BIKIRA YA BIBI HARUSI (27))

SEHEMU YA 27

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA 26: “vipi aibu imeisha?” aliuliza Edgar, na Monalisa akaitikia kwa kichwa, kukubari kuwa aibu ime isha, “haya twende zetu” alisema Edgar huku anamshika mkono Monalisa, na kuanza kuongoza kukifwata kile kinjia, upande walio ambaiwa inaenda kutokea kijijini, lakini awakufka mbari, wakasikia ‘pah! pah! pah! pah!’ ilikuwa ni milipuko ya risasi za SMG, kutoka nyuma yao, endelea…..
“Hao wamesha fika” alisema Monalisa akizidi kujisogeza karibu kabisa na Edgar, kihasi cha kifua chake kugusana na kifua cha Edgar, huku mapigo yake ya moyo yakiongeza kasi, na pumzi kumtoka kwa fujo, “watakuwa pale kwenye vibanda” alisema Edgar, huku anageuka na kutazama, kushoto na kulia, mbele na nyuma, “sasa wana mfyetua nani?” aliuliza Monalisa kwa uoga, “akuna wengine zaidi ya wale jamaa tulio waachapale” alisema Edgar, huku akianza kutembea mbele, inakoelekea ile njia, akiwa ameukamata mkono wa Monalisa, kwa nguvu, “he! jamani wasije wakatusingizia sisi” alisema monalisa huku akifwata nyuma ya Edgar, alie kuwa amemshika mkono, “ilo siyo la kuuliza, kama siyo kutusingizia sisi, basi wata wasingizia wale jamaa kuwa ni majambazi” alisema Edgar, huku wakizidi kuchapa mwendo, na ulikuwa mwendo wa haraka kidogo, tofauti na mwanzo, na sasa walikuwa wana shuka kitu kama bonde flani, ambalo kimwonekano nikama vile kunashughuli za kilimo zilikuwa zina fanykaga, ndani ya bonde ilo lenye unyevu unyevu.
Walitembea kama mita mia moja mbele tayari walisha lifikia bonde hilo ambalo lilionekana wazi kuwa linatumika kwa kilimo, maana ukiachilia miwa na miti mingi ya mapera na matunda mengine, miti ya mianzi iliyo kuwa imetegeshewa vigemeo (mbeta), pia kulionyesha dalili ya kuwepo na mzao mengine, yaliyo vunwa siku zakaribuni, pia kulikuwa na vinjia njia vya kuingilia ndani ya mashamba hayo, ambayo haya kuwa na mtu, akika ilikuwa dalili tosha kuwa, huko mbele kuna makazi ya watu, Edgar akasimama na Monalisa nae akasimama, akatazama nyuma ya Edgar, ambae alitazama kushoto na kulia, “alie ogopa kulowa, alikosa kitoweo cha samaki” alisema Edgar huku ana ongoza kuingia upende wa kushoto akikifwata kinjia afifu sana chenye nyasi nyingi, zilizo shika umande, na sasa walikuwa wanatembea kama vile wanavuka mto, maana walilazimika kuinua ataua zao juu na kukanyaga kwa tahadhari, kama vile wananyemelea.***
“nazani sasa mmepata picha ya kinachotukabiri” alisema Kanali Kisona, akiwaelezea watu wake, baada ya kulishuhudia gari la polisi likiyumba yumba kwa bleack za ghafla, na kisha kukaa sawa na kuchapa mwendo, likitokomea mjini, “lazima tuta liona tena kabla atujaenda porini” Kisona huku anampa ishara baba Edgar, kuwa aondoe gari, “inanyesha awa jamaa wamepania sana, na nia yao ni kuakikisha wana mwangamiza kijana wangu” alisema baba Edgar, huku akiondoa gari taratibu, kuingia barabara kuu na kuongeza mwendo, kuifwata njia panda ya Mbeya,
“Kata kulia, fwata bara bara ya Mbeya” alisema Kisona wakati wana karibia pachani, mzee Mbogo akapunguza mwendo na kukata kona kuelekea upande wa kulia, kuifwata barabara ya Mbeya, akiongeza speed, “ukivuka njia ya kwanza, punguza mwendo kata kushoto” alisema Kisona, baada ya kuona kuwa wanaweza kupitiliza, ikawa hivyo, baba Edgar akapunguza mwendo mala tu baada ya kuiona njia ya pili, akawasha taa ya kuonyesha kuwa ana kata kushoto, na wakati huo huo wakaliona gari aina ya land rover mia na kumi, la polisi, likiwa lime simama upande ule ule wanao enda wao, likiwa na polisi wawili nyuma wenye bunduki zao, pia wawili walikuwa mbele, kanali Kisona alie kuwa makini sana kutazama kama kuna ane wafwwatilia, aliwatazama sana polisi hawa, ambao awakuonyesha kuwajali, zaidi polisi alie kaa set ya pembeni ya dereva aliwapungia mkono, kuwasalimia, wakati wana pita pembeni yao, Kisona nae akapuna mkono, “nyoosha moja moja kwa moja, mpaka kwenye majengo yale ya mbele” alisema Kisona, na baba Edgar aka kanyaga mafuta kuongeza mwendo, nikama alikuwa anaona anachelewa kwenda eneo la tukio. ***
Saa mbili na nusu, hii ndio mida ambayo Erasto aliishiwa kabisa usingizi, maana alipoingia tu kwenye chumba chake, namba kumi nasita, pale serena Hotel, akajilaza kitandani nakupitiwa na usingizi, mpaka mida hii ambayo usingizi ulikatika, na kila alipjaribu kulala tena aikuwezekana, alitulia kwa muda kidogo mala akasikia simu ya mezani ndani ya chumbakile ikiita, akanyoosha mkono wake na kuipokea, “hallow,” aliita Erasto, habari za asubuhi, hii kutoka mapokezi, kifungua kinywa chako kipo tayari, uletewe chumbani au utakuja ukumbini?” ilikuwa sauti nzuri ya kike, iliyo utekenya moyo wa Erasto ambae jana akupata demu, kama anavyoitaga yeye mwenyewe, Erasto alitabasamu kidogo, japo alijuwa kuwa chai asingeweza kunywa ata kidogo, kisha akajibu, “nanywea huku chumbani” ilikuwa sauti nzito ya pozi flani hivi, simu ika katwa, Erasto akainuka toka kitandani alikolala na nguo zake zote, kama alivyo kuja nazo utoka Songea, akachukuwa mswaki na dawa yake, ambayo uweka kila siku katika vyumba hivi, kwaajili ya wageni, kisha akaingia bafuni, ambako hakutumia ata dakika tatu aatoka huku ana jifuta maji usoni,
Nawakati huo huo akasikia mlango wa chumba chake ukigongwa, “nani?” aliuliza Erasto, japo alijuwa kuwa ni mhudumu analeta chai, huku anaingiza mkono mfukoni mwake na kutoa kikasha cha pete, akaiweka mezani, na kuzamisha mfuko mwingine, akaibuka na pochi yake, wallet, “mhudumu naleta kifungua kinywa” ilijibu sauti ya kike, hapo Erasto alifungua pochi yake haraka na kutoa noti kadhaa za fedha, akaziweka mezani na kuegeshwa kikasha cha pete, “ok! ngoja nikufungulie” alisema Erasto huku anatazama tazama mle chumbani, kana kwamba kunamgeni anakuja na hakutaka kuwe na makosa yoyote, alipo jilizisha akaufwata mlango na kuufungua.
Naam Erasto alikutana na sura ya mwanamke mmoja, nikama wa makamo flani, lakini kwa kijana huyu ange mtosha kabisa kuipitisa siku yake, alimtazama kuanzia juu mpaka chini, ukweli sura yake aikuwa mbaya wala nzuri sana, alikuwa wakaida, ikisaidiwa na mafuta ya kumng’alisha, anayo tumia, maana ngozi yake nyeusi ilimelemeta, unene wake ulikuwa sehemu zote kifani tumboni, ata maklioni na majani, huku kisket chake kifupi chenye mpasuo mlefu kihasi kikishindwa kuifazi taiti iliyoonekana kwa chini kidogo, “habari za asubuhi” alisalimia yule dada mhudumu, ambae kimtazamo alimzidi Erasto miaka ata kumi au zaidi, huku anainama na kuweka meazni trey yenye sahani iliyo funikwa, chupa ya chai na kikombe, pia macho ya mhudumu huyo yaliziona zile noti mezani, “ni mbaya dada yangu, Njombe baridi kari sana kuliko ata Songea” aliongea Erasto kwa kujilalamisha mbele ya huyu mhudumu, ambae aligeuka na kumtazama Erasto usoni, huku anatabasamu kidogo, baridi ina dawa yake, au songea amjuwi dawa ya baridi?” aliuliza yule hudumu, ambae sasa alisimama mbele ya Erasto, “mh! labda uniambie wewe” Erasto alijifanya hajuwi, maana ya yule mhudumu, wakati alikuwa anajuwa fika alikuwa anamaanisha nini, yule mhudumu alitazama chini na kujichekesha kidogo, “nikuambie dawa ni nini, au nikupe dawa?” aliuliza yule mhudumu, akiwa bado ametazama chini anacheka cheka, “nazani itakuwa vyema ukinipa dawa” alijibi Erasdo, huku ana sogelea mezani, na kufunua sahani iliyo funikwa, “unaijuwa dawa yenyewe lakini?” aliuliza yule mhudumu huku akijichekesha chekesha, hapo Erasto akajifanya kama ana waza kidogo, kisha akajibu, “ata kama siijuwi lakini nazani nitaipenda” hapo yule mdada aka msogelea Erasto, alie kuwa anatazama mkate selesi mbili na yai la kuchemsha kwenye sahani, akamwekea mikono yake mabegani, kisha aka usogezea mdomo na kumbusu mdomoni, “nitakuja mchana nikimaliza zamu yangu” alisema ule mhudumu ambae alisha sikia kwamba wakina Erasto watakuwepo pale kwa siku mbili, pengine na zaidi, “sawa lakini usiniangushe, ila naomba nikuagizie supu, maana chai sitoiweza” alisema Erasto, huku ana chukuwa noti mbili za mia mbili miambili, na kumkabidhi yule mhudumu ambae hakuwa anamfahamu jina, “supu na nini?” aliuliza dada mhudumu, “na chapati kama zipo” alijibu Erasto, kisha yule mhudumu akatoka nje ya chumba namba kumi na sita, akamwacha Erasto anakichukuwa kikasha cha pete, na kukifungua, akatoa pete moja ya dhahabu, iliyokuwa inang’ara kweli kweli, akaitazama kwa sekunde kadhaa, “huyo mshenzi kwanini anaumiza myongu hivi, yani fitina zote zile bado ana mng’ang’ania mchumba wangu?” aliwaza Erasto, akionyesha uchungu moyoni mwake, “siku akikamtwa lazima nimzibue ngumi ya usoni” alijisemea Erasto, akiwa ameshika pete ambayo ilitakiwa amveshe Monalisa.
Wakati huo huo chumba cha baba na mama Monalisa, walikuwa wanabembelezana, “mke wangu, naimani Mona ata salama, na tuta mpata hivi karibuni” alisema mzee Anderson, akimweleza mke wake alie mlalia kufuani, wakiwa juu ya kitanda cha chumba namba sita, cha serena hotel, “lakini baba Mona ebu fikilia kwanza mtoto atakuwa anaishije huko aliko, tuna uakika gani kama yupo salama” aliongea mama Mona huku akitokwa na machozi, yaliyolowesha kifuani kwa baba Mona, “ila akika huyu kijana atalipia mateso yote anayo msababishia mwanangu” alisema baba Mona, kwa sauti iliyo jaa ghazab, na wakati huo huo mlango wa chumba chao ukagongwa, alikuwa mhudumu alie kuwa anawaletea kifungua kinywa, ***
sajent Idd Kibabu alikuwa bado kwenye kichaka, pamoja na askari wake watano na dereva wao, pale walipoficha gari lao, wakiwatazama askari watano, walio kuwa juu ya kimwinuko, wame kaa tayari kushambulia gari wanalisubiri, kulishambulia kwa silaha nzito, “afande vipi awa jamaa mbona wanachelewa sana, au bado hawaja waona?” aliuliza askari mmoja kati ya wale watano, “ngoja kwanza tusubiri, maana lazima wapiti hapa kutu julisha kama wanakuja” alijibu Kibabu, ambae alikuwa anajitaidi kutazama huku na huku, kuona kama wale skari walio tumwa wanakuja.
wakati huo kilomita tisa mbele toka walipokuwepo wakina Kibabu, SSP Kingarame alikuwa ame simamisha gari, na kushuka pamoja na askari wake, ni kama walikuwa wanasubiri jambo flani, ambalo askari wale hawakujuwa lolote, zadi ya yeye Kingarame, alie kuwa anaasubiri matokeo ya shambulizi la kushitukiza lililotegwa na wakina Kibabu, juu yak anal Kisona. **
Wakati huo kanal kisona alikuwa ana malizia maongezi yake na bibie Rehema Haule, walie mkuta pale dukani kwake, na kuwakaribisha ndani, akiwaandalia chai, na viazi mviringo,
Rehema alimsimulia Kisona kila kitu, mpaka alipoenda kuwaacha kule porini, baada ya kuvuka kijiji cha Utwango, “kwakweli ningejuwa mapema, ninge waficha hapa nyumbani mpaka uje” alijilahumu Rehema, “ila pengine inge kuwa hatari zaidi kwao, endapo wange bakia hapa Makambako mjini” alisema Kisona ambae aliagiza ramani toka kwenye gari, kisha ikatandikwa mezani, na kuanza kuonyeshana sehemu zile ambazo ziliwekwa alama, “mimi niliwaacha hapa,” alisema Rehema, akionyesha kwa mkono mbele kidogo ya kijiji cha utwango, kabla ata ya kufikia barabara ya vumbi inayo katiza kwenye msitu mkubwa sana, “ok! jamani mnawea kuona vizuri kuwa, hii barabara inaelekea mashariki, na inazidi kurudi upande wa kushoto kilomita kama tisa hivi, kinakaribiana na kiki hiki hapa, japo hakuna bata bara kuu, lakini kuna vinjia vinavyo iunganisha, na kutoka utwango mpaka kijiji hiki, kuna kilomita tatu, hivyo wakina Edgar iwapo watakuwa wameelekezwa vizuri, basi wata kuwa wanakitafuta kijiji hiki” alisema Kisona akionyesha kwenye ramani yake, “nazani hatuna aja ya kupoteza muda, “ alisema mzee Mbogo, na wote wakamuunga mkono, na kuinuka ili waanze safari ya kuelekea, nje kupanda gari, wakimweleza Rehema, kuwa watamtembelea iwapo wataitaji msaada wake, “twende mpaka mbele kidogo ya kijiji cha utwango” alisema Kisona, wakati gari likiwa limeshaondoka nyumbani kwa rehema. ***
Wakati huo huo Koplo Mapombeka alikuwa anasaidiana na askari wake wawili na dereva wake, kupakiza chakula kwenye gari, na walipomaliza kupakiza waka ondoa gari lao, safari ya porini ikaanza, huku wakiwa naimani kuwa, leo watamaliza kazi, na kulala majumbani kwao na familia zao, ***
Dakika kumi natano mbele, kilomita kumi toka Makambako mjini, kijijini Utwango, lilionekana gari aina ya Toyota land cruzer, likiwa lime egeshwa pembezoni mwa nyumba moja kati ya nyingi, zilizomo pembeni ya barabara kuu, mita kama sitini toka barabarani, huku askari walipo ndani ya gari hilo wakitazama barabarani kwa umakini, wakitazama kwa umakini sana, magari yaliyopita. asa yale yaliyoelekea Njombe.
Nawakati huo ndio wakaliona land rover mia na kumi, likipita mbele yao, na sasa lilitembea kwa mwendo wa kawaida, “ok! ondoa gari ondoa gari! tena tembea haraka uwapite awa washenzi” alisema Koplo Lusinde, na hapo hapo dereva wake akaondoa gari kwa speed, akiifwata bara bara kuu, mpaka anaikamata barabara kuu, waliweza kuliona gari la jeshi, likiwa mbele yao, umbali wa mita mia mbili, “tembea uwapie haraka, tukawajulishe, kwenye ambush” alisistiza Lusinde, huku dereva wake akikanyaga mafuta kwa nguvu, na kuwasogelea kwa speed ya hajabu wakina Kisona waliokuwepo ndani ya gari lao,
Kumbe basi wakina kisona dakika chache zilizopita, wakiwa wanaingia hapa utwango, na kupunguza mwendo ili waweze kuonyeshana, bahaadhi ya vitu flani flani, ikiwa na njia ya kuelekea kwenye kijiji flani ambacho walihisi kuwa wakina Edgar watakuwa wana kifwata, ilikupata msaada, lakini wakati wanaonyesha, njia na mazingira, wakaliona Toyota land ceruze, la blue, lile walilo liona karibu na tazara, nawao wakaambizana waasi onyeshe kama wame liona, hivyo wakaendelea kutembea taratibu, wakikatiza kikiji hiki, lakini kabla awaja fika mwisho, waka liona lile gari likiwapita kwa speed ya ajabu, “nilijuwa tu! lazima watatusubiri huko mbele” alisema bwana Kisona, huku anatabasamu, “kwa hiyo tunafanyaje, tuwawai au tuachane nao?” aliuliza dereva, ambae ni baba Edgar, “achana nao, ila tuwe makini sana, inaonekana huko mbele kuna kitu tumeandaliwa” alisema Kisona huku wakiendelea kutembea kwa mwendo wa kawaida, na baada ya dakika tano walisiha iacha utwango, na kusimama sehemu moja ambayo walihisi kuwa pengine wakina Edgar walishushiwa hapo.
Wote walishuka na kuanza kukagua eneo lote, mpaka walipoona maganda mengi ya risasi, “mh! uwezi amini, kama risasi zote hizi ziliwashambulia awa watoto, na wamewakosa, basi hawata kaa wawapate tena” alisema Kisona kwa mshangao, uku wengine nao wakashangaa, kasoro baba Edgar, ambae aliishia kutabasamu, “bwana mbogo huyu kijana anamafunzo mengine yakijeshi, uliwai kumpa, zaidi ya kutumia silaha?” aliuliza kanal Kisona, akimtazama baba Edgar, wakati huo walikuwa wanatazama mtaro ambao ulionyesha waazi kuwa ndimo walimo torokea wakina Edgar wakati wa mashambulizi, “hapana, zaidi yakuwa yeye nikijana mwelevu, na mwepesi wa vitendo” alijibu baba Edgar, huku anageusa macho yake samba mba na Kisona na askari wengine, kutazama barabarani, kulitazama land rover 110, la polisi, lililokuwa linapunguza mwendo na kusimama karibu na gari lao, kisha wakamwona askari polisi mwenye cheo cha koplo akishuka toka kwenye seat ya mbele, Kisona alimtambua koplo huyu, akimkumbuka kuwa alimwona kule mjini, akiwa na gari hili na askari hawa hawa.
“Jambo afande” alisalimia yule koplo kwa kupiga salut, Kisona nae aka itikia kwa saluti “hooo afande naona unatazama jinsi tulivyo mkosa kosa huyu jambazi” alisema koplo Mapombeka, huku akiwatazama wale askari wa jeshi la ulinzi mmoja baada ya mwingine, huku macho yake yakigota kwa mzee mmoja alie valia nguo za kaki iliyo karibia kijani lakini yenye muundo wa kombat yakijeshi, ambae alikuwa amemkazia macho flani ambayo koplo huyu akuweza kuyatafsiri, Kisona aliona jinsi mzee Mbogo alivyo chukizwa kwa mwanae kuitwa jambazi, akamwonyesha ila ya kutuliza hasira, “jambazi gani tena huyo?” aliuliza Kisona kana kwamba akuwa anajuwa lolote, “hivi nyie niwageni hapa makambako?, kuna jambazi mmoja juzi aliteka binti mmoja mzuri huyo, sijuwi anataka kwenda kumfanyia nini” alisema baba kijacho Mapombeka, na hapo hapo Kisona akapachika swali, “kwa hiyo ni jambazi au mtekaji?” aliuliza Kisona huku akiendelea kutazama, kwenye mtaro, ambao walitolokea wakina Edgar, “ni jambazi, alafu mtekaji” alijibu Mapombeka, kwa sauti flani kama vile alikuwa anaji uliza jambo, “wakati mna mshambulia huyu jambazi mtekaji, yule mwanamke alie mteka alikuwa nae” hapo kidogo Mapombeka aka vuta na kushusha pumzi nzito, kisha akatazama chini huku akijishika kiunoni mwake, “alikuwepo nae” jibu lake lilitoka kwa sauti flani yachini hivi, iliyo ashiria kunakitu tofauti juu ya hilo, Kisona aktazamana na mzee Mbogo, “ila ukiachilia hayo yote, huyu bwana anacha kulipia ameuwa vijana wangu wengi sana” aliongeza Mapombeka, kwa sauti yenye machungu, “ukiachilia hayo yote, kama yepi bwana koplo?” aliuliza Kisona, kwasauti tulivu, huku akijichekesha kidogo, “ha! afande tuyaache tu! unajuwa siri kubwa wanayo awa wenzetu wa songea, maana huyu kijana inaonyesha ni mwanafunzi kutokea mbeya, pamoja nahuyu mwanamke, alafu wanasema nijambazi alikuwa anashirikiana na jambazi mmoja anaitwa Lukas walimuuwa wenyewe, na mbaya zaidi kinacho changanya, japo wanasema kauwa huyu kijana ame mtea yule binti, ila ukweli nitofauti kabisa, kama ungewaona ungesema ni mtu na ndugu yake wa damu, kwajinsi yule kijana anavyo jitaidi kumwokoa, kweny mashmabulizi ambayo hayachagui mtekaji na mtekwaji” alieleza yule koplo, Mapombeka pasipo kujuwa anatoa hari kwa watafuta habari, “kwa hiyo bwana Koplo ndio unelekea huko?” aliulizaq baba Edgar, “yah! napeleka chakula” alijibu Mapombeka, “kwahiyo kwa sasa mnamsaka sehemu gani?” lilikuwa swali kutoka kwa Kisona, hapo Mapombeka aliwaaza kidogo, kisha akajibu, “kwa sasa kundi langu limeelekea upande wa huku Makambako, sababu jana usiku tulisikia mlipuko wa risasi ndani kabisa ya pori, upande huu wa makambako” alijibu Mapombeka, na kufanya wana jeshi awa watazamane, kwamaana wazo la Kisona, lilikuwa linaekeea kuwa kweli, “ok! bwana koplo tusi kucheleweshe, ila jaribu kuwa makini katika safari yako” alisema Kisona, akiwa na nia thabiti ya kuwa mapombeka aondoke, ili nawao wawai kule waliko zania wakina Edgar wanaelekea kabla hwaja kutwa na polisi.
Ilikuwa hivyo, koplo John Mapombeka aliingia kwnye gari baada yakuwa amesha piga saluti ya kuaga, na dereva akaondoa gari, kuelekea upande wa Njombe, ndani yagari Mapombeka alikuwa akama ameshikwa na mawazo ya ghafla, “afande mbona kama unawaza sana” aliuliza dereva, huku gari likiwa katika speed, “unajuwa nimeongea na wale jamaa kwa muda mfupi, lakini maswali yao yalikuwa na maana kubwa sana, naisi kama……. naisi kkama nilikuwa nahojiwa katika chumba cha upelelezi” alisema Mapombeka kwa sauti flani hivi ambayo ilikuwa ina ung’amuzi ndani yake, “maswali kama yepi?” aliuliza yule dereva, “ni machache tu, ila yame nifanya nipate majibu harisi toka kwenye majibu yangu mwenyewe, kuna mchezo mchafu kwenye huu masako, inatakiwa tuongee na wakubwa” alisema Mapombeka, akionekana kuingiwa na mashaka makubwa,
wakati huo walikuwa wanakata kona kuingia barabara yavumbi, “alafu kuna kitu nimeambiwa, nanzani kinamaana kwetu, wanasema tuwe makini na safari yetu” **
Kumbe wakati huo kilomita nne mbele yao, gari aina ya Toyota land cruzer, lililo kuwa katika mwendo mkali sana, lilipunguza mwendo na kusimama mita chache kabla ya kuikuta kona ya ghafla, iliyopo kwenye kipando ambacho na chenyewe cha ghafla, mala akaonekana askari mmoja wa jeshi hilo hilo la polisi, akiwafwata mbio mbio, “waambieni wawe tayari wanakuja” alisema koplo Lusinde, kisha wakaondoa gari kwa speed kari sana, kuelekea mbele, wakikatiza sehemu ile ambayo ilikuwa na kona ya ghafla na mwinuko, huku yle askari alie pewa ujumbe akikimbilia kwenda kwa wale askari walio jiega kwa mashambaulizi, na kuwapa ujumbe kuwa, wawe tayari gari litakalo jitokeza ni la wale wanajeshi wanao wasubiri, hawakujuwa kuwa gari linalo kuja ni la polisi wenzao, tena lilikuwa lina waletea chakula, na sasa lilikuwa linakuja kwa speed kutokea barabara kuu, itaendelea ……….. hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!