chache kutimiza mwaka mmoja nanusu, sasa alikuwa anatembea na kukimbia kabisa, huku akiendelea kumung’unya maneno, na kilicho mshangaza Denis, kitendo cha France kupenda sana michezo ya ngumi, juma moss moja, saa nane mchana, Denis akiwa na familia yake, ambao walipanga waende kutembea mjini, kisha kutafuta sehemu nzuri wa furahie siku, ** wakiwa ndani ya chumba cha mahabusu, cha kituo kikuu cha polisi, Denis na mke wake, alie fungwa minyololo mkononi na miguuni, Denis alimkatiza mke wake, “subiri kwanza mama France, nazani akija huyo Johnson hapa, anaweza kunifukuza, ebu chukuwa kabisa hivi vitu” aliongea Denis, kwa sauti ya chini sana, akimwambia mkewake, ambae siku zote alikuwa akimsifia wazi wazi, huyu mwanamke muuwaji, pasipo kujuwa ni mkewake, huku anaweka vinganja vyake kwenye viganja vya Jackline, kisha kwasiri kabisa, aka mkaabidhi kile kidude kama kishikizo, na kile kikaratasi kidogo kilicho fungwa, Jackline akavipokea huku akitazama kushoto na kulia, ambapo aliona Askari mmoja amewakazia macho, “ok! nieleze haraka haraka, jinsi ulivyo mpata huyu wameisho, maana France nae akichachamaa huko hapata kalika” aliongea Denis kisha Jackline aka tabasamu kidogo, “lakini usije ukanikimbia kwa uoga” aliongea Jackline kwa utani wote wakacheka, “nazani unakumbuka ile juzi, tulipofika mbezi tukakuta kunafoleni na msongamano wa magari, tukaamua tupitie kinyelezi” alikumbusha Jackline, Denis akaitikia kwa kichwa, kukubari kuwa anakumbuka, maana ilikuwa ni sikutatu tu! zimepita toka siku hiyo, basi ikawa kama bahati hivi, tulipo pata pancha pale kinyerezi mwisho” aliendelea kusimulia Jackline ****jumamosi hii mzee Masinde alikuwa ndani ya bar moja changamfu sana pale kinyerezi mwisho, akiwa pamoja na vijana wake wawili, akiendelea kupata kinywaji, sambamba na walinzi wwake hao, huku macho yake yakipepesa huku na huku kuona kama kuna uwezekani wa kupata mschana wa kwenda kulala nae, wakati huo huo, polisi kumi ambao walikuwepo kwenye eneo la bar hiyo, wachache wakiwepo ndani ya bar ile ile aliyopo mzee Masinde, na wengine walikuwa kwenye bar za jirani, wakitega macho na asikio kusikia au kuona lolote litakalo tokea kwa mzee masinde aku kumwona nyemelezi yoyote, mala likaonekana gari moja aina ya Toyota Noah liki simama pembei ya bar ile, akashuka kijana mmoja mtanashati na kuanza kukagua tairi, likionekna wazi kuwa lilikuwa lina pancha, mala akaonekana mschana mmoja mrembo sana akishuka toka kwenye lile gari, akiwa amemshika mkono mtoto anea jitembeza mwenyewe, na kuingia kwenye ile bar, macho ya wote yalielekea kwa mrembo huyo, yakiwemo macho ya mzee Masinde, “yes, leo nitafaidi” aliwaza mzee Masinde, ambae alikuwa amebakiza siku moja tu! kupeleka moyo wa binadamu aliemuuwa kwamkono wake, itaendelea…….

