BIKIRA YA BIBI HARUSI (06)

SEHEMU YA SITA

ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO : Sasa basi baada ya kuwa amemwona tena kijana huyu, akiwa anaingia kwenye Dutsun, akaona afanye juhudi za kulitahalifu jeshi la polisi, ukweli simu kipindi hiki zilikuwa ni zakampuni ya simu ya serikari pekee, kwa hiyo kijana huyu, baada ya kuulizia sehemu ambayo anaweza kupata simu akaelezwa kuwa aende kwenye kituo cha afya cha mlilayoyo, akatimua mbio kuelekea huko, ** endelea ……….
Mama Edgar akiwa amechoka na kwa pilika pilika za mchana kutwa, kuzunguka kwenye maduka, ali kusanya mizigo yake, ikiwa pamoja na maandalizi ya zawadi na chakula kizuri kwaajili ya kijanawao ambae amewatoa kimaso maso, kwa kumaliza chuo na kujipatia degree yake, mama huyu alikuwa ametulia mbele ya maduka mapya, uswa wa duka la sonara ya muhindi Kanjubay, kama alivyo aidiana na mume wake, walikubaliana aje amchukuwe hapo, huku macho yake yakiwa kwenye moja ya nguzo za duka hilo, akitazama picha mtu mmoja, anae tafutwa na polisi, kwa shutuma za ujambazi, nikama ana mfahamu kijana huyu, akajaribu kuvuta kumbu kumbu juu ya kijana huyu, wakati anavuta kumbu kumbu kwamba kijana huyu aliwai kumwona wapi, ghafla aka stuka akizolewa kikumbo, na mtu mwenye nguvu zake, nusu mama Edgar ajibwage chini, maana aliyumba kwanguvu, huku bahadhi ya vitu alivyo shika mkononi, vikimtoka na kudondoka chini, “mnazidi kushangaa, hivyo mpo songea ingekuwa dar si mngegongwa na magari?” alisema yule kijana alie msukuma mama Edgar, huku akiendelea na safari yake, mama Edgar aka mtazama kijana huyu, ambae yeye anamwita alie kosa adabu, alikuwa ni kijana alie valia kitanashati kabisa, akiingia kwa sonara, tena mama Edgar anamfahamu vyema kijana huyu, toka akiwa mtoto, aliwai kukaa jirani na wazazi wake, huko mtaa wa mahenge, “hivi huyu si yule mtoto wa mama Erasto” alisema mama Edgar kwa mshangao, akitazama mpaka Erasto Richaard, au bwana harusi mtarajiwa, alipo potelea ndani ya duka la sonara, “vipi mke wangu mbona kama ume duwaha, mpaka umeshindwa kusikia gari kama limefika” alistuliwa mama Edgar na mume wake, ambae alisha fika eneo lile, “walimwengu mume wangu, yani watoto wamekosa adabu kabisa” alisema mama Edgar huku wakianza kusaidiana kupakiza mizigo kwenye gari, “imekuwaje tena, kwani kuna kijana ame kuvunjia heshima?” aliuliza baba Edgar kwa utani, “ungenikuta nime anguka kama gunia, yani huyu Erasto amezidi kuwa mtoto wa hajabu sana” alisema mama Edgar, nakumsimulia mume wake jinsi ilivyo sukumwa na Erasto kisha kumtolea maneno ya kashfa, “haaa! funika kikombe ya pite, ndio maana nawasi wasi na kiindi kile huyo mtoto alichangia kwa kihasi kikubwa ugomvi wetu na bwana Anderson” alisema baba Edgar, huku wakimalizia kupakiza mizigo kwenye gari lao, na kuanza safari yao kurudi nyumbani, “ndio maana ujio wa Edgar unaumuhimu sana, maana angekuwepo hapa lazima kingesha eleweka” alisema mama Edgar, na kumfanya baba Edgar acheke kidogo, “alafu nika animesikia anataka kumwoa yule binti wa Anderson” alisema baba Edgar, kama vile hakuwa na uakika na jambo hilo, ***
Saa nane mchana gari la polisi liliondoka kwenye kituo cha afya cha Mlilayoyo, ikiwa ni baada ya kukutana na mtu alie wapigia simu, lisaa limoja lililopita, akiwajulisha kuhusu kumwona mtu wanae mtafuta, mtu huyo alisha wajulisha aina ya gari alilokuwa amepanda kijana Lukas, kwa hiyo polisi waliondoka hapa, wakiwa wamesha juwa Lukas amepanda gari gani, polisi hawa wakiwa wameondoka mjini, nusu saa kasoro, kuja hapa Mlila yoyo, wakiwa navifaha vyao kanakwamba wanaanza safari ya kutoka nje ya mkoa, wakimwacha mkuu wakitengo cha upelelezi, akifanya mawasiliano na mkuu wa upelelezi mkoa wa Iringa, ili kumjulisha kuwa, kuna vijana wake wanaingia mkoa wake, kwa kazi mahalumu, (kipindi hicho njombe na makambako ni sehemu ya Iringa) pia akiomba msaada wa askari wengine kwa msaada zaidi, **
“kanal unazani kuna ulazima wa kulifwatilia jambo hili?” aliuliza Brig Gen Fransis Haule, akiwa anamtazama bwana Joseph Kisona, wakiwa ndani ya ofisi ya mkubwa huyo wa brigade, “afande ulazima hupo, maana naona vifo vimesha fikia tisa, na kwa matumizi ya silaha niliyo ya shuhudia, nazani tutaendelea kusikia taharifa zaidi za vifo” alisema kanal Kisona alie kaa mbele ya meza ya mkubwa wake huyu, ambae alitulia kidogo kama alikuwa anatafakari jambo, kisha akainua uso na umtazama bwana Kisona, “lakini mpaka sasa hatujapata kibari cha kulifwatilia swala hili, sasa tunafanyaje hapo?” aliuliza brigedia Haule, “afande nazani unajuwa kazi ya kitengo changu, chakufanya wacha nianze kufwatilia kwa siri, mpaka tutapopata sababu ya kufwatilia wazi wazi swala hili” alisema Kisona na hapo mzee Haule akatulia tena na kusikilizia kidogo, alafu akainua usowake akiwa anatabasamu, “naamini unapofanya kazi zako uwa unatumia hakili nyingi, nakupa kibari cha kufanya kazi hiyo” alisema Haule, na hapo Kisona akaachia tabasamu la ushindi, “sito kuangusha afande, naamini tuta fanikiwa” **
Tukirudi Chuo kikuu cha biashara Mbeya, mida hii tayari mkuu wa chuo alikuwa amesha maliza mahafali ya wahitimu wa digree ya utunzaji wa fedha, wanafunzi walikuwa wanatoka nje ya ukumbi huku wakipongezana kwa furaha na bashasha, lakini tofauti kwa kijana Edgar, yeye alitembea taratibu, kichwa ameinamisha chini, mikono ame iweka nyuma, akionekana kusongwa na mawazo mengi sana, kihasi cha kuonekana wazi kabisa, kuwa kijana huyu alishikwa na unyonge, ungesema kuwa hakutaka kumaliza chuo.
Lakini aikuwa hivyo, ukweli ni kwamba kwa siku za hivi karibuni alionekana kuibukiwa upya na mawazo juu ya Monalisa, mwanamke ambae akuwai kuacha kumpenda toka wakiwa watoto, lakini kwa sasa akuweza tena kumweleza swala hilo, kwa sababu nyingi ambazo Edgar mwenyewe aliziona ni kikwazo, ukiachilia tukio lili mtokea kipndi wakiwa darasa la sita, pia kwa sasa mwanamke huyu alizidi kuwa matawi ya juu zaidi, tofauti na ile hali ya utoto, ata kumhudumia ingekuwa vigumu kwake, pia ata ukaribu wao aukuwa kama wa siku zanyuma,
Edgar alijikuta anatembea kama mtu alie poteza fahamu, mpaka alipoingia kwenye chumba chake bwenini, bila kuji juwa kuwa amefikaje, ndani ya chumba hicho, mawazo yalirudi baada ya kujikuta amesimama katikati ya chumba hicho, akiwashuhudia wenzie wakibadiri nguo zao, tayari kuondoka chuoni hapo, maana wengi walipanga kuanza safari siku hiyo hiyo, asa wale waliokuwa wanakaa karibu, Edgar akiwa hajuwi la kufanya, akatoka nje ya chumba, akiwaacha wenzie wanaendelea na pilika za safari, akaenda kukaa kwenye ngazi za kuingilia kwenye chumba chao, akiwatazama wanafunzi wenzie waliokuwa wana pita mbele ya bweni lao na mabegi yao, wakionyesha kuwa wanasafiri siku ile ile, japo kuna wachache walio amua kubakia pale chuo mpaka kesho asubuhi iliwaanze safari, hiyo ni kwa wale waliokuwa wanatokea mbali,**
huku nako Monalisa na rafiki yake Stella walikuwa wamesha maliza kubadiri nguo zao, wote wakiwa wame vaa suruali za jinsi nyeusi, na matishet, walichukuwa mabegi yao, Monalisa akiwa na kibegi chake cha ziada mgongoni na lile kubwa kichwani, waka toka nayo nje, alafu wakatazama huku na huku, wakawaona wenzao wakiwa na pilika pilika za kuondoka pale chuo kuelekea nje ya chuo kisha kwenye stendi ya magari yaendayo njombe na mikoani, “hoyo mtu wako yupo wapi?” aliuliza Monalisa, ambae licha ya kuamua kuondoka leo, akalale mbele ya safari lakini, bado roho yake kama iliingia ganzi hivi, sababu hakuwai kufikilia kulala guest house, labda kutokana na sifa zipatikanazo kwenye neno guest house, “atakuwa anatusubiri nje, siunajuwa gari litatufwata mpaka hapo nje?” alisema stella, kisha wakanyayua mabegi yao na kuanza kutembea kuelekea lilipo gate kubwa la chuo, “bye bye chuo” alisema Monalisa, kwa utani wakacheka kidogo, huku safari inaendelea, wakiongozana na watu wengi waliokuwa wana elekea nje ya chuo, “Stella ebu agalia, upande wangu kule kwenye bweni la wavulana” alisema Monalisa, wakiwa usawa wa bweni moja la wavulana, “maskini yule kaka, mbona anaonekana kama anaumwa, alafu ana tutazama sana” alisema Stella kwa sauti iliyo jaa huruma, ni baaada ya kutazama kule alikoambiwa na Monalisa, “achana nae anamambo yake yana msumbua kichwa” alisema Monalisa, huku wanaendelea kutembea, kuelekea nje,
Waschana hawa hawakujuwa kuwa Edgar alikuwa katika wakati mgumu sana, akiwaza juu ya Monalisa, ambae leo asubuhi amezidi kuutibua moyo wake, ulio zidiwa na hisia za mapenzi juu ya mrembo huyu, ambae mida hii alikuwa ana pita mbele yake akiwa amependeza ndani ya tishet na jinsi, Edgar aliwasindikiza kwa macho huku wivu ukijaa moyoni mwake, sababu mwonekano wa Monalisa, ni kwamba alikuwa anaondoka leo leo, lakini ukweli ni kwamba Monalisa asinge weza kufika songea leo hii, kwahiyo binti huyu alie unyanyasa moyo wake toka miaka mingi iliyopita, akiwa mdogo, anaenda kulala kati ya Mbeya mjini, makambako au Njombe, swali, je anaenda kulala na nani, na kama siyo hivyo kwanini aondoke mida hii, maana gari la mwisho la Mbeya songea linatoka hapa saa saba, na kufika songea saa tano usiku, na kama kuwai makambako yanayotokea Dar na Iringa, uwa yana pita makambako nusu saa ijayo na kwa sasa wasinge wai, sababu toka hapa Mbeya kwenda makambako ni mwendo wa lisaa na nusu, “labda baba yake amemfwata” aliwaza Edgar, ambae alijuwa kuwa asinge pata lifti, ata kama wazazi ndio walio mfwata, sababu yeye ndio chanzo cha wakina Monalisa kuhama mtaa waliokuwa wanakaa nao, yani mtaa wa Mahenge, na kuhamia mtaa wa Luhuwiko, kwenye nyumba yao mpya, ambayo kipindi hicho aikuwa imemalizika vizuri, kama ilivyo sasa.
Sijuwi kwa nini Edgar alijikuta akiinuka ghafla, pale alipo kaa, na kuingia ndani ya chumba chake na kuanza kubadiri nguo haraka haraka, akivaa suluali ya jinsi nyeusi na tishet nyeusi na viatu vya ruber, akiwa kama mtu aliegandwa na hakiri, Edgar aliweka vitu vyke vizuri kwenye begi lake, kubwa la mgongoni, huku akiwa hajuwi kwanini ameamua kuanza safari mchana ule, maana mpaka ananyanyua begi lake kubwa la mgongoni, pamoja na kibegi kidogo cha mgongoni pia, alicho kishika mkononi, na kutoka nje ya chumba hicho cha bweni la Uhuru, ilisha timia saa tisa na nusu, lakini Edgar akujari swali lake la kuwa, kwanini anaondoka mida ile, yeye alitembea taratibu kuelekea nje ya geti, wivu ukiwa umemshika vibaya sana, akiambatana na wanafunzi wachache, wale wamwisho mwisho, maana wengi walisha toka nje.
Naam, kijana Edgar alitokea nje ya geti la chuo, akaona wanafunzi wengi sana wakiwa wana subiri usafiri, wakiwepo Monalisa na Stella pia karibu yao alikuwepo mwanafunzi mwenzao wakiume alie mtambua kwa jina la Denis, ambae anafahamika pale chuoni kama ni mpenzi wa Stella, kuna wakati Edgar alimwona Monalisa, akiwa ana tazama huku na huku, kama vile kunakitu ana tafuta, na ata macho yao yalipogongana, Monalisa aliishia kutabasamu tu!, japo alionekana kuwamwenye mawazo mengi sana, Edgar akuwa na ujannja wa kusogea eneo lile, yani karibu na Monalisa, sababu akuwa na sababu ya kusogelea, kama ni ujirani na urafiki alisha uvunja muda mrefu sana, unajuwa aliuvunjaje?, nazani tujuwa mbele ya simulizi.
Edgar aliendelea kusimama pale alipo kuwa amesimama, yani pembeni kidogo ya kituo cha kusubiria magari, huku akimtazama Monalisa bila kummaliza, pasipo kujuwa kuwa na yeye kuna watu walikuwa wana mtazama, kama yeye alivyokuwa anamtazama Monalisa, huku akiona magari yana kuja na kuchukuwa watu walio eka oda zao, yaani booking, “uchizi, kumpenda mtu siejuwa kama unampenda” alijisemea Edgar Mbogo, kisha aka tazama kushoto na kulia kama vile amegutuka toka usingizini, akaliona gari moja dogo aina ya suzuk likija na kusimama ene la kituo, akataka kuwai akajaribu bahati yajke, lakini akasita kidogo, ni baada ya kuwaona wakina Monalisa Stella na Denis wana weka mizigo yao kwenye gari ambalo ndani yake kulikuwa na vijana wawili wakiume, kisha na wao wakaingia ndani ya gari, na gaari likaondoka, ukuwakipungiwa mikono ya kwaheri ya kuonana,
Kitendo hicho nikama kili amisha tena hakiri za Edgar, ambazo sasa alijawa na wivu mkubwa sana, maana alihisi kuwa kati ya vijana wale wawili mmoja wao lazima akale kitumbua cha Monalisa, mschana ambae yeye binafsi akuwai kuacha kumpenda toka wakiwa wadogo, japo akupata nafasi ya kuwa mpenzi wa mrembo huyu, ilifikia kipindi Edgar alijikuta akiishiwa nguvu ya miguu, na kuliona begi lake lina mzidi uzito, akalishusha chini, toka mgongoni mwake, na kuendelea kusimama akiwa hana mpango wowote wa usafiri, huku aiwaona wenzie wana kuja kuchukuliwa na magari mbali mbali, wengine binafsi, wengine mabasi madogo, lisaa izima lilikatika akiwa pale stendi wenzie wakizidi kuungua pale kituoni, ilisha timia saa kumi na robo,
“Eddy unaitwa kwenye gari lile pale” alistuliwa Edgar na mtu alie kuwa jirani yake, yani mwanafunzi mwenzie, Edgar akatazama, upande ule alio onyeshwa, je unataka kumjuwa alie mwita Edgar?, vipi kuhusu Lukas unzani atafanikiwa kufikisha mkanda huo sehemu salama, je kusu Edgari kumteka Monalisa, ilikuwaje, nazani kesho tutapata majibu, endelea kufwatilia mkasa huu, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!