CONNECTION YA BALTASAR (03)

SEHEMU YA 03

“Eh.ehee nipokee ili iweje hela umetoa  wapii,Huna kazi huna badhi kazi yako  kulala tu nakula hayaa nambie  hiyo hela umetoa wapi Dinaa kama umeanza michezo michafu Dina nakukata hilo kojoleo lako mbwa wewe hivi unanielewa??’

“Jamani mamaaaa!!!”

  “Jamani Ng’ong’oooo ,Nyooo!!!”

  😔😔Niliamua kuingia zangu tu ndani kwa hasira yaan mama yangu hana hata shukrani  kila siku ananitukana mie kazi yangu kula na kulala nimeferi Form four, ananiita mie mmbea naweza hiyo kazi tu 

Mtaa mzima wanajua mie  nilipata zero mama yangu hajui kuongea taratibu  hapo penyewe mtaa mzima wamejua kama mie nimeleo nimenunua mihogo kwa hela ya kuhongwa mama akaikataa ile mihogo  ..

    Nikajitupa zangu kitandani  nikachukua simu nikawasha data , vimeseji vijaingia kwa kuongozana nilipo fungua ni yule Kaka wa jana alie nitumia video anatumia jina la Mussa shango
 
(Hujaamka tu mrembo)

(Uko poa)

(Siku njema)

Mmmh🙄nikasema huyu kaka nae vipi mbona kama ananishaukia, nikaingia kutazama Profile yake , hakukua na picha hata mojaa 
Mmh nikasema hapa si ndio watu wanakutanaga na majini jamani  naskiaga story  za majini hivi hivi

  Nikaachana nae nikaendelea kusaka habari za Mr Mianne , mama akaingia ndani

  “We Dina ,Umetoa wapi hela ??”
  Yaan mama yanguuu😟😟😟khaaa!! 

“Mi nikajua yameshakwishaa?? Daaah ?”

“Yanaishajee??”

  Yaan huyu mama yangu Amekuwa ananikagua mie tangu mdogo mpaka najielewa , kila siku kunipachua chupi ananikagua  kama nimeanza wanaume mama yangu ni mkaliii , sijawahi kumzoea japo mimi ndio kipenzi chake lakini nikileta ujinga weeh nafumulia mie kama hanijuii , Yaan hapa huwezi amini tunagombania   mihogo ya elfu mbili na sukari robo jamanii🙌🙌🙌

  Mama yangu ana maisha magumu sana lakini sio wa kutegemea mtoto wake  wa kike zaidi wa kiume  , kaka yangu ndio huwa anatutetea nyumbani kwa vitu vyote kula hata mimi shule ,japokuwa na yeye bado anajitafuta huko …

  Mama katuzaa wawili tu mimi na kaka yangu yeye yupo mkoa mwingine anajitafuta

Elfu tatu tu na chench inarudi lakini imekuwa kesi ya jinai , hapa mama kawa mbogo mie nilijua atafurahi mana hatukuwa na ratiba ya tunakula nini asubuhi  nina uhakika mama amelala na hela yake ya mtaji tu wa mkaa na sio ya kulaa lakini ona anavyonichamba …

“Bwana mama me sijapewa na mwanaume wala sina huyo mwanaume??”

“Enhee umetoa wapi, Au tuvuane chupi unataka??”
    

  “Mamaaaa!!!”

“Nyokooo!!”

.”vua hiyo chupii”

“Mamaaaaa!!! Kwahiyo mimi kukusaidia kununua chakula imekuwa shida??”

“Sio kununua  chakula shida hela umetoa wapi Dina, hela hizo miambili zisikudanganye mwanangu hivi unanielewa vizuri  , kufeli shule  sio kufeli maisha  sio ujirahisi kwa hawa wavuta bangi wa hapa mtaani  Dina hivi unanielewa??”

“Maaamaaaaa aah  Nakuelewa wala mie siwezi  siwezi mama siweziii aaah”

“Hayaa kalete mihogo  “

“Saaa mama unanipa hela ya mihogo wakati nimenunua mihogo  hii hapa  mama sijahongwa hii hela jamani wala sina bwana”

Mama yangu aligoma kabisa kula hiyo mihogo asojua imetoka wapii  namie kumwambia nilipo toa nilikuwa nashindwa

  Ilibdi nimwambia mama  nilikuwa na 3000 nilimuibia ibia kwenye mkaa wake yaan niliikusanya kidogo kidogo  

Mama angu huwa ananiamini sana tu mana ananipenda mno na anajua mie siwezi  kwelii  kugeuka mashart yake na kila siku najitunza mie

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata