: BIKIRA YA BIBI HARUSI (49)

SEHEMU YA 49

ILIPOISHIA SEHEMU YA 48: “kivipi Kisona, ebu tueleze” alisema RPC Iringa kwa sauti iliyo jaa msisitizo, “swala ni kujuwa, huyu askari mala ya mwisho kuonekana jana, alikuwa na wakinani” alisema Kisona huku ana tabasamu, hapo makamanda nikama walikumbuka kitu, wote waka mtazama SSP Kingarame, endelea………
Ambae alistuka sana, akijuwa tayari Kisona kasha msukumia zigo la uchafu, “tulimwacha kule porini, jana usiku” alijibu Kingarame haraka sana, baada ya kuona wenzake ni kama walisha gundua kuwa yeye, ndie alie ondoka na Isaya, “haa! Kumbe, kwani uliondoka huku porini jana usiku?” aliuliza RPC Iringa, ambae mawazo yake nikwamba Kingarame alilala huku kambini, na ndio maana wali mtazama ssp huyo, wakijuwa kuwa ndie alie bakia na askari kule porini, na siyo kwamba waliona Kingarame akitoka na yule askari, “nilikuja kulala mjini, lakini nilichelewa sana” alijibu Kingarame, huku akimkata jicho Kisona, ambae alimhisi kuwa, ndie alie usika na kifo cha Isaya, “kwa hiyo huyu askari, atakuwa alitoroka kufwata wanawake huku?” aliuliza RPC Iringa, huku akimtazama Kingarame, lakini wakati huo bahadhi ya askari wa liokuja na Kingarame, walikuwa wamesha juwa kilicho mkuta mwenzao.
Kwajinsi Makamanda awa walivyo kichukulia kifo cha Isaya kiuwepesi, ilimsikitisha sana Kisona, ambae akuwa na la kufanya, maana angeongea ukweli ange sababisha mambo mawili makubwa, lakwanza likiwa ni yeye kuingizwa hatiani, wakati ushaidi baado auja kamilika, pili kuwa fanya polisi awa, wafiche ushaidi kwa kumwokoa mwenzao na kulitunzia heshima jeshi la polisi, “kwa hiyo katika mawazo yetu, huyu kijana atakuwa alikuwa anarudi au anakwenda, na ameuwawa na watu gani?” aliuliza Kisona huku akiwatazama wale makanda mmoja baada ya mwingine, ambao nao walitazamana, wakitegemea mmoja wao anaweza kutoa jibu, lakini akukuwa na jibu, “jibu ni kwamba, tilia mashaka kila unachokiona sehemu ambayo siyo mahali pake” alisema Kisona kisha aka watazama wenzake na kuwapa ishara waondoke, na wakina baba Edgar na wale askari wa jeshi la ulinzi, wakaingia kwenye gari lao na kuondoka, wakielekea Makambako, wakiwaacha makamanda wale wakuu wa mikoa, wakiwasindikiza kwa macho, huku kila mmoja akiwaza lakwake, “jamani aliyo sema Kisona, yana maana kubwa sana, endapo tuta yapuuza tutajikuta tume ingia pabaya zaidi” alisema RCO Iringa, kwa msisitizo, akiungwa mkono na wenzake, kasoro SSP Kingarame peke yake, alie kuwa ametazama chini huku mikono yake ikiwa kiunoni, na kama wenzake wange mtazama usoni, wange shuhudia kijasho flani chembamba, licha ya baridi kali iliyo kuwepo asubuhi ile, “hapa inabidi tufanye jambo moja, vinginevyo tutaonekana watu wazembe sana” alisema RCO Iringa akionyesha kuwa kuna wazo alikuwa amelifikiria, “nikweli RCO, lakini tufanyeje, kama jana tume poteza risasi nyingi, mwisho wasiku tume kuja kusaidiwa na watu wengine, au unataka kusema tuombe jeshi la ulinzi watusaidie?” aliuliza RPC Ruvuma, akionyesha kutotaka kusikia jambo kama hilo, “hapana afande, wazo langu nikwamba, waletwe wale mbwa wa kufwatilia nyayo” alisema RCO Iringa, na hapo makamanda wote wakatabasamu, safari hii ata Kingarame alitabasamu pia, “wazo zuri RCO, nazani hilo jambo lifanyike mala moja” alisema RPC Iringa.
Dakika chache baadae RPC Iringa aliamrisha kuwa, gari la OC CID, wa Iringa liondoke na mwili wa Isaya, lielekee Njombe, kwenye hospital ya Kibena, kwenda kuuhifadhi, pia alipewa maagizo ya kupiga simu makao makuu ya polisi mkoa wa Iringa, aagize mbwa waletwe haraka sana,
Pia RPC aka amrisha watu wengine wote waondoke kuelekea kule porini, kwenye kambi yao ya muda, ili wakajipange vyema ili waanze kuwasaka majambazi, wakizania kuwa wapo wengi sana, ili wamwokoe Monalisa, na kuwatia mbaloni majambazi hao,**
Ndani ya Hospital ya kanda ya jeshi la ulinzi, mida hii ndio mida ambayo, mke wa mapombeka alistuka toka usingizini, na kutazama kwenye kitanda cha mume wake, akika aliona mabadiriko makubwa sana, yaliyo tia moyo, kwa maendeleo ya afya ya mume wake, ambae alikuwa ana onekana wazi akihema kawaida, tofauti na mwanzo, ambapo ilikuwa mpaka watumie BP machine kupima mapigo yake ya moyo, ndio wange juwa kuwa yupo hai,
Mke wa Mapombeka akatoka mbio, kwenda kumweleza doctor, lakini akufika mbali akakutana na doctor alie kuwa ana kuja kule hodini, “doctor doctor, mume wangu ana pumua vizuri” alisema Caroliner, kwa shahuku kubwa sana, baada ya kukutana na doctor wa zamu, ambae alicheka kidogo, “shemeji bwana, nilisha ona toka saa tisa usiku, ukiawa umepitiwa na usingizi, inaonyesha kuwa muda sio mrefu watafumbua macho” alisema yule doctor ambae sasa alikuwa ana elekea kwenye hodi, akifwatiwa na mke wa Koplo Mapombeka.
Baada ya kua kuwa kagua kwa malanyingine wagonjwa, doctor aka mgeukia mke wa mapombeka, “shemeji wagonjwa wote wanaendelea vizuri, sasa unaweza kwenda nyumbani kuoga na kupata chai, ila kuwa makini kama ulivyo ambiwa, na yule kanali Kisona” alisisitiza doctor kisha aka mruhusu shemejii yake huyu aondoke, kwamba arudi kuanzia mida ya saa nne,
bila kuchelewa huku aiwa na matumaini ya kumwona mume wake akiwa katika hali yake njema ya kiafya, mke wa Mapombeka akaondoka pale Hospital ndani ya kambi la jeshi, na kuelekea uswa wa geti kuu, la kutokea pale kambini, na dakika kumi baadae alikuwa kwenye kituo cha dala dala akisubiri magari yaendayo mjini, huku kichwani mwake akiwaza mawili matatu juu ya matukio ya jana yaliyo mtokea mpaka kukutana na mtu alie kusudia kuwangamiza mume wake na wenzake, akujuwa kuwa, mita chache pembeni yake, nyuam ya kibanda kimoja chakavu, kulikuwa na mtu anae mfwatilia, akiwa amejibanza.
Kabla ata gari alijapitaa, mala mke wa mapombeka aliona gari la jeshi lina kuja kutokea mjini, na lilipo fika usawa wake, lika punguza mwendo, nikama lilitaka kusimama, lakini kitu cha kushangaza, dereva wa gari lile akanongeza mwendo na kueleka kambini, **
Ok! mida hii huku kwenye kambi la muda, la jeshi la polisi, linalo shiriki operation ya Kifo Mkononi, lililopo pembeni ya mashamba na makazi ya wakulima, ma Asistant camissioner waliokuwepo pale, wakishilikiana na masajent na makoplo, walisha amka mapema sana na kuendelea kuzungukandani ya vichaka vya jirani endapo wangeona chochote cha kuwasaidia, juu ya mtu alie mfunga askari wao na kumnyang’anya nguo, kisha kuingia ndani ya kambi lao, na kuiba bahadhi ya vitu na magazine za Risasi,
“Jamani Njooni hapa muone” alipaza sauti askari mmoja, alie simama pembeni ya kichaka kilicho fungana kidogo, hapo karibia kundi lote la polisi waliokuwpo eneo lile, walikimbilia kule alikoita mwenzao, kati ya askari hao, walikuwepo sajent Idd Kibabu na koplo Lusinde, ambao walikuja mahali hapa ,mbio mbio, wakizania kuwa kuna kitu muhimu kimeonekana, na siyo kingine, labda kinacho usiana na ile tape ya video.
Lakini walishangaa baada ya kuwakuta wenzao wakiwa wame zunguka mestin na chupa ya chai mahali pale, “inamaana wasenzi awa wali kuja kuchukuwa chakula?” aliuliza ASP Ogwambo, kwa mshangao wa hasira, “tena walikuwa na chai kwenye Thermos, wakati sisi tume kunywa chai kwenye vikombe vya bati” alilalamika polisi mmoja, kati ya wale waliokusanyika, “ila jamani ebu subirini kwanza, awa wali iba hivi vyakula au walipewa, hii thermos wame itoa wapi?” aliuliza ASP Msengi, na hapo wote waka tazamana, wakionyesha swala hili lime waingia.
Kabla awaja pata majibu mala waka sikia miungurumo ya magari, yakiingia kambini, yakitokea mjini, “mmoja achukuwe hivi vyombo, twende kwa wakubwa tuka toe report” alishauri Ogwambo, kisha wakafanya hivyo, ***
Msafara huu wa magari ndio ulio mstua Monalisa alie kuwa ame lala kwenye kifua cha Edgar, alie egemea mti, huku ame yatoa macho yaliyo kuwa mekundu, kwa kukosa usingizi wa siku kadhaa, “magari hayo” alisema Monalisa, huku akiiuka hara toka kwa Edgar, nikama aliekuwa na mang’amu ng’amu ya usingizi, lakini Monalisa akaona kimya, nikama alijistukia, maana akuna alie mjibu, Monalisa akainua uso na kumtazama Edgar, Monalisa alikutana na tabasamu jepesi, la kivivu, toka kwenye midomo ya Edgar, alie kuwa anamtazama usoni, na yeye akatabasamu, “kwani na leo ujalala?” aliuliza Monalisa huku akimtazama Edgar, “siwezi kulala, wakati kifo kipo mikononi mwetu” alisema Edgar huku akijiinua na kusimama, nikama vile macho ya Monalisa yalikuwa na kimbele mbele, yakatazama usawa wa lisani ya Edgar.
Naam alicho kiona ni utata mtupu, sehemu hiyo ya mbele ya Edgar ilikuwa imetuna vibaya sana, ikionyesha dudu ya kijana huyu ilikuwa imesimama vibaya mno, Monlisa alimwona Edgar akitembea hatua chache mbele na kumgeuzia mgongo, kisha akamwona ana fungua zip haraka haraka, kisha ikafwata ‘chrooooo’ yani mkojo kama wote, “alishindwa kukojoa mapema kwaajili yangu” aliwaza Monalisa, huku moyo wake ukishikwa na simanzi, akimwonea huruma Edgar, ambae alimwaga mkojo wa maana, ulio tumia kama sekunde stini hivi kumwagika, wakati huo Monalisa nae alihisi kuitaji kitu.
Edgar alipomaliza aka jiweka sawa, nakurudi pale alipokuwepo Monalisa, “tuondoke haraka, maana atupo mbali na kambi yao” alisema Edgar alie kuwa na kila kitu chake, yani SMG na begi lake dogo mgongoni, kama Monalisa ambae alikua bado ame kaachini, ana mtazama Edgar kama vile akusikia alichosema Edgar, “Mona inuka twende, au unatamani kusikia milio ya risasi?” aliuliza Edgar kwa mshangao, lakini nikama Monalisa akuyajari maneno ya Edgar, “mimi nataka” alisema binti huyu kwa sauti flani, iliyo jawa na aibu, huku anainuka na kusimama nyuma ya Edgar, “haaa! hivi wewe unajifanya ume sahahu kashehe ya awa polisi?” aliuliza Edgar huku ana geuka nyuma kumtazama Monalisa, ambae alimwona kama analeta utani, lakini ghafla Edgar alistuka, na kutumbua macho, “ho! kumbe ulikuwa unataka hivyo” alisema Edgar baada ya kumwona Monalisa akiwa anafungua kishikizo cha suluali ya jinsi, na kukifungua,…… itaendelea,…… hapa hapa,

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!