
SEHEMU YA 12
Hivi ushawahi kukataliwa wewee?? Yaan mwanaume amekunyandua halafu anakukatia hapo hapo bila hata chenga haulizi wala hakwepesh yaan ile No kukupa matumainiii
Kwanza nilihisi utani mana mussa kwa hizi siku nilizomjua alikuwa mtu wa utani utani sanaaa
Kwahiyo mie nikachukulia hivyo hivyo kwamba ni mtu wa utani na hapo ananitania
Nikasema mussa acha utani !!” Huku najikaliza vizuri kwenye kochi
Akanambia Yeah I’m Serious siwezi kukupa moyo Dina wala siwezi kuoa
🙄🙄mungu wanguuuuu🙆♀️🙆♀️🙆♀️na nilisema swala la kuoa wala sikua namaanisha unajua ni kama nililopoka tu sikutegemea kukutana na haya majibu
“Dinna unajua Umeni surprise sana ,sikutegemea kama naweza kukuta ukiwa hivyo ,yaan nashindwa hata niseme nini but sorry sana Dinna “
Uwiii😭😭😭Nikamuona huyu kaka kichaa ndio nikaanza kulia sasa ile ya Serious mana mwanzo nilikuwa nalia kwa kudeka hee kumbe hakuna mtu wa kumdekea hivyooo😭😭😭
“We kaka weweeee aah””
“Sorry Di..” nilimuweka bonge wa kibao nikainuka haraka nikatoka nje nakimbia akawa ananiita mie nikafungua geti nae akatoka mbio ananiita Dina njoo tuongee sikusimama hata nikachukua Boda mbele nikamwambia nipeleke kituoni
Nimefika kituoni na gari inafika nikapanda yaan nimekuja kukumbuka yule kaka sikumpa hata hela ya boda atajua yeyeee😭😭
Kondaa kaja kudai nauli sina hata mia wacha niangue kilio cha nguvu abilia wote wananishangaa mimi tu mmoja akaniambia njoo ukae hapa yeye akainuk mana mie nilikuwa nimesimama
Konda hakuniuliza tena hata nauli ,sasa zile foleni za kutoka mbezi nimefika kwetu giza limekorea kweli kweli
Ile nashuka kwenye dala dala ndio najikuta nipo peku sasaa😫😫😫😫kumbe hata viatu niliacha kwa mussa jamani
Simu sinaa 😭😭walai nimevurugwa miee daaah
Nilifika nyumbani nikamkuta mama anaangalia Tamthilia zake
“We nae ndo unanirudia sa hizi,pamekuwa kwako hapa et??”
Maneno ya mama yalikuwa kama mkuki moyoni mwanguu😭😭😭🙏 eeh mungu wee nililia kwa sautii mama akabaki ananitazama kwa mshangao
Nilienda nikapiga magoti mbele yake
🙏🙏 “mama yangu mamayangu nimekosa mie mama yangu ,walau ningekusikiliza kidogo tu mama kidogo tuuu labda nngekuwa na heshima yanguu , ulinambia mama mwanaume anakupenda akiwa hajapata anachotak kwenye nguo zako akipata tu anakuona kama paka ,Mama yule mwanaume ameniona mie mbwa mamaaa😭😭 mama niuwe kabisa mama yangu we niuwe tu “
“Embu nyamaza halafu ongea vizuri unanichanganya mjinga wewe”
Mama aliongea kwa kufoka lakini sauti yake ilikuwa na wasi wasi mwingiii wenye Hofuu
Mie ndio nakazana kulia sanaa yaan yale majuto yananikaba kwenye koo mpaka basii najuta najuta najutaa
Mama akanituliza kwanza sikuwa na mtu wa kumlilia nilimuhadithia mama yotee kama kunipiga acha anipige ili akili inikae sawa
Nikamwambia mama umenifunza vyema sana lakini mie nimekataa sasa naona ulimwengu umenifunza kwa ukali naumia mama nilimpenda yule mwanaume bila hata kumjua vizuri mamaaa
Mama akanambia tulia Dinaa mwanangu tulia mwache na inshaallah utapata aliesahihi muda sio mrefu achaa chochote kinachotokea mungu ndio kapanga yeye kakuumiza basi amini ataumia zaidi yako hata kama usipo muona lakini ataumia kuliko hata wewe “
Nikamwambia mbona haunipiga mamaa na nimevunja usichana ulio ulinda kwa nguvu zote??😭😭
Akanambia haina hajaa hata hivyo umejitunza sana mtoto wangu upo tofauti sana na ma bint wa mtaani hufanani tabia na watoto wa wanawake wenzangu wengi najivunia wewe , umeshaona kile nilichokuwa naulindia sio usichana bali sikutaka uchezewe sikutaka uumie kisa mwanaume lakini nimeshindwa na umeumizwa tena mara ya kwanza tu , sasa kuanzia hapa Jilinde mwenyewe kuanzia hapa jitunze mwenyewe huwezi kulazimisha moyo wa mtu ukupende hata tukitumia nguvu utaumia zaidi huko mbele
Kaa tulia utapata aliesahihi kwa wakati sahihi na utafurahia mahusiano kamwe usijitoe kama njungu mtaani kisa tu kukataliwa na mbwa mmoja sawaa”
‘”Asante mama yangu Asante “😭🙏
“Hayaa kaoge uje ulee , ulale sitaki tena ulie wala umkumbuke huyo mpumbavu”
“Sawa mama”
Niliinuka nikaenda kuoga lakini swala la kumsahau mussa aisee lilikuwa gumu sanaa yule mtu nilikuwa nimeshampenda sanaa yaan nimezama mwili na moyo ,figo mpaka maini kutoa kutoa vyote ndio na mie nitoke sio haraka hivyo aisee
Bafuni nililia sanaa mpaka mafuaa, mama alipoona nimeingia moja kwa moja akaja akaniita nikafuta machozi nikatoka sikuwa na hamu ya kula ,
Nyie mapenzi kumbe ndio yanauma hivii yaan kama kuna donda kubwaaa kati kati ya moyo kila ukipiga Du Du Du ,ndio unaenda kutonesha lile donda maumivu makali nayasikia
Nikamwambia mie naenda kulala nimeshiba akanambia sawa wala hakunilazimisha kula akanambia kama unasikia uchungu lia sanaa sintakuzuia ila iwe leo tu hakikisha usiku wa leo ndio mwisho wa kumlilia mpuuzi ambae yeye huko alipo anafurahia wakati wewe unauma
Nikasema sawa mama😭😭 nikaingi kulala jamni nyieee🙌😔😔 Usingizi hauji nalia mbona mie mzurii tena sanaa tu sasa mbona mussa amenifanya hiviii au kwakua anahelaa au amenionaje miee
Nilitamani hata kumpigia labda niongee nae lakini simu nayo nimeacha huko huko kwake
Nilikuwa nakumbuka yale mapenzi the way alivyokuwa nananipapasa kwa mahaba mazito zile sifa alikuwa ananimwagia ile miguno yake 🙌🙌🙌mamaee kumbe alikuwa ananiigiziaaa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU