
SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI (52)
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI (50): Huku nako Edgar na Monalisa waliendelea kukimbia kuelekea upande wa walio tokea, yani mashariki, lakini baada ya mita chache waka tahamaki kundi la Ogwambo likiwa mbele yao mita mia mbili, likija kwao kwaspeed ya juma ikangaa, ENDELEA……..
….
Hapo Monalisa akahisi kuwa huu ndio mwisho wao, maana kule walikotoka hakukuwa na usalama ata kidogo, na mbele yao ndiyo hivyo tena, waliweza kuwaona askari polisi wakija mbio mbio, huku wakianza kuziinua silaha zao, na kuzielekzea kwao, Edgar aka msomba Monalisa na kujirusha nae pembeni kidogo, huku ikifwatia na mlipuko wa risasi, ‘pah!’ akika aikuwa moja pekee, mlio huo ulikuwa kama fungulia mbwa, ilifwatia milipuko mfululizo ya risasi, ambazo zili mfanya Edgar ashindwe kuinua kichwa na kutafuta target, iliajibu mashambulizi, ambayo yalikoma baada ya sekunde mbili, na wale polisi ambao awakuachiana nafasi katika kushambuliwa, wote walisikika wakibadiri mikebe ya risasi zao, iliyo ishiwa risasi, baada ya kuzimimina kwa fujo, Edgar akaona hii ndio ilikuwa nafasi pekee kwake, kushambulia.
Hapo Edgar akainua SMG yake na kuiekeza kule kwa polisi, ambao nikama maadui kwake, kisha aka ibana vizuri kwenye bega lake, akililaza shambu lake kwenye kitako cha bunduki yake, na kuoanisha kilengeo cha mbele na cha nyuma kwenye kichwa cha polisi mmoja, na kuachia risasi moja, “anashambulia laleni chiniiii!” zilisikika sauti za watu kadha zikitoa tahadhari ile, ni baada ya kuona mwenzao mmoja ameanguka chini baada ya kusikika mlio wa risasi, lakini aikuwa hivyo, maana wale askari polisi walipo anza kutawanyika kutafuta maficho, waka stuka askari mwingine akidondoka, huku milio wa risasi ukifwatia, sijuwi inakuwaje, kichwa cha risasi kina tembea haraka kuliko sauti ya mlipuko wake.
Yani mpaka wana chukuwa cover na kujificha tayari ilisha sikikamilio minne na watu wanne walisha dondoka, na wakiwa wame tobolewa sehemu muhimu za miili yao, kama vile kichwani, kifuani na shingoni, “Mona tambaa kuelekea huko chini” alisema Edgar, huku akimwonyesha Moalisa upande wa kusini, huku yeye Edgar akiwa ameshika silaha yake akitazama upande wa mashariki walipo kuwepo wale polisi, wame chukuwa maficho, “naogopa” alisema Monalisa kwa sauti ya uoga kweli kweli, “usiogope Mona siwezi kukuacha ufe, mimi nakupa cover” alisema Edgar, na hapo Mona nikama alipata kaujasiri flani, akaanza kutambaa, akitembelea magoti na mikono, kuelekea upande alio onyeshwa na Edgar, ambae alikuwa ame tazama upande wa adui zake huku silaha yake kiwa tayari kwa mashambulizi.
Nikama aliwaza kinacho tokea, maana wakati ule ule, akasikia “shambuliaaa” hapo Polisi wakainuka ghafla toka mafichoni, na silaha zao mikononi, lakini ilikuwa ni zaidi ya haraka, Edgar aka achia risasi mbili, zilizo wa shusha polisi wawili, wengine wote waka jificha tena, hapo Edgar aka tulia kwa sekunde kadhaa, akiendelea kutazama polisi atakae inua kichwa, toka mafichoni, ili acheze nae, wakati huo uo alikuwa anamwesabia Monalisa, ambapo alipo fika mbali kidogo, Edgar aka achia risasi kama mbili hivi, kwa hatua, yani kwa kuziishanisha sekunde kadhaa, kishaakaanza kutambaa kuondoka mahali pale, akiwaacha polisi bado wame chukuwa maficho ya uoga, **
Baada ya kuona askari wake watatu wameuwawa, Kingarame na askari wake, wakajikusanya ilikujaribu kuwasaidia askari wale, lakini awakuwa na uwezo zaidi ya kuwaweka vizuri marehemu, maana tayari walisha uwawa, na wakati huo huo, ndipo walipo sikia mapigano yana tokea kule walikokimbilia wakina Edgar, ilionyesha kuwa ni karibu kabisa na pale walipokuwepo, “twende tuka wasaidie wenzetu” alisema Kingarame, huku akionyesha ishara ya watu waelekee kule yanakoendelea mapigano, “samahani afande, kuna kitu atuja kitazama” ilisikika sauti ya Hokololo, wote waka acha kuondoka na kutazama upande ilikotoke sauti yaa Hokololo, wakamwona anakuja toka kwenye gari la kwanza alilo panda Kingarame, huku anaonyesha kwenye lile lori (gari kubwa lililokuwa lina badirishwa tairi) wote waka tazama, wakaona vijana ka wanne hivi, wakiwa wame jibanza pembeni ya gari hili la mizigo, huku wenzao kadhaa, wakiwa wame lala chini, wamekufa na wengine wana tapatapa kwa majeruhi waliyo yapata, baada ya kutandikwa risasi, zilizo nunuliwa kwa kodi zao, toka kwenye bunduki zilizo nunuliwa kwa kodi zao, “dah! umeongoea jambo muhimu sana, maana tukiwaacha hawa itatuletea madhara makubwa sana” alisema Kingarame, huku akisisitiza kuwa jambo hili lifanyike haraka kabla wenzao awaja sogea, maana wakati huo awakuwa wanasikia mapigano kule porini,
SSP Kingarame na askari wake waliwasogelea wale jamaa, kwenye lile gari, ambao walikuwa wana tetemeka kwa uoga, maana walisha ona kila dalili ya kuwa awapolisi awakuwa wema kwao, kutokana na kuwa waishaona, na kugundua kuwa, Risasi zilizo wauwa na kuwa jeruhi wenzao, zimetoka kwenye bunduki za polisi hao hao, ambao sasa walikuwa wana wasogelea, mmoja akachomoka mbio akijaribu kukimbilia kichakani, lakini aikuwa bahati yake, maana alichakazwa na risasi za mgongoni kama zote, ambazo zili mwangusha chini, huku wenzake wakianza kuomba wasi uwawe, “haaa! huyu Edgar nikijana hatari sana, ameuwa raia wengi sana, nambaya zaidi ame lipua gari lao kwa risasi, zilizo gonga kwenye tank la mafuta” alisema Kingarame, kwa sauti flani ya utani, huku askari wake wakicheka kwa kejeli, huku wakiwatazama wae raia mbao awakuwa wanajuwa maana ya maneno ya Kingarame, ambae baada ya kuongea hayo, akageuka na kuelekea kwenye gari, huku akiwaacha askari wake wanawanyooshea mitutu ya wale raia, “jamani tunaomba mtu…” sijuwi kama walipata bahati ya kusali sala zao za mwisho.**
Ogwambo na sajent Kibabu wakiwa na askari wao, walio jificha kwenye maficho ya uoga (yani pasipo kuona kabisa mbele/kujuwa adui yao yupo wapi) mala wakasikia milio ya risasi, kama mitatu hivi, aikitokea kule waliko isikia mwanzo, ndio chanzo cha wao kukimbilia huku, na kukutana na waki Edgar, kisha kika pita kimya kidogo, alafu wakasikia milio mingine ya risasi, safari hii ikiwa ni mfurulizo, ikifwatiwa na mlipuko mkubwa, kama wa bomu, huku wakiona moto mkubwa sana mbele yao, “twendeni tuka wasaidie wenzetu, wana shambuliwa” ilisikika sauti ya Ogwambo, hapo kwa tahadhari kubwa sana, askari na viongozi wao wakainuka taratibu, wakiofia kutandikwa risasi za vichwa, lakini ikawa kimya, hapo kwa tahadhari kubwa wakaelekea kule kwenye mlipuko, ***
labda nikukumbushe tulipo ishia kule Njombe mjini nyumbani kwa Mapombeka, Kijana Elisha, askari alie jifanya muuni flani, kwa mavazi yake baada ya kutumwa na boss wake SSP Manase Kingarame, akamfwatilie mke wa Mapombeka ilikujuwa mwenzao Isaya yupo wapi, alifanikiwa kuingia nyumbani kwa mwanamke huyu mjamzito, na kumkaba akimlazimisha amtajie Isaya yupo wapi, ndipo aliposikia sauti toka nyuma yake, “sasa atakujibuje wakati ume mkaba?” Elisha aka stuka na kumwachia mke wa Mapombeka, ambae alipata uafueni na kupitisha hewa kwenye koo lake, huku Elisha anageuka nakumtazama alie mwuliza swali, lakini alicho kutana nacho, ni zaidi ya baraha, ilikuwa ningumi nzito iliyo tuwa kati kati ya mcho na pua, na kumrudisha nyuma kihasi cha kutaka kumgonga mke wa mapmbeka, hap akupwe nafasi hiyo, maana ingeleta madharakwa mjamzito, Elisha aka stuka akipigwa tke la kichwani, na kurushwa mita kadhaa, akituwa kwenye meza ya mbao, ambayo ilikuwa nabahati ilitengenezwa na fundi ambae alikuwa mwaminifu kama siyo alimwogopa Mapombeka sababu ni polisi, maana licha ya Elisha kutuwa na kukibamiza kiuno chake, kwenye kingo ya ile meza lakini aikuvunjika, huku akihisi minyizi ya joto la vugu vugu, inatoka puani kwake, hapo ndipo Elisha alipo pata nafasi ya kumtazama vizuri mshambuliaji wake, alimwona mtu ambae ana mfahamu vyema, ni kijana mdogo alie valia mavazi ya kijeshi, huku minyota ikining’ini mabegani mwake, ambae wamesha kutana mala kadhaa, ata kule porini alimwona jana, kisha akamtazama yule mwanamke, akamwona akiwa amesimama pembeni anamtazama, kwa macho ya uoga.
Elisaha akutaka kusikilizia maumivu, wala kujali damu iliyo kuwa ina toka puani kwake, na kusambaa mpaka mdomoni, akajiinua haraka sana, na kujiweka katika mkao wa kupambana, kwa mikono mitupu, wajapan wanaita KARATE, lakini Joseph Kisona aka mtazama Elisha kwa nukta chache, kisha akatabasamu, “nivyema ukawa mpole, ili ujipunguzie kipigo..” kabla Kisona ajamaliza kuongea, Elisha akafyetuka na kurusha ngumi mija nzito, ambayo kama inge mfikia Kisona usoni, kama iliyo kusudiwa, nazani Doctor Elizabeth, asinge mtambua mwanaume huyu, Kisona alinesa pembeni na kuudaka mkono wa Elisha, huku ana mtandika ngumi ya ubavuni, kisha aka mwongeza ya shavuni na kumwangusha chini, kisha aka akamkandamiza kwa goti, maeneo ya kifuani, “mtaje aliekutuma, na kwanini mnafanya hivi?” alisema Kisona, kwa sauti yaghadhab, lakini kitu cha kushangaza Elisaha alijaribu kucheka, huku damu ziki endelea uchuruzika puani kwake, kicheko kilicho mkela Kisona, maana kiliashilia dharau, hapo hapo kisona alishusha ngumi moja nzito pale pale ilipo tua ngumi yakwanza, yani kati kati ya pua na macho, “mama uananiua” lilimtoka yowe languvu, kijana Elisha, Kisona aka mziba mdomo ulio tapakaa damu, kwa kiganja chake cha mkono, alifanya hivyo kwa sekunde kadhaa, kisha akamwachia, “nazani sasa unaweza kuweka utani pembeni, na kuniambia nani ame kutuma, na kwanini anafanya hivi?” msimuliaji wa mkasa huu wa mwak 1997, anasema sauti na sura ya Kisona wakai huo, ilikuwa imebadirika kwa hasira, na kuwa yakutisha,
“kwakweli siwezi kukueleza chochote..” alisema Elisha, kwa sauti kavu iliyo tawaliwa mna maumivu, “nazani sikuzako zimefikia mwisho, siwezi kukulazimisha kuishi” alisema Kisona, kwa sauti kavu ya hasira, na hapo mke wa Mapombeka, alishuhudia kitu ambacho kilimsaidia sana katika uzazi wake wa mtoto wakwanza, wa kiume, zili shuka ngumi mfululizo usoni kwa Elisha, ndani ya sekunde tano, mke wa mapombeka, akuweza kuuona uso wa kijana huyu, ambae jana alimtandika kofi, kwa jinsi damu zilivyo tapaa usoni kwake, huku nyingine zikimwagikia chini, na nyingine zikiingia mdomoni na kupenya kwenye koo, kila alipo jaribu kupiga yowe, na kumpalia, vibaya sana, kiasi cha kushindwa kupumua, hapo wakamwona akirusha rusha miguu, kama vile ng’ombe alie chinywa, mpaka Kisona ana mwachia Elisha, tayari kijana huyu alikuwa amesha tulia, akionyesha kuwa amesha kata roho, mke wa kopo Mapombeka alistuka sana.
“mama tumbo langu….” ghafla ilisikika sauti ya mke wa Mapombeka, Kisona aka geuka na kumtazama mwanamke huyu, akamwona ame hikilia tumbo lake kwa mkono wa kushoto, na mkono wa kulia umeshikilia kiuno kwa nyuma, “shemeji nisaidie tumbo linauma sana” alisema mwamake huyu, ambae usowake ulionyesha kuwa, alikuwa katika maumivu makali, “poe shemeji, usiwe na wasi wasi, tunawai hospital sasa hivi” alisema Kisona huku ana kimbilia mlangoni, kumbe Katembo alikuwa pale nje ana angalia usalama, wa Kisona wakati alipokuwa ndani, “zunguka mtaa wapili waambie walete gari haraka, tumwaishe mke wa huyu askari Hospital” alisema Kisona na Katembeo aka timua mbio kuwenda kuwaita wakina mzee Mbogo, walio kuwa wana wasubiri mtaa wapili,**
Kilomita nne upande wa kusini, kilomita sita kusini Mashariki, toka eneo la tukio la mashambulizi, na mlipuko kumbwa sana, kikundi cha Msengi, alicho saidiwa kukiongza na koplo Lusinde, kilisikia vyema kabisa mapambano hayo, “jamani twendeni tuka wasaidie wenzetu, nazani wamesha waona majambazi” alisema Msengi, na hapo bila kuchelewa, wakabadiri uelekeo na kuelekea kaskazini magharibi, wakifwata moshi mnene ulio onekana kwambali, **
Ogwambo na kundi lake la polisi, waliwai pale barabarani, ambako ulisikika mlipuko, na wakuwakuta wakina Kingarame wame simama mita hamsini, toka kwenye gari lililo kuwa linawaka moto, wakiutazama ule moto mkubwa, “nini kimetokea afande?” aliuliza Ogwambo, kwa mshangao huku sajent Idd kibabu akiwa anasikilizia jibu toka kwa boos wake SSP Kingarame, au King kama anavyopenda kumwita, “huyu kijana ni hatari sana, ama teketeza gari la awa raia wema, na wenyewe wakiwa ndani ya gari” alisema Kingarame kwa sauti ya huzuni kubwa sana, “na mbaya zaidi tume shindwa kuwa saidia, maana mlipuko ulikuwa mkubwa sana” aliongezea Kingarame, kwa sauti ile ile ya huzuni.
Akika uzuni ile iliwashika wengi, wakiwepo askari aliokuja nao Ogwambo, na Ogwambo mwenyewe, kasoro sajent Idd Kibabu, ambae alitazama pembeni na kutabasamu, kwa kebehi, maana alijuwa fika kuwa huu mchezo siyo wa Edgar, ila ni boss wake, “lakini huyu mshenzi ame fikaje huku, wakati alikimbia huku baada ya nyie kumshambulia” ilo swali la mashaka lilikuwa ndio ukweli wenyewe, kwa mtu yeyote atake sikia jinsi tukio hili lilivyo kuwa, lazima ange jiuliza inawezekanaje Edgar arudi tena kule alikokimbia mwanzo, na kufanya shambulizi, kama lile, tena mbele ya polisi wale waliokuwepo eneo lile, “kwa hiyo nani ana danganya?” aliuliza Kingarame kwa sauti iliyo jaa hasira, na kumfanya Ogwambo atulie kimya.
Hapo ukafanyika utaratibu wa kukusanya marehemu wa kule porini, na awa waliokuwepo hapa barabarani yani wale polisi, maana raia waliteketea ndani ya gari, kisha wakapakiza kwenye gari na kupekea Njombe mjini, huku Ogwambo akiingia porini kuendelea na msako, kisha Kingarame akaelekea barabara kuu, kule liliko elekea gari lililo beba marehemu, ***
Serena Hotel, kwenye sehemu ya kupatia chakula, ambayo jioni utumika kwa vinywaji, baba na mama Monalisa wakiwa na dereva wao, walikuwa wanaendelea kupata sup, huku wana ongea mawili matatu, “mke wangu iliwazo la Erasto kumvesha pete, Monalisa, mala tu ! tukifanikiwa kumwona, minazani siyo vyema” alisema baba Monalisa, kwa sauti tulivu, “lakini baba Mona, kama watoto wana pendana, kwa nini tusiwaache waveshane pete?” aliuliza mama Monalisa, akionyesha kuwa akutaka kuchelesha jambo hili, “unauakika kuwa Mona amelidhia kuwa mchumba wa Erasto, maana kwa kiasi kikubwa, nikama ulikuwa unamlazimisha” alisema baba Monalisa, huku akiendelea kufakamia supu yake ya kuku, iliyo jaa kwenye bakuri, “lakini kunafaida kubwa, Monalisa akiolewa na Erasto” alisema mama Monalisa, ambae kama mume wake, aliendelea kushndilia supu ya kuku iliyo jzwa limao na pili pili, “faida gani unayoona itapatikana?” aliuliza baba Monalisa, kwa sauti ya mshangao, huku akiacha kunywa supu yake na kumkazia macho mkewake, wakati huo dereva alikuwa anawasikiliza, pasipo kuchangia neno, zaidi ya kuendelea kufakamia supu, “kwanza tutakuwa tume dumisha urafki wetu, pili atutakuwa na wasi wasi, kuhusu mtoto wetu, sababu atakuwa anaishi na mtu tunae mfahamu, tatu ata malizetu hazito tawanyika” alisema mama Monalisa, kwa kujiamini kabisa, lakini baba Monalisa alicheka kidogo, kicheko ambacho kiili mshangaza ata mama Monalisa, ambae alimtazama mume wake kwa mshangao, “kwanini unacheka hivyo?” aliuliza mama Monalisa, “bado uja mjuwa Erasto, nasiku utakayo mjuwa nazani unaweza kufanya jambo la hajabu sana” alisema baba Monalisa, kama vile anatania, “lione kwanza, hivi umeanza lini hiyo tabia ya kumchukia mkweo?” aliuliza mama Monalisa kwa sauti ya utani, na kuendelea kupata supu, “tatizo unataka kuendekeza hakiri ya mwana Mona, bola tumwache aolewe tu, mwishoe akaja kutuletea aibu” alisisitiza mama Mona.
Hapo baba Monalisa akatulia kidogo, kama vile anapanga jambo flani, kisha aka mtazama mke wake, “eti mama Mona, utachukuwa maamuzi gani, kama ukimkuta mkweo, yupo na mwanamke mwingine?” hilo swali lilikuwa gumu kidogo, kwa mama Mona, maana alitulia kidogo kisha akatabasamu, akia chia mgono, “mh! sijuwi nitafanyaje” alisema mama Monalisa, ambae alikuwa ametulia kidogo pasipo kula supu yake, akawa kama bado anaendelea kutafakari, baba Mona na dereva wake walikuwa wametulia wakitabasamia ndani, “kwanza kwanini ume niuliza hivyo?” aliuliza mama Mona huku ana mtazama mume wake, kwa macho yaliyoonyesha hasira ya chinichini ***
Wakati mjini yanaendela hayo, huku Monalisa akiwa ameshikwa mkono na Edgar walikuwa wana ingia kwenye killing zone nyingine, yakina Msengi, ambao walikuwa wanakuja kutokea juu kushuka chini, wakikimbilia kule kwenye moshi mzito, na wakina Monalisa walikuwa wana pandisha mwinuko huo huo, “wale paleeeeee” ilisikia sauti ya askari mmoja, toka kule juu, hapo Edgar na Monalisa wakainua macho yao, na kuwaona askari wakija mbio mbio kama vile askari wa jamhuri ya VIETNAME, ambao awakuwa na simile, wakainua silaha zao na kuzielekeza mbele, yani wanakotokea wakina Edgar, hapo Kitendo bila kuchelewa, Edgar akiwa ameushikilia mkono wa Monalisa, aka badiri uelekao, na kupinda kulia, na kulifwata korongo moja kubwa sana, mita hamini mbele yao, huku wakisikia milipuko ya risasi mfurulizo, na kushuhudia risasi zikigonga karibu yao, “inama” alisema Edgar akimweleza Monalisa, ambae bahati mbaya, katika kukimbia. itaendelea hapa hapa
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU