: BIKIRA YA BIBI HARUSI (46)

SEHEMU YA 46


ILIPOISHIA SEHEMU YA 45: wakati anapanga hayo, mala akamwona akskari polisi mmoja ana sogea kichakini kujisaidia, ni mmoja kati ya wale waliokuwa wanaota moto, huku wana kunywa ulanzi, Edgar akamvizia yule askari ambae SMG yake ilikuwa mgongoni, lakini ile ana mkaribia nikama yule askari alichezwa na machale, maana aka geuka na kumtazama Edgar, ENDELEA……..
…….
Akija pale alipo simama, kwa mwndo wa kunyemelea, moja kwa moja nikama yule askari aligundua kuwa Edgar akuwa mtu mzuri kwake, kwa jinsi aivyo kuwa ana mnyemelea, hivyo akaikamata bunduki yake iliyo kuwa mgongoni kwa lengo la kileta mbele ili amshambaulie, lakini ghafla akamwona Edgar akimjia kwa kasi ya hajabu na kumchapa ngumi ya shingo lchini ya kisogo, hapo hapo yule askari akatulia, na kulegea, huku Edgar akimdaka ili asi anguke kwa fujo na wenzake wakasikia, baada ya hapo Edgar alimvutia kishakani yule askari mlevi, na kumvua nguo zote, za kipolisi, na kuzivaa yeye mwenyewe, alafu aka chukuwa kamba za viatu vyake na kumfunga yule jamaa, huku aki mziba mdomo kwa kutumia nguo za ndani za yule askari pamoja na sox zake yule askari.
alipo akikisha amezaa vizuri zile nguo za polisi, Edgar akajitoa pele kichakani, akiwa amebeba smg ya yule askari, alie kuwa amezimia kule kichakani, akaanza kusaka sehemu waliyo kuwa wana pikia chakula, ambapo kutokana na udogo wa kambai hili la muda, alitumia muda mfupi sana kuipata sehemu hii, “we! vipi, bado ujala tu!” aliuliza mtu alie onekana kuwa ni mpishi wao, “ndio nilipitiwa na usingizi” alijibu Edgar ambae alikuwa ameshusha kofia yake mpaka usawa wa macho, licha ya hivyo inge kuwa vigumu kumtambua kwa usiku ule, na ule mchanganyio wa askari toka Iringa, Songea na Njombe, “we endekeza usingi tu! uta lala na njaa, nake sho asubuhi mnaamkia porini” alisema yule askari mpishi, huku ana fungua box na kutoa mbakuri flani ya kona nne ya bati mawili, na moja aka weka wali akimiminia maharage juu yake, na nyingine aka weka nyama na mchuzi wake, “hizi mestin uzitunze ndio zitakuwa vyombo vyako vya chakula kila siku” alisema yule polisi mpiishi, hapo Edgar aka geuka na na kutaka kuondoka, “we! askari ebu subiri” alisema yule askari mpishi mwenye sauti ya kibabe, hapo Edgar aka simama, akihisi kuwa mambo yamevurugika, akawa ana piga mahesabu ya kuchomoka na kile chakula kwenye bakuli za chuma, wenyewe wanaita mestin, “mbona unaacha chai, itakusaidia na hii baridi” alisema yule polisi mpishi huku ana pekua pekua kwenye box, akitafuta kitu ambacho Edgar alihisi kuwa ni kikombe, ambacho alikikosa.
mwisho yule askari aka mgeukia Edgar, alie mzania kuwa ni askari kweli, “sikia PC, na kuazima hii chupa ya chai, ni ya afande OC FFU, irudishe mapema sana, kabla wakuu awajafika” alisema yule askari mpishi huku ana ichukuwa chupa chai, na kuijaza chai, kisha aka mpatia Edgar, ambae aliishka anavyo juwa yeye, maana alionganisha na mshikio wa ile mestin moja, “asante sana” alisema Edgar na kutaka kuondoka, lakini yule mpishi aka mzuwia tena, “chukuwa na huu mkate, utakusaidia polini kesho” alisema yule askari mpishi huku ana mpatia Edgar mfuko wa mkate, kwakeli Edgar alishuru sana, maana kazi yake ilikuwa lahisi sana, kisha akaondoka zake, kuelekea upande wa mahema ya kulala askari, kazi ilityo fwatia hapo, ni zaidi ya balaha, akikuta SMG imewekwa vibaya alikuwa anavua magazine na kuondoka nayo, alizichukuwa tano tu, akishindwa kubeba nyingi kutokana na mizigo mingi alyoi kuwa nayo.
Baada ya kuona amelizika na mzigo alio kuwa nao, alirudi pale kichakani alipo mwacha yule askari alie mfunga kamba, na kubadiri nguo zake, kisha aka ondoka zake akimwachia smg bila magazine na nguo zake pembeni, na kutokomea kichakani, upande alio tokea mwanzo, yani kule alikomwacha Monalisa, **
Wakati huo SSP Kingarame, ambae akuondoka na wenzake, ndio alikuwaanaondoka eneo hili la kambi ya muda, akutaka kuongozana na wenzake, kutokana na mabo aliyo itaji kuyafanya usku huu, ukiachilia kwenda kumfwata Isaya alie mpa kazi ya kuwaangamiza wale polisi majeruhi, yani wakina Mapombeka, pia kuna maelekezo alitakiwa ayatoe kwa Basso, kule songea, maana yale maelekezo ya kutafuta mmiliki wa magari yaliyo tumiwa na wakina Ngigo, yali mchabfanya sana Kingarame, ambae alijuwa kuwa, endapo bwana Kanjubahi, ayakamtwa na kbinywa kidogo, lazima ataongea ata yasiyo takiwa kiongelewa, maana wahindi ni watu waoga sana.
kitu cha mwisho ambacho Kingarame akujuwa kimekaaje, ni kuto kumwona Ngigo, kati ya wale marehemu, “wata kuwa wame mchukuwa au?” alijiuliza King, huku hokololo akiwa pembeni yake anakanyaga mafuta***
“vipi Erasto, naona umesha pumzika kidogo?” aliuliza baba Erasto huku ana tabasamu, Erasto hakujibu kitu, zaidi alitabasamu tu, na kuagiza pombe nyingine, “ungekula kwa nza bwa Erasto, maana hivi itu vina itaji nguvu” alisema Anderson na hapo wapo waliostuka, na wapo waliochukulia kawaida kuwa pombe inaitaji nguvu, Misago na mke wake wakatazamana, nikama walikuwa wanaulizana “ame gundua au?” kisha wanandoa hawa waka mtazama kijana wao, mdio kwanza wakamwonaana mtazama yule dada mhudumu huku wakikonyezana, hapo haraka wakamtazama mzee Anderson, yani baba Monalisa, wakizani kuwa atakuwa ana mwona kijana wao, kwa kitu alicho kuwa anakifanya, lakini ndio kwanza alikuwa anainua grass ya pombe na kuiweka mdomoni, hapo nikama wawili awa walishuha pumzi za hofu,
Wakati huo huo, waka waona makamanda wa polisi, wanaingia pele hotelini na kuelekea ndani kabisa ya jengo la hotel, “nikama na mwona RPC wa Songea” alisema mzee Anderson, huku wote wanatazama kule hotelini, “nazani hili jambo limeshakuwa kubwa sana, maana wale wote wanaonekana wanavyeo vikubwa sana” alisema dereva wa bwana Anderson, “ngoja ni wai nika mwulize jinsi mambo yanavyo enda huko porini” alisema Anderson huku anainuka, “hapana boss, ungesubiri, watoke nje nazani watakuja kula muda siyo mrefu” alisema dereva wa Anderson,huku anamzuwia boss wake, ambae alikuwa mpole, akiunga mkono ushauri wa dereva wake.***
“hii ni brack Mamba snake venon, (sumu ya nyoka) sijuwi ime kuja vipi humu ndani” alisema doctor hukwa sauti iliyo jaa wasi wasi. na kumshangaza mke wa Mapombeka, hapo Kisona aka mtazama mke wa Mapombeka, “eti shemeji unasema huyo jamaa ulie kuja, nae unamausiano nae gani?” lilikuwa wali lililo toka kwa kisona, likitumia sauti ya kawaida tu! “ni kaka yangu ametokea tanangozi, kuja kumwona mume wangu” alisema mke wa Mapombeka, kwa sauti iliyo onyesha dalili flani ya mashaka, kwamba inawezekana vipi ilesumu aje nayo yule kaka Isaya, “anafanya kazi gani?” aliuliza Kisona akiwa amemkaziamacho mke wa Mapombeka, “mchungaji ni mchungaji tena kesho anaenda mbeya, kwenye semina” alijibu mke wa mapombeka, ambae sasa, alianza kuona mashaka waliyo nayo wale makanda wakijeshi, asa Kisona, kwa jibu hili Kisona alitabasamu kidogo, kisha aka mtazama mke wamapombeka, “shemeji unafanya masihara” alisema Kisona kwa sauti ya taratibu, kama vile wanaongelea kitu cha kawaida, lakini aikuwa hivyo kwa mke wa mapombeka, ambae nikama alistuka kidogo, “shemeji unataka kusema kuwa nadanganya?” ilikuwa ni sauti ya mshangao wa mstuko, toka kwa mke wa mapombeka, “tena ni uongo wenye hatari kubwa sana, ata sijuwi ni kwanini umekubari kudnganya na kumleta huyu mshenzi huku ndani, aje amuuwe mumeo” alisema Kisona huku ana uvuta mwili wa Isaya toka uvunguni mwa kitanda, hapo doctor wa zamu na mke wa Mapombeka wakashangaa, “shemeji inamaana mume muuwa, aliuliza mke wa mapombeka kwa sauti ya mstuko mkubwa sana, “ndio nilimkuta anataka kuchoma drip kwa sindano” alisema Kisona, huku ana inama chini na kuchukuwa sindano, yenye sumu.
Hapo mke wa Mapombeka ambae alisha elewa kilicho mleta mle hodini kijana Isaya, alisimulia jinsi walivyo kutana na kumwamini kijana huyu, kisha kukubariana aje kumwona mgonjwa, “basi huyu alitumwa kuja kuwamaliza wote awa, na ni polisi ambae siyo mwaminifu, na hayo yote yaliyokutokea, ni mipango ya hao hao washenzi” alisema Kisona, huku ana waonyesha kitambulisho cha Isaya, kilicho mtambulisha kuwa ni polisi.
Mke wa mapombeka alipewa onyo la kuo kufanya mazowea na mtu yoyote, iwe anamfahamu au asie mfahamu, na asimweleze mtu yoyote kuhusu kifo cha Isaya, ambae wakina Kisona walimwingiza kwenye gari, na kwenda kumtupa njia panda ya kwenda porini, pembeni kidogo ya barabara ya vumbi, huku njiani wakipishana na gari la polisi, aina ya Toyota land cruzer, lililo mbeba SSP Kingarame alie elekea Makambako.
Huku wakina Kisona wakielekea Njombe, ****
Monalisa na Edgar walikuwa wamesha maliza kula chakula, walichoiba kwenye kambi ya polisi, wakisukumia na chai yamoto, ndicho kipindi walich sikia kelele za filimbi zikipigwa kwa fujo, kwenye kambi la polisi, wote wakatazama upande kambi lilipo, wakawaona polisi wana jikusanya na kuanza kutawanyika na tochi zao mikononi, wakizagaa kwenye machaka yaliyo zunguka kambi lile, inaonyesha waligundua jambo, …. itaendelea…….. Hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata