BINTI MDUNGUAJI (75)

SEHEMU YA SABINI NA TANO

 

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA NNE: “weee kijana ebu njoo hapa?” ilisikika sauti kari ya polisi wakike toka nyuma yake, Denis akajuwa na yeye anaendwa kuunganishwa na mkewake, akasimama malamoja, huku mwili una mtetetmeka utazani ame simama mbele ya simba mnyama, endelea ………..
“wekaka mbona unapitiliza, umeshau kama umemwacha mwanao hapa?” ilisikia tena ile sautiya kike, hapo Denis akashusha pumzi nzito, akarudi haraka sana pale mapokezi, “asante sana dada tangu” aliongea Denis akimchukuwa mwanae, ambae alikuwa anashangaa shangaa, asijuwe kinacho endelea, “we! jifanye umechanganyikiwa tu!, tena shukuru na wewe ujausishwa kwa kukaa na gaidi” aliongea yule polisi, wakati huo Denis akusikiliza lolote, “mama ileeee” alisikika France aliekuwa amebebwa na baba yake akitazama Yuma, yani wanakotoka, Denis akageuza shingo na kutazama nyuma, hapo yeye mwanae wakakutana uso kwa uso na Jackline, aliekuwa anapitishwa kwenye kolido, na kuingizwa kwenye ukumbi wa mikutano, huku tabasamu likiwa lime chanua usoni mwake, France akapunga mkono kwa mama yake, ambae ali endelea kutabasmu, mpaka alipopotea, akisindikizwa na polisi sita, wenye silaha, ile Denis ana tokeanje ya jengo la polisi, akakutana na waandishi wengi wa habari, waliokuwa wana subiri kuingia ndani baada ya mahojiano ya kwanza yanayo mhusu mwanamke huyu gaidi, kuisha, ndipo wao waliokuwa wanatamani kupata picha ya mwanamke huyo hatari, wata ingia ndani kwenda kuiga picha, bahati nzuri wanahabari awakumtambua Denis kuwa ni mume wa Jackline Nyati, hivyo Denis akatiza kwenye kundi la wanahabari, walio kuwa na vyombo mbali mbali vya kuchukulia tukio hilo, na kuelekea kwenye gari lake, aina ya Toyota noah, akafungua milango na kuingia ndani, akampigia simu mzee Nyati, “ndiyo baba tayari nimesha toka,” aliongea Denis kwa sauti ya knyinge sana, iliyo ambatana na simanzi, “ok! sikiliza sasa, tafuta sehemu nzuri, maeneo ya karibu na muhimbili, ukae na mtoto apate chai, usizime simu nitakupigia, kama ukiweza kunywa bia uzembe ukutoke” aliongea mzee Nyati kisha wakakata simu, Denis akaondoa gari, wakiifwata barabara ya kuelekea muhimbili, sasa France alikuwa macho, “mama kowapi?” aliuliza France, aliekuwa amekaa kwenye seat ya mbele, “atakuja baadae” alijibu Denis, huku akihisi kama kitu flani kikimkaa kwenye koo na kutamani kuachia kilio, “baba! baba! polishi” alisema France ambae alionekana kutaka kujuwa mengi zaidi, ** leo mitaa ya jiji la dar salaam watu wote walikuwa wanazungumzia kukatwa kwa chana hatari sana, alie nyofoa roho za watu wengi sana, na habari kubwa ilikuwa ni tukio la jana, na jinsi alivyo poteza maisha ya polisi wengi sana, huku kivutio kikubwa ikiwa ni habari ya mzee alie katwa sehemu zake siri, na kuchomwa visu vingi sana, “lakini bado mzima huyu shetani, uta kuwakazi ya kwanza ya Jack” aliwaza alisema mzee Nyati, ambae alikuwa amekaa seat ya pembeni ya mke wake alie kuwa anaendesha gari, huu mzee uyu akisoma gazeti, sijuwi Michael Nyati na mke wake, walikuwa wanafwata nini hapa hospital ya muhimbili, maana waliingia nagari lao taratibu, wakatiza kwenye gate kubwa la kuingilia magari, ambapo pasipo kukaguliwa, walipewa card ya maegesho ya magari, ambapo walipitiliza, na kwenda kusimama nje ya jengo kubwa lililo andikwa emergence, wakalipita kidogo na kwenda kusimama kwenye maegesho ya magari ya madoctor, mda wote mzee Nyati alionekana kuwa makini sana, akifwatilia sauti iliyo kuwa inasikika toka kwenye kispeeker kidogo alicho kifaa kwenye sikio lake la kushoto, (hear phone), mama Jack naomba uwe makini sana, kwani kosa moja tu! tuta mpoteza Jack” alisema mzee Nyati, akimtazama mke wake, “ondoa shaka mume wangu, sipo tayari kumpoteza Jack” alisema mama Jack, huku akiuvua mfuko mmoja mkubwa toka seat ya nyuma ya gari hilo, na kutoa koti moja jeupe, la kidoctor, akalivaa, “vipi nime pendeza hen?”aliuliza mama Jack, huku aki jitikisa kidogo, “bado uja pendeza, ukiwa na hii ndio utapendeza sana” aliongea mzee Nyati akimkabidhi mke wake kibeji flani cha plastiki cha kona nne chenye kamba ya kuvalia shingoni, maandishi ya utambulisho pamoja na picha yake, mama Jack, au Anitha, aka kipokea na kukivaa shingoni, kisha akafungua mkebe wa kwenye dash board, akatoa kichuma flani kinacho fanana na funguo lakini akikuwa na meno, ila kilikuwa na kitufe chekundu, kwenye mshikio wake, akakiweka kwenye mfuko wa lile koti, pia akachukuwa bastora na kuiviligia kwenye kitambaa cheupe, akiwa amesha ikagua na kuakikisha kuwa ina risasi, mwisho aka chukuwa maji yaliyopo kwenye kifuko cheupe cha plastic, (drip) akakiweka kwenye mfuko wapili wakoti lake, mzee Nyati allafungua mke uliopo mbele yake, kwenye dash bord na kutoa Bp Machine, akampa mke wake, ambae iitundika shingoni, kama wafanyavyo madoctor wenyewe, hapo sasa umependeza, alisema mzee Nyati, “ok! baba kazi kwako, mlinde mkeo na mwanao” alisema mama Jackline, kisha akafungua mlango na kutoka nje ya gari nakufunga mlango, akimwacha mzee Nyati peke yake, ambae ali shuka toka kwenye gari na kuamia seat ya nyuma ya gari, akapeleka mkono kwenye sakafu ya gari na kuibuka na begi dogo jeusi, lile lile alilokuwa anatumia Jackline, akaanza kutoa kifaa kimoja baada ya kingine cha mugnum sniper rifle, na kuiunganisha, kumbe basi, mzee Nyati na mke wake, waliingia Dar es salaam, mapema sana, saa kumi na moja kasoro, wakitokea Songea, kwakuwa alikuwa anapajuwa nyumbani kwa Denis wakaenda moja kwa moja na kusimamisha gari mita mia toka kwenye nyumba hiyo, wakichunguza kama kuna mtu alikuwa ana ichunguza na kuifwatilia nyumba hiyo, lakini aikuwa hivyo, wakatulia ndani ya gari lao mpaka walipo mwona Denis anatoka na gari lake akiwa na France, ndipo mzee Nyati, mbae alisha wai kuja maali hapa na kujuwa ifadhi ya Jackline ya silaha, akaingia kwenye sehemu ya kuegeshea gari, na kuchukuwa begi dogo Jeusi, ambali polisi walifanya kosa kubwa sana kuto kuli ng’amua lilipo, nandipo walipo anza kumfwatilia Denis, kwakutumia simu tracking, kupitia simu ya Jackline ambayo kwa sasa alikuwa nayo Denis, wakiwa tayari wamesha panga jinsi mchezo utakavyo kuwa, mzee huyu aliendela kufunga silaha hiyo huku macho yake yakiwa kwenye mlango wa jengo la hospital, na msikio yake kwenye hear phone, ** ndani ya chumba cha mikutano Jackline Nyati alikuwa amesimamishwa mbele ya wanadhimu wakuu wa jeshi la polisi, walioongozwa na mkuu wajeshi hilo, CGP, ambae kabla ajaongea lolote akatazama huku na huku ni kama aliona kuna mtu muhimu amepungua, akamnongoneza kamanda mkuu msaidizi, “mbona yule insp simuoni tena” hapo makamu aka mnong’oneza mkuu wa upelelezi, akimwulizia kuhusu Johnson, ndipo zilipo anza kupigwa simu kumwulizia mtu huyu, muhimu alie fanikisha zoezi hili na kulipatia heshima na sifa jeshi la polisi, licha ya kupigiwa simu lama kdhaa, lakini akupokea simu, wanadhimu wakaingiwa nawasiwasi, akatumwa mtu kuulizia mapokezi kama kuna taalifa yoyote, wakati huo Jackline alikuwa amesimama kati kati ya ukumbi hule, akiwatazama makamanda wakuu wajeshi la polisi, lakini kichwa chake alikitazamishia chini, pande zote polisi sita wenye silaha kali, walikuwa wanamlinda, mala yule alie tumwa mapokezi akarudi, akaenda kumnong’oneza kamanda mmoja wapolisi, nao makamanda wakanong’onezana, kisha ujumbe ukamfikia CGP, “anaenda kufanya nini Hospital, wakati kazi yake imesha kwisha, ebu fanyeni kilalinalo wezekana, kwenye kikao na waandishi awepo” aliongea CGP, kwa sauti ya ukari sana, hapo mkuu wa kitengoo cha upelelezi akainujka na kutoka, akaagiza pale mapokezi itafutwe namba ya simu ya askari aliepo kule muhimbili, kati ya wale wanao fanya ulinzi kule, kisha waongee na insp Johnson wamwambie aripot haraka sana pale kituo kikuu, baada ya kukamilika hayo ndipo wanadhimu walipo kumbuka uwepo wa Jackline Nyati pale mbele yao, wote wakamtazama yule mwanamke alie tikisa nchi, kitu cha kushangaza wakamwona mwanamke huyo akitokwa na jasho jingi sana, mwilini mwake, wote wakashangaa, “jamani nini kinamtokea huyu mwanamke?” aliuliza CGP, kwamshangao mkubwa sana, akuna alie jibu, zaidi walimkodolea macho na kumwona binti huyu akianza kuishiwa nguvu, na kuregea kabisa, kishaa kubwaga chini kama kiroba, huku akijitaidi kuinuka tena na kushindwa, “ebu waini haraka mkamtazame huyo mwanamke, isije kuwa amekula sumu” alipiga kelele CGP, akimaanisha kuwa isije kuwa Jackline ametumia mbinu za kijasusi, za kujiuwa kwa sumu, akikwepa kutaja wausika wenzake, itaendelea………

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata