BIKIRA YA BIBI HARUSI (07)

SEHEMU YA SABA
 .
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA : huku akiwaona wenzie wana kuja kuchukuliwa na magari mbali mbali, wengine binafsi, wengine mabasi madogo, lisaa lizima lilikatika akiwa pale stendi wenzie wakizidi kupungua pale kituoni, ilisha timia saa kumi na robo,
“Eddy unaitwa kwenye gari lile pale” alistuliwa Edgar na mtu alie kuwa jirani yake, yani mwanafunzi mwenzie, Edgar akatazama, upande ule alio onyeshwa, endelea …………..
Akaliona gari moja dogo aina ya mercides Benzi la kifahari sana, ambalo ndani yake walikuwa wamekaa watu wanne, mzee mmoja mtu mzima mwenye hasiri ya kiarabu alie valia kanzu nyeupe na baraghashia kichwani, na mmama mtu mzima, ambae pia alikuwa ni kama mume wake, yani mwenye dalili ya uarabu, alie valia baibui jeusi, na kitambaa kichwani wenyewe wanaita hijab, pia seat ya nyuma alionekana binti mmoja mrembo, anae mfahamu kwa jina la Salma Mohamed, ni mwanafunzi mwenzie, mwenye hasiri ya uchotara, wa kiarabu kama wazazi wake wanavyoonekana mbele ya gari, nae akiwa amevaa kama mama yake, watu hawa walimtazama huku wanatabasamu, akaanza kutembea kulifwata lile gari la kifahari, lakini akamwona yule mzee ambae ndie alikuwa dereva, akimwonyesha ishara kuwa abebe mabegi yake, Edgar aka rudia mabegi yake na kuyabeba, kisha akasogea kwenye lile gari, “shikamoni mzee” alisalimia mtoto wa mzee Mbogo, kwasauti iliyo jaa heshima kubwa, “marahaba bwana Edgar, mwenzio amekupa lift, kama utojali tuka kuache makambako sisi tunaenda mafinga” alisema yule mzee ambae Edgar alimtambua kuwa ni baba wa Salma, binti ambae anafahamika sana pale chuoni kutokana na upole na uzuri wake, pia mavazi yake maharufu sana ya kistaharabu, magauni marefu, na muda wote akijihifadhi nywele na maungo yake ya mwili, “asante sana mzee, utakuwa umenisaidia sana” alijibu Edgar huku anamtazama Salma ambae alikuwa ameachia tabasamu mwanana, ambalo halikumwacha salama kijana huyu,
Dakika tano mbele tayari mzee Mohamed alikuwa amesha fungua buti, na kuweka begi la Edgar na kuondoka zao, huku Edgar akiwa anajishangaa moyoni, kwanini apewe lift yeye, na sio wanafunzi wengine, “bwana Edgar kwanza hongera sana kwa kumaliza chuo” alisema mzee Mohamed, huku akiendesha gari kwa mwendo wa kawaida kabisa, wakiitafuta Makambako, “asante sana mzee” alijibu Edgar alie kuwa ameka seat ya nyuma, karibu kabisa na Salma, “pia usijiulize sana kwanini umepewa lift, ni kwamba nilikufahamu mwaka jana, kipindi kile, mlipokuja kucheza mpira mafinga, ulini flaisha sana uchezaji wako wa mpira wakikapu” alisema mzee Mohamed akiungwa mkono na mke wake, “kweli kabisa, yani mimi uwa sipendi mpira lakini sikuile nilijikuta na nashangilia mwenyewe” hapo safari ilikuwa ni ya maongei na vicheko vya furaha, “toka sikuile ukuwai kuni toka kichwani, mpaka leo nimekuona tena, ila kijana usije ukaacha kucheza” alisema mzee Mohamed huku gari likizidi kuyoyoma, kuelekea makambako,
Maongezi yaliendelea kwa muda mrfu kidogo, kabla hayaja koma, kwa kila mtu akiwaza lakwake, huku Edgara akirudisha mawazo yake kwa Monalisa na kuanza kukumbuka miaka mingi sana nyuma. kiprndi hich kiwa darasa la tano shule yamsingi Matagoro, shule ya mazoezi ya chuo cha ualimu,**
Safari ya Lukas na Mtutuma ilikuwa nzuri sana, licha ya maumivu ja majeraha ya risasi, lakini Lukas aliweza kupata nafasi ya kusinzia, na kupumzika kidogo, maana maisha yake tokea jana, yalikuwa ni mshike mshike, hakuwa amepata nafasi kama hii, hivyo alipata usingizi mzito, akiwa na uakika kuwa yupo salama, hakujuwa kuwa nyuma yake kuna watu wana kuja kwa speed ya hajabu,
Mida hii ya saa kumi na moja za jioni, walikuwa wame simamisha gari lao pembeni ya barabara kuu iendayo Makambako, iringa na Mbeya, yaani walikuwa ndani ya mji wa Njombe, pembeni kidogo ya stendi kuu, watu walikuwa wengi pembezoni ya barabara, wengi wao wakiwa ni wa nunuzi wa bidhaa mbali mbali zilizo uzwa na wa chuuzi, waliopanga biashara zao pembezoni mwa bara bara,
Lukas na Side Mtutuma walio egesha gari lao sehemu nzuri ambayo aikumbughuzi mtu yoyoye, wala wafanya biashara, walishuka na kuingia madukani, ambako walinunua vitu vichache, ikiwa na bwana mtutuma kununua sigara kama kawaia yake, kisha wakarudi na kuingia kwenye gari, na kuendelea na safari yao, wakipanga kuwai makambako ambako Lukas alipanga akapumzike mpaka kesho atakapo wai mabasi ya asubuhi, yaendayo dar, maana Mtutuma alikuwa anaelekea Mbeya, licha ya yote pia Lukas alipanga kuwa, endapo ata pata gari lolote la mizigo liendalo dar, angeondoka muda wowote.
Hivyo walianza safari, huku Lukas akiwa amejikagua vizuri kwenye kipochi chake kiunoni, na kuona kuwa kila kitu kipo salama, pamoja ile tape ya video ambayo ndiyo ushahidi wa kumweka huru yeye, akaendelea na safari yake, huku akihisi maumivu kwenye majelaha yake ya risasi, “nazani kesho uta wai mapema sana kuingia dar, maana kuna basi linaanzia safari hapa Njombe” alisema Mtutuma, huku wakiiacha kibena, na kuingia kwenye mashamba ya chai, “ni kweli ila nikipata ata magari ya mizigo naondoka muda wowote” alisema Lukas, pasipo kujuwa kuwa, wakati huo huo gari la polisi toka songea, lililo wabeba polisi nane, yaani pamoja dereva, lilikuwa linaingia Njombe, na sasa lilisimama pale pale walipokuwa wamesimama wao, muda mfupi uliopita, akashuka sajent Kibabu na kuelekea kwa wafanya biashara ndogo ndogo, walio tanda pembeni ya barabara, akauliza kama kuna gari aina ya Dutsun wagon limekatiza eneo lile, wakamwambia kuwa, gari ilo lilikuwa muda mfupi uliopita mahali hapo, na limeondoka nusu saa iliyo pita, na kwa mahesabu ya haraka, ni kwamba limesha karibia utwango, maana yake dakika kumi na tano au ishirini mbele, litakuwa linaingia Makambako, na hapo inge kuwa shida kwao, kujuwa kama gari hilo limeelekea Iringa au Mbeya, kwa hiyo, ni lazima wajitaidi kupiga simu mbele, ili wakina Lukas wazuiliwe, na wao walitakiwa wawai haraka sana, wakaichukue tape, kabla ile tape aija chukuliwa na polisi wengine,
“pumbavu kabisa huyu mshenzi, yani ana sumbua kihasi hiki, wacha nimkamate, nita muuwa kikatili sana” aliwaza Kibabu huku ana wai kwenye kibanda cha simu, kwa nia ya kupiga simu polisi Makambako, wamzuwie Lukas aliepanda gari aina ya Dutsun. ***
Kumbukumbu ya miaka zaidi ya kumi iliopita, kipindi hicho Edgar na Monalisa wanasoma Darasa la sita, shule ya msingi Matogoro, wawili hawa walikuwa marafiki wakubwa sana, muda wote unge waona wapo pamoja, na hiyo ni toka wakiwa na umri mdogo kabisa, maana ata wazazi wawo walikuwa ni marafiki sana, urafiki ulio sababishwa na ujirani, waliokuwa nao pale mtaani mahenge, japo urafiki wa familia mbili hizi ulipungua miaka micache iliyo pita, baada ya bwana Misago na familia yake, kuhamia mtaani hapo, ambao kutokana na baba mona na baba Erasto kuwa wafanya biashara, wakajikuta wanakuwa marafiki wakubwa sana , na kuufifisha urafiki wa familia ya Anderson na bwana Mbogo,
Kingine kilicho changia kuaribu urafiki wa familia hizi, ni kauri yautani ya mama Edgar, aliyoitoa kipindi hicho wakina Edgar na Monalisa, wakiwa darasa la tano, iliyo sababishwa na tukio lakitoto, ambalo lilikuwa hivi, siku hiyo ilikuwa ijumaa, mida ya jioni, Monalisa alienda kununua vitumbua, ni moja ya kitu ambacho yeye na Edgar walikuwa wana penda sana kula, wakiwa nyumbani au shuleni, wakati huo Edgar alikuwa uwanjani, anachaze mpira wa kikapu, na watoto wenzie, na baada ya kununua kununua vyake, Monalisa kama ilivyo kawaida yake na Edgar, kuwa mmoja akinunua kitu, lazima ampatie mwenzie, na mala nyingi upenda kununua vitumbua, hivyo Monalisa akapitia uwanjani kumpelekea Edgar pipi, alipofika uwanjani, akamkuta Edgar yupo kati kati ya mchezo, hivyo Monalisa akalazimika kusubiri, na kifuko cha vitumbua mkononi mwake, aikuwa kazi ngumu kwake, sababu mala nyingi uwa anakaa pembeni ya uwanja akimtazama Edgar akicheza mpira,
Monalisa akiwa amekaa mahali pale, akitazama mpira, sambamba na watoto wengine waumri wao au walio mzidi kidogo, akiwepo Erasto ambae pia alikuwa anakaa jirani yao, na nirafiki yao pia japo siyo sana, na alikuwa ame wazidi umri zaidi ya miaka miwili, kipindi hicho Erasto alikuwa darasa la saba, kosa alilo lifanya Monalisa, ni kuchukuwa kitumbua kimoja kati ya vinne vilivyo kuwa ndani ya mfuko, na kuanza kula, hapo akawaona watoto wawili wavulana walio mzidi kidogo umri, wakimsogelea na kutaka kumnyang’anya vitumbua vyake, ukweli hakuwa na ubavu wa kuwazuwia, maana ata alipo jaribu kuzuwia wasi chukue wakataka kumpiga, mtu ambae angeweza kuwa saidia Monalisa, ni Erasto, lakini ukweli Erasto akuonyesha dalili ya kumsaidia Monalisa,
Ndipo Edgar akaliona tukio lile, na kutoka uwanjani, Monalisa alimwona Edgar akipambana na wale wavulana wawili, ambapo mwisho wa siku, aliwashinda na mvulana mmoja akaishia kulia huku mwingine akitoka damu kwenye meno, wengine walisema ni kwa sababu alikuwa apigi mswaki,
Sasa tatizo likaja baada ya kurudi nyumbani, ambapo Monalisa aliwakuta mama yake, mama Erasto na mama Edgar, wakiongea na kucheka, ndipo Monalisa aka wasimulia kilicho tokea uwanjani, na jinsi Edgar alivyo msaidia, “lazima akusaidie rafiki yako” alisema mama Mona, baada ya Monalisa kumaliza kusimulia, kisha akadakia mama Erasto, inaonyesha Edgar ni mgomvi sana” aliongea hivyo akionyesha kuto furahishwa na kitendo cha Edgar kuwa piga hao watoto wenzie, “siyo mgomvi, alikuwa ana mtetea mchumba wake” alisema mama Edgar, hapo mama Erasto aka mtazama mama Edgar kwa macho makali sana, baada ya kufanya hivyo kwa sekunde kadhaa, kisha aka mtazama mama Mona, ambae alikuwa ana mshangaa mama Erasto kwa kumtazama vile mama Edgar, “mama Mona unajuwa ni tabia mbaya sana ameonyesha huyu rafiki yako” alisema mama Erasto, akiuonyesha kuwa akupendezewa na maneno ya mama Edgar, “kwanini mama Erasto, kwani kuna ubaya?” aliuliza mama Monalisa, “ndiyo kuna ubaya, ujuwe watu kama awa ndio wanao watongozea watoto wao wana wanawake, tena kuwa makini sana” ukweli kauli hiyo, aikumpendeza mama Edgar, samahani mama Erasto, naomba tuheshimiane” aliongea mama Edgar kwa sauti isiyo na mzaha, hapo yakaanza marumbano, na mwisho wasiku, ikapelekea kupungua urafiki wa mama Edgar na wa mama hawa wawili,
Lakini aikupunguza urafiki wa Monalisa na Edgar, ambao waliendelea kuwa pamoja na urafiki wao ukizidi mala dufu, huku wakizidi kupevuka kimwili na kihakiri, ikafikia kipindi wakaanza kuoneana ahibu, na kubadiri ratiba yao ya kuonana, licha ya kuwa darasa moja sasa usinge weza kuwaona kila wakati wakiwa pamoja, ila onge waona saa nne, wakiwa kwa mama muuza vutumbua, hapo wataongea kidogo wakiwa wamesha nunua vitumbua, au kununuliana, kisha unge waona jioni wakati wa kurudi nyumbani,
utaratibu huo ulidumu mpaka walipo fikia darasa la sita, kipindi hicho Erasto akiwa kidato cha kwanza, na alianza kuwa karibu sana na Edgar, na ndicho kippindi ambacho Erasto alimshawishi Edgar amtongoze Monalisa, na njia kuu ya utongozaji ilikuwa ni barua, ambayo Erasto aliahidi kuipeleka mwenye kwa Monalisa,
Siku ya tukio ilikuwa ni jumapili, tukio ambalo Edgar lina msumbua mpaka leo, siku hiyo asubuhi Edgar alichukuwa fedha yake aliyo kuwa ameitunza kwa wiki nzima, akikosa kununua vitumbua, akaenda mjini na kununua chupi moja nzuri nyekundu, ambayo aliamini ingemtosha Monalisa, kisha aka rudinayo nyumbani akiwa ameiweka kwenye mfuko, kipindi hicho ilikuwa mifuko ya kaki peke yake, akaandika barua nzuri ya mapenzi akiambatanisha na mchoro flani wa vimauwa, na vilove, kisha akaiweka kwenye ule mfuko na kumpelekea Erasto, tayari kuupeleka kwa Monalisa,
Ilikuwa saa mbili usiku, siku hiyo hiyo ya jumapili, siku ambayo Edgar anaikumbuka kwa machungu makubwa sana, walikuwa mezani wana kula wali na samaki kambare, chakula ambachoo Edgar anakipenda sana, mida hiyo ndiyo mida ambayo walisikia mlango wa nyumba yao ukigongwa hodi, “hodiiii! hidii jamani” ilisikika sauti ya mama Monalisa, hapo mapigo ya moyo ya Edgar yakalipuka vibaya mno, ilikuwa ni kihoro cha kawaida kwa kijana anae jifunza kutongoza, ila Edgar aka changanyikiwa baada ya mlango kufunguliwa, akaingia mama Monalisa, akiwa ame mshika Mona lisa kwa mkono wa kushoto, na mkono wa kulia ameshika karatasi, ambalo Edgar alilitambua mala moja, kuwa niile barua aliyo mwandikia Monalisa, ukweli nikwamba ata utamu wa wali kambare uliisha pale pale, akahisi kama mdomoni alikuwa amekula udongo, “haya mama Eddy kile ulicho kiongeaga ndicho hiki ambacho mwanao ana kifanya” alisema mama Mona, kwa sauti iliyojaa hasira, huku ana nyoosha mkono wake wa kulia, kumpatia mama Edgar lile karatasi, ambalo mama Edgar, alilipokea na kuanza kulisoma kimya kimya,
Wakati mama Edgar, anaendelea kuisoma ile barua, mama Mona alie ndlea kuongea maneno ambayo yalimaanishia kuwa, mama Edgar alimtuma Edgar aandike ile barua, wakati huo Edgar alijitaidi kujizuwia kumtazama Monalisa lakini kunakupindi macho yao yaka kutana, na hakuna alie weza kuendelea kumtazama mwenzie, maana kila mmoja alitazamisha uso chini, huku Edgar akihisi kuwa Monalisa ndie aliemsemelea kwa mama yake.
Baada ya mama Edgar kumaliza kusoma lile karatasi kimya kimya, akatikisa kichwa kwamasikitiko, huku ana mkabidhi baba Edgar lile karatasi, kumbuka kipindi hicho mzee Mbogo, bado alikuwa bado ni mwanajeshi wa jeshi la ulinzi, ambae alipokea lile katarasi na kulisoma kimya kimya kama mkewake alivyo fanya, kisha akainua uso wake na kumtazama mama Monalisa ambae alikuwa amesimama toka amefika pale, “shemeji samahani sana kwa tukio hili, naomba uniachie nita limaliza mimi mwenyewe” alisema baba Edgar, akimaanisha kuwa ata mwazibu mwanae, hapo Edgar akjuwa yamekwisha, maana aliofia sana kuadhibiwa mbele ya Monalisa, na pia alijuwa fka kuwa baba yake asinge mwadhibu, maana uwa ni vigumu sana kwake kumwadhibu mwanae.
Mama Monalisa na Monalisa mwenyewe waliondoka huku mama huyu akiwa bado ame kasirika sana, walipotoka nje baba # Edgar aliangua kicheko kikubwa sana, akimcheka Edgar kwa maneno aliyo andika kwenye ile barua, mpaka saa tatu Edgar anaanza kusinzia, baba yake hakuwa ame mpatia adhabu yoyote, na kwa umri wake ilikuwa adhabu kubwa ni viboko tu!, lakini akiwa anaanza kupata usingizi ndipo akamwona mama yake anaingia akiwa ameshika bakora mbili mkononi, “najuwa baba yako ataki kukuchapa, ungejuwa ahibu uliyo niletea we mtoto, akika ungesha kimbia nyumba hii” alisema mama Edgar huku akimchomoa mwanae toka kwenye kitanda na kuanza kumtandika viboko, na ilikuwa mvua ya viboko kweli kweli,
Week ilikatika hakuna alie msogelea mwenzie, siyo Edgar wala Monalisa, wala wazazi wao, ambao ni kama waliingia katika mzozo mkubwa sana, huku wazazi wa Erasto na wazazi wa Monalisa wakizidi kuwa marafiki, kilicho mshangaza zaidi Edgar nikwamba ata Erasto pia akutaka kuongea nae tena, japo Edgar alishukuru sana kuto kuonyeshwa kwa zawadi ya ile chupi, lakini pia alishangaa kuwa ilikuwa wapi, au aikumfikia Monalisa,
Week mbili baadae Edgar alishuhudia wakina Monalisa wakihama, akika yeye binafsi hakujuwa walipo hamia, huku Monalisa akihamishwa shule, ila baada ya mwezi mmoja wakina Erato nao wakahama, hicho ndicho chanzio cha Edgar na Monalisa kupoteza urafiki wao, na kuendelea kuonana mala chache wakipishana kama watu ambao awakuwai kuwa marafiki, “kijana unaonekana kuwa na mawazo mengi sana” aliongea mzee Mohamed baba yake Salma, aliekuwa akienda gari kwa mwendo wa wastani, akimtua Edgar toka mawazoni, “atakuwa ana waza uwa kosa marafiki zake, wa chuo” alisema mama Salma alie kuwa amekaa seat ya mbele, karibu na mume wake, wote wakacheka, Sasa walikuwa wamesha tembea karibia nusu ya safari, toka mbeya kwennda makambako ***
Naam ilisha timia saa kumi nambili, Lukas na Mtutuma walikuwa wamebakiza kilomita chache kuingia makambako mjini, ndipo Mtutuma alipoanza kuona mabadiliko, ni baada ya kila gari walilopishana nalo, kuwa washia taa za tahadhari, ikionyesha mbele kuna jambo, mala nyingi madereva uwashiana taa hizo, endapo mbele kuna polisi wa salama barabarani, “kaka huku mbele kunaonyesha kuna jambo, ngoja kwanza tu ulizie kwanza maana naona jamaa wanawasha taa nyingi sana” alisema mtutuma huku akipunguza mwendo zidi na kuliegesha gari pembezoni mwa barabara, sehemu ambayo ilionyesha kuwa ni kituo cha daradara, mala wakaona linakuja bus dogo linaloelekea Njombe, wakalisimamisha…. itaendelea……. , endelea kufwatilia mkasa huu, hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!