BIKIRA YA BIBI HARUSI (19)

SEHEMU YA KUMI NA TISA
.
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA NANE: Hapo Kingarame ambae aliona dariri za kustukiwa, kwa mchezo mchafu anao ucheza, akasimama haraka ili kuweka sawa, “afande hapo kuna jambao ambalo tunatakiwa tulifahamu, ni kwamba huyu jambazi alimteka Monalisa kama kinga ya kuto kushambuliwa na polisi, wakati anawakimbia” alisema Kingarame, endelea……
Hapo kikapita kimya kidogo, watu wote mle ndani wakisubiri kauri ya RPC alie onekana, kuwaza jambo, kisha akainua usowake na kumtazama RCO Kingarame, “kwanini iwe Monalisa, mschana ane mfahamu, nasiyo mwanamke mwingine hapo Makambako?” swali la RPC, lilimstua Kingarame, ambae alificha mstuko wake, “afande mazingira yalikuwa ni ya hotelini, ambapo binti huyu alikuwa amefikia, na ndio sababu ya wawili hao wanao fahamiana kukutana, na nio muda ambao askari wetu walikuwa wanamvamia jambazi huyo, alie amua kumteka Monalisa kama kinga yake, zidi ya polisi” aliongea RCO Kingarame, na hapo wakuu wote mle ndani wakaoneka wakitikisa vichwavyao, juu chini, wakionyesha kuwa wamekubari na kuelewa kilicho ongelewa na kamanda mwenzao, SSP Kingarame, “ok! nakuagoza RPC, ukalitangaze hilo kwenye redio, kisha na wewe mwenyewe, uende ukaungane na na askari waliopo Makambako kumsaka huyo jambazi, maana jukumu ili limesha kuwa kubwa kuongozwa na sajent, ukichukulia tumesha wapoteza askari wawili” alisema RPC, alieonekana kuchanganywa na na jinsi mambo yalivyoenda, “RCO inaitajika umakini wa hali ya juu, inaonyesha huyu jambazi wa pili ni hatari sana, maana yule wakwanza aja sababisha kifo wala majeruhi, ila huyu, leo tu! amesha wapoteza wawili” alisema RPC, kwasauti iliyo onyesha msisitizo, ***
Kanali Joseph Kisona, akiwa amesha sikia taharifa ya kamanda wa polisi upelelezi, mkoa wa Ruvuma, juu ya tukio la utekaji lililo fanywa na kijana Edgar Eric Mbogo, alishuka toka kwenye gari lililo simama nje ya nyumba namba 26, ikiwa ni nyumba moja wapo, kati ya nyingi zilizo kaa kwa mpangilio na kufanana, ni baada ya kubadirisha uelekeo akiwa njiani kwenda kwa brigedia Haule,
Kisona aliufwata mlango namba ishilini na sita, tayari kuugonga, yani kupiga hodi, lakini labla hajafanya hivyo, akauona mlango ukifunguliwa, na hapo aka mwona koplo Katembo akitokea, akiwa ndani ya bukta na tishet, “umeona mchezo unao endelea, Katembo?” aliuliza Kisona baada ya kusalimiana na Katembo, wakibakia wamesimama nje ya nyumba hii, katika nyumba za kuishi askari, “kwani linausika na tukio la NMC?” aliuliza Katembo, “siyo kuhusika, ni mwendelezo wa tukio lile” Kisona alimsimulia Katembo jinsi mambo yalivyo kuwa, na kisa cha wakina Monalisa na Edgar, “alafu unajuwa, kuwa huyu kijana ni mtoto wa yule mzee alie staafu miaka mitat iliyo pita?” alikumbusha Katembo na hapo Kisona akapata ufahamu, “kumbe ni Edgar yule, ambae kunakipindi tulimtumia kwenye timu ya jeshi ya mpira wakikapu?” aliuliza kwa mshangao Kisona, “ndio maana yake, tena baba yake anaishi hapo seed farm” alijibu Katembo, akiwa na uakika na anacho kisema, “napajuwa kwa mzee Mbogo, tena yule kijana anasoma chuo huko MBEYA, wacha mimi niende nikaongee na wazazi wake, maana najuwa watakuwa katika wakati mgumu sana” alisema Kisona, na wakati wao wakiongea hayo, mala wakasikia mskia dereva anawaita, “afande nivyema mkaja kusikia taharifa hii kwenye redio” wote waka sogelea gari huku masikio yao wakiwa wameyatega kama antenar, “kijana huyu ambae jana usiku alimteka, Monalisa, imebainika kuwa ni jambazi sugu, alie kuwa anashirikiana na jambazi Lukas, jambazi Edgar Mbogo, ame tekeleza mauwaji ya askari polisi wawili, leo mapema, katika majibizano ya risasi” lisikika sauti ya kamanda Kingarame toka kwenye redio ya gari, hapo Kisona na Katembo wakatazamana, huku macho yao yakionyesha mshangao, “bado tunaendelea kufanya juhudi za kumnasa jambazi huyo” aimaliza kutangaza SSP Kingarame, “siwezi kumwacha huyu kijana wammalize, ngoja niende kwa mzee Mbogo, kuna mambo nataka kujuwa” alisema Kisona huku ana ingia kwenye gari na dereva aka washa gari tayari kuondoka, “na wewe akajiandae nikukute ofisini, mpigie simu mkuu mwambie nikitoka seed farm nitaenda nyumbani kwake” alisema Kisona akimwambia Katembo, “nilisha lijuwa hili kabla ujasema” hilo lilikuwa jibu la Katembo ambae aliingia ndani haraka na kuanza kujiandaa, akijuwa kuwa ile safari iliyo ghairishwa jana usiku, ndiyo hii imewadia, **
Wakiwa njiani, ndani ya land rover 109, mzee Mbogo na mama Edgar, wawalionekana kushtushwa sana na taharifa hii yapili, kuliko ile ya kwanza, ya utekaji, “nilijuwa kutakuwa na tatizo, ona sasa mwanangu ujambazi ameanza lini?” aliuliza mama Edgar kwa sauti iliyo ambatana na kilio, “kuna mchezo unachezwa, juu ya Edgar, eti anashirikiana na jambazi Lukas, wakati mtoto alikuwa Mbeya, anasoma, inawezekana vipi?” aliuliza mzee Mbogo ambae alikuwa anaendesha gari kwa kasi ya hajabu kuelekea seed farm, nyumbani kwake, ata mke wake akujuwa mzee huyu anawai kitu gani huko nyumbani, “unaenda wapi sasa?, twende polisi tukawaambie kuwa Eddy siyo jambazi” alisema mama Edgar kwa sauti ile ile iliyo ambatana na kilio cha kwikwi, “polisi awawezi kubadiri mawazo yao, mpaka waakikishe wame muuwa Edgar, bora tu, niwai Makambako, nika msaidie” alisema mzee Mbogo, huku akizidi kupanga na kupagua gia, huku pedor yam mafuta ikikanygwa kiasi cha kugusa sakafu ya gari, **
wakati Songea mambo yakiwa hivyo, huku porini mpakani mwa makambako na Njombe, Edgar alikuwa amesimama pembeni ya Monalisa, aliekuwa amekaa kwa kunyoosha miguu, akifaidi kimvuli cha mti huu mkubwa kihasi kuliko miti iliyopo eneo hili, wawili hawa kila mmoja alikuwa anawaza la kwake, wakati Edgar akiwaza kuhusu, namna ya kutoka huku porini na kufika songea, akiwa na Monalisa, kitu ambacho aliamini kita msafisha na kumfutia makosa aliyo yafanya miaka yanyuma ya kumpatia binti huyu mrembo barua ya mapenzi na zawadii ya chupi nyekundu.
Monalisa yeye akiwa amesha sahau kuwa leo ndio siku ya kuvalishwa pete na Erasto, alikuwa anawaza yake, kwanza uchovu aliokuwa nao, pili alijiona amemwingiza Edgar kwenye matatizo makubwa, maana ukiachilia wote wawili kuandamwa na polisi, pia Edgar amesingiziwa kuwa amemteka yeye, “Edgar tukifika salama, nitakutetea kuwa hukuniteka” alisema Monalisa aliekuwa anamtazama Edgar kwa macho ya huruma, lakini akashangaa kumwona Edgar anacheka kidogo, huku ana geuza shingo kumtazama, macho yao yaka kutana, “jifikilie wewe Mona, awa watu wanataka kutu angamiza, siyo wewe siyo mimi, akuna wanae mtaka zaidi ya huo mkanda wa video” alisema Edgar, kisha aka tazama upande mwingine, wa lile pori.
ila kutazama tu! ghafla aka jiangisha chini, kitendo kilicho mstua sana Monalisa, ambae alikurupuka pale chini akitaka kuinuka, lakini Edgar aka wai kwa kumbana na mguu wake, huku ana iweka sawa buduki yake, na wakati huo huo, ikasikika mvua ya milipuko ya risasi mfululizo, wenyewe wanaita rapid, na kupita juu kidogo ya wakina Edgar, “usiinue kichwa!” alipiga kelele Edgar huku ana iweka sawa bundki yake, na kuikoki, akiweka risasi chemba, kisha akiweka vizuri, akikiegemeza kitako cha SMG kwenye nyama za kwenye bega lake, la mkono wa kulia, na na kupeleka kidole kwenye kifyetulio, (trigger) kisha aka achia risasi tatu mfurulizo, “jificheni anashambulia huyoooo!” ilisikika sauti toka upande unaotokea mashambulizi, huku mapigo ya risasi ikikoma, “nisaidieni jamani, ameni piga kwenye bega” ilisikika sauti nyingine, sambamba na migumo ya maumivu, ikionyesha kuwa, mmoja wa askari wanao washambulia wakina Edgar, amechapwa risasi, kumbe tayari kikundi cha polisi wanao ongozwa na PC Khassim, kilikuwa kimeshafika.
hapo Edgar akaona huo ndio wasaa wa kuondoka eneo hili, kimbia upande wakulia” alisema Edgar akimweleza Monalisa, ambae akusita, aliinuka nakutoka mbio, huku Edgar akiendelea kupiga risasi tatu tatu kuwazuwia wale askari wasiweze kujitoa kwenye maficho yao, Edgar aliendele kuiga risasi kwa ungalifu wa kuto kuzimaliza, mpaka alioona Monalisa amfika mbali kidogo, ndipo na yeye akaanza kupiga huku anarudi nyuma, mpaka lipoona amefika sehemu ambayo anaweza kukimbia pasipo kuzurika na risasi, akatimua mbio huku akimtazama Monalisa alie kuwa mbele yake umbali wa mita miamoja, na polisi huku nyuma yao wakaanza tena kushambulia, huku wakiwafwata, inaitwa mapigo yana mwendo, (fire and movement)
Sasa basi, wakati Edgar ana kimbia huku akimfwata Monalisa alie kuwa mbele yake, kwa umbali huo wa mita 100, Edgar akaona kitu kama vumbi likitimka, kuja uswa wa kule wanako kimbilia, kwa haraka haraka ungesema kimbunga, ila kutokana na mtindo wa mwendo wa vumbi hilo, na kasi yake, akajuwa kuwa ni gari, japo akusikia muungurumo wa gari hilo, kutokana na sauti za milipuko ya risasi za polisi, kwa hiyo mbele yao kulikuwa na barabara ya vumbi, akiwa bado anakimbia Edgar akamtazama Monalisa akamwona akiongeza speed kukimbilia mbele huku akipiga kelele, “tusaidieni tuna kufaaaa!” inamaana Monalisa alisha liona lile gari na kuona kuwa, ndio msaada pekee ulio bakia, hapo Edgar akatazama tena kule kwenye lile vumbi.
Naam alicho kiona ni gari aina ya rand rover 110, ni lile la polisi, inamaana Monalisa hakuwa amejuwa kuwa lile gari ni lapolisi, “Monaaaa, usi ende hukooooo!” alipaza sauti Edgar, lakini aikuwa na mafanikio, maana Monalisa aliendelea kukimbilia kule kwenye barabara, huku akionekana wazi lengo lake ni kuliwai gari kabla halija katiza usawa wake, hapo Edgar akajuwa kuwa akichelewa ata mpoteza Monalisa, hivyo aka ongeza speed kumkimbilia Monalisa, alie kuwa amebakiza hatua chache kuifikia barabara ya vumbi ambayo sasa walikuwa wanaiona kwa ukaribu zaidi, huku Edgar akiweza kuwaona askari nyuma ya gari wakiwa wameweka bunduki zao tayari kuchukuwa uhai wa mtu atakae jitokeza, na kwa sasa ni Monalisa, ambae alikuwa karibu na barabara.
Edgar alikimbia kwanguvu sana, huku ana badiri mkebe wa risasi, akiutoa ule wenye risasi chache na kuuweka ule ambao akuwa ameutumia kabisa, maanayake ulikuwa na risasi 30, aklipo upachika kwenye bunduki yake, ambayo tayari risasi moja ilikuwa chemba, kutokana na kuwa ametoka katika mapigano, EDGAR akaiweaka usawa wa bega lake na kulilenga lile gari ambalo sasa alikuwanaliona vyama kabisa, lakini kutokana na mbio alizokuwa ana timka, akashindwa kuliweka katika kilengeo, hivyo aka ukadiria umbali wa maadui zake wanyuma, na kuona anaweza kufanya jambo kabla awaja mkuta, hivyo akasimama na kuiweka bunduki vizuri akiibana vyema kwenye bega, na kufumba jicho la kushoto, akalijaza gari kwenye kilengeo cha nyuma na mbele. **
Nyumbani kwa bwana Anderson, tayari watu walikuwa wamesha tawanyika, na kubakia wachache, ambao walikaa nje ya viunga vya nyumba hii, wakinywa pmbe ambazo tayari zilinunuliwa kwaajili ya kunyweka, huku ndani ya chumba kimoja cha sebule ndogo ya ndani kabisa ya nyumba ile, kuna maongezi yalikuwa yanaendelea, “yule mwanamke alimlea vibaya sana mwanae” alisema mama Erasto, akimshutumu, mama Edgar, mbele ya mama Monalisa na wengine wote walio enda kituo cha polisi, na sasa walikuwa nyumbani kwa kina Monalisa, yani kwa mzee Anderson, “nilijuwa tu huyu mshenzi ata taka kuni komoa” alisema Erasto huku akiinua chupa ya pombe kari, na kubugia, funda moja, hapo hakuna wakumshangaa mwenzie, maana wazee wote wawili pamoja na Erasto na mama yake walikuwa wana kunywa pombe, “yani naaidi huyu mtoto akikamatwa nita ghalamia hukumu yake, na hivi ameuwa polisi, lazima anyongwe tu!” alisema baba Monalisa, kwa sauti yenye ghadhab, kisha aka chukuwa chupa ya bia mezani na kuiweka mdomoni, kisha aka piga mafunda mamwili kwa mkupuo, na ikuishusha mezani ile chupa ya bia, “ila nivigumu kuamini, yani mwanangu sijuwi ana mfanya nini huko?” aliongea mama Monalisa, ambae alikuwa, katika hali ya uzuni sana.
Mlendani maongezi yaliendelea huku wakimshushia shutuma Edgar, pasipo kujuwa ni kitu gani kinaendelea kwa Monalisa na Edgar, kule porini. **
Wakati huo huo Kisona alikuwa ameshafika nyumbani kwa mzee Mbogo, ambapo walimkuta dada wakazi alie waambia kuwa, baba na mama wameenda mjini kumpokea Edgar anakuja kutokea mbeya, alikokuwa anasoma, “ok! nitakuja baadae, akija mwambie asitoke mpaka nije” aliaga Kisona na kuelekea kwenye gari, lakini kabla gari alijaondoka, wakaliona gari ain ya land Rover likija lwa speed, na kusimama kama vile limegonga ukuta, yani kwa bleack za ghafla, kisha akashuka mzee Mbogo toka kwenye gari, na wakati huo huo Kisona nae akashuka toka kwenye gari, na kukutana na mzee huyu ambae anamfahamu vizuri sana, ni mzee ambae alimpokea wakati Kisona anaamia hapa songea, “karibu afande” alisema baba Edgar, huku akipeana mkono na bwana Kisona, ambae alimwamkia, na kisha wakaingia ndani, na kuanza maongezi, huku bwana kisona akitaka kujuwa mambo machache toka kwa baba Edgar, “unazani ni kweli Edgar ame mteka Monalisa?” aliuliza Kisona, akimtazama mzee Mbogo, alie kuwa amekaa karibu na mke wake, “kumteka hiyo hapana ila, inawezekana kuwa wapo pamoja” alijibu baba Edgar, “mzee Mbogo, tuna mpango wakuelekea Makakambako, kwaajili ya swala hili, je una zani kwanini Edgar ameusishwa na haya yote, amaanisha utekaji na ujambazi?” aliuliza Kisona, alie onyesha kuwa makini sana, kutafuta sababu ya kuelekea Makambako, “hayo yote hayawezekani, sababu Edgar na Monalisa, wanafahamiana toka wakiwa watoto wadogo, licha ya mambo yaliyotokea hapa kati kati lakini, sizani kama yanaweza kuwafanya wasahau urafiki wao wa utotoni, ukichukulia wameishi pamoja huko chuo kwa muiaka mi tatu, alafu aje kumteka leo?” aliuliza mzee Mbogo, na hapo Kisona akakaa kimya kidogo kama anatafakari jambo, na wakati huo huo mzee Mbogo, akaendelea, “alafu wanasema eti anashirikiana na jambazi Lukas, kufanya ujambazi NMC, inawezekana vipi wakati jana alikuwa anamaliza chuo huko Mbeya?” aliogea mzee Mbogo kwa uchungu, huku akimkazia macho bwana Kisona, ambae alionekana kutafakari jambo, “mzee Mbogo, kunatatizo lolote ambalo liliwai kutokea kati ya familia yako, na familia ya bwana Anderson?” aliuliza bwana Kisona, na hapo mzee Mbogo akasimulia kisa cha barua iliyo andikwa na Edgar kwenda kwa Monalisa, “ukweli yalikuwa ni maneno ya mapenzi ya kitoto, nasijuwi kwanini Edgar aliandika ule upuuzi, maana walikuwa marafiki wa muda mrefu, na walicheza na kushinda pamoja muda wote” alisema mzee Mbogo, na kisha akaendelea, “Kisona naomba unipe muda nijiandae, naitaji kuelekea Makambako” alisema mzee Mbogo na kumfanya Kisona acheke kidogo,
“mzee Mbogo hilo swala ndilo lililo nifanya nije hapa kwako, sababu tunaitaji kuelekea huko makambako, kwaajili ya kuakikisha kijana wako na huyu binti wanapatikana, maana tunahisi kuwa wanaushaidi muhimu sana waka kesi ya NMC, hivyo jiandae tuta kupitia baada ya masaa mawili, tuanze safari” alisema Kisona, kisha akaaga na kuelekea nyumbani kwa brigedia mbako alitoa report na maamuzi aliyo amua kuyachukuwa, ikiwa ni kuchukuwa askari wa tano na kuelekea nao Makambako,
Brigedia Haule aliunga mkono uamuzi wa kanal Kisona, na kumpa kibari cha kwenda makambako, maana alishaona kuna ubabaishaji mkubwa sana, katika jambo hili, “namfahamu yule kijana, akikisha anapatikana akiwa salama” alisistiza mzee Haule, pia akisistiza kukutana na familia ya mzee Anderson nakawawke sawa, na kuwaondoa wasi wasi juu ya tuhuma za Edgar, hapo kisona aka toka nje ya nyumba ya brig Haule, nakuingia kwenye gari, akipanga kupitia kwa kamnda Kingarame, baada ya kutoka Luhuwiko kwa mzee Anderson,**
wakati huo huo kamanda wapolisi upelelezi mkoa, SSP Manase Kingarame, alikuwa ofisini kwake, akionekana kuwaza jambo lililo muumiza kichwa, “iliswala linaonekana kuwa hatari sasa, wacha niweke mambo sawa alafu, niweondoke zangu kulekea Makambako, lazima niakikishe huyu mpuuzi ana uwawa haraka sana” aliwaza bwana Kingarame, ambae alishazowea anapofanya tukio kama hili, uwa analimaliza kimya kimya.
Kingarame aliakikisha yanaandaliwa magari mawili, na askari kumi, alio wachagua yeye mwenyewe, akiwa na maana kubwa sana, hao ni askari ambao uwa ana watumia mla kwa mala, katika kazi zake za ukiukaji wa taratibu na sheria za jesi hilo la polisi,***
Ndani ya msitu uliop kati kati ya mji wa Makambako na Njombe, Koplo Mapombeka akiwa kilomita nne toka barabara kuu yarami, na gari lenye silaha nyingi za maangamizi, na askari kadhaa, alimsisitiza dereva wake, azidi kukanyaga mafuta ili kuliwai gari la wenzao, ambalo sasa waliona vumbi kwambele yao, japo kwa kilomita kama moja hivi au moja kasoro, ili wawai eneo la tukio, ambako alipania sana kumwangamiza jambazi Edgar.
wakati huo huo Mitamia sita toka lilipo gari la kina Mapombeka, mschana mrembo, Monalisa alizidi, kukimbilia barabarani kuliwai gari alilo liona likija upande alipokuwa anakimbilia, kwa lengo la kuomba msaada, maana polisi waliokuwa wana washambulia , walikuwa wanazidi kumja huku wakimwandama Edgar, huku milindimo ya risasi ikiendelea kusikika, na kumfanya Monlisa azidi kuisi kuwa, Edgar yupo kwenye wakati mgumu kuliko yeye.
Lakini ile Monalisa ana karibia kutokea barabarani tu! kwamacho yake akawaona, askari polisi kadhaa, wakiwa nyuma ya gari lile, wame mwelekezea mitutu ya bunduki zao, tayari kumfyetua, hapo aka jaribu kujizuwia, iliasimame na kubadiri uelekeo, kitendo kilicho sababisha apige mweleka, na kujibwaga chini, akiangukia barabarani, na kupigiza goti lake chini, ambapo aliliona lile gari likisimama ghafla. hapo Monalisa alijiwa kuwa tayari mwisho wake umeshafikia, “mama yangu, nimekwisha” aliwaza Monalisa huku anainua usowake kulitazama gari hili lililo simama karibu yake, akitarajia kusikia milipuko ya risasi, na kwamala ya kwanza aone kufa kuna kuwaje.
Wakati huo huo sajent Kibabu nae, akiwa amekaa seat ya mbele ya gari hilo, aliweza kumwona vyema kabisa Monalisa, akikimbia na kuangukia barabarani, hapo sajent Idd Kibabu akaachia tabasamu la fisi, “kiulaini kama kumsukuma mlevi” alisema Kibabu akitegemea kusikia miripuko ya risasi, zikimiminika kwa Monalisa, na kweli mala ikasikika pah! pah! pah! pah!, (wadau bado nasumbuka sana kwa tatizo la modem, ndiomaana nachelewesha story) itaendelea hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata