BINTI MDUNGUAJI (74)

SEHEMU YA SABINI NA NNE

 

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TATU : wakati ana mfunga minyololo kwenye miguu na kuiunga nisha na mikononi, utani wa insp ukaonyesha kumpendeza Jackline, maana alitabasamu kidogo, kisha akamtazama insp aliekuwa anamalizia kumfunga minyololo, na kulifunga gate lenye nondo kubwa za mm 20, “asante sana, insp Johnson, kwa kunikaribisha chakula, naomba kiwe cha kesho jioni, nyumbani kwako” endelea ………

kiukweli ata kama ungekuwa wewe, ungezani kuwa Jackline ni taahila, kwa maneno aliyo yaongea mbele ya insp, ambae aliona kuwa mwanamke huyu amesha changanyikiwa, hivyo akaondoka zake, mpaka mapokezi, “maagizo hakuna mtu yoyote kumwona huyu shetani zaidi, kuna mtu mmoja tu! mume wake, ambae nae atarhuhusiwakumwona malamoja tu!” aliongea Johnson, kisha akatoka nje ya kituo hicho, akachukuwa gari moja la polisi na kueleka Hospital, wakati huo wakubwa wake walikuwa wamesha ondoka zao, ** usiku ule insp alienda mpaka hospital kuu ya muhimbili, akaelekea kwenye chumba maalumu cha wagonjwa VIP wadharula, ambako aba yake alikuwa amelazwa, nje alikuta walinzi wa polisi, wakiwa na silaha zao, na mavazi maalumu ya kuzuwia risasi, wakamsalimia kijeshi kwa kumpigia saluti kisha yeye akaingia ndani ya chumba hicho alicho lazwa baba yake, ambae alimkuta akiwa amesha patiwa matibabu na ikiwepo kufanyiwa operation ya kuziba sehemu alizo chomwa na visu, na kushonwa sehemu ilipo katwa dudu yake wakiakikisha tundu la mkojo likiwa wazi, na sasa alikuwa amelala kimya, huku amefunikwa shuka mpaka kifuani, kwamacho tu! alionekana kupua, kama mtu alie lala, usingizi wa kawaida, “bado kaputi aija isha, mpaka asubuhi atakuwa amesha rudiwa na fahamu” ilikuwa nisauti ya mhuguzi mmoja wakike, aliekuwa mle ndani ya chumba kile, pasipo kusema kitu insp akamtazama baba yake, kwa dakika kadhaa, kisha akaongea kwa kunong’ona, nimejitaidi kadiri ya uwezo wangu, lakini amekupata, ila baba taalifa njema nikwamba, nimesha mkamata, ato kusumbua tena” yule muhuguzi alikuwa amesimama oembeni akimtazama insp kwa macho ya huruma, “samahani kaka polisi, huyu mzee umesema ni baba yako” hapo insp aka geuka na kumtazama yule mhuguzi, akaitikia kwa kichwa, akijitaidi kuzuwia machungu na hasira ya wazi, aliyokuwa nayo, “ok! dada nita kuja kesho mapema sana” alisema insp Johnson huku akitoka nje na kuacha maagizo kwa walinzi wadumise ulinzi, nakwamba watapokelewa na wenzao, kesho mapema, kisha akaondoka zake kuelekea nyumbani kwake mbezi beach, ** siku yapili saa kumi na mbili kamili, lisaa limoja kabla Denis ajafika pale kituoni, kukutana na Jackline mkewake, insp Johnson aliingia kwenye kituo cha polisi, na kupitiliza moja kwamoja kwenye chumba cha mahabusu, cha magaidi, ambacho leo hii alkuwemo Jackline Nyati, akamkuta mschana huyu akifanya zoezi ya push up, licha ya kuwa alikuwa amefungwa mivyololo mizito lakini dada huyu mrembo alionekana kipiga push up kwa speed kari sana ata baadhi ya askari wake wasingeweza, “karibu insp tupate chai” aliongea Jackline, huku akiendelea kupiga push up, mfululizo, akionyesha kuwa alikuwa amenza muda mrefu, maana mwili wake, ulikuwa ume lowa jasho sana, na majasho mwengine kudondoka chini na kulowesha sakafu, utazani pame mwagiwa maji, kitendi kile kili shangaza insp Johnson, ambae akutaka Jackline ajuwe, kuwa ameshangazwa na kitendo kile, “naona unajiandaa kwenda kupambana na wakina chilumba, huko kuzimu” aliongea insp kwakejeli, “insp kazi ya kuni liwaza kwa maneno kama hayo, ni ya mumewangu, siyo wewe” aliongea Jackline kwa lengo la kumwondoa hapo insp Johnson, ili kusiwepo na kikwazo chochote endapo Denis atakapokuja, na kuitajai kuingia, insi akacheka kidogo, “hahahaha, Jack bwana, umesahau kuwa wewe ni mwanafunzi mwenzangu?, yakwamba tullisoma wote” aliongea Johnson akimkumbusha Jackline sikulile aliyo mkuta nyumbani kwake, yupo na mke wake, hapo Jackline aka jifyetua kwa wepesi sana, akasimama, na pinguzake mkononi, aka kumsogelea insp, kisha wakasimama wakitenganishwa na gate la nondo, “insp mimi siyo muhimu kwako, achana na mimi, muwai baba yako hospital, pengine akakueleza machache ambayo akuwai kukueleza, pia msaidie kuficha ushaidi wa yule mwanamke kahaba, wa hotelini, waliotaka kumchinja” hapo insp akaduwaa, kama ameuona mzimu, kisha Jackline akarudi pale alipo kuwa anafanya mazoezi, kisha akasimama kidogo na kumtazama insp, “mengine tutaongea kwenye chakula cha jioni nyumbani kwako” hapo insp akaona Jackline bado amechanganyikiwa, akaondoka na kuelekea mapokezi, “sitaki mtu yoyote akutane na huyu gaidi, zaidi wale walioandikwa kwenye horodha tu” alisema insp kwa ukari, na kuondoka zake kuelekea hospital ya muhimbili, kumwona mgonjwa, ** baada ya Deins kukutana na baba yake Jackline, ambae alimtambua kuwa ni mzee alie mwona malambili, siku ambayo Jackline alisukuma meza yao kwa bahati mbaya, na siku yapli yake, ambayo Jackline alikuwa ameshikwa na uchungu wa ghafla, wa kujifungua mtoto wao wapekee, akapewa vile vitu viwili yani unga mweusi, na kishikizo kilicho viligiwa kitambaa, kisha wakaachana maeneo ya fire, yeye akaelekea kaliakoo, kilipo kituo kikuu, na gari aina ya Toyota v 8, likakata jushoto na kulekea upanga, ** Denis alimtazama mke wake, kwa macho ya mshangao mkubwa sana, kama vile anasema ‘watakunyonga mke wangu’ “Denis, nazani mpaka hapo, nazani umenielewa, mimi ni ninani, na kwa nini nilifanya hayo yote” alisema Jackline huku akiifadhi vizuri zile vitu alivyo pewa na Denis, Denis akaitikia kwakichwa, huku akitazama kushoto na kulia, kuwatazama watu wngine waliokuwa wanaongea na mahabusu, “Denis mpenzi wangu, ulisema unampenda BINTI MDUNGUAJI 🔫🔫 siyo?” aliuliza Jackline akimtzama Denis usoni, huku ameachia tabasamu, Denis nae aliekuwa analngwa lengwa na machozi, akatabasamu huku anaikia kwa kichwa, “kwa hiyo unazidi kuni penda mume wangu sindiyo?” aliuliza tena Jackline huku akimkazia macho mume wake, “Jackline, unafahamu kuwa sina mwanamke mwingine ninae mpenda zaidi yako, sasa unazani nitaishije bila wewe, siwata ….” alishindwa kumalizia Denis akaanza kuachia kilio cha kwikwi, “Denis mume wangu si umkuja kuni toa mahabusu, sasa kwanini unalia, awawezi kuninyonga” aliongea Jackline kwa sauti ya chini sana, hapo Denis akakata tamaa yamaisha kabisa, ni baada ya kusikia maneno hayo ya mke wake, akahisi mke wake amesha changanyikiwa kwa kuhofia kunyongwa, Denis akazidi kuangua kilio cha chini chini, “Denis mume wangu unawasi wasi gani?, ebu nyamaza bwana, leo tutakuwa wote usiku” Denis alimsikia Jackline akiongea maneno kama chizi, kwa sauti ya chini, akionyesha msisitizo, sasa baada ya kulia Denis akaangua kicheko kilichoambatana na uchungu, mkubwa sana, uchungu ambao ulimfanya Jackline ayahisi mapenzi makuwa aliyo nayo mume wake, juu yake, “usijari mama kweli, leo tutakuwa wote” alisema Denis akiendelea kucheka kwa uchungu kubwa sana, uku akimtazama mke wake, ambae alimtazama kwa tabasamu, huku akipeleka mikoni yake, mdomoni mwake na kuwa maka ana ficha tabasamu lake, kisha akaitoa mdomoni ile mikono yake iliyo fungwa kwa pingu, na kuisiogeza kichwani kwake, akajikuna kidogo kwenye nywele zake alizo zisuka jana, hapo ndipo Denis alipo elewa kinachoendelea, ni baada ya kuona mke wake akipachika kile kishikizo kwenye nywele zake, hapo Denis akamtazama Jackline usoni, Jackline akamkonyeza kimahaba, kwa jicho la upande, “jiandae leo unipe kama juzi” aliongea Jackline kwa sauti ya kunong’ona, akiachia tabasamu huku midomo yake ikicheza cheza, akionyesha kuwa anatafuna kitu flani, “haya kijana muda wa umekwisha, Jackline Michael Nyati, anaitajika kwa mahojiano na wakuu, ikiwa ni kuonyeshwa kwa waandishi wa habari” ilikuwa ni sauti toka pembeni yao, wote wakaangalia upande uliookea sauti hiyo, wakawaona polisi saba, wakiwa wamesimama pembeni yao sita wenye siraha wakiwa wamesimama atuwa tano, toka walipo kaa wao, alafu mmoja asiyekuwa na bunduki, alikuwa karibu yao kabisa, akionekana kuwa navyeo vikubwa mabegani kwake tofauti na yule aliye kuja kumkamata jana, huku akitikisa fimbo yake ya kipolisi mkononi mwake, hapo Denis akamtazama Jackline kwa macho ya kweheri, akamwona akimalizia kumeza kile alichokuwa anatafuna, Jackline kama limwelewa mpenzi wake, “nenda kaandae mvinyo mume wangu, usiku wetu utakuwa mzuri sana” aliongea Jackilene kwa sauti yachini, huku akiiweka mikono yake juu ya magoti ya Denis, ambae alikuwa anainuka taratibu, na kwa unyonge wa hali ya juu sana, “askari mchukueni,” Denis alisikia amri ikitoka kwa yule asfisa wapolisi alie simama karibu yao, hapo nikitendo bila kuchelewa, haraka sana wale polisi sita wali msogelea Jackline, na wawili wakamshika huku na huku na kumnyanyuwa toka kwenye kiti alicho kwa amekalia, kisha wakaanza kutembea nae kutoka nje ya kile chumba wawili wakiwa mbele, na wawili nyuma, huku wakiwa wamekata silaha zao vyema kabisa, wakiwalinda wale wawili walio mshikilia Jackline, aliekuwa anatembea kwa shida, Denis akatoka nje ya chumba kile na kuelekea mapokezi, akiwa na mawazo mengi sana kichwani mwake, akiamini kuwa, swala la Jackline kuchomoka kwenye mikono ya polisi lilikuwa ni ndoto, “weee kijana ebu njoo hapa?” ilisikika sauti kari ya polisi wakike toka nyuma yake, Denis akajuwa na yeye anaendwa kuunganishwa na mkewake, akasimama malamoja, huku mwili una mtetetmeka utazani ame simama mbele ya simba mnyama itaendelea …..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!