BIKIRA YA BIBI HARUSI (42)

SEHEMU YA 42

ILIPOISHIA SEHEMU YA 41: aling’aka mzee Mbogo, huku akitaka kuinuka ili kusonga mbele, Kisona akamuwai kwa maneno, “wenzako wana fanya hivyo hivyo, ebu subiri usikie mchezo, “alisema Kisona huku ana jinyanyua na kuchungulia kwenye darubini yake, alicho kiona kilimfanya atabasamu, kidogo, kisha aka mpatiua mzee Mbogo, “ebu ona Edgar alicho kifanya” alisema Kisona, huku akimtazama mzee Mbogo, akamwona akiwa ame duwaha, endelea ………..
Unajuwa alicho kiona mzee Mbogo?, mzee Mbogo alimwona Edgar akikimbilia upnde wa chini, kwa kifupi ni kule alikotoka, wakati huo kundi la mbele la polisi na kundi la wakina Ngigo, ambao wote kwa pamoja walisha sikia milio ya risasi, ambayo bwana Kisona alisha gundua kuwa zilipigwa hewani, ndio maana akawasimamisha askari wake, akiytaacha makundi yale mawili yakija kwa speed pale ilipotokea milio ya risasi, pasipo kujuwa Edgar ana wakutanisha katikati, kwa leongo la kupata njia ya kuondokea mahali hapo, akipitia kule ambako polisi walikuwa wanatokea, yani pembezoni mwa mto.
Naam ikawa kama ilivyo pangwa, hamad Polisi waka waona wakina Ngigo, na hapo moja kwa moja waka juwa kuwa hawa ndio wale majambazi wanao saidiana na Edgar, hivyo moja kwa moja wakaingia kwenye majibizano ya risasi, “huyu mtoto hii akiri ameitoa wapi?” alisema mzee Mbogo, huku ana tazama kwkenye darubini, ambapo alishuhudia majibizano ya risasi kati ya kundi la polisi na lile la kina Ngigo, yakiendelea, na alipo tazama kule alukokuwepo mwanae akamwona ana mchukuwa Monalisa, kisha wana ondoka, wakipitia pembezoni mwa mto, “tuana fanyaje ili tuwapate, mana wanaondoka” aliuliza mzee Mbogo, huku akitazama mbele zaidi ya usawa wanao elekea wakina Edgar,
“Mama yangu, Kisona inabidi tufanye jambo la haraka” alisema mzee Mbogo, ambae aliona makundi ma wili ya polisi, yaliyo achiana mita kama mia mbili hivi, moja likiwa mbele kama umbali wa mita mia tatu, toka walipo wakina Edgar, ambayo yalikuwa yanakuja mbio mbio, ikionekana wazi walikuwa wana wai yapao tokea mapigano, mabaya zaidi, kundi la nyuma lilionekana kuwa na silaha nzito, kama RPC na MMG, pia ilionekana wazi kuwa Edgar na Monalisa hawakuwa wana taharifa ya kundi hilo. Kisona ali chukuwa darubini toka kwa mzee Mbogo, na kutazama kule, alikokuwa anatazama mzee Mbogo, na kuiona hatari iliyopo mbele ya kijana wao, sijuwi ni kitu gani kili mtuma Kisona kutazama upande wapili wa mto wa maeno yale waliyopo wakina Edgar, ambao nao bila kujuwa kuwa kuna polisi mbele yao, walikuwa wana kimbilia kaskazini, akaona kuna sehemu moja mitachache toka walipo kuwepo wakina Edgar, mto ulikuwa na mawe makubwa, kwa haraka haraka wenge weza fanya jiti hada za kuvukia upande wapili, lakini alipo tazama juu kidogo up[ande wa pili, aka ona kundi la tatu la polisi, likiwa umbali wa mita kama mia nne hivi, nalo linakuja mbio mbio, kama makundi haya mengine mawili, ikiashilia wana wai kwenye mapambano.
“hatari!!! ebu twendeni haraka” alisema Kisona huku akianza kutimua mbio kuelekea kule mbele, na wenzie wakaunga mibio, lakini kabla hawaja fika mbali waka liona kunsi la kina Ngigo likiwa shinda nguvu polisi, ambao walianza kurudi nyuma na kukimbia ovyo ovyo, huku askari kama watatu wakiwa wamesha chalazwa risasi, na kupoteza maisha.
Wakina Kisona waliokuwa wanazidi kusonga mbele, waliwaona wakina Ngigo wakizidi kuwa shambulia Polisi ambao walisha farakana, na baada ya hapo wakaonekana wakianza kuondoka eneo lile, wakipandisha upande wa juu, ambako kulikuwa na ile barabara afifu, hapo Kisona aka waonyesha ishara askari wake kuwa wasimame, na kisha aka tazama kwenye darubini, upande ambao Edgar alikuwepo.
Naam huko sasa ilikuwa nginja ngija, kama ni hajari basi ya boda boda na semi, maana Kisona aliweza kuwa ona wakina Edgar wakiwa karibu kabisa na ile sehemu yenye mawe, ambayo yeye aliiona wanaweza kuvukia, bahati nzuri nawao walionekana kuiona sehemu hiyo, maana aliwaona wakikatiza na kuanza kusaidiana kuvuka, lakini wakiwa wanajaribu kuvuka, mala Monalisa akateleza juu ya jiwe na kutaka kuelekea kwenye poromoko moja la hatari, haraka sana Edgar aka mdaka mkono, na kuanza kumvuta, pengine kama angeanguka lazima angejibamiza kwenye miamba mikubwa ya mawe, au kwenye maji, lakini kutoka inge kuwa kazi ngumu, na ingewezekana kukutwa nna maadui, walio tapakaa kila kona ya eneo lile na mbaya zaidi walizidi kusogea pale walipo, kingene ambacho ata Kisona akukijuwa ni kwamba, ile tape inge haribika, na kupoteza ushaidi ambao ni moja ya vitu ambavyo vinge mtoa Edgar kwenye shutuma hizi, za hajabu.
Ile Edgar ana fanikiwa kumvuta Monalisa mala waka sikia “tyuuu!” maana yake ilikuwa ni mvu, warisasi ulio fwatia na paaah! paah!, yani milipuko ya Risasi iliyo lindima kwa vujo kuwa fwata, inamaana tayari kundi la pili la polisi, lilisha waona, hapo sijuwi ata nguvu ilitokea wapi, maana Monalisa ali kimbia juu ya mawe yale makubwa, akiwa mbele ya Edgar, ambae alikimbia huku ana tazama maficho, ng’ambo ya mto, huku mivumo na milipuko ya risasi iki sumbua masikio yao, “inamaa” alisisitiza Edgar, na Monalisa akawa anakimbia huku ame inama, maana aliamini kuwa kila anacho ambiwa na Edgar kina kuwa ni msaada kwake, yani ilikuwa kama mganga, akikuambia hiki ni dawa utakunywa tu,
Naam ile wanakaribia kumaliza mto, yani walipo kuwa wame bakiza atuwa kama kumi hivi kufika ng’ambo ya mto, wote wawili waliona kundi kubwa la polisi, mita kama hamsini mbele yao, na hapo Monalisa alie kuwa mbele aliwaona polisi kadhaa, wakiinua silaha zao na kuzielekeza kwao, maana yake ndio alikuwa analengwa, maana yeye ndie alikuwa mbele, hapo miguu ikaiisha nguvu, akisubiri kusikia jinsi risasi inavyo umaga ikiingia mwilini, au jinsi inavyo kuwa ukiwa umekufa.
lakini aikuwa hivyo, Monalisa alie anza kupunguza mwendo,kwa kukata tamaa, aka stuka aki shikwa kwa nguvu na Edgar alie mkumbatia kwa mikono yote miwili, na hapo kama kimbunga, Monalisa akajikuta akiwa ahewani ame kumbatiwa na Edgar, “paaah!” nikama walipiishana na risasi ya askari awa, ikifwatiwa na milipuko mingine mfulizo, huku wao wakitua ng’ambo ya mto, Monalisa akiwa kwenye mikono na kifua salama cha Edgar, kisha Edgar aka vilingika kulifwata jiwe moja kubwa lilo kuwa pembeni yao huku akimweka Monalisa chini, na yeye kuwa juu, Edgar aka iweka silaha yake vizuri, na kuielekeza kule aliko tokea, ambako sasa polisi walisha fika pale walipo vukia wao.
Duh! hapo nikama hakuwa na haraka sana, Edgar aliekuwa kwenye maficho yenye hali mbili, kwa maadui wa upande huu alipo kuwepo macho yalikuwa mazuri, lakini kwa upnde wa ng’ambo ya pili yalikuwa dhaifu, ndio maana akaona bora awa pin down wa ng’ambo kisha achomoke na wa huku aliko kuwepo, Edgar akiwa ameiweka silaha usawa bega, na macho kwenye vilengeo, aka aachia risasi ya kwanza, ambayo mlipuko wake, ulienda sambamba na poli mmoja alie nguka chini na kupiga kelele ya kuchapwa risasi ya mguu, nikama wenzie awa kuwa wame sanuka, Edgar aka iachia yapili, ikawa kama yakwanza, mtu wapili akaenda chini, hapo pilisi waka sanuka, “take cover” ilikuwa ni kelele ya polisi mmoja, alie watahadharisha wenzie, lakini walichelewa tayari risasi kama tano hivi zilisha lia, na askari watano walionekana wakigaragara, chini wakiwa awana shikilia miguu yao, sekunde saba zilitosha kwa askari awa kuwa wamesha jificha.
Lakini aikuwa hivyo kwa upande huu aliopo, maana waliendelea kusikia milindimo ya risasi, na vitu kama tumawe mawe, tukigonga kwenye lile jiwe, “tyuuu!” Edgar aka tazama upande wa mto, akika wainge weza kupitia ndani ya maporomoko yale, maana ni mbali mno, na sasa upande wapili kwa mbali waliona kuna dalili za ujio wa kundi jingine la polisi, hapo Edgar akatulia kidogo na kumtazama Monalisa, alie kuwa ame lala pembeni ya jiwe, huku uso wake ukiwa ume sawajika kwa hofu kubwa, Edgar aka mtabasamulia kidogo, hapo Monalisa nae akatabasamu, huku anameza mate kwa hofu.
Bado milindimo ya Risasi ilikuwa ina zidi kusikika, na sasa ilionekana polisi wapo karibu yao kabisa, Edgar aka ichomoa magazine ya risasi na kuitazama, akaona zime bakia risasi kama nne tu, kwenye ile magazine, aka ichukuwa nyingine na kuiweka kwenye SMG yake, kisha aka ikoki silaha yake na kuiweka risasi chambe, aka zitoa zile risasi nne za kwenye magazine, kisha aka liishika kopo la magazine likiwa tupu, alafu aka fanya kama anaesabu, yani moja mbili tatu, alafu aka lirusha kwa nguvu, kama vile ma bibi harusi wanavyo warushia watu mauwa, “boooom! take cover” zilisikika sauti za polisi nyuma yao, huku milindimo ya risasi ikikoma, na kubakia michako ya nyasi ikionyesha wale polisi wana kimbia, mazine ya risasi, waliyo zania kuwa ni bomu, “kimbilia huku chini” alisema Edgar huku ana inuka na bunduki yake akiielekeaza kule polisi waliko kimbiliam ba kuanza kuachia moja moja, kuwa zuwia polisi awa wasiinue vichwa vyao, kujibu mashambulizi.
Monalisa akaona hii ndio nafasi ya kufuata maelekezo ya Edgar, nae aka chomoka mbio kuelekea kusini aliko elekezwa na Edgar, akifwatiwa na Edgar mwenyewe. Lakini awa kufika mbali wakasikia polisi wakianza kujibu mapigo, hapo Edgar akawa ana jitaidi kujibu mapigo huku wanazidi kusogea mbele, maana alikuwa ana kimbia atuwa kazadhaa, kisha ana geuka na kujibu mapigo, hapo polisi nao waka jibanza, na Edgar ana kimbia kumfwata Monalisa, huku polisi nao wanapoona kimya wana jifichua na kumkimbiza tena Edgar, na sasa makundi mwili yali ungana, kumfukuza Edgar, huku kundi mmoja likienda kulisaidia lile la Ogwambo, na Kibabu, ambao sasa waliwakuta wamesha poteza watu watatu, na mmoja amajeruhi, na maadui zao wamesha kimbia, ikaanza kazi ya kuwarudisha majeruhi wote sita, pamoja na marehemu, pale kwenye makao makuu, ya muda.***
“Mbogo unauakika mwanao alikuwa anasoma, au alienda kujiunga na jeshi flani” aliuliza Kisona ambae nikama alishuhudia mpambano wote, “vipi kwani amefanikiwa kuwatoroka?” aliuliza mzee Mbogo, ambae wasi wasi wake, ulikuwa mwingi sana, “dah! yani utazani amejifunza gorila fight, ame wapiga chenga moja ya hatari, sasa anaelekea magharibi, polisi wana enda kusini, hapo kwa sisi watemi, una wazungukia kwa nyuma na kuwa tafuna risasi” alisema Kisona huku ana iweka tena Darubini yake machoni na kuangalia kule walokoelekea kwakina Ngigo, “safi kabisa” alisema Kisona huku anaishusha Darubini, kisha akawatazama wenzake, “twendeni tuka fanye jambo moja ambalo lita wafumbua hakili wakina kingarame, wote tukaingie kwenye gari?” alisema Kisona, ni baada ya kuwaona wakina Ngigo, wakiwa wameshaifikia barabara, na wana kimbia kuelekea upande wa juu, maana yake walikuwa wana ya fwata magari yao. ***
Mida hii mke wa bwana Mapombeka alikuwa anashuka toka kwenye dala dala, akielekea nyumbani kwake, huku akiwa amebeba kapu lenye vyombo vya vyakula, ambavyo mgonjwa akuweza kugusa, kutoka na kuwa ame poteza fahamu kabisa, mama kijacho huyu akiwa ame tanguliza tumbu lake, la miezi nane, alitembea taratibu huku mawazo mengi kichwani ya kimtawala, juu ya mepenzi wake kijana Mapombeka John, ambae toka jana bado ajaweza kufumbua macho, pamoja wenzie.
Akiwa anatembea huku mawazo yakimsongolota, kichwani mwake, akikatiza kwkenye kwenye chochoro ya kutokea mtaani kwao, mala mama kijacho, aka stuka aki pigwa kibega, aka geuka na kutazama, akawaona vijana wawili, wenye mwonekano wa kiuni uni, wakiwa wana mtazama kwa macho ya ghazab, hapo mke wa mapombeka akajuwa yupo hatarini, “usishangae we mama, ebu tupatie fedha ulizo nazo” alisema moja wa vijana wale wauni kweli kweli, kutokana na jinsi walivyo vaa, “jamani mbona mimi sina kitu, natoka hosptal kumwona….” akupewa nafasi ya kumalizia sentesi, alistuka kifi zito likitua usoni mwake, “mama nakufa” alipiga kelele mke wa mapombeka, huku akiachia vyombo alivyo shika mkononi, na kujiziba uso wake, “towa ulichonacho kabla hatuja kutumbua ilo tumbo we mwanamke, alisema tena mmoja wawale vibaka, akika dada huyu, moyo wake ulipatwa na uchungu mkubwa sana, na kujiona mwenye mikosi kwa kipindi hiki kikubwa,
Lakini, ile kufumba na kufumbua, mala aka mwona kijana mmoja mwenye suit nyeusi, akija mbio mbio sehemu ile na kuanza kupambana na wale vijana, ambapo nikama walikuwa wanapigana kwa mtindo wa karate, za kwenye video, mpaka wale vijana wawili walioonekana kuzidiwa, walipo kimbia na kutokomea zao, ndipo yule kijana aka msogelea mke wa Mapombeka, “pole sana dada yangu” alisema yule kijana mtanashati, lakini mke wa mapombeka akawa kama ameshikwa na butwaha, maana majinsi mambo yaliyo tokea, aliona kama yupo ndotoni, “dada naitwa Isaya, sijuwi mwenzangu ni9 nani na unaishi wapi?” alisema yule kijana alie jitambulisha kuwa ni isaya, “na itwa Caloline, nakaa hapo mbele” anikama alikuwa ame zinduka toka kwenye usingizi, alijibu Mke wa mapombeka, “twende ni kusindikze, nyumbani, maana inaonekana huu mtaa ni wa hajabu sana” akika mke wa mapombeka alimwona kaka huyu, kama ni malaika alie tumwa kuja kumsaidia, hivyo akakubari kuongozana nae, kuelekea nyumbani kwake, ***
Mida hii Serena Hotel, palisha changamka, ni kama jana wanafamilia hawa baada ya kuwa wamesha pata chakula cha mchana, sasa walikuwa wanapata vinywaji, yani pombe, lakini tofauti ilikuwa kwa baba Monalisa, ambae alikuwa anamtazama kwa umakini Erasto, ambae alikuwa akikonyezana mala kwa mala na yule mhudumu, ambae alimwona asubhui akiingia chumbani kwake, ambae sasa alikuwa amekaa meza kama ya tatu toka walipo kuwa wao, “huyu mshnzi ndio maana ame mtia mikosi mwanangu” aliwaza baba Monalisa, ambae alikuwa anapanga jinsi ya kumweleza mke wake juu ya tabia ya mkwe wao, maana mke wake alikuwa aambiliki juu ya hii ndoa, baba Monalisa ana kumbuka jinsi mke wake alivyo nuniana na mwanae, kuhusu hii ndoa, pale mwanae Monalisa alipo kataa kuolewa na Erasto, “we ngoja tu, lazima wata endelea awa, kwani vitamu uliwa mala moja?” alijisemea mzee Anderson, ambae wenzie wote walijipa moyo, juu ya uwezekano wa kupatikana kwa Monalisa, asa baada ya redio ya taifa kutangaza kuwa polisi wengi wameongezwa kwenye msako,
Waiwa wana endelea kulewa, wakidai wanapoteza mawazo, dereva wa bwana Anderson alikuwa ana mtazama kwa umakini boss wake, ambae alihisi kuwa amesha gundua mchezo mchafu wa Erasto, ambao yeye uwa ulimkela sana leo mapema na muda ule ambao alimwona Boss wake pale korodoni, akihis kuwa ame sha stukia mchezo ule, wa mkwe wake mtarajiwa.
dereva nae aliona jinsi boss alimwo kuwa anamtazama mkwewe, alie kuwa busy akimkonyeza demu wake, pasipo kujuwa kuwa, kuna watu walikuwa wana mwona, tena ni watu ambao awakutaka kabisa kuona vitendo hivyo. ***
Mita mia mbili toka kwenye mashamba ya viazi mviringo, saa kumi za jioni, kwenye makao makuu ya oparetion, roho mkononi,ndani ya hema moja, kati ya kumi yaliyopo eneo lile, walionekana makamanda wa wakuu wa polisi mikoa, na wanadhimu wao wakiwa wame tandika ramani yao, huku wakipatazama kwa umakini mkubwa, sehemu moja, pembezoni mwa mto upande wa kusini mashariki, “lazima watakuwepo hapa, ndio panapotokea mapigano” alisisitiza RCO Iringa, huku wenzie wakitaja eneo la mbele kidogo, ni baada ya kusikia milipuko ya risasi, masaa mawili yaliyopita.
Wakati wana endelea kubishana, mala akaja askari mmoja, mmbio mbio, “afande ni vyema kama mkija kuona” alisema yule askari, baada ya kupiga salut, nao wakainuka na kutoka ndani ya hema, wakimfwata yule askari, polisi alie elekea kwenhe hema moja walilo liteua kama hospital, ambalo nje yake walionekana askari kashaa waliotoka porini wakiwa na wana nawa damu mikononi mwao huku nyingine zikiwa zime watapakaa kkwenye uniform zao.
Walitumia sekunde chache tu, kufika na kuingia ndani ya hema lile, “mungu wangu nini, hiki?” aliuliza RPC Iringa, akimtazama Ogwambo, alie simama ana watazama mdoctor, walio kuwa wana washuguri kia majeruhi sita, huku askari wengine watatu wakionekana, wakiwa wame lala kwa utulivu kabisa, awakuwa na uhai tena, “afande wale watu siyo wa kawaida” alisema ASP Ogwambo afisa, mdogo wa polisi, toka Iringa, huku akiwa ameinamisha kichwa chini, kwa uzuni, “kwa hiyo unataka kuniambia kuwa tumwambie IGP, kuwa tume shindwa kuwadhibiti awa majambazi” aling’aka RPC Iringa, huku RPC Ruvuma akidakia, “kwa hiyo mme waaacha waende bila askari wa kuwa fwatilia?” hapo Ogwambo, aka eleza kama ilivyo kuwa, “akika atuja juwa mapaka sasa, alie piga risasi ni nani na alikuwa anamshambulia nani” alieleza Ogwambo, jinsi walivyo kimbilia kwenye milio ya risasi na kukutana na wale majambazi, kisha kuanza kushambuliana, na wale majambazi waliokuwa juu, kuwashinda nguvu, “tatizo wenzetu walichelewa, nao walikutana na kijana mwenye yule mwanamke, ambae walishambuliwa pia, na ndipo walipo patikana majeruhi awa watano, huyu mmoja alipatikana kule juu, ambapo wenzake waliuwawa” hapo wote waka hema, kwa mchoko wa nguvu, “kazi hipo, lakini aimaanisha kuwa tuna waacha waende, lazima tuwapate na walipie” alisistiza RPC, Iringa, baada ya Ogwambo kumaliza kusimulia.
“Madical Oficer, fanya utaratibu, wa kuwapeleka hao majeruhi mjini, magari yapo na yote yana mafuta” alisema RPC, Iringa akimtazama mganga mkuu wa polisi, waliekuwa nae pale, kisha wao wakatoka.***
SSP Manase Kingarame au King kama wenzake wanavyo mwita, mida hii alikuwa ametulia ndani ya gari, lililo egeshwa kwenye chochoro moja ya mtaa wa Kilolo, hapa mjini Makambako, pamoja na Hokololo na askari wake wachache, sijuwi wengine alienda wapi, maana nikama Kingarame alikuwa anasubiri kitu, “hii inshu ime kuwa ngumu sana, sijuwoi kwa nini?” alisema Kingarame, alieonekana amechoka kwa mawazo, “lakini afande naimani lazima tuta fanikiwa tu! maana hakuna atakae wa kamata wale watoto wakiwa hai, lazima wata wauwa tu!” alisema Hokololo.
Nawakati huo huo, wakaonekana vijana wawili waliovaliia kiuni, wakija haraka na kupanda ndani ya gari ili la mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa ruvuma, kisha wakaanza kubadiri nguo zao na kuva uniform za polisi, akika kama kuna raia ange ona, ange shangaa sana, “vipi mme fanikiwa” aliuliza Kingarame alie kuwa anachungulia kwenye dirisha la gari, “ndiyo afande tume fanikiwa, na mchezo umeenda vizuri kabisa” alijibu nnoja wawale vijana ambao kama una kumbuka vizuri, ndio wale walio mzabua kofi mke wa mapombeka, “dah! afadhari kwa hiyo mambo yameendaje huko?” aliuliza Kingarame kwa shahuku, ya kutaka kujuwa, hapo mmoja wao akasimulia kama ilivyo kuwa, “yani afande, kama yule mwanamke ange kuwa siyo mjamzito, Issa mida hii ange kuwa anajilia vyake, kwa jinsi alivyo jikombea ujiko” hapo wote wakacheka, “ok! sasa wacha turudi porini, nazani issa tuta mfwata usiku” alisema Kingarame huku wanasubiri wenzao wamalize kubadiri nguo, alafu waondoke zao.***
Baada ya kukimbia sana huku wakishambulia, pasipo kuona majibizano yoyote ya risasi, mala askari polisi aliekuwa anacheo kikubwa kati ya polisi wote wa makundi haya mawili aka wasimamisha wenzake, “ebu subirini, mnajuwa kama tumesha kimbia mbali sana, pasipo kuona dalili ya uwepo wa hawa jamaa?” aliuliza ASP Msengi, baada ya askari wote kijikusanya sehemu moja, “inawezekana ame topotea hapa kati kati” alisema Sajen Kibabu, ambae akuataka kuwa mbali na wakina Edgar, ili aakikishe kuwa wana uwawa na yeye anachukuwa ile tape, namuda umesha enda naona ina elekea saa kumi na moja, nivyema kama tutaanza kurudi, nazani mpaka tukifika ngomeni, tayari giza litakuwa limeingia” alishauri ASP Msengi nao wakaanza kurudi walikotokea, huku wakisimuliana jinsi kila mmoja alivyo jificha wakati wana shambuliwa na umaili wa Edgar kwenye mapigano, “lakini kunakitu kime nishangaza” alisema mmoja wa askari, “kitu gani tena?” aliuliza ASP Msengi, huku wana tembea kurudi waliko tokea, “hivi mliona jinsi yule jamaa alivyo mwokoa yule mwanamke alie mteka, una juwa nime shangaa sana” alisema yule PC, na hapo kila mmoja akaanza kuchangia lakwake, “alafu mbaya zaidi ata sisi, atuja kumbuka kuwa huyu dogo alikuwa na mateka” alisema wakwanza, mwingine akadakia, “alafu zinga la demu” alisema mwingine na hapo hapo mmoja akatoa hoja iliyo mstua sajent Kibabu, “jamani mbona kama yule demi aonyeshi kama ametekwa?” hapo wote kama waka kubariana na ile kauri ya mwenzao, “kweli bwana, si umeona ata demu mwenyewe anavyo tukiambia?” alisema mmoja wao na ASP Msengi aka sema, “nitaenda kumweleza mkuu, maana isije kuwa demu amesingizia ametekwa, kumbe nae ni jambazi, au ni demu wa yule jambazi” wazo ilo liliungwa mkono na watu karibia wote, ispo kuwa polisi wachache kutoka songea, walio kuja na SSP Manase Kingarame, na sajent Kibabu mwenyewe, ndio walitazamana kwa macho ya fedhea,
Wakiwa katika mijadala hiyo, mala wakasikia tena pah!, sekunde kidogo pah!, ilikuwa ni milio ya risasi kama nane hivi, alafu ika gota, lakini safari hii milio hiyo ilisikika mbali sana, lakini upnde ule waliko shambuliana mwanzo, “mh! kime nuka tena, yani utazani ni vita” alisema mmoja wao, huku wakitega masikio kusikia kama kuna mlipuko mwingine uta fwatia, lakini ikawa kimya, na hawakujuwa ninani anae shambulia, na nani anashambuliwa, ila nazani mdau wewe unatamani kujuwa hizo risasi zime mshambulia nani.**
Kama unakumbuka ilikuwa hivi, “safi kabisa” alisema Kisona huku anaishusha Darubini, kisha akawatazama wenzake, “twendeni tuka fanye jambo moja ambalo lita wafumbua hakili wakina kingarame, wote tukaingie kwenye gari?” alisema Kisona, ni baada ya kuwaona wakina Ngigo, wakiwa wameshaifikia barabara, na wana kimbia kuelekea upande wa juu, maana yake walikuwa wana ya fwata magari yao, ambayo wao walipishana nayo wakati wana kuja huku.
Kisona ali mgeukia mzee Mbogo, “mzee Mbogo kachue gari, rudi na barabara kwa mwendo mdogo” alisema Kisona huku ana iweka darubini yake kwenye mfuko wa kombati, na kuikamata bunduki yake, “wewe ongozana na mzee mbogo” alisema Kisona huku akimwonyeshea kile askari mmoja, alafu aka mtazama Katembo, “sasa twendeni tuka toe sanaka ya ardhi, uelekeo ni huu” alisema Kisona huku akianza kutembea kuelekea kule alikowaona wakina Ngigo wana kimbilia, akifwatiwa na askari wake, pamoja ana koplo katembo, walitembea kwa mwendo wa haraka sana, huku wakikatiza kwenye nyasi kama vile wana pita kwenye lami, pasipo kelele wala vishindo, akika ilipenza, kama ungeona ungezania kuwa ni pecial force toka marekani.**
Baada ya kusaidiwa na yule kijana mtanashati alie valia suit nyeusi, mke wa bwana mapombeka aliongozana nae mpaka nyumbani, huku wana ongea hili na lile, “awa vijana wabaya sana, yani unamkaba mtu chana wote huu, tena mjamzito, bila aata huruma,” alisema Isaya kwa sauti ya upole yenye masikitiko, “yani kaka mi mwenyewe sijuwi nikushukuruje, ille kutokea kwako ndio imekuwa afadhari kwangu” alisema mke wa Mapombeka, kwa sauti iliyoonyesha anaongea toka moyoni.
Walipofika nyumbani mke wa Mapombeka alimkaribisha mgeni, aka mwacha sebuleni na yeye akaingia chumbani ambako akukaa sana, akarudi kama ame kumbuka jambo, “samahani kaka Isaya, kwa ni wewe ni mwenyeji wa hapa Makambako?” aliuliza mke wa Mapombeka, huku akikaa kwenye kochi, na kutazamana na mgeni wake, alie tabasamu kidogo, “hapana mimi siyo mwenyeji, nimpita njia tu, natokea Morogoro, naelekea Mbeya, kwenye semina, nilipanda gari la songea, hivyo nimeona nipumzike Makambako, alafu kesho nielekee Mbeya” alisema Isaya kwa sauti folani ya upole, na hatua, kama unge msikiliza vizuri unge juwa kuwa ni mtu mwenye busara nyingi sana, “hivyooo! kwa hiyo wewe ni mwalimu au?” aliuliza mke wa mapombeka, alie onyesha kumwamini sana Isaya, alie tabasamu kidogo “mimi siyo mwalimu, ila ni mchungaji, naenda Mbeya kwenye semina ya dini” hapo Isaya akaliona tabasamu moja matata sana usoni kwa mwana dada huyu, “kumbeeee! yani leo na bahati kubwa sana kusaidiwa na mchungaji, lakini mbona ujuwa kupigana hivyo?” lilikuwa swali lililo mtabasamulisha tena Issaya, “nilijifundisha wakati nasoma seminali, huko hanga songea” alijibu Isaya, ambae Moyoni alisema, “unabahati una mimba kubwa, leo ninge punguza gundi”
Basi hapo yakaendelea maongezi kwa sakika kadhaa, kabla Isaya ajaingia kwenye lengo lililo mleta, “sahamahani dada toka nime fika, sija mwona shemeji, au amesafiri?” aliuliza Isaya, na hapo Carolina aka msimulia Isaya kilicho mkuta mume wake, akimweleza kuwa ameumia huko porini waliko kuwa wana saka majambazi, “hooo! pole sana dada yangu, lakini mungu wetu ni mwema, mungu wetu ni mponyaji, ata msimamia shemeji ata pona tu!” alisema Isaya, akika unge msikia ungejuwa kuwa ni mchungaji kweli, “yani hapa nimekuja kuoga tu! nika lale Hospital” aliongea mke wa mapombeka kwa sauti ya uzuni kidogo, “kwa ni ame lazwa wapi, situnaweza kuongozana nika mjulie hali shemeji, maana huu ndio mwanzo wa kufahamiana” alisema Isaya, hayo maneno ya busara iliyo pitiliza, “haaa! aita wezekana, ame lazwa hospital ya jeshi, yani naruhusiwa mimi tu kumwona, na wakubwa wake wapolisi” alisema Mke wa Mapombeka, hapo kikapita kimya kidogo, kama kila mtu alikuwa anawaza lakwake, mala mke wa mapombeka aka inua uso, nikama alikuwa amepata jibu, akainua uso, na kumtazma kaka yake wa kupanga, lakini naweza nikasema kuwa wewe ni kaka yangu, umekuja kumwona sehemeji yako, baada ya kusikia ana umwa” hapo Issaya alitulia kimya kama anatafakari hilo jibu, kumbe kimoyo moyo alijisemea, “pumbavuuna tafuta fo cha mumeo kwa hakiri yako mwenyewe” Isaya aliinua uso, akiwa ame uwka kimasikitiko, “japo nizambi kwa mungu wetu, kudanganya, lakini atuna budi, kufanya hivyo, maana ata yesu aliwatembelea wagonjwa na walemavu” alisema Isaya kwa sauti ya kinyonge, huku ana papasa mfuko wake wasuit na kugusa bomba la sindano na kijupa flani.
Huo ndio ulikuwa mapango wa Issaya na Mke wa mapombeka, ambae hakujuwa kama ana msogeza israel kwa mume wake mpendwa,***
Huku nako baada ya kukimbia kwa mwendo mrefu kidogo, vifua vyo viki kata pumzi, bundukizao wakizona mzigo, Ngigo aka simama na kujishika magoti, “awawezi kutufikia tena, nazani wana mkimbiza yule dogo, tuvute pumzi, alafu tuwafwate wakina chiza” alisema Ngigo huku ana hema juu juu, na wenzake waliokuwa wamefanya kama yeye, nao wakamuunga mkono.
Lakini wakati wana hema ovyo ovyo, mala wakasikia ngurumo ya gari, wote waka stuka na kutazama kule walikotokea, kwambari wakaliona land rover la kijani, likija taratibu kabisa, “sikieni tujifiche upande mmoja” alishauri Ngigo, huku ana kimbilia porini upande wa kushoto wa barabara, akifwatiwa na vijana wake nane, wakaenda na kujificha umbali wa mita ka aishirini toka ilipo njia, wakilala kwenye majani na kushindwa kuonekana kwa mtu ambae ata pita barabarani, “sikieni hawa ni moja ya madui zetu, kama alivyo sema King, kwa hiyo likikatiza tu hili gari, ni kumimina risasi kwa kwenda mbele” alisema Ngigo, na hapo vijana wote waka nyoosha silaha zao kutazamisha kwenye barabara, wakisubiri ile gari likatize, walimiminie risasi,.
Walitulia kwa dakika kadhaa, pasipo kuona gari likipita, sasa ata ngurumo ya gari ilibadirika na kuwa kama lililo simama, “au wame tustukia nini, mbona awaji?” aliuliza Ngigo, ambae alisha wai kufanya kazi nyingi za hatari, “mh! wame tutega” alisema Ngigo huku anainuka na kuanza kumbia kuelekea mbele zaidi akifwatiwa na wenzake, akika yalikuwa ni machele ya hali ya juu. itaendelea Hapa hapa kwa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!