
SEHEMU YA 19
Akanivuta akawa amenikumbatia akanambia naomba tuongee mke Wang”
Nikamwambia acha kuniigizia wewe!!
“Noo Mamyyy mie mbona sikuigiziii”
“Utajua wewe!!”
Alinivuta kwa nguvu akanikumbatia kwa nguvuuuu akanambia Dina kweli ukweli nilikupenda tangu nilipo kuona kule fb ile siku nilikupenda lakini sikujua kama tutafika huku”
Yaan huyuuu😫😫 enhee alijua tutaishia wapiii si ndio mie nasema hanipendi huyu kaka huyuuu
“Embu nisikilize Dina naomba unisamehe mama yangu nakuombaa , najua halikuhusu lakini naomba nikuambie hili lililofanya mie nisiwatamani wanawake kuwaweka karibu yangu walau nisikilize tuuu nilitoe la moyoni “
“Enhee nakusikia”
“Keti basiii” nilivuta kiti kwa hasira kwali nikaketi
“Unajua mie nilishawahi kuwa na mke hapo zamani nikajaariwa mtoto mmoja , mtoto wangu alikuwa ndio kila kitu nilimuweka mbele kwa kila kitu mke wangu nilimpenda sana, lakini unajua alikuja kufanya ninii??”
Nilitikisa Kichwa kuwa sijui alifanya nini!!
“Yule mwanamke alikuwa na kaka yake ambae alimuombea kazi kwangu , alikuwa shemeji yangu, nilimpatia usimamizi kwenye kitengo flani kwenye kampuni wala hakuwa na uzoefu wala elimu lakini ni shemeji nilimpa nafasi
Shemeji yangu nilimpa nyumba ya kuishi baada ya mke wangu kumuombea sehemu ya kukaa ,
Ndie mtu aliekuwa karibu mnoo na mke wangu karibu kuliko kawaida nilikuwa nikisafiri kaka yake anakuja nyumbani pale kukaa mpaka nitakapo rudi ndie nae anaondoka
Mke wangu alikuwa anasema kukaa peke yake kwenye nyumba kubwa anaogopa ..
. Alishika ujauzito akajifungua mtoto wetu wa kwanza alifanana kila kitu na kaka yake kila kituuu
Mtoto alivyofika miaka minne ndio nilianza kuona mambo ya ajabu mke wangu na kaka yake walikuwa wakigombana sana kuhusu mtoto sanaa
Mda wote kaka yake alikuwa anamchukua mtoto anavyojisikia kitu ambacho mke wangu alikuwa hapendi sana
Mwenyewe nilikuwa namwambia embu mwache mtu na Uncle wake tu hao wanapendanaa
Siku moja nilikuwa natoka safari nilikuta ugomvi nyumbani mkubwa sana shemu akawa anamwambia dada yake mwambie ukweli mumeo kama ukishindwa mie nitasema
Hawakuwa wanajua kama nimefika niliuliza ukweli gani??
Dada yake akaanza kulia akanambia et nyumbani mama anaumwa sana kwahiyo natakiwa kwenda nilikuwa sitaki kuondoka kukuacha wakati ndio kwanza umetoka safari
Nilimwambia mbona hakuna shida mke wangu hakuna shida kabisaaa nenda nyumbani ,tutaondoka wote kesho asubuhi akanambia hapana we baki mie nitaenda kesho na kesho kutwa nitarudi akiwa vibaya nitakwambia uje
Tulielewana hivyo lakini kaka yake aliondoka bila hata kuaga na wala hakunisemesha alikuwa kama ana hasira sanaaa
Nikamuuliza dada yake vipi akanambia achana nae basi mie nikaachana nae
Asubuhi nilimpeleka mke wangu standi ili aende kwao yeye kwao ilikuwa ni mtwara .
Siku zote nilikuwa naamini wanawake wenye elimu ni wasumbufu wanawake wenye kazi siwawezi mke wangu nilimpata tu mtaani mwanamke wa kawaida sana na nilimpenda sanaa ..
Shemeji yangu alikuwa anakuja kazini lakini haongei na mimi kama mtu mwenye hasira
Na zilikuwa sikumbili tangu dada yake aondoke nyumbani kwangu
Nilipo toka kazini ile usiku niliamua kwenda nyumbani kwa shemu ili niongee nae mana nilihisi ana tatizo na mimi kabisaaa
Nilifika mpaka nyumbani kwake mhu ajabu sana sana ile siku naiona kama jana tu
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU