BIKIRA YA BIBI HARUSI (29)

SEHEMU YA 29

ILIPOISHIA SEHEMU YA ISHIRINI NA 28: “mh! sawa, lakini sijuwi nilikuwa na waza nini, sikuzote nilikuwa nawaza unione nikiwa nimevaa” alisema Monalisa huku akicheka kidogo, ata Edgar alicheka kidogo, “Mona inamaana uwa unakumbukaga?” aliuliza Edgar jwa mshangao, “siyo ku kukumbuka tu! ata ile nguo nime itunza mapaka leo?” alisema Monalisa huku najichekesha, “mh! acha uongo wako” alisema Edgar na wakati huo huo, wakasikia sauti ya muungurumo wa gari, mita kadhaa mbele yao, endelea…..
“umesikia gari hilo? kumbe barabara bara hipo karibu, tungekuwa karibu tunge pata lift” alisema Monalisa, huku akisimama, na kujaribu kuangalia kule kulikosikikika mlio wagari, na akafanikiwa kuona vumbi likitimka, “lift ya kwenda wapi?, kuzimu?” aliuliza Edgar kwasauti isiyoonyesha utani, hapo Monalisa akatuliza hakiri, “inamaana tumekaribia ile barabara yavumbi ya jana?” aliuliza Monalisa, kwa sauti ya mshangao, huku akikaa chini, nauo na hiyo ni sauti ya one ten, moja ya yale yaliyo tushambulia” alisema Edgar huku anamaliza kumenya kipande cha mua na kumkabidhi Monalisa, “kula mua, uongeze nguvu za kutembea” alisema Edgar, na Monalisa akapokea, na kuanza kula kimya kimya, kama vile kuna jambo anawaza.
Kimya kilidumu kwa dakika nzima, huku Monalisa Aki endelea kula mua wake, na Edgar akfungua kifurushi cha nya na kuanza kula kipande kimoja kati yavinne, na kimoja aka mkabidhi Monalisa, “hivi Eddy, tutafika nyumbani kweli?” ilikuwa sauti ya kinyonge toka kwa Monalisa, Edgar aka mtazama Monalisa, akamwona jinsi alivyo nyongea, “Mona usiwe na wasi wasi, naamini tuta fika na roho zetu, kumbuka sisis hatuna kosa lolote, hivyo mungu yupo upande wetu” kusikia hivyo Monalisa akamtazama Edgar usoni, kwa macho ya mshangao, “mh! hivi, ata sehemu anayo kaa mchungaji unaijuwa kweli?” aliuliza Monalisa, kwa sauti iliyojaa mashaka, “kwahiyo, kama siendagi kanisani, ndio si stahiri kulindwa napoonewa?” aliuliza Edgar, huku moyoni mwake kijisuta, Monalisa akaachia kicheko kikali sana.
Kicheko kilicho dumu kwa dakika mbili nzima, yani alicheka kiasi cha kujishika tumbo, alafu kicheko kika koma ghafla, akamtazama Edgar, kwa macho ya tahadhri, maana alikuwa ameshika kipande cha mua, ame kiinua usawa wake, nikama anataka kumpiga nao, “samahani Eddy, lakini si utani tu” alisema Monalisa kwa sauti ya kubembeleza, lakini Edgar hakuonyesha dalili ya kumsikiliza, ndio kwanza akajiweka sawa.**
Dakika mbili baadae waka yaona magari mawili yapolisi, yanayo fanana yakiingia pale, kwenye eneo la tukio, huku Kingarame akionyesha mstuko wa wazi, nazani ni baada ya kuwa ona askari wanne wakiwa hapa, sehemu ambayo walitegemea kukuta majeluhi au marehemu peke yao, Kanal Joseph Kisona, alisha litambua gari moja wapo kati ya haya mawili, nilile, lililokuwa nyuma ya gari la SSP Kingarame, ambayo yalifika na kusimama, hapo haraka sana wote wakashuka toka kwenye gari wakiwaacha madereva peke yao, “kimetokea nini hapa kanali Kisona, na wewe umefwata nini huku?” lilikuwa swali toka kwa SSP Manase Kingarame, ikiwa ni sauti kali ya kufoka, uku Kingaarame akimsogelea kamanda huyu wa jeshi la ulinzi, huku askari wapande zote mbili yani wa jeshi la ulinzi na wajeshi la polisi, wakisikiliza na kuwatazama wakubwa wao,wakati huo wale askari wanne wa makambako, wakikimbilia kwkenye lile gari lililo lipuliwa, huku wanapiga kelele, za majonzi, “kwanza punguza jazba SSP, pili juu ya nini kime tokea, wewe ndie unae juwa, mimi nilikuwa mbali sana na hawajamaa, maana walinipia kule barabarani, kunasehemu nilikuwa naikagua, na kuhusu mimi kuwepo hapa, sizani kama nina mipaka katika nchi hii ya Tanzania, katika swala la ulinzi” alisema Kisona kwa sauti tulivu, iliyo tafsiliwa, kuwa ni zarau na Kingarame, na askari wake, “mimi najuwa vipi wakat wewe ndio nime kukuta hapa?” alisema Kingarame kwa sauti ile ile ya jazba, huku ana pepesa macho kutazama eneo lilipo gari pengine angeona majeruhi, “kuna gari limeondoka hapa kuelekea ulikotokea wewe, unataka kuniambia ujakutananalo?” aliuliza Kisona, kwa sauti ile ile tulivu, siyo Kingarame peke yake, alie stushwa na lile swali, ata askari wa Kingarame aliotoka nao Songea, nao pia walistuka, “amejuwaje huyu mshenzi, au aliwai hapa?” alijiuliza Kingarame, huku ametoa macho ya mshangao yaliyochanganyika na hasira,
Ukweli Kisona alitambua kuwa, kuna gari lime toka sehemu hiyo, na kujipa uakika huo, ni kwa mambo mawili, moja aliona alama za matairi ya gari, yani lile la wakina Kibabu, pili aliliona gari ambalo lilikuwa linawafwatilia kule mjini na barabarani, lipo hapa na Kingarame mwenyewe, nyie ebu angalieni kama kuna majeruhi, tuwakimbize Hospital,” alisema Kingarame, akiwaambia wale askari aliotoka nao mjini, huku kwa kutumia hakari nyingi sana akiwakonyeza, akiashiria kuwa hakuna kupona mtu yoyote watakae mkuta, Kisona aliekuwa ana mfwatilia kwa umakini mzee huyu, aliona ule mkonyezo, akatabasamia pembeni, “sijaona wala kupisha na gar lolote, vipi umekuja na usafri gani?” aliuliza Kingarame, ikiwa ni kupoteza mtililiko wa maswali toka kwa Kisona, “nime kuja nagari, lime wapeleka majeruhi hospital” alijibu Kisona huku anajifanya kutazama kule kwenye gari, kisha anaanza kutembea huku kwa macho ya wizi ana mtazama mzee huyu, alie mwona akistuka kwa kusikia kuwa, amewapeleka majeruhi hospital, Kingarame nae aka mfwata Kisona, “kanal, nazani umeona kwa macho yako, ubaya wa kutetea majambazi?” aliuliza Kingarame, akitaka kupata uakika kama Kisona aliona tukio au kustukia mchezo huu,
Lakini kabla ya kupata jibu, “afande hakuna mtu” alisema mmoja wa wale askari, lakini Kingarame akumjari yule askari wake, zaidi alimtazama Kisona alie kuwa ana inama na kuokota kichwa cha risasi, “hii risasi ni 7.62 mm, imepigwa kutoka mbari, na sauti zilizo sikika ni za medium machine gun” alisema Kisona huku anamwonyesha Kingarame kile kichwa cha risasi, kwani aiwezekani jambazi kutumia MMG?” aliuliza Kingarame nikama anataka kushinikiza swali lake lijibiwe kuwa ndiyo kuna ubaya wa kutetea majambazi, lakini aikuwa hivyo, ndio kwanza Kisona akageuka na kulitazama gari ambalo lilikuwa limelala chali, kisha aka tazama pembeni yake, akaonyesha kwa kidole, “kile ni kipande cha bomu la RPG?” sasa Kisona nikama alikuwa anauliza, “kwahiyo ujawai kusikia kuwa majambazi wana tumia RPG?” aliuliza Kingarame kwa jazba, maana aliona nikama Kisona anaulizia nangurukuru, wakati kasha fika lindi, au hupo himo, unaulizia njia ya kwenda nyumba ya mungu, lakini Kisona taratibu akamtazama Kingarame, kwa mcho matulivu yenye maswali ya mashaka, “ni kweli majambazi wana weza kutumia RPG, na mmg, pengine ata zaidi, sababu watakuwa wengi, lakini sizani kwa huyu jambazi mmoja, ambae anaangaika kumlinda mwanamke asitoroke, wakati huo huo anatumia mmg, na wakati huo huo anatumia RPG, kwenye ambush moja” alisema Kisona, akiwa bado anamtazama Kingarame, ambae nae alikuwa anamtazama Kisona kwa macho ya mshangao, kama vile ameona mzimu, umesimama mbele yake, alafu nikama alikuwa anatafuta cha kujibu, “pengine.. pengine… yupo na wenzake” alisema Kingarame kwa sauti ya kubabaika kidogo, alafu akaonekana kutabasamu kidgo, “ndiyo huyu jambazi atakuwa na wenzie, wamekuja msaidia” aliongea tena Kingarame, kwa sauti ya juu, iliyo changamka, kiasi cha kuwa fanya wale askari wengine wageuke na uwatazama, wakuu wao,
“Lusinde askari wako waingie kwenye gari langu haraka, na wale waliokuwa kwangu wabakie hapa walinde hili gari mpaka litakapo kuja kuchukuliwa, taharifa hisifike kwa familia kwanza, ngoja sisi tuka waone majeruhi” alisema Kisona huku ana elekea kwenye gari lake, akifwatiwa na askari watano walio ingia nyuma ya gari hilo, na Hokololo akaondoa gari kuelekea mjini, wakimwacha Kisona akishangaa, pasipo kujuwa afanye nini, “huyu mshenzi anaenda kuwamaliza wale majeruhi” aliwaza Kisona, huku anatazama gari la Kingarame lililo kuwa lina timua vumbi, kuitafuta barabara kuu,
Kisona alitazama lile gari mpaka lilipopotea, kisha aka wageukia wakina Lusinde, ambae nae alikuwa analitazama gari la SSP Kingarame, kisha aka wageukia wale askari waliokuwa katika majonzi mazito, “nyie wa nne subirini hapa, wacha mimi nika watafute wenzetu” alisema Lusinde, alisema Lusinde, kisha akaingia kwenye gari na kuondoka zake, kwenye gari wakiwa yeye na dereva pekee, wakiwaacha wale askari wanne wa polisi, na wale askari wa nne wajeshi la ulinzi, yani pamoja na Kisona, alie watazama kwa zamu na kungundua majinzi yaliyomo ndani yao, maana walikuwa wamejiinamia huku SMG zao zikiwa migongoni, akatabasamu kidogo, “inabidi nipate habari, kutoka kwa hawa askari” aliwaza Kisona ***
PC Khassim na PC Mike, pamoja askari wao, nao walisikia mlipuko wa bomu na risasi za mmg, ambazo uliaji wake askari wengi wanaufahamu, kipindi hicho, walisha maliza mapumziko yao na kuamua kurudi walipotoka, kujaribu kufwatilia walipo chepuka wakina Edgar, wakiwa karibu na bonde la kilimo, mita chache kabla awajafika pale walipo wauwa wale wawindaji haramu, “wata kuwa wame waona au?” aliuliza Khassim akimtazama Mike, “pengine wamesha wapata, ebu tukatize usawa hilo bonde, nazani tuta tokea barabara kuu” alisema Mike, huku wanaanza kutembea kushuka pale bondeni, “alafu wale wajinga awaweai kurudi pale, lazima watakuwa wame elekea huko huko barabarani, kwa lengo la kuelekea Njombe, au kufika barabara ya lami,” aliongezea Khassim, kisha askari mmoja akadakia, “itakuwa hivyo sasa pengine wamekutana na ambushi ndio hiyo milipuko tuliyo isikia” wote wakacheka, huku wanaendelea na safari, pasipo kujuwa kuwa wenzao wa makambako, wamesha ingia kwenye ambush. ***
Edgar alikuwa ameinua kipande cha mua, nikama anataka kumpiga nao, Monalisa “samahani Eddy, lakini si utani tu” alisema Monalisa kwa sauti ya kubembeleza, lakini Edgar akuonyesha dalili ya kumsikiliza binti huyu alie onyesha dalili zote za uoga na wasiwasi, ndio kwanza Edgar akajiweka sawa, kisha akauinua zaidi ule uwa alioushika kwa mikono mwili, hapo Monalisa akaufumba macho kwani hakutaka kuona kinacho mtokea, zaidi ya kusikilizia maumivu ya mua utakaposhuka kichwani mwake, lakini akasikia ‘puuh!’ inaamaana ule mua ulipiga chini, yani pemni yake kalibu kabisa na makalio yake hao Monalisa akafumbua macho kwa mstuka na kutazama pembeni ulipo shukia mua, lakini aliona Edgar ndiokwanza ana inua ule muwa na kubiga tena sehemuile, na mcho ya Monalisa yakashuhudia kipande cha mua kikishuka kwenye kichwa kikubwa cha nyoka, hapo Monalisa akaduwaa akitoa macho, kama vile ameshikwa na bumbuwazi, akimwona nyoka mkubwa na mrefu akirusha tusha kiwiliwili chake na kuunyonga nyonga mkia wake mrefu, ndipo Monalisa alipo gutuka na kuinuka haraka, na kusogea pembeni, “mamaaaaa!” alipiga kelele Monalisa, huku Edgar akizidi kushusha muwa kwenye Kichwa cha yule nyoka, mpaka kilipo onekana kime pondeka pondeka, ndipo Edgar akaacha kumpiga na kumrushia kwenye majani akitumia ule mua, ambao nao aliurusha pamoja na yule nyoka, ambae bado alikuwa ananyonga nyonga mkia wake, “tuondoke, atakuja mume wake” alisema Monalisa huku ana okota kibegichake na kukivaa mgongoni, Edgar akacheka kidogo, “kwani huyu dume au jike?” aliuliza Edgar, “mwulize mwenyewe, kwani uoni alivyo kuwa na kimbele mbele?” alisema Monalisa huku ana mtazama Edgar alie kuwa ana kusanya vitu vyake, pamoja SMG, iliyo kuwa ya mwisho kuiokota pale chini, kisha aka jivw=esha mkanda wake, akiilaza mbele bunduki yake, mkono wa kulia aka shika nyama zilibakia, ukiachilia zile za kwenye Kibegi, mkono wa kushoto ukidakwa na Monalisa, safari ikaanza kuifwata barabara ya vumbi, ambayo waliamini kuwa hipo karibu yao baada ya kuwa, walisikia mlio wagari, ***
gari aina ya Land cruzer, Toyota la polisi, liliingia kwa speed ya hajabu ndani ya lango kuu la hospital ya Kibena mjini Njombe, huku wananchi na raia waliokuja pale hospital kwa mambo mbali mbali, wakilipisha gari hilo la polisi, wakichelea kifo, akijarisha mgonjwa wala msindikizaji, wote walipata wepesi, na unafuu, wakulipisha gari hilo, ambalo lilienda nakusimama mbele ya mlango wa kuingilia ndani ya jengo la hospital, kisha kama umeme akashuka SSP Manase Kingarame, na kuingia ndani akisindikizwa na askari wawili, huku akipishana na wauguzi nane, waliobeba machela mbili, “vipi afande kuna wagonjwa kwenye gari?” aliuliza mmoja kati ya wale wauguzi, Manase Kingarame, akujibu, zaidi aliongoza moja kwa moja mapokezi, ila askari mmoja kati ya wawili wasindikizaji akajibu, “hakuna mgonjwa,”
Kingarame, aliongoza moja kwa moja mpaka mapokezi, “wagonjwa walioletwa wapo sehemu gani?” aliuliza Kingarame kama vile amepagawa, yani bila salamu wala nini, muuguzi alie kuwepo pale mapokezi akaonekana kuduwaa, “mbona akuna mgonjwa alie letwa leo” alisema yule mhuguzi wakike wapale mapokezi, ambae alimwona Kingarame akigeuka kwa mshangao kuwatazama wale askari wake, “ilakuna mgonjwa watatu, walioletwa jana, ni wale walio umia wakati wana msaka jambazi huko porini” alisema yule mhuguzi, kama alie zinguka toka usingizini, “wapo kwenye ward ya wanaume…..” atakabla ajamalizia tayari, yule mhudumu, aliwaona wakina kingaramem wakiondoka haraka haraka kuelekea nje ya jengo la hospital, “inazidi kuchanganya, huyu jamaa anataka kunichezea mchezo wa hajabu, sijuwi kwanini nilimsikiliza” alilalamika Kingarame, akismshutumu Kisona huku akiingia kwenye gari, “endesha twende kituoni,” Kingarame alimweleza Hokololo, ambae bila kuchelewa aliondoa gari kuelekea barabara kuu, ili waende kituo cha wilaya, “lazima ni fanye jamba leo hii, huyu jamaa anaweza kutuharibia sana” alisema Kingarame, huku anauma meno kwa hasira, “kwanza inabidi tuwai kuongea na redio ya taifa, pili niongee na baso”.
Hivi mdau unajuwa kilichotokea?, mpaka wagonjwa hwajafika hospital Kibena, ebu basi tuone, na itakuwa vyema tukianzia pale kwenye ambush, ***
Mala baada ya mzee Mbogo, koplo Katembo na yule askari mmoja, kuondoka na wale majuruhi ambao walikuwa wana lalamikia maumivu yao, wakionyeshan hali mbaya usoni mwao, kabla wajafika barabara kuu, mzee Mbogo akasema, “unajuwa hawa jamaa ni muhimu sana kwa ushaidi wa matendo aya hawa wenzao?” katembo na mwenzie walikuwa nyuma wana waweka vizuri wagonjwa, “ni kweli ndio maana ta afande amesisitiza tuwapeleke hospital” alijibu Katembo, huku akisaidiana na yule askari kuwa angalia kwa umakini wakina mapombeka, “ujuwe nini Katembo?, awa polisi inabidi wawe chini ya uangalizi mkubwa sana, kwa faida yao na sna faida ya Edgar mwanangu” alisema baba Edgar, huku akipunguza mwendo kidogo, kuingia barabara kuu, akitazama kushoto na kulia kama kuna gari linakuja, na kuliunga mazima akikata kona upande wa kulia, kuelekea makambako, akikanyaga mafuta nakutoka speed ya 180, “nikweli mzee Mbogo, sasa tuna wapeleka wapi?” aliuliza Katembo wakati gari lime shika mwendo kuelekea Makambako, “nivyema tumpeleke kwenye hospital ya kanda ya kijeshi, kisha tuta mweleza afande awajulishe polisi, na sisi tutakuwa tumesha mjulisha Kisona”
Ndivyo ilivyo kuwa wakina mzee Mbogo na wagonjwa wao wakaelekea Makambako badala ya Njombe, ***
Kundi la PC Khassim na PC Mike, wakiwa wanaendelea kusonga mbele, ndani ya pori ili ambalo, sasa walikuwa wanatembea kwenye nyasi fupi, za usawa wa magotini mpaka kiunoni, wakitembea kilmita kadhaa bila kusikia sauti wala kukutana na mtu yoyote, ndipo ghafla, waliposikia kelele za mwanamke, kutoka mbali kidogo, nikama mita mia nne, toka walipo kuwepo, maana ilisikika kwambali kidogo “haoooo! sijuwi wame patwa nanini?” aliuliza Khassim, kwa mshangao, huku ni porini kunamambo mengi ebu tuwai upande huo” alisema Mike, huku akiongoza upande uliosikika sauti hiyo, huku Khassim akionekana kushangaa kidogo, “lakini tulisikia ile milipuko inamaana hawakuwa wao walio shambuliwa?” aliuliza Khassim, huku akitembea kuwafwata askari wenzie, waliokuwa wana mfwata Mike, “nazani una mfahamu sasa huyu jambazi, ni mjanja na mwelevu sana, pengine alikimbia” alijibu Mike, huku akizidi kusonga mbele, “lakini kutoka kule ilikosikika milipuko, na huko inakosikika sauti hiyo tunayo ifwata, nimbalisana kwa muuda muda huu mchache watakuwa wamefika kwa usafiri gani?” hayo yalikuwa mashaka ya Khassim, hakuna alieweza kujibu, zaidi Mike alisema “uoande hap juu tutaweza kuwaona, na hapo tutawatambua kama niwao au siyo wao”.***
Mida ya saa nane kasoro, Serena Hotel, familia hizi mbili, yani ya Anderson na mke wake, Misago mke wake na kijana wao, pia dereva wa Anderson, zikiwa kwenye ukumbi wa vinywaji, kila mmoja akipata kinywaji anacho kipenda baada ya kuwa wamesha maliza kula, chakula cha mchana, kwakile walicho zania kuwa wanapunguza mawazo, huku wakisindikiwa na kipindi cha chaguo la msikilizaji, kutoka kwenye redio ya taifa, na sasa ulikuwa unapigwa wimbo wa vijana jazz, uliombwa na Maneti uitwao ogopa matapeli, kiukweli ilikuwa ni furaha ya muda, maana waliendelea kunywa na kuongea huku wakicheka mala chache, ata mama Mona leo alionekana kuwa mchangamfun mala moja moja,
Lakini katikati ya furaha yao ghala mziki uka katika, na ikasikika milio kama alarm za kwenye saa, ikifwatia na sauti ya mtangazaji, “Redio yataifa kanda ya Njombe, kuna taharifa ya zarula ianawajia hivi punde” baada ya maneno hayo ya mtangazaji, ikasikika tena ule mlio wa alarm, ulio rudia mala mbili, kisha ikasikika sauti nzito na kali ya kiume, “SSP Manase Kingarame, RCO mkoa wa Ruvuma” alijitambulisha mwongeaji, na hapo watu wote waka shtuka na kutega masikio yao, wakisubiria kusikia taharifa ile, kama itakuwa nje au mbaya kwao, “jambazi Edgar Mbogo, akishirikiana nawenzake, leo ameshambulia gari la polisi, na askai wetu watatu wapo katika hali mbaya, hospital waliyo lazwa, tutawatajia baadae, maana walipelekwa huko kwa msaada wa jeshi la ulinzi lililowai kufka eneo la tukio, na kutoa taharifa katika kituo cha polisi Makambako” hapo Kingarame akaweka kituo kidogo, “jeshi lapolisi linaendelea kuwa saka majambazi hao aambao bado wana mshikilia binti Monalisa Anderson, tuna waomba wazazi na majirani kuwa watullivu wakati jeshi la polisi lina fanya juhudi za kuwasaka na kumwokoa Monalisa” huo ndio ulikuwa mwisho wa matangazo,
“Sijuwi wana mfanya nini huko binti yangu” alisema mama Mona huku akianza kuangua kilio, ukweli hali iligeuka na kuwa uzuni kwa wote, ata Erasto alie kuwa ana masubiri yule mhudumu alie kuwa ana maliza zamu yake saa tisa. ***
Taharifa hiyo iliwafikia wakina mze Mbogo, wakiwa njiani kuelekea kule porini walikokuwepo wakina Kisona, “unaona mchezo unavyochezwa kwa umakini?” aliuuliza mzee Mbogo, akiwa anapunguza mwendo na kukata kona kushoto, kuingia barabara ya vumbi, kisha akanyaga tena mafuta kwanguvu, “lakini siyo mbaya, ushaidi tunao, kilicho bakia ni kumpata Edgar na wenzie, maana wote wapo katika matatizo” alisema Katembo, “kwani licha ya kotokea hukorofi wa kipindi hicho, waliendelea kuwa marafiki?” aliuliza yule askari mdogo, walie kuwa nae, mzee Bogo alicheka kidogo, kisha akasema, “sijajuwa kama walirudish urafiki wao wazaani, lakini huko waliko watakuwa marafiki wakubwa, tena ndicho kitakacho mponza kama atokuwa makini, nazani atoweza kumwacha aingie kwenye matatizo yoyote” alimaliza kuongea mzee huyu, huku ana simamisha gari, pembeni ya barabara atuha kama kumi hivi kutoka lilipo anguka gari la kina Mapombeka, wakiwaona wakina Kisona na wale polisi wanne, wakiongea na Kisona, huku askari wa jeshi la ulinzi wakiwa wamezunguka lile eneo wakifanya ulinzi,***
Baada ya kumaliza kuongea kwenye Redio ya taifa, bwana Kingarame alirudi kwenye ofisi ya OCD, ambako aliomba kuongea na simu, OCD akampisha mkuu wake, ambae alipiga namba kadhaa za simu akimwulizia Basso, mpaka alipo mpata bado, “sikia Basso mambo yame kuwa magumu, nenda kwa bwana Wamboli Shilinde, mwambie aandae vijana wake wote kumi na saba, alafu nenda kwa yule mhindi tulie msaidia kwenye kesi ya pembe za ndovu, Rajani, akupe gari mbili za kuwasafirishia hao wakina Shilinde, waje huku, sasa hivi isiziidi saa limoja wawe wawmeondoka, uasiku waleo, lazima wawe huku, hii inshu ikivuka kesho tumeumbuka” yalikuwa maagizo mazito yakiharifu kwenye simu ya serikali, (kumbukeni story majina na matukio ni yakubuni, hayafanani wa kulinganga na matukio mengine) itaendelea…… hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!