BIKIRA YA BIBI HARUSI (31)

SEHEMU YA 31

ILIPOISHIA SEHEMU YA 30: “Eddy usiniache, peke yangu wataniua” alisema Monalisa, kwa sauti ya kukata tamaa, ambae bado alikuwa kwenye tope, akimtazama Edgar aliekuwa nje ya tope, akamwona ana geuka nakumtazama yeye, yani Monalisa, ambae alikuwa ameonyesha sura ya kukata tamaha, lakini alipo tazama kule kwenye nyasi tayari polisi walisha sogea karibu kabisa, na walibakiza mita kama kumi tu! kutokea za pale walipo kuwepo wao, ata nyasi ziliaza kusikika zikipiga kelele,
Monalisa akajuwa kuwa Edgar lazima amkimbie. endelea…….
lakini mala Monalisa akamwona Edgar akilala chini, na bunduki yake, akiishika kama wafanyavyo wanajeshi wakiwa kweuwanja wa shabaha, akaiweka sawa SMG yake, ambayo muda wote ilikuwa ina risasi kwenye chember, kisha aka ielekeza kule kwenye kichaka, uswa wa yeye Monalisa alipo kwama kwenye binde la tope, “bonyea chini” akapiga kelele Edgar, na Monalisa bila kujiuliza, ata mala moja akabonyea chini haraka sana, akajikalisha kwenye tombe ambalo lilimgusa kwenye kifua chake, hapo kilichofwata ni “pah! pah! pah!” hapo Monalisa akasikia mfululizo wa milipuko ya risasi, ikielekea kule waliko tokea, huku akiona bomba la bunduki ile aliyo ishika Edgar, ikitetemeka, huku inatoa moshi na miali yamoto.
Kule kichakani sasa, vilisikika vilio vya hajabu, vya watu wazima, huku nyasi zikitikisika kurudi nyuma, ilichukuwa sekunde kama 30 hivi, pakawa kimya, huku vilio vya maumivu vikisikika kule kichani, Edgar akainuka haraka na kwenda kumchomoa Monalisa pale kwenye tope, kisha yeye akavuka lile bonde, safari hii kwa umakini zaidi, akichagua sehemu ya kupita, akirudi kule walikotokea, akimwacha Monalisa upande wapili, akijificha kwenye kichaka.
Edgar aliingia kwenye kile kichaka, huku silaha yake aina ya SMG, akiwa ameielekeza mbele, huku ameibana kwenye bega lake la kulia, macho yapo lwenye kilengeo, ndani ya kichaka aliwaona askari kama wanne hivi wakiwa wamesha poteza maisha huku watatu, wakiwa wana tapatapa kukata roho, kwa kuugulia maumivu, akaanza kuwa kagua wale askari wengine walio kufa, huku akichukuwa mikebe ya risasi iliyo jaa risasi, na vitu vingine alivyoona vita msaidia mbele yasafari, kama vile, kiberiti, kamba, navinginevyo, kisha akamsogelea mmoja ambae, alikuwa anaafadhari kidogo, “sito kuuwa ila mwambie mkubwa wenu, mkiendelea kuni fwata, mjuwe vifo vyenu vipi mikononi mwenu” baada ya hapo akachukuwa mkebe wake wa risasi na ile ya wale wengine, kisha akaondoka zake, na kuvuka upande wapili, “umewauwa?” aliuliza Monalisa, baada ya kujitoa kichakani, “unazani sifa, kuuwa wenzio?” alijibu Edgar huku akimshika mkono Monalisa na kuanza kuongoza kuelekea kule waliko kuwa wanaelekea, yani njiani, ambapo walikuwa wamebakiza mita chache, **
Land Rover mia na kumi, lilisimama kwenye kijiji kimoja kidogo, nje kidogo ya mji wa Makambako, kilomita kumi toka Utwango, kanal Kisona na wenzake wakiwa ndani ya gari, akafungua ramani yake, na kuitazama, kisha akatowa compas (dira) aka iweka juu ya ramani, hukuwenzake wakimtazama, kila alicho kifanya, mkubwa wao, “unaona hen, kuna hii njia kusini mahariki mwa kijiji hiki, kwa hiyo mzee mbogo, tafuta njia ya kufika hapa, tuiangalie njia hii” alisema Kamanda kisona, na wote waliona kwenye ile ramani, iliyoonyesha njia ya kuingia porini,
mzee Mbogo akakanyaga krutch na kuingiza gia namba moja gari likaanza kutembea taratibu akipita kwenye vinjia vya kijiji kile, huku Kisona akiwa ame ishikilia hile DIRA, (compas) toka china, mpaka walipo fika nyumba ya mwisho kabisa ya kijiji kile. “ok! simama hapo” alisema Kisona, na mzee Mbogo, ambae aliona wanachelewa kuwa pata wakina Edgar, akasimamisha gari, Kisona akatazama moja ya nyumba zilizopo karibu yao, akaiona moja kuna watoto wana cheza nje ya nyumba ile, na wakati huo walisitisha michezo yao na kulisogelea gari hili la jeshi la ulinzi, “Katembo nipe box mbili za biscuit” alisema Kisona na kopolo katembo aka mpatia, zile biskuti, ambazo kipindi hicho walikuwa wanaziita biscut mbao, kisha kisona akawatazama wale watoto, ambao umri wao ulikuwa kati ya miaka miwili mpaka tisa, huku anatabasamu, “amjambo watoto” alisalimia Kisona kwa sauti ya mwalimu wa chekechea, hapo ikawa ni kwa pamoja, “atujambo shikamoo” ila hiyo shikamoo ilikuwa kila mmoja alitaka kusikia akiitikiwa yakwake, maana ilikuwa “shikamoo” “shikamoo” “shikamoo” ambayo ilimaliza dakika mbili nzima, huku Kisona akijitaidi kuitikia kila shikamoo, “haya watoto wazuri mnaijuwa hii” aliuliza Kisona huku akiwaonyesha biskuti moja, “tunaijuwa” waliitikaia karibu watoto wote, wakati huo kuna mama mmoja mtu mzima alikuwa anasogea pale walipo.
Kisona akaanza kugawa biscuit kwa wale watoto, ata yule mama alipowafikia akasalimia “shikamoni” akika wakuitikia ilesalamu alikuwa ni mzee Mbogo peke yake, “Marahaba, za hapa nyumbani” alisema mzee Mbogo, ambae watu wote ndani ya gari walikuwa wanamtazama, salama baba, kulikoni leo naona mapolisi, na wanajeshi kwani kuna vita” aliuliza yule mama kwa rafunzi ya kibena, “hakuna vita dada, tupo kwenye mazoezi” alijibu baba Edgar huku wote wakicheka kidogo, “sawa baba, maana asubuhi kuna mapolisi wengi, walikuja na njia hiyo, wakarudia huko huko” alisema yule mama na wakina baba Edgar na wale askari wengine wakatazama, kasolo Kisona ambae alimtazama yule mama, ok! nasisi tunaelekeaa huko, ila sijuwi gari linaweza kupita?” aliuliza kisona, na hapo yule mama nikama alitiwa ndimu, “kama unavyo iona, labbda baada ya kuvuka bonde” alijibu yule mama, “katembo na omba bif mbili” alisema Kisona, na kisona akamkabidhi Kisona kopo mbili za nyama ya kopo (biff) kwa wasio fahamu, ni nyama yakusagwa, Kisona akamkabidhi yule mama, ambae alishukuru sana japo mwanzo hakujuwa ni kitu gani, lakini baada ya kuelekezwa kwa kupitia picha ya kichwa ng’ombe iliyo po kwenye lile kopo, akaelewa, na wao wakaanza safari, taratibu wakiifwata njia afifu, waliyo onyeshwa na, yule mama, na ndiyo waliyo iona kwenye ramani, mzee Mbogo aliendesha gari taratibu na kwa hakiri nyingi, mana njia hii aikuwa lasmi kwa kupitisha gari,
safari yao ilikwama mita kama miatano mbele, baada ya njia hiyo kuzidi kuwa finyu sana, ikiambatana na mashimo ya maana, “tuta vunja spring, au kutoboa tairi kabisa” alisema mzee Mbogo, baada ya kusimamisha gari, “aina shida” alisema Kisona huku anashuka kwenye gari, kisha akamtazama Katatembo, chagua askari wawili wakubakia hapa, sisi tusonge mbele” alisema Kisona, na ikawa hivyo waliwaacha askari wawili, na wao wakasonga mbele, pamoja na mzee Mbogo, huku wakiwa na silaha zao mikononi, akasolo mzee Mbogo peke yake, akuwa na silaha yoyote,
walitembea taratibu huku wakitazama mazingira kwa umakini sana, na kufwatilia nyayo za viatu vya jeshi, sasa walikuwa wanashuka kuelekea kwenye bonde flani, kama unakumbuka mdau ndilo bonde ambalo, wakina Edgar walichepuka, ile mida ya asubuhi, na ndiko walipoelekea wakina PC Mike na PC Khassim, pamoja na askari wao, na ndipo walipo sikia milipuko ya risasi, nao wakasimama ilikusikia ile milipukao imetokea wapi, “nazani kuna mashambulizi yanaendelea huko” alisema koplo Katembo, huku wote wakitazama upande ambao milipuko ya risasi ilikuwa inatokea, “ok tusonge mbele, ufwate nyayo zao” alisema Kisona, nao wakaanza kutembea kusonga mbele, wakifwatilia nyayo za viatu vya polisi****
Kibabu ambae alikuwa ameachana na SSP Manase Kingarame mudu mrefu uliopita, akiwa na askari wake walikuwa wamesimamisha gari kilomita kamaa saba hivi, toka pale walipo sababisha mahafa ya askari wenzao, na hapo ndipo alipo sikia SMG ikikohoa, mita akama mia nne toka walipo, akajuwa kuna tukio maeneo yakaribu, na bara bara, tena ni mita mianne kule walikotoka, umbali ambao ata SMG, inauwezo wa kuuwa bila kikwazo chochote, “shukeni kwenye gari haraka, twendeni tuka mnase huyu mshenzi” alisema sajent Idd Kibabu, maana alijuwa wazi kuwa ule mlio wa bunduki, ilikuwa ni wa Silaha moja, na hivyo ni kwamba mpigaji ni Edgar ambae wanamtafuta, sababu kama wangekuwa ni polisi, laazima zinge sikika bunduki nyingi, wale askari wake wakashuka haraka, wakiwa tayari kwa mapambano,”ebu chukueni hgizo silaha za maana” alisema Kibabu huku akiwasisitia wale askari wabebe MMG na RPG, labda mafano wake, ni kwkamba, MMG niile yenye mnyololo wa risasi, na RPG, kama ile ya lambo yenye bomu mbele, ina kuwa kama muhanzi,
Kama vile wezi, walichangamka faster na kugawana zile RPG mbili na MMG mbili, huku watatu wakiwa na SMG, Kibabu na dereva wake wakabakia kwenye gari, wakiwatazama askari wenzao wakianza kutembea kusonga mbele, “akikisheni mnaipata tape” alisisitiza Kibabu, ambasiyo siri alisha ingia upoga juu ya kijna Edgar, akihisi kuwa kijana huyu anatumia ushirikina, katika mapambano. ***
PC Mike na PC Khassim, wakiwa na askari wao mmoja walikimbia mbio nyingi sana, wakirudi waliko toka, mpaka wanakumbuka kuwa wamesha waacha wezao na simama tayari walisha fika sehemu waliyo ingilia, pale kwenye kijinia panda cha kwenda kule kwa wawindaji haramu walio wauwa, huku Mike na yule askari wakiwa wametupa SMG zao, wakiona kwa zilikuwa zinawapa uzito kwenye kukimbia, “jamani wenzetu wapo wapi?” aliuliza PC Khassim, hapo Mike na yule askari, wakatazama walikotoka, labda wangewao wenzao, ambao wa nne kati yao walisha poteza maisha, “au wamepigwa risasi?” aliuliza yule askari mwenzao, “inabidi turudi tukawatazame” alisema Khassim, na hapo Mike akamtazama Khassim, kwa mshangao, nani arudi kule, inabidi ruwapate wenzetu ndio turudi” alisema Mike akionyesha kuwa akuwa tayari kwenda kule walikotoka, kwa hiyo tuwaache wenzetu, bila kuwajuwa wanahali gani?” aliuliza yule askari mdogo,
wakati wanaendelea kubishana, wakastuka na kugeuka kutazama mbele yao, baada ya kusikia nyayo za michakacho ya nyasi, ikiashilia kuwa kuna watu wana kuja pale walipo, nikweli waliwaona makamanda watano wa jeshi la ulinzi wakiwa karibu yao kabisa, nao wakashangaa, maana siyo kwa kuwaona tu! pia hawakutegemea kuwaona watu hawa, maana toka asubuhi awakujuwa uwepo wa Kisona, ndani ya uwanja wa mapambano.
“Vipi makamanda kuna tatizo?” aliuliza Kisona baada ya kuona wale askari polisi watatu, yani Mike Khassim na yule PC mdogo, wakiwa wameduwaa wakiwashangaa, bila kuongea lolote, huku wawili kato yao wakiwa hawana silaha mikononi mwao, “tume shambuliwa na jambazi” alisema Khassim pasipo kusalimia salamu yoyote, iwe ya kijeshi au ya kiraia, huku Mike, akimtazama Kisona kwa umakini kabisa, maana alisha kumbuka kuwa juzi alikutana nae wapi, “jambazi au majambazi, maana na wezenu kule inasemekana wameshambuliwa na jambazi” aliuliza Kisona swali la mtego, huku ana geuza macho kumtazama Mike, “ni jambazi tena ni bwana mdogo kabisa, labda huko kunajambazi mwinginge, huyu wa huku ndie alie mteka yule binti, aliongea kwa pupa Khassim, wakati huo macho ya Kisona na Mike yalisiha kutana, “hoooo! kamanda, naona tumekutana tena, na sisi bado tuna mtafuta huyu jambazi wapili, mnaonaje tukimtafuta pamaoja” alisema Kisona akimtazama Mike, ni kama alisha juwa jibu lla Mike litakuwaje, “afande sina malaka ya kuungana na wewe, naona nyie endeleeni na opareshini yenu” alisema Mike, ambae toka amemwona Kisona alionekana kuingiwa na waasi wasi mwingi sana, “ok! lakini uoni kama ni hatari kuwinda paka anae jitetea?” aliuliza Kisona, huku ana tabasamu, wali ambalo liicha ya kumstua Mike, alieona kama mchezo wao ume fahamika, pia ulimwacha mdomo wazi Khassim na mwenzie, ambao hawakujuwa maana ya ule msemo.
Kisona alipoona hakuana jibu lolote, aka watazama wezake, “jamani hizi ni opration mbili tofauti, ebu tuendelee na safari yetu” alisema Kisona kisha wakaanza kutembea kuifwata chochoro waliyo jia wakina Mike, yani walielekea kule waliko shambauliwa wakina Khassim, huku wakina Mike wakiwasindikiza kwa macho, “lakini kwanini tusi wafwate awa jamaa, ili tuka waone wenzetu, na kuokota bunduki zetu?” aliuliza yule askari mdogo, lakini Mike akamwonyesha ishala ya kuziba mdomo, na kuendelea kuwatazama wakina Kisona, mpaka walipo fika umbali wa mita kama mia moja hivi, “tatizo nyie hamuwajuwi awa jamaa” alisema Mike, huku bado ametazama upande hule, walioelekea wakina Kisona, wakina Khassim wakatega sikio kusikiliza anachotaka kuwaeleza Mike, maana walisha onekana kufahamiana na wale askari wa jeshi la ulinzi, Mike akawatazama wenzake, “huyu jamaa, ni rafiki mkubwa sana wa yule jambazi tulie muuwa jana” aliongea tena Mike, akizipima hakiri za wenzake, kuwa wanalipokeaje neno lake, akawaona waki stuka baya sana, “kumbeeee! unajuwa ata mimi nimeshangaa sana, kuwaona wanajeshi huku” alisema Khassim, na hapo Mike akachomekea neno, “sasa tuwatafute wenzetu ili tuwaeleze kuwa kuna awa jamaa” wakati wana ongea hayo, mala, kwamabali wakasikia kishindo kikubwa cha kitu kama bomu, kikisikika kule walikotokea, wakatazama kwa mshangao, kisha wakatasamu, “tayari huyo mshenzi kapatikana” alisema Mike, maana walizingatia kuwa, Edgar hakuwa na bomu wala kombora la aina yoyote, hivyo ni wenzao ndio wame mtandika,
Mlipuko huo uliwafikia ata wakina Kisona, ambao walihisi kuwa Edgar na Monalisa, watakuwa katika wakati mgumu, hiivyo lazima wawai kuwasaidia, akika unge mwona mzee Mbogo, ungejuwa ni kijana mdogo anae jiunga na jeshi leo hii, maana aliungana na wakina Kisona, kukimbia mbio za nguvu, huku wakiruka vichaka, kufwata kule mripuko ulikotokea,akika uchungu wa mwana. **
Sajenti Idd Kibabu, akiwa umbali wa mita kama mia tatu hivi, toka walipo askari wake, akiendelea kuwatazama, jinsi walivyo kuwa wanasonga mbele kwa tahadhari kubwa, waki huku silaha zao ambazo uwa zinatumika kama silaha za msaada katika vita, zikiwa mikononi mwao, “huyu mshenzi lazima apatikekane, na akichomoza tu achomoki, cha msingi lazima niipate video tape” aliwaza Kibabu, huku akiendelea kuwatazama askari wake, ambao aliwaona wakiendelea kutembea kwa tahadhari.
Mala ghafla, mbele ya wale askari wake, mita kama mia moja hivi, akawaona watu wawili ambao hakuwatambua malamoja, kutokana na kubadiirika kwa rangi za nguo zao, kabla ajagundua kuwa lilikuwa ni tope, hapo akawaona askari wake wakianza kujiweka sawa ilikuwashambulia, watu wale ambao aliwatambua kuwa ni wale vijana wawili wakike na wakiume wanao watafuta, Kibabu aliwaona wale vijana wakisimama ghafla na kuwa shangaa askri wake, ambao walikuwa wanafanya maandalizi ya kuwashambulia vijana awa, wakitumia sekunde kadhaa,
unajuwa nini mdau hapa kawa hasikari mmwepesi wa kutumia silaha hizi, lazima ange tumia ata sekunde tanoi kuweka chini mmg na kuikoki kwaajili ya kushambulia, na pia kupakia bomu la RPG, mala nyingi ufwanywa na watu wawili, kama unge fanya mwenyewe mpigaji unge tumia mudamrefu zaidi,
Lilikuwa kosa kubwa sana, maana vijana hawa hawakumjuwa viziri Edgar, ambae akuwapa muda kumaliza kujiandaa, akaonaekana akimsukuma yule mschana ale kuwanae, ambae alirudi kwenye kichaka cha pembeni ya barabara, huku kijana huyu, akiinua SMGyake, na kuiweka vizuri usawa wabega lake, akiibana vizuri, na kutazama vilengeo, “pigeni nyie wapumbavuuuuuuu” Kibabu alipiga kelele ambazo azikuwa za amri, ila ni hofu kuu, maana alijuwa kitakacho fwata, na ukichukulia askari awa awakuwai kuingia kwenye mtego wa bwana mdogo huyu,
Lakini kelele hizo azikusaidia kitu, maana ika sikika “pah, pah! pah!” ni milipuko mitatu tu! ya risasi hizi za SMG, ikifwatiwa na kishindo kikubwa sana cha, mlipuko, yani “booom!” huku akilala chini, kuepuka vipande vya bomu, ambavyo ata hivyo, visingeweza kumfikia kule alikokuwepo, hapo Kibabu alishuhudia, mlipuko mkubwa ukitokea kati kati ya askari wake, akika baada ya hapo hakuona kitu, zaidi ya moshi mzito, ambao ulitumia dakika kama mbili hizi hivi kupungua, na yeye akatazama vizuri, akika hakuona mtu yoyote alie sismama, wala Edgar akuonekana tena, kule mbele.
Kibabu akiwa anahisi kuchanganyikiwa, akiomba iwe ndoto, alijiinua toka pale chini, huku yeye na dereva wake, wakikodoa macho macho kutazama kule mbele, ambako mwanzo walikuwepo askari wenzao, ambao sasa hawakuonekana, zaidi waliweza kuona kunavitu vime lala, nikama zile bunduki na RPG, kulionekana vitu vingine, zikiendelea kufuka moshi, wakaingia kwenye gari, haraka na kuelekea kule kwenye mlipuko.
Akika walicho kishuhudia, kilimfanya sajenti Kibabu shikwe ma bumbuwazi, maana waliona vipande vya askari wenzao sita, vikiwa vimetapakaa hovyo hovyo, wakiwepo wakina Charles, ambao masaa kadhaa yaliyopita waliwashambulia wakina Mapombeka, “simama haraka simama” alisema Kibabu, huku anafungua mlango wagari, kabla gari lenyewe alijasimama sawa sawa, akifwatiwa na dereva wa gari hilo, yani polisi mwenzie ambae nikama alishikwa na kiwewe, wakasaidia kuokota silaha, ambazo zilikuwa, zinaonekana kama vyma chakavu, huku wakipishana na vipande vya miili ya wanadamu wenzao, ikiwa na vipande vya miguu vilivyo bakia kwenye viatu vyao.
walipomaliza kuweka silaha kwenye gari wakaingia na kuondoka zao kuelekea upande wa barabara kuu ya lami, huku macho yao yakivuja machozi, ya uchungu.
unajuwa ulie mlipuko ulitokea je mdau, nazani bado unajiuliza. basi tuungane kesho katika sehemu ya 32, Hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata