BIKIRA YA BIBI HARUSI (44)

SEHEMU YA 44

ILIPOISHIA SEHEMU YA 43: Dakika tatu baadae msafara ukaondoka kuelekea mashariki, akiwemo bwana Kingarame, ambae sasa alikuwa anahisi presha inapanda, presha inashuka, maana akujuwa kilicho watokea wakina Ngigo, Endelea…………
“awa wachungaji wanamoyo sana, yani am katisha matembezi yaka kwaajili ya kunipeleka kwa mgoniwa” aliwaza mke wa Mapombeka, wakati akiwa ana maliza kujiandaa, kwa safari ya hospital ya kanda ya kijeshi, kumwona mume wake, “yani nnge kuwa siyo mjamzito ninge sema kuwa, ana nitamani, ila ukweli ni kwamba huyu kaka ana moyo wa peke yake kaisa” aliendelea ku mwaga sifa kimoyo moyo, huku ana toka chumbani kwake na kujitokeza sebuleni na kumkuta Isaya, akiwa ametulia anasinzia, kwa usingizi wa jana usiku porini, “pole kaka nime kuacha peke yako” alisema mke wa Mapmbeka, huku anaachia tabasamu, pana akimtazama Isaya alie kurupuka toka usingizini, “haa! usijari shemej… dada” alisema Isaya akionekana ana mang’amu ng’amu ya kusinzia, “haya kaka mi nipo tayari tuna weza kwenda” alisema mke wa mapombeka alie kuwa amashika kikapu che nye chombo cha kuweka chakula,
Safari ilianza mala mojakuelekea Hospital, wakipitia hotelini kununua chakula ambaho waliona kita mfaha mgonjwa, maana muda wa kupika aukumtosha mwanamama huyu mjamzito wa mimba ya kwanza, baada ya hapo ikaanza safari ya kuelekea kituo cha dala dala, wa safari ya hospital, huku njiani wakiongea mawili matatu. **
Mama na baba Erasto walitembea haraka mpaka koridoni, na kutzama kule kwnye chumba namba kumi na sita, waka mwona dada mhudumu anaenda moja kwa moja na kufungua mlango wa chumba hiicho, na kuzama ndani, waka tazamana na kucheka kabisa, huku wanashikana mikono na kuelekea chooni, “huyu mtoto sijuwi amemlithi nani?” alisema mama Erasto huku anacheka sambamba na mume wake, “lazima ajifunze utundu wa kitandani, akikapata katoto ka Anderson aka fanye ukweli” alisema Misago na hapo wakacheka tena, “tena ina bidi umpe mbinu za kutoa bikira, kama ulivyo nifanyaga mimi” alishauri mama Erasto, huku wanaendelea kucheka na kugongeana mikono, kwa furaha, kabla awaja tengana na kuingia vyooni.
Dakika tano badae waka kutana tena nje ya choo na kuelekea kule waliko waacha Anderson na mke wake, “nime ipenda sana hii safari” alisema mama Erasto wakiwa wana karibia kwenye meza waliyo kaa wenzao na dreva wao, “yani mama Erasto, tukimpata Mona, nitakunywa pombe mpaka nitambae” alisema mama Mona, kwa sauti ya kilevi, wakati Misago na mke wake wakiwa anakaa, kwenye viti vyao, “yani sana, tena tunaanza pati ya kuveshana pete hapa hapa” alisema mama Erasto na wote waka shangilia, kasoro baba Mona, peke yake, dereva alitabasamia pembeni, “jamani mna zani ni hivi ni vitu lahisi?,” aliuliza baba Mna kwa sauti flani iliyo wagutua washangiliaji, wote waka mtazama, wakiwa wameacha kucheka, “yani hamjuwi mtoto atakuja akiwa katika hali gani, alafu mnapanga kusherehekea, sijuwi kuvalshana pete” yani nikama mzee huyu alijikuta ameongea tu! japo Dereva alijuwa kila kitu, lakini na yeye akatulia kumtazama mzee Anderson, “lani baba Mona, wewe sindie unasema kuwa unamwamini Edgar ato mfanyaia Mona kitu kibaya?” aliuliza mama Mona, kwa sauti iliyo jaa mshangao, huku akimtazama mume wake kwa macho ya mashangao, “ndio lakini si ame mteka, n bado atujuwi kwanini ame fanya hivyo” alisema baba Monalisa huku ana chukuwa pombe yake na kuinywa, kwa mikupuo miwili mfululizo, nauwa anafanya hivyo akiwa na kitu kilicho mkela, “huyu Edgar ameamua kumkomoa mwanangu” alisema mke wa Misago, kwa sauti ya kulalama, “kwani Edgar na Erasto waliwai kuwa naugovi wowote?” aliuliza Dereva na hapo mzee Anderson aka tazama kiti cha Erasto kilicho kuwa wazi, “labda yeye ange tuambia, kwani yupo wapi huyu?” aliuliza mzee Anderson, hapo wakaonekana baba na mama Erasto ana tazamana, kama wanaulizana kitu cha kujibu, “kweli jamani yani toka ameondoka ajaarudi kabisa” alisema mama Mona, huku mzee Anderson alie kuwa anajuwa kuwa wazee awa walikuwa wanajuwa fika kuwa, mtoto wao amesha jifungia chumbani kwake, na mhudumu wa pale Hotelini, “atakuwa amejifungia chumbani kwake, siunajuwa kuwa anajisikia uzuni sana, kwa hili lililo mkuta mchumba wake” alisema mama Erasto akijifanya kuigiza sauti ya uzuni, “dah! nikweli jamani, unajuwa kumwacha peke yake anaweza kujidhuru, ebu nimfwate nika mlete tuwenaae karibu” alisema mzee Anderson huku akiinuka toka kwenye kiti chake, ***
saa mbili na nusu za usiku, ndio mida ambayo makamanda wa polisi mikoa, walikuwa wame fika kwenye eneo la tukio, kama walivyo elekezwa na Kisona, alie waletea silaha tisa, “mungu wangu wakinani hawa?” lilimtoka swali kamanda wa polisi mkoa wa Iringa, huku akiikodolea miili ya vijana wawili walio lala pembeni ya magari mawili, aina ya land Rover mia na kumi, yenye namba za kiraia, “mh! afande huyu kijana una mkumbuka?” aliuiza OC FFU, wa Ruvuma, akimtazama RPC Ruvuma, “sura siyo ngeni kabisa, ila sikumbuki nilimwona wapi” alisema RPC Ruvuma, huku akizidi kuukodolea macho mwili mmoja kati ya miwili ya wale marehemu, “huyu ni yule kijana tulie wai kumkamata kwenye inshu ya meno ya ndovu, na jambazi mmoja hivi tuna mtafuta sana yule mwenye madevu, anaitwa Ngigo” alikumbusha OC FFU, toka mkoa wa Ruvuma, mapigo ya moyo ya Kingarame, yakaongeza kasi, na mbaya zaidi , RPC Ruvuma aka kumbuka, “ok! nimeshakumbuka, tena yule jamaa anagenge kubwa la waalifu” alisema RPC toka Ruvuma, wakati huo askari polisi walikuwa wana endelea kuzagaa eneo lile, kwa maelekezo ya wakubwa ao, kama walivyo elekezwa na Kisona, “kwa hiyo ni kati ya wale tulio waona kule mtoni asubuhi?” aliuliza RPC Iringa, “ndiyo wame tokea songea, na lazima Madevu atakuwepo mahali hapa” maneno hayo ya OC FFU, yalizidi kumkoroga Kingaame, ambae alikuwa ana omba asipatikane mtu ata mmoja alie hai, maana siri ina weza kuwa hadharani.
Bahati ilikuwa upande wa Kingarame, mana baada ya askari polisi kuzunguka kwa muda wa nusu saa, ndipo walipo ikuta miili ya watu wanane, ikiwa ime lundikwa sehemu Moja, kitu hiki kilimpendezesha sana Kingarame, japo makamanda wa nao walifuraia kwa msaada wa kuwapunguza maadui wao, ambao mpaka sasa hawakujuwa idadi yao.
Lakini kilicho mashangaza Kingarame ni kuto kumwona mtu mmoja, ambae nibwana NGIGO, na kulicho mchanganya zaidi ni kwamba, silaha ziliuja kumi na moja, na watu wame patikana Tisa, “je mmoja yupo wapi?” alijiuliza Kingarame, wakati huo hakujuwa kama kuna mazito yana fwatia “eti! unaonaje ukiwasiliana na RTO Ruvuma, kutafuta usajili wa magari haya, ili kujuwa mliki wake?” lilikua wazo zuri, toka kwa RPC Iringa, kwenda kwa RPC Ruvuma, wazo ambalo lili mstua sana Kingarame, “ni kweli bwana, inaweza kusaidia, eti OC ebu kumbuka kumpigia simu RTO, tukifika mjini, nazani tuta pata muusika mkuu wa tukio hili, toka NMC, mpaka huku, porini” alisema RPC, pasipo kujuwa kuwa muusika mwenyewe yupo karibu yake kabisa, na anasikia lika kitu, na sasa alikuwa anatabasamia pembeni, “ndiyo afande itatekelezwa kama ilivyo amriwa” alijibu OC FFU,**
Safari ya kwenda hospital ilichukuwa muda mrefu kidogo, maana mke wa Mapombeka na kijana alie msaidia toka kwa vibaka, yani PC Isaya, baada ya kufika kwenye kituo cha kusubiria magari, walikaa sana pasipo gari lolote kupita, mida kama hii magari uwa machache sana asa upande huo, maana walitegemea magari yaendayo mafinga na nyororo, baada ya nusu saa ndipo walipo liona gari moja likipita japo lilikuwa lime jaa, lakini aliweza kupata nafasi ya kusimama, ambapo kilomita nane mbele, wakashuka, kwenye kituo cha station, yani Tazara, mita kama mia mbili hivi toka kwenye lango kuu la kuingilia kambini, ambapo walitumia dakika zisizo zidi tano kulifikia, “eleza shida yako” aliuliza mmoja wa askari wa jeshi la ulinzi, kati ya wawili waliokuwepo pale langoni, “mimi ni mke mmoja wa polisi walio umia huko porini” alijitambulisha mke wa mapombeka, “na wewe ninani, na shida yako nini?” lilikuwa swali kwenda kwa Isaya, lakini kabla ajajibu mke wa mapombeka akadakia, “huyu ni kaka yangu, ame tokea tana ngizi, kuja kumwona mgonjwa” hapo yule askari, aka mtazama Isaya, kisha aka sema “sina mamlaka ya kumluhusu kuingia, labda muonane na ngazi za juu, sababu akijatolewa kibari cha mtu yoyote kuingia kwenda kumwona mgonjwa zidi yako” licha ya maneno hayo, askari ule aliwaruhusu waende kumwona mkuu wa ulinzi, nao waka fanya hivyo wakijieleza kama walivo fanya mwanzo, pale getini, lakini jibu likawa lile lile, kuwa “sina mamlaka ya kukuruhusu, ila ngoja ni wasiliane na ofisa wa zamu” ikawa hivyo ata ofisa wa zamu alipo kuja, na wakina Isaya kujieleza, naea aka waruhusu, lakini kwa sharti mja, “auta ruhusiwa kulala ndani ya hospital, unamwona mgonjwa kisha unaondoka” hivyo ndivyo mke wa Mapombeka alivyo fanikiwa kumwingiza adui wa mume wake hospital, pasipo yeye kujuwa mpango wa Isaya, juu ya mume wake mpendwa.
Moja kwa moja waka eleka Hospital, na kupokelewa na doctor wa zamu, “karibu shemeji bila shaka ni wewe mke wa koplo Mapombeka?” alisema yule doctor, akionyesha kuwa amepewa maagizo ya kuwa mama huyu atakuja usiku ule, kwaajili ya kulala, “ndio mimi shemeji, nime kuja na kaka yangu anakuja kumwona shemeji yake” aikuwa kazi ngumu kwa mke wa mapombeka, kumweleza doctor “huyu ambae hakuwa na malaka ya kumzuwia Isaya, kumwona mgonjwa, “hakuna tatizo shemeji, unaweza kwenda kumwona mgonjwa, ila bado aja fumbua macho, yapo vidole vina cheza” alisema yule doctor na wakina Isaya waka elekea moja kwa moja kwenye ward special waliyo lazwa wale askari wa jeshi la polisi walio shambuliwa kule porini,
Ndani ya ile ward Isaya aliweza kuona ilikuwa tulivu sana, huku wagonjwa wote wakiwa katika hali tulivu, madrip yana ning’inia pembeni ya vitanda vyao, yakiichuruzisha maji taratibu, kupia kwenye milija myembamba, kwenda kwenye miili yao, ikitumia sindano zilizo dungwa kwenye mikono yao, iliyo kuwa ina chezesh vidole, kila baada ya sekunde kadhaa, hapo Isaya alimtazama mke wa mapombeka alie enda moja kwa moja, kwenye kitanda cha mume wake, na kumzatazama usoni kwa dakika kadhaa, kisha akageuka na kumtazama yeye Isaya, “kaka unge kaa hapo” alisema mke wa mapeka, huku akionyesha kitanda, cha pembeni ya kitanda cha Mapombeka ambacho akikuwa na mtu, nandicho kitanda alicho lalia dada huyu usiku uliopita, kwa maana hiyo na leo ata lalia hichohicho, “asante dada, ila inaonyesha wata fumbua macho, muda siyo mrefu” alisema Isaya, huku ana kaa kwenye kitanda, na ,kono wake mmoja akajipapasa, kwenye mfuko wake wakoti la suit, aka gusa bomba la sindano na kichupa cha sumu alicho kabidhiwa na Boss wake SSP Manase Kingarame, “nita shuru kwakeli yani hawa majambzi ni watu wabaya sana” alisema mke wa mapombeka kwa sauti ya kinyonge sana,
hapo yaka fwata maongezi ya hapa na pale, huku Isaya kisubiri mke wa Mapombeka ampe nafasi ndogo, ya kufanya yake, ***
“atakuwa amejifungia chumbani kwake, siunajuwa kuwa anajisikia uzuni sana, kwa hili lililo mkuta mchumba wake” alisema mama Erasto akijifanya kuigiza sauti ya uzuni, “dah! nikweli jamani, unajuwa kumwacha peke yake anaweza kujidhuru, ebu nimfwate nika mlete tuwenaae karibu” alisema mzee Anderson huku akiinuka toka kwenye kiti chake, lakini bwana Misago aka mdaka mkono, “tulia bwana Anderson, aina haja ya kuangaika, atakuja tu!” alisema Misago yani baba Erasto huku akijuwa fika kuwa mwanae kule chumbani alikuwa na yule dada mhudumu, baba Monalisa aka jikalisha kwenye kiti kama mzigo, kutokana na ulevi, nikama aitaka kuinuka tena, lakini nikama alivurugwa na ujio wa polisi mmoja mwenye nyota mabegani kwake, alie onekana akikatiza eneo lile na kuingia moja kwa moja kwenye jengo kubwa, la hotel, “haa! yule siyo polisi wa songea” alijisemea Anderson, baada ya kushindwa kumtambua, OCD wa Njombe ambae alielekea moja kwa moja mapokezi, na kuweka oda ya vyumba sita, vya makamanda wenzake wapolisi, toka songea na iringa.
nanusu saa baadae wakamwona yule dada mhudumu akirudi kwenye kiti chake na dakika chache baadae akafwatia Erasto, wakina baba Erasto wakihisi kuwa mchongo ule wana ujuwa wao tu!, kumbe kati yao ni mama Mona pekee ndie alie kuwa hajuwi lolote, “vipi Erasto, naona umesha pumzika kidogo?” aliuliza baba Erasto huku ana tabasamu, Erasto hakujibu kitu, zaidi alitabasamu tu, na kuagiza pombe nyingine, “ungekula kwa nza bwa Erasto, maana hivi itu vina itaji nguvu” alisema Anderson na hapo wapo waliostuka, na wapo waliochukulia kawaida kuwa pombe inaitaji nguvu, ***
Mida hii ndio mida ambayo Kisona na wenzake walikuwa wana malizia kumkabidhi Ngigo, kwenye ofisi ya Military Polisi, (MP) “awe anachangamshwa mala kwa mala” aliagiza Kisona wakati anataka kuondoka,
“vipi afande uendi kuwatazama wagonjwa ilitujuwe wanaendeleaje?” aliuliza Katembo, na hapo Kisona akawa kama ame kumbushwa jambo, “hoooo! nikweli Katembo, ebu twendeni tuka waone wale wagonjwa, alafu tuka pumzike, naimani Edgar atakuwa sehemu salma kabisa” alisema Kisona akiwa amesha kaa kwenye kiti chake, yani ndani ya gari, hapo mzee mbogo aligeuza gari na kuelekea kwenye Hospital ya kanda mle mle ndai ya kambi kubwa la kijeshi, **
Haya sasa, Edgar na Monalisa mida hii nao walikuwa pembeni kidogo ya eneo la wakulima, nikama mita miambili, wakitazama mianga ya moto, iliyokuwa ina tokea eneo lile, ambalo walitamani kwenda kuomba msaada, wachakula, maana ukiachilia baridi iliyo kuwa ina wachamanda, pia wawili awa, awakuonja kitu toka asubuhi, “nikama kuna watu wame ngezeka pale, mbona kwa kule mbele naona kama kuna mioto mingi sana, alafu kuna watu wana pita pita” alisema Edgar, huku Monalsa akiwa nyuma yake wame chuchumaa, wakitazama kule mbele, “alafu nasikia arufu nzuri ya vyakula” alisema Monalisa, huku tumbo lake likiunguruma kwa njaa,
Ukweli ni kwamba, baada ya kuwaimbia polisi, na kufanikiwa kuwachenga, walitaafuta sehemu na kupumzika, huku Monalisa akipitiwa na usingizi, ambao aukudumu muda mrefu baad ya kuamshwa na njaa kali, mida ya saa moja, ndipo walipo amua kutafuta chakula, na kuangaika kwa muda mrefu bila mafanikio, lakini mwisho wake wakaikuta barabara ile ile waliyo itumia jana usiku, na kuapata wazo la kwenda kwa wakulima, kutafuta chakula,
“Mona wale ni polisi, siunaona ata nguo, walizo vaa?” alisema Edgar, huku akiuvua mkanda wa SMG yake toka begani, na kumpa Monalisa, “yanini sasa?” aliuliza Monalisa, huku akipokea ile SMG, yani sub machine gun, “nisubiri naenda kukuletea chakula” alisema Edgar, ambae ungemsikiliza, ungezani anatania, “sasa mbona unaiacha bunduki?” aliuliza Monalisa, kwa mshangao, “aina kazi nitatumia hii pale itakapo bidi” hili lilikuwa jibu la Edgar alie kuwa ana ifunga kiwamba sauti ile bastora aliyo wapola wakina Mike, kule hoelini, kisha aka jipapasa kiunoni na kukigusa kisu chake, nikile alicho kichukuwa kwa wawindaji haramu, kisha aka jiinua na kutaka kuondoka, Monalisa aka mshika mkono, kama anamzuwia, Edgar aka geuza shingo, kumtazama Monalisa, ambae macho yake yalionyesha kuitaji kuwa na Edgar, “Eddy uwe makini, urudi salama” alisema Monalisa, kwa sauti flani tulivu iliyo jaa uitaji wa mtu huyu, kuwa salama, Edgar aka tabasamu kidogo, kisha aka usogeza mdomo wake kwenye shavu la Monalisa na kumlamba kabusu laini, “lazima nirudi, ili nikuletee chakula, ila usiondoke hapa” alisema Edgar, na Monalisa akaitikia kwa kichwa, lakini nikama machozi yalisha anza kumlenga lenga, huku Edgar akiinuka na kuelekea kwenye kambai la muda la polisi, kwenda kufwata chakula, na wakati huo huo waka ona msafara mdogo wa magari una elekea mjni, itaendelea………. HUU NDO MWISHO WA SEASON TWO

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!