: BIKIRA YA BIBI HARUSI (48)

SEHEMU YA 48

ILIPOISHIA SEHEMU YA 47: “inawezekana majambazi, walikuwa na silaha ya akiba” alisema RPC Iringa, “lakini kwa jinsi navyo mjuwa Kisona, nivigumu sana kushiriki ujinga huu” alisema OC FFU wa Ruvuma, hapo walijadiliana mpaka walipo mkumbuka, RCO Ruvuma, “jamani hivi Kingarame yupo wapi?” aliuliza RPC Iringa, wote wakatazamana, endelea ………
Ikionyesha kuwa hakuna alie juwa sehemu aliko Kingarame, “lakini nakumbuka tulimwacha kule porini, na alisema atakuja baadae” alisema RCO Iringa, baada ya kukumbuka, “nikweli tulimwacha, kule porini, ila anaonyesha kuwa ana uchungu sana na askari walio uwawa” alisema RPC Iringa, na wote wakakubariana kwa hilo, asa waka linganisha na utendaji wake, wa hali ya juu katika operation hii, pasipo kujuwa kuwa mwenzao alikuwa amejiegesha kitandani akijawa na mawazo mengi sana.
“Lazima kesho niakikishe na wamaliza awa washanzi, kisha nammaliza Kisona, na wakina Mapombeka, maana wao ndio kikwazo kikubwa sana” aliwaza Kingarame akiwa kitandani, “sijuwi BOSSO amefikia wapi, juu ya kumziba mdomo Kanjibhai?” aliendelea kuwaza Kingarame, ambae aliwaacha porini wakina Kibabu na Lusinde, “kwanza inabidi, kesho nipate jibu la Isaya, na Bosso, kisha nichague kikundi changu, niingie porini kivyangu kuakikisha wale watoto wanakufa kesho hiyo hiyo, na wakina Kisona wakijipendekeza, nawamaliza” hayo yalikuwa mawazo ya Kingarae, kabla ajapitiwa na usingizi, na kuamka wa kwanza, mapema sana saa kumi na moja, za alfajili, siku iliyofuta, akajiandaa na kumpitia dereva wake Hokololo, ambae leo alichukuliwa tena chumba namba kumi na saba, kisha saa kumi na mbili kasolo robo, ndio safri yao ikaanza, wakiwapitia askarin wengine watano, ambao jana usiku aliwaacha kwenye mabweni ya askari kwenye kambi ya plisi wilaya ya njombe.
Kisha safari ikaanza kuelekea Makambako, kwaajili ya mambo mawili, moja kuiga simu kwa Bosso, ilikujuwa maendeleo ya kazi aliyotoa jana usiku, na mbili ni kumfwata Isaya, ambae mpaka mida ile akujuwa kama alisha tekeleza kazi aliyo mpatia au la!, akiacha huku nyuma wenzie ndio wana hamka, na kuanza kujiandaa, na safari ya kwenda porini kuendelea na operation Kifo mkononi, pasipo kujuwa kuwa mwenzao ameshatangulia, lakini kapitiliza makambako.
saa kumi na mbili na robo ndio muda ambao makamanda wakuu wapolisi, walikuwa wanatoka Hotelini kuelekea porini, wakiwa katika msafara wa magari sita, na askari wao walio wapiti pale kwenye kambi ya polisi Njombe, ambako nusu saa iliyopita alikuwa amepita Kingarame, akichukuwa askari kama wao walivyo fanya. kisha safari ikaanza kuelekea porini, huku wakiwaacha wakina Kisona wakijiandaa kutoka, huku askari wao mmoja, akiwahesabia wale makamanda, lengo likiwa ni kuto kutangulia kule porini, mana wange tangulia wao, wangeusishwa na kifo cha Isaya malamoja, nawao hawakutaka litokee hilo, hivyo baada ya kuona wale makamanda wamesha ondoka, robo saa baadae nawao wakaondoka, “dafari makambako kuchukuwa chakula na mafuta, kisha tumwone mahabusu wetu, alafu tuingie porini, tuakikishe Edgar na Monalisa tuna wapata, kabla polisi awaja mpata” alisema Kisona huku baba Edgar akiendesha gari kwa speed kari sana, kuelekea Makambako.
Robo saa baadae yani saa kumi na mbili na nusu, msafara wamakamanda awa wapolisi ndio ulikuwa unakata kona pale njia panda, mala wakaliona moja ya gari ambalo uwa yana enda kuchukuwa viazi na matunda kule porini, kwa wakulima , likiwa limesimama mita chache toka barabara kuu, walipotaka kulipita lile gari, mala wakamwona mtummoja ana wasimamisha, huku mwingine akitokea pembeni na kusaidia kuwa simamisha, nao wakasimama, wakijuwa kuwa wale ni wafanya biasara wanao enda kufuata mazao mashambani,
“kumbe ni polisi? itakuwa afadhari” alisema mmoja wa wale wasimamishaji, baada ya kuona na kuyatambua yale magari, kuwa ni yapolisi, “kuna nini?” alisema OC FFU wa Ruvuma alie kuwa kwenye gari la mbele kabisa huku anashuka, toka kwenye gari hilo, sambamba makamanda wenzake na askari waliokuwa nyuma ya magari yao, wakiwa na silaha zao mikononi mwao, “mzee kuna jambo hapa limetokea, ni muhimu mkiona kabla amja endelea na safari yenu” alisema yule wakwanza kusimamisha, ndie alie onekana kuwa ni mtu mzima kidogo, na hapo ndipo makamanda awa walipo gundua kuwa, watu awa wenye hili gari la mizigo, walikuwa sita, ni baada ya kuwaona wengine wanne wakiwa wame zunguka kitu flani pembeni kidogo ya barabara.
Makamanda wote wakasogea mahalipale, huku wale watu wakiwapisha ili nao waone walicho kuwa wanakishangaa, hapo makamanda wa polisi mikoa, waliona mwili wa kijana alie valia suit nyeusi aakiwa ame lalachini, huku macho ame yatumbua, ikionyesha kuwa, alikutana na kimminyo cha nguvu, kabla ya kifo chake, “mungu wangu, huyu ni Issa” ilikuwa ni sauti ya mshangao ya OC FFU, alie utumbulia macho mwili wa kijana Isaya, “unamfahamu huyu kijana?” aliuliza RPC Iringa, huku akiutazama ule mwili wa Isaya, “huyu ni PC Isaya, ni askari wetu, na tuponae kwenye hii operation” alifafanua RPC Ruvuma, ambae mshangao wake ulikuwa mkubwa kuliko ata mshangao wa OC FFU, mshangao ulio waambukiza makamanda wengine wa kutoka Iringa, “imekuwaje amekutwa hapa, tena kwenye nguo za kiraia?” aliuliza RPC Iringa kwa mshangao, lakini hakupata jibu toka kwa wenzake, hapo RPC Iringa, aka watazama wale Raia wema, walio ugundua mwili wa Isaya, “eti nyie, imekuwaje mpaka maka mkuta hapa huyu mtu?” lilikuwa swali lililo ambatana na sauti iliyo jaa hasira na mshangao, toka kwa RPC Iringa.
Hapo wale wafanya biashara, wali eleza jinsi walivyo fika hapa na kuuona mwili wa kijana Isaya, wakati wana elekea kwa wakulima kuchukuwa mazao ili wayapeleke mjini, kwaajili ya kusafirisha kwenda Dar es salaam, “hapa tulikuwa tuna tafuta namna ya kupeleka taharifa polisi mjini, ili waje kuona, bahati nzuri ndio tuka waona nyie” alieleza mmoja kati ya wale wafanya biashara.***
Wakati huo huo, Kingarame alisha maliza mambo yake yote aliyo kusudia kuyafanya Makambako, ikiwa na kupiga simu Songea, kwa kijana Bosso, ambae pia ni askari wa jeshi la polisi, ambae alimweleza kuwa tayari alisha mzimisha Khanjibay, na haja acha ushai wowote, ila shughuli ilikuwa ni kumpata Isaya, maana walizunguka kila kona, mpaka nyumbani kwa mapombeka, lakini akukuwa na dalili ya kuwepo kwa mtu yoyote ndani ya nyumba hile.
Hivyo walielekea Tazara, yani karibu na kambi la jeshi la ulinzi, “sikia Elisha ebu bakia hapa Makambako, akikasha unamwona Issa, pengine atakuwa amelala ndani ya hospital” alisema King na kumwacha Elisha, akiwa amevalia zile nguo ambazo jana walizitumia kujifanya vibaka, pindi walipo mshanbulia mke wa Mapombeka, kisha wao aka ndoka zao, wakipanga kurudi saa nne,
Awakutumia muda mrefu sana kufika njia panda ya kwenda porini, na kuwakuta wenzao wana upakiza mwili wa kijana Isaya, kwenye gari OC CID wa Iringa, tayari kuupeleka Njombe, “kuna nini kimetokea hapa?” aliuliza SSP Manase Kingarame, alieshuka haraka toka kwenye gari lake, hapo RPC Ruvuma akamsimulia kingarame tukio lile kwa sauti ya uzuni, Kingarame alistuka sana kwa taharifa ile, “mungu wangu, nani amefanya kitu kama hiki” aliuliza Kingarame kawa sauti ya mstuko mkubwa, “atujuwi na mbaya zaidi ameonekana akiwa katika mavazi ya kiraia” aliuliza RCO Iringa, na hapo, Kingarame ndio aka gundua jambao ambalo lita mwingiza matatizoni,
Nawakati huo huo wakina kisona waliokuwa wanapita kuelekea Makambako waliingia mahali pale baada ya kuona kuna magari mengi ya polisi, “poleni na majukumu jamani” alisema Kisona baada ya kushuka kwenye gari na kuwasogelea makamanda wa polisi, “haaa! bwana Kisona, mambo yana zidi kuwa na utata, yani mmiliki wa magari yale yajana ameuwawa huko songea, kabla ajatiwa mbaloni, na kama aitoshi, tume mkuta huyu askari wetu hapa, ame uwawa” alisema RPC Ruvuma, kwa sauti ya uzuni kama mwanzo, akieleza na baadhi ya maswali waliyo jiuliza, kama vile alfikaje pale, na imekuwaje amevaa mavazi ya kiraia, “lazima kuna mtu anausika na kifo hiki, na ndie huyo huyo anae usika nawizi wa NMC, na ndie mkuu wa majambazi waliopo huku porini” aliongea Kingarame kwa sauti ya jazba, “nazani maneno ya Kingarame yana ukweli ndani yake, na kumgundua mtu huyo ni lahisi sana” alisema Kisona kwa sauti tulivu kama ya utani hivi, makamanda wote wakamtazama Kisona, huku macho yake yakikutana na macho ya Kingarame, ambae alikuwa ametoa macho kama vile amekabwa, “kivipi Kisona, ebu tueleze” alisema RPC Iringa kwa sauti iliyo jaa msisitizo, “swala ni kujuwa, huyu askari mala ya mwisho kuonekana jana, alikuwa na wakinani” alisema Kisona huku ana tabasamu, hapo makamanda nikama walikumbuka kitu, wote waka mtazama SSP Kingarame, itaendelea……. hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!