
SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA MBILI : Lakini wakiwa wana karibia kuufikia mlango mdogo wa chuma wakutokea nje, upande nyuma mala wakasikia, “wale kule” hapo wote wawili wakageuka na kutazama nyuma yao, naam wote wawili wali waona wale vijana wawili walio ingia mala yamwisho chumbani kwa Monalisa, wakiwajia mbio mbio, na bastora zao mikononi, Endelea…………..
Hapo bila kuuliza wala kulezwa na mtu, Edgar akajuwa kuwa alichoambiwa na Monalisa ni ukweli mtumtupu, kuwa watu hawa wata wauwa, hivyo Edgar akushangaa, yani akiwa bado ameushika mkono wa Monalisa akamvuta kwanguvu na kuutanguliza mbele, usawa wa mlango mdogo wachuma na yeye akifwatia, nyuma yake, haraka kama upepo, wawili hawa walifanikiwa kupita kwenye kile kimlango, ambacho wengi ukitafsiri, kuwa ni kimlango cha watu wazinzdi kuingilia kwenye nyumba za wageni, walipofika nje wakaanza kukimbia kwenye barabara ya pembeni yenye vumbi (service Road) kuelekea upande wa kuelekea mbeya, pasipo Edgar kumwachia mkono Monalisa,**
“Pumbavu inakuwaje nyie wajinga, mnazidiwa maharifa kijinga namna hii, tena na binti mdogo kabisa?” alisema Kibabu huku akiwa tazama Charles na Mike, waliokuwa wanarejewa na fahamu, kwa macho yaliyo jaa hasira kali, “akuwa peke yake afande, ilikuwa ghflasasna alipovamia kijana mmoja mtukutu” alijitetea Mike, wakati huo askari wengine wawili, walisha toka kwenda kuungana na wale wawili wengine, kwenda kuwaandama wakina Monalisa na Edgar, “inukeni haraka kachukueni SMG kwenye gari” alisema sajenti Idd Kibabu, huku anatoka nje na kuelekea nje kabisa ya bar, walikosimamisha gari lao, la jeshi la polisi, akifwatuiwa na wakina Charles, huku wakipita pale kwenye ukumbi wa bar, ambapo waliwapita watu weni wakiwa wanaendelea na starehe zao, pasipo kujuwa kuwa kunamatukio yamepita huko ndani,
Kibabu na wakina Charles waliingia kwenye gari, na kuzungukia upande wa barabara, walikohisi kuwa wakina Edgar wamekimbilia, wao walipita barabara ya rami, na sasa walipishana na magari makubwa ya mizigo na vibasi vidogo vya abaria, vilivyo kuwa vinatokea Mbeya, baada ya kutembe kidogo, waliweza kuwaona wale askari wake wanne walio kuwa wana wafukuza wakina Edgar wakiendelea kuwa fukuza vijana hwa wawili, waliokuwa mita chache mbele yao, “mnasubiri nini nyie” alipaza sauti Kibabu huku anatoa bastora yake na kuifunga kile kibomba cha kuzuwia sauti, wakati huo aliwaona wale askari wake alio wapigia kelele, wakiinua basor zao na kuanza kufyetua risasi, ambazo zilitoka kimya kimya, lakini bahati ilikuwa upande wa wakina Monalisa na Edgar,
Maana wakati wakina Edgar wanapata wazo la kuingia chochoroni kupa mwanga wa gari la polisi, baada ya kumsikia sajent Kibabu akipia kelele kuwa ‘mnasubiri nini nyie’ na ndio wakati walipo shuhudia risasi ziki gonga pembeni yao, na wao wakaingia kwenye moja ya chochoro na kupotelea gizani, na walipo imaliza nyimba moja waka kata kona kushoto, wakawa kama wanarudi walikotokea, yani Makambako mjini, lakini kwa njia ya uchochoro, na baada ya nyumba moja tena waka kata kulia, wakizidi kuzama kwenye giza, na kuelekea wasiko kujuwa, lakini hawa kupita ata nyumba tatu, waka kata tena kona upande wa kushoto, ambako Edgar aliamini upande huo hauta mpoteza, sasbabu ndiko waliko tokea, yani makambako mjini, sasa hawa kuweza kuhisi mtu yoyote akiwafwata, na hakuna kati yao alie hisi kuchoka, kiasi cha kumshangaza Edgar, maana akutegemea kama monalisa, angeweza kukimbia vile, na viatu mkononi, maana yake, alikimbia peku peku ****
Kibabu aliwashuhudia wale askari wake, wakizama uchochoroni, kule walikoelekea wakina Edgar, akamwambia dereva asimamishe gari, na wao wakashuka, sasa walibeba SMG, wakaingia kule uchochoroni, lakini hawakufika mbaliwakawakuta wale wenzao wanashangaa wasijue wakina Monalisa wameelekea wapi, “mpaka hapo hawa nao sio wakuwaacha, maana wanaonekana wamesha juwa kinacho endelea” alisema kibabu, kwa sauti iliyo jaa hasira kali sana, “ok! Mike na Charles nifwteni, nyie wengine gawaneni njia, endeleeni kuwasaka, kumbukeni mkiwapata ni kuwa uwa kabisa na kuchukuwa tape” alisema Kibabu na kuanza kuondoka, kuelekea kwenye gari lao, huku akifwatiwa na wakina Mike, wakiwaacha wale askari wanne wakigawana wawili wawili kila kindi likipita upande wake kuendelea kuwasaka wakina Edgar, leongo ni kuwa uwa kanibisa,
Sajent kibabu alirudi pale hotelini na kumwona manage wa hotel, wakajitambulisha kuwa ni polisi, na wanaitaji kufanya ukaguzi kwenye vyumba viwili yani namba kumi na nane, na kumi na saba, manage wa hotel hii ambae alikuwa ni kijana mmoja wa kiume, hakuwa mbishi, aka wa ruhusu, pasipo kuhoji maswali mengi, japo alipatwa na wasiwasi kidogo, polisi hawa, walioongozwa na sajent Kibabu, waliingia chumba namba kumi na nane, yani kile cha Monalisa, na kuanza kupekekuwa begi lake kubwa, ambamo ndani walikutana na nguo na vitabu, na album ya picha, za mrembo huyo, na katika upekuzi huo wakafanikiwa kutambua kuwa mschana huyu mrembo ana itwa Monalisa Andersn, na atokea Mbeya chuo cha biashara, anaelekea songea, “huyu ni binti wa mzee Anderson” aisema Kibabu, “unamaanisha yule mzee tajiri, anae kaa Luhuwiko?” aliuliza Mike, “ndio ni yule mwenye maduka ya vifaha vya ujenzi na magari yaendayo tunduru na masasi” alijibu sajenti Kibabu, ambae alitulia kidogo na kushindwa kuongea zaidi, sababu manager wa hotel alikuwepo mle ndani ya chumba,
Baadaa ya kulizika na msako wa chumba hicho, wakaamia chumba cha pili, ambacho kilikuwa cha Edgar, huyu awakupata kazi kujuwa utambulisho wake, maana ile kuingia tu, wakakutana na bastora kitandani, pamoja na kitambulisho chini ya sakafu, “Edgar Eric Mbogo” alisema Kibabu akiwa ameshikilia kitamburisho cha Edgar alichokuwa anakitumia kipindi yupo chuoni, pia sajent Kibabu aka pekua kwenye begi la Edgar na kukuta vitu vingi sana, ikiwepo mavazi na vitabu vya chuo, pia kama walivyo kuta kwa Monalisa, walikuta album ya picha, ambazo zilitosha kuwajulisha kuwa kijana huyu mwanamichezo, na alitokea Songea, ni baada ya picha zake nyingi, kuwa za michezo, na zilipigiwa Songea, akachukuwa picha mmoja iliyo onekana vizuri kisha akamtazama meneja wa hotel hii, “manager ifadhi mizigo ya hawa vijana, endapo wata kuja hapa kuifwata, piga simu kituo cha polisi haraka” alisema Kibabu, wakati wana ondoka zao, ***
“nikama naona kesho inachelewa” alisema Erasto, kwa sauti ya kilevi, akiwa amekaa kwenye kiti, iliyo tanguliwa na meza ndogo, iliyo tapakaliwa na chupa kadhaa tupu za pombe, ikisalia moja tu yenye pombe, “unanitamanisha au una niumiza?” aliuliza mwanamke mmoja alie kuwa amekaa kwenye kiti cha jirani yake, mwenye kuvalia shati jeupe na sketi fupi sana nyeusi, “hapana bwana siunajuwa sija mwona muda mrefu” alijibu Erasto hku akiinua chupa ya bia na kuiweka mdomoni, aka gugumia kidogo, kisha akaishusha, “najuwa akija, ndio itakuwa basi tena” alisema yule mwanamke kwa sauti ya kulalamika flani hivi, “haaaa wapi, mambo yetu yataendelea kama kawaida” alisema Erasto huku ananyoosha mkono kuupeleka kwenye apaja ya mschana huyu, ambayo yalikuwa nje nje, kutokana na kushindwa kuifaziwa na kile kisketi kifupi, sijuwi akuwa anasikia baridi, maana ukiachilia baridi iliyo kuwepo, pia walikuwa nje, sambamba na wateja wengine pale mwembeni bar, “niache kumfaidi bikira wangu, nije niangeike na wewe” alijisemea Erasto kimoyomoyo, huku ana papasa paja la mwana dada huyu.
Huyu alikuwa ni Erasto Richard Misago, ambae akujuwa kuwa mwanamke anae mzungumzia kwasasa yupo katika hali ngumu.**
“Mama Eddy, mbona kama umekosa amani ghafla?” aliuliza baba Edgar akimtazama mke wake, ambae alionekana kuwa mnyoge ghafla, “baba Eddy, unajuwa toka nikiwa jikoni, zimenijia hisia mbaya juu ya mwanangu, yani ghafla nimekosa amani, sijuwi ana tatizo gani huko” alisema mama Edgar, wakati huo walikuwa mezani wana kula chakula cha jioni, mzee Mbogo akatabasamu kidogo, “umeshaanza mke wangu, na wewe unajiwa ukianza kuwaza hivyo, kunajambo linatokea kweli” alisema baba Edgar huku akiendeleakukamua msosi, “siyo hivyo mume wangu, lakini ujuwe Edgar haja piga ata simu kutuambia kama kesho anasafiri amala” alisema mama Edgar huku akishindwa kabisa kula chaula, “basi hivi ulivyo mkumbuka na yeye ametukumbuka, atapiga simu sasa hivi” alisema baba Edgar akimwondoa wasi wasi mke wake. ***
wakati mama Edgar anapata hisia hizo juu ya mwanae, Edgar na Monalisa nao walikuwa wana katiza chochor ndani ya mitaa ya Makambako, nasasa walisha fika mbali kidogo, “Edgar miguu inauma siwezi kukimbia tena, alisema Monalisa alie shikilia viatu mkononi na kifuko cha vitumbua, huku kishkwa mkono na Edgar, hapo Edgar akaacha kukimbia na wakaanza kutembea, nikweli Monalisa aliekuwa peku peku, alikuwa anachechemea, “unge vaa viatu kwanza utawezaje kutembea peku peku usiku huu” alisema Edgar ambae alionekana kutoelewa elewa jinsi mambo yanavyo enda, “watatukamata, bola tutafute kwanza sehemu ya kujificha” alisema Monalisa, huku wakizid kusonga mbele, na sasa walitokea kwenye sehemu ya wazi, “kwani hawa jamaa ni wakina nani?” aliulliza Edgar huku akisimama, kufwatia Monalisa kusimama ghafla akishindwa kutembea, kutokana na miguu kuzidi kuuma, “wale ni polisi, wame muuwa mtu” alisema Monalisa, huku akitaka kukaa chini, “ebu subiri kwanza, hapa siyo sehemu ya kukaa, tunatakiwa tutatufute sehemu tupumzike” alisema Edgar huku akimnyanyua, Monalisa, na sasa aka upachina mkono wa monalisa begani kwake, alafu taratibu wakaanza kutembea kuelekea ndani kabisa ya mtaa. ****
Songea mjoni, mtaa wa mahenge A, ndani ya nyumba moja ubwa sana ya kifahari, mkuu wa kitengo cha upelelezi wa makosa ya jinai, bwana Manase Kingarame, alionekana ndani ya chumba kimoja kidogo, akiwa amesimama mbele ya kamasha kdhaa ya chuma, ni yale yaliyo ibwa kule hifdhi ya mali za wanachi, akalifungua moja yakasha, kati ya makasha hayo, ambalo lilikuwa na dhahabu nyingi sana, mzee huyu mwenye mwili wa mviringo kutokana na kuwa mfupi alafu mnene, akatabasamu kwa furaha, kisha akalifunga na kufungua jingine, ambalo lilkuwa na ma vitu mchanganyiko, vyote vikiwa vya thamani kubwa sana, sasa alichekelea kabisa,
Wakati bwana Manase Kingarame anaendelea na ukaguzi huo, akasikia mlio wa simu toka sebuleni, akatoka mle chumbani na kuifwata simu ile, huku akijuwa kuwa mpgaji ni mmoja wa vijana wake wakazi maana ni watu wachache sana walio juwa umiliki wake wa nyumba hii, zaidi ni askari wacache wasio zidi kumi na saba, ambao uwatumia kwenye kazi zake nje ya utumishi wa serikali, yani pamoja na wakina kibabu, na dereva wao, “hallow King naongea hapa” ndivyo anavyo jitambulisha mzee huyu akiwa ndani ya nyumba hii, ambayo ata familia yake ambayo hipo Tanga, aijuwi kama mzee huyu ana nyumba hii, “mzee ni mimi Kiba, mambo yameenda tofauti kidogo, lakini sasa tuna karibia kufanikiwa” ulisikika upande wapili, ambapo alikuwa ni bwana Idd Kibabu, alie msimulia bwana Kingarame jinsi walvyo mtekekteza Lukas, na kwamba sasa wana wasaka vijana hawa wawili walio kabidhiwa tape, “hapo tumia hakiri ya kuzaliwa, kwanza kabisa huyu kijana wakiume apewe kesi ya utekaji, yani kamteka huyo binti, unajuwa maana yake?” aliuliza Kingarame, bado sijakuelewa mzee, maana huyo binti ndie alie kabidhiwa tape na kuelezwa kitu na Lukas, huyu kijana nikama alivamia ugomvi asio ujuwa” alisema Kibabu akifafanua jinsi ilivyo, “sikia Kiba, kesho mchana natanga utekaji huo baada ya nyie kutanga huko, alafu baada ya mambo kukamilika itabakia kuwa, mtekaji alimuuwa binti na yeye ame uwawa katika majibizano ya risasi na polisi” ilikuwa ni jambo jepesi kulipanga kwa mdomo, lakini sijuwi kwa vitendo itakuwaje, **
Denis Stella na wenzao wawili, baada ya kukaa kwamuda mrefu, wakimngoja Monalisa bila mafanikio, Denis na Stella waliamua kwenda tena chumbani kwa Monalisa kumtazama, akikawalikuta chumba kitupu kabisa, wakashangaa, ikabidi watoke na kwenda kuulizia mapokezi, ambako dada wa mapokezi aliwakutanisha na manager, ambae mwanzo alihisi kuwa watu hawa ndio wnao uliziwa na polisi, “wewe ndio Monalisa?” aliuliza meneja, akimtazama Stella, “hapana mimi naitwa Stellani raiki wa Monalisa, tumekuja nae toka mbeya, sasa toka alipoingia ndani kwake hatuja mwona tena” alisema Stella, akisha akamwona yule meneja pasipo kujibu kitu akiinua mkono wa simu na kubnyeza namba flani, kisha akapiga, na sekunde chache baadae akaanza kuongea, na simu pasipo wao kusikia upande wapili, “ndio mzee ni meneja wa ile hotel uliyo kuja muda mfupi uliopita…… siyo wao ni rafiki zao… sawasawa” alimaliza kuongea yule meneja, kisha aka kata simu na kuwatazama wakina Stella na Denis, “tunawaomba msubiri kidogo hapa hapa” alisema meneja, na wakina Denis wakatazamana kwa macho yenye maswali mengi,
Baada yakuwa amesha wasiliana na bwana Kisona, na kumweleza jinsi alivyo shuhudia Lukas akipoteza maisha, mwana dada Rehema Haule ali tulia dukani kwake na kuanza kufanya hesabu ambayo alikatiza wakati ule, huku ikimjia picha ya kijana Lukas alie kuwa amelala bara barani, akivujwa nadamu nyingi sana, “Wakatili sana wale mashetani, sijuwi kaka wawatu ame wafanyan nini?” aliwaza Rehema, huku akiendelea kufanya mahesabu yake, haraka haraka, maana muda wa kufunga duka ulisha fikia, ilisha karibia saa nne, “habari za kazi dada” Rehem alistuka baada ya kusikia sauti hiyo iliyo msalimia, akainua usowake na kutazama msalimiaji, macho yake yakakutana na watu wawili kija awakike na wakiume, walio shikana kanakwamba huyu wakike ameumia mguu, “nzuri vipi huyu mwenzako anaumwa?” aliuliza Rehema huku akimtazama Monalisa, “ndio tunaitaji kununua dawa za vidonda na bandeji” aljibu yule kijana wa kiume, hapo Rehema aka mtazama tena yule wakike, “hooo pole sana” alisema Rehema akainuka haraka na kuanza kuchukuwa dawa, “asante” alijibu Monalisa akijikakamua kwa kuonyesha tabasamu usoni kwake, akificha maumivu ya nyayo zake, Rehema aliwa chagulia dawa kadhaa za vidonda ikiwepo na spirit, pia pamba na bandeji, alafu akawakabidhi, “elfu mbili” hiyo ndiyo ghalama ya dawa na bandeji, ilikuwa rah asana kippindi hicho, nazani kwasasa ni kama la teni hivi lingewatoka, “asante sana” alijibu Edgar, huku anapokea dawa na kukabidhi elfu mbili katika noti za elfu moja moja, “samahani dada, kuna guest yoyote hapa karibu?” aliuliza Monalisa, Edgar akamshangaa mschana huyu, lakini hakuongea kitu, “huko mbele upande wenu wa kushoto, mtaona kuna kama kibar flani kidogo sasa nyumba ya pili toka hapo, kuna guest” aliwaelekeza Rehema, ambae alihisi kuwa wawili hawa ni wapenzi, kwa jinsi walivyo onekana kupeana uangalizi wa hali ya juu asa wakati wa kuondoka, maana Edgar alimkokota taraibu na kwa umakini mkubwa sana Monalisa, “yani majanga yote haya anakumbuka kulala” alijiuliza Edgar moyoni mwake, **
Dakika chache baadae, sajent Kibabu na askari wake wawili, yani Mike na Charles, waliingia pale hotelini wakimwacha dereva akiwa nje na gari, wao wakaingia moja moja mpaka mapokezi ambako walimkuta meneja na wakina Stella, ndipo mahjiano yalipoanza ni baada ya wakina Kibabu kujitambulisha, kuwa wao ni polisi,
Maswali na jibu yalikuwa ni kama yale yale tu, majina kamili, wanatokea wapi ilikuwaje wakampoteza mwenzao, na wana mfahamu vipi Edgar, baada ya hapo wakina Stella wakaelezwa kuwa Edgar alikuwa anashirikiana na jambazi mmoja alie kuwa anaitwa Lukas, ambae ame uwawa, na yeye Edgar ame mteka Moalisa na kutoweka nae, hivyo wakijuwa wapo wapi watoe taharifa kituo cha polisi, hivyo ndivyo mchezo ulivyoanza, kumwelemea Edgar, maana Denis na Stella waliamini moja kwa moja ata bila kujiuliza inawezekana vipi, wakati Monalisa alitoweka wakati wao wakiwa na Edgar. ***
“tulikuja kuulizia vyumba hapa” alisema Monalisa, wakati yeye na Edgar wakiwa wamesimama mbele ya mlango wa jengo moja chakavu la guest house, siliso na jinakipindi hicho waliita guest bubu, wana msubiri mhudumu wa vyumba, ambae tayari walisha mgongea mlango, na kuwaammbia kuwa wamsubiri anakuja, “lakini walisema kuna chumba kimoja tu” alisema tena monalisa, itenelea…… hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU