: BIKIRA YA BIBI HARUSI (53)

SEHEMU YA HAMSINI NA TATU (53)

ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI (52): aka badiri uelekao, na kupinda kulia, na kulifwata korongo moja kubwa sana, mita hamini mbele yao, huku wakisikia milipuko ya risasi mfurulizo, na kushuhudia risasi zikigonga karibu yao, “inama” alisema Edgar akimweleza Monalisa, ambae bahati mbaya, katika kukimbia. ENDELEA………..
Alijikwaa na kuangauka chini, huku akiponyoka kwenye mkono wa Edgar, ambae alipiga hatua tatu mbele na kujiiangusha chini, kiisha aka tambaa haraka mpaka alipokuwepo Monalisa, na kumshika mkono kisha kuanza kufuta, na kutambaa pamoja wakizidi kulifwata bonde, huku mivumo ya risasi ikipita juu yao, “fyuuuuuu” ungezani miruzi. huku bahadhi ya risasi zikichimba karibu yao, hapo Edgar akajuwa kuwa asipo fanya jambo inakula kwao, hivyo haraka sana akamwachia mkono Monalisa, na kujibiringiisha, akirudi nyuma ya Monalisa, huku ameikamata vyema SMG yake, “endelea kusongea mbele, nenda kwenye hilo bonde” alisema Edgar huku, ana iweka swa bunduki yake na kuielekeza kule waliko polisi, yani zinakotokea risasi, kisha aka songeza kidole kwenye trigger, na pasipo kuona adui maana nyasi zilikuwa zime mzidi kimo, Edgar aka minya trigger, akiachia risasi tano mfurulizo, hapo aka zikasika sauti za “take cover, take cover” alafu ikawa kimya, kwa sekunde kadhaa, pasipo milindimo ya risasi, Edgar akatumia nafasi hiyo kumsomba Monalisa alie kuwa anajikongonja kwakutambaa, na kuangukia nae kwenye korongo dogo kama unge simama linge fikia kifuani, huku atua chache mbele yao kukiwa na korongo kubwa sana, lililo ambatana na mto chini yake.
Nawakati huo tayari polisi walisha anza tena kushambulia kwa fujo, ikionyesha walisha chukuwa maficho salama kwao, Edgar na Monalisa wakiwa wame jificha kwenye lile korongo ambali ungezania kuwa ni andaki, waliwezxa kusikia risasi zikichimba kulizunguka lile korongo, “wamekimbilia pale shambulieni” ndivyo ilivyo sikika wakati polisi wana shambulia, Edgar na Monalisa wakiwa wame jificha kwenye lile korongo ambali ungezania kuwa ni andaki, waliwezxa kusikia risasi zikichimba kulizunguka lile korongo, “wamekimbilia pale shambulieni” ndivyo ilivyo sikika wakati polisi wana shambulia, “Eddy, leo tunakufa” alisema Mononalisa, kwa sauti iliyo tawaliwa na uoga, akikaribia kuangua kilio, Edgar alimmtazama Monalisa, kisha aka jitabasamulisha kumliwaza Monalisa, japo Moyoni mwake alijuwa kuwa mambo yalikuwa magumu kwa upande wao, “Mona, siwezi kuacha jambo baya likutokee, niamini lazima tutafika nyumbani tukiwa na roho zetu” alisema Edgar, huku wana sikilizia milindimo ya risasi.
Baada ya sekunde kama kumi na nane hivi, Edgar nikama alikumbuka jambo, aka ikamata magazine ya silaha yake na kuitoa, kisha akaitazama, nikama alikuwa anazitazama risasi zilizomo, Kisha aka iweka kwenye begi, na kuichukuwa nyingine, alafu akaitazama, nikama alilizika nayo, aka ipachika kwkenye bunduki, “nisubiri hapa, nikuonyeshe inavyo kuwa” alisema Edgar, kisiha akaanza kutambaa kuelekea upande wa mashariki akifwata uelekeo wa lile korongo dogo, akimwacha Monalisa ana msindikiza kwa macho, akimwona rafiki yake huyu, ambae wamerudisha urafiki wao, hivi karibuni, akimwona ana tambaa na silaha yake mkononi, milindimo ya risasi ikiendelea, Edgar alipofikia umbali wa mita kama 30 hivi, alisiha toka kwenye mlango wa mashambulizi, aka inuka na kuanza kukimbilia juu zaidi, sasa monalisa alianza kuisi polisi wana shambulia huku wana sogelea pale alipojificha yeye, akika Monalisa akahisi kuwa sikuzake za kuishi hapa duniani zime kwisha, na kinachofwata nikukabidhi roho kwa muumba, “au ameamua kuniacha peke yangu” aliwaza Monalisa, huku aki tokwa na machozi.
Lakini ghafla aka sikia milio mingine zaidi ya risasi, iliyo kohoa kwa mtindo wa rapid, “jificheni anatushambulia toka nyuma, “zilisika sauti za mayowe za polisi, walio kimbia ovyo ovyo, huku wengine wakawa wana kimbilia kule aliko jificha Monalisa, lakini ilionyesha kuwa Edga alisiha juwa kosa alilo lifanya, na kuliweka sawa, aka mimina risasi kule waliko kuwa wana msogelea Monalisa, na kuwa dondosha wawili walioangukia karibu kabisa na binti huyu mrembo, wakiwa wame tandikwa risasi za mgongoni, na kupoteza maisha, lakini Monalisa ambae sasa matumaini yalisha rudi, alitulia akikodomlea maiti za askari wale wawili, walio lala karibu yake, huku wengine wakitawanyika hovyo.
Kikafwata kimya kidogo, baada ya sekunde chache, polisi wakaanza kushambulia kule ziliko tokea risasi za Edgar, huku wana kimbilia upande huo huo, ikionyesha Edgar alikuwa ana kimbilia upande wa mashariki, wakati huo zilisikika sauti za kuugulia maumivu, ikionyesha maeneo yale kulikuwa na polisi walio jeluhiwa.
Milio ya risasi na kelele za polisi waliokuwa wanamfukuza Edgar, zilizidi kutokomea mahashariki, mwisho milio ika koma na kelele zilisikika kwa mbali sana, “msakeni atakuwa hapa hapa na ameishiwa risasi” inamaana ilionyesha kuwa, walisha mpoteza Edgar, hapo Monalisa akatulia kidogo kumsikilizia Edgar, lakini baada ya kupita dakika tano, Monalisa ambae alitamani kujitoa eneo lile ambalo, aliliona kuwa siyo salama kwake, aka mwona Edgar akiibukia kwenye korongo refu, “twende zetu, nime waacha wanashngaa huko” hapo Monalisa hakusubiri kuambiwa kwamala yapili, aka jiokota haraka sana, na kuudaka mkono wa Edgar, kisha wakazamia korongoni na kutokomea nalo, wakifwata ulekeo wa lile korongo lililo kuwa linaelekea upande wa kusini mashariki, wakiwaacha polisi wana rusi eneo la tukio, na kukagua walio kufa na walio jeruhiwa, “mashenzi sana huyu jamaa, lazima aya kuiuwa ni mwanajeshi tu!”**
Joseph Kisona na kundi lake, sasa walikuwa ndani ya gari lao, land rover mia na kumi, na mwili wa kijana Elisha, wakielekea porini, ni baada ya kumpeleka mke wa Mapombeka, hospital na kumwamcha akiwa amejifungua salama mtoto wa kiume, ambae mke wa Mapombeka aliomba ampe jina la kamanda Kisona, yani Joseph,
“sasa huu si ushaidi lakini?” aliuliza mzee Mbogo, akiwa katika mwendo mrefu sana, kama kawaida yake, “huu siyo ushaidi, hili ni onyo kwa Kingarame” alisema Kisona huku safari inaendelea, “kwa hiyo unaenda kumpelekea?” safari hii aliuliza koplo Katembo, wakati wana kakona kushoto, kwenye njia panda ya porini, “we niachie mimi uone” alijibu kisona huku, na baada ya kutembea kama mita hamsini, kisoma akasema, “simamisha gari” mzee Mbogo akasimamisha gari mala moja, na hapo hapo kisona akatoa amri kuwa, mwili wa Elisha utupwe mita chache toka barabarani, yani kwenye kichaka, lakini kwa macho ya kawaida wange weza kuiona, kwa yoyote atakae pita njia.
Kiisha pasipo kupoteza muda wakaingia kwenye gari lao na kuondoka zao, kuelekea kule porini, huku mbele yao wakianza kuona moshi mzito, ukifuka usawa wa barabara, kilomita ka asaba hivi mbele yao, “mh! tayari kimenuka huko” alisema Kisona, huku mzee Mbogo akinyaga mafuta kwa nguvu, kuelekea kule kunakofuka moshi, ambao walitumi dakika zisizo fika kumi, eneo lile wakakuta tupu, zaidi waliona gaari likiwa linaendelea kuteketea, kwa moto, Kisona akashuka na kukagua eneo liole na kuona mambo mawili matatu, ikiwa ni maganda ya risasi kadhaa, takiwa katika makundi, “mh! hapa Edgar amepewa kesi” alisema Kisona wakiwa njiani wanaesonga mbele, kuelekea kwenye kambi ya polisi, kule kwa wakulima, ***
Mafinga mjini, ni kimji kidogo, kilichopo kilomita mia moja na hamsini toka makambako, ndani ya nyumba moja kubwa ya kifahari, ikionekana mercidis benzi moja jeusi nje , alionekana binti chotara, wa kiarabu salma akiingia ndani ya nyumba kubwa na kuelekea moja kwa moja sebuleni, ambako aliwaona baba na mama yake wakiwa wame tulia mezani wakipata chai, lakini nikama walikuwa wame ganda, huku wame tega masikio kwenye redio, ikionyesha walikuwa wanasikiliza kitu muhimu sana, “jambazi huyu alie julikana kwa jina la Edgar Mbogo, bado anaendelea kumshikilia binti Monalisa Anderson, kwa siku ya tano sasa, akiongea msemaji wa heshi la polisi, ambae yupo huko porini wanako msaka jambazi Edgar, anasema kuwa jeshi la polisi linaendelea na juhudi za kumsaka jambazi huyu pamoja na washirika wake, aliosafiri nao toka mbeya, kuja kumsaidia mwenzao toka songea, alie uwawa katika mapambano na polisi, akiendelea kuongea msemaji wa polisi, alisema kuwa pia jeshi la polisilina fanya jiti hada za kumwokoa binti Monalisa” maneno hayo yalisikika toka kwenye redio kubwa iliyopo ndani ya jumba hili la mzee Mohamed, “unajuwa hizi habari zina nichanganya sana toka nimeanza kusikia” alisema mzee Mohamed, ambae kiukweli habari hizi zili wanyima amani yeye na familia yake, ambao waliamini kuwa Edgar awezi kuwa jambazi, “jamani sisi sindo tume mwacha pale hotelini makambako?” aliuklliza mama salma, na salama akadakia, “yani mimi nilikuwa siamini kama kweli kuna watu wanasingiziwa kesi, sasa ndio naamini” alisema Salma,na hapo ukazuka mjadala mrefu wakiongea na kukumbushana jinsi safari yao ilivyo anza, na kufika makambako, na kumwacha kijana huyu walie mpa lift,
“Jamani mimi naenda Njombe, kukutana na RPC, nika mweleze kuwa kijana huyu siyo jambazi, na mimi ndie nilie mwacha makambako, ili asubiri usafiri siku ya pili” alisema mzee Mohamed, huku mke wake na mwanae Salma, wakipendekeza waende wote, ili wakatoe ushaidi, kuwa nawao walikuwepo wakati wana safari na Edgar.
Hapo mzee Mohamed na familia yake, walijiandaa kwa safari, na baada ya lisaa limoja mbele, walikuwa ndani ya benzi jeusi wakielekea Njombe, kutoa msaada wa kishaahidi, kwa RPC, ilikumwokoa Edgar, pasipo kujuwa kuna kamanda Kingarame, yupo ndani ya mchezo huo. ***
Saa sita na robo, ndio muda ambao Kisona aliingia kwenye kambi ya muda ya polisi, akipishana nukta chache na magari mawili ya polisi, yaliyo kuja na mbwa wanne wakubwa, wenye mafunzo ya kufwatilia nyayo na arufu, toka Iringa, kwaajili ya kumsaka jambazi Edgar, pale makamanda awa kumjari Kisona, haraka sana wakaamuru mbwa waingizwe msituni kumsaka Edgar, ikawa hivyo, wakaondoka, polisi kumi na tano, wakiwa na wale mbwa wanne, wakienda kuanzia kule yalikotokea mapigano mala yamwisho,
“ndiyo bwana Kisona, za toka asubuhi?” sasa RPC, aliongea huku akimtazama Kisona, “kwangu ni salama, sijuwi upande wako?” alisema Kisona, ambae wenzake aliwaacha kwenye gari, nikamaRPC Iringa alivuta pumzi ndefu na kuzishusha kwanguvu, “kwakweli huyu jambazi Edgar amezidi kupunguza askari wangu, yani tokea asubuhi tuna endelea kupokea maiti, mpaka sasa wamesha kufa zaidi yakumi, namajeruhi kibao” alisema RPC, kwa masikitiko makubwa, hukuwenzake wakiwa kimya kabisa, “dah! pole sana, vipi lile gari lililo ungua pale barabarani?” aliuliza Kisona, swali ambaloi, yeye binafasi jibu alikuwa nalo, “yani kwakweli alicho kifanya yule kijana, lazima akilipie, siku akamatwa, unajuwa ame lipua lile gari, likiwa na watu ndani” alisema RPC Iringa kwa sauti iliyo jaa uchungu mkubwa, huku OCFFU, RUVUMA akidakia, “yani huyu mshanzi sito kuwa na hurunma nae, inabidi akiuwawa mwiliwake ubebwe na kutembezwa hadharani” hapo Kisona alicheka kidogo, kiasi cha kuwashangaza makamanda wale, “Kisona kuna cha kuchekesha hapo, au unataka kuongea tena mafumbo yako?” aliuliza RPC Ruvuma, kwa sauti iliyo jaa mshangao, “hapana mzee wangu, ila nacheka kwa uzuni” alisema Kisona, na hapo wale makamnda waka shusha pumzi, na RPC, Ruvuma, akaongea, “nikweli bwana Kisona, ina tia uchungu, yani vijana wetu wana uwawa ovyo hovyo, alafu kajitu kenyewe akaeleweki ata kidogo” hapo Kisona aka cheka tena, “siuzuniki kwaajilli ya waliokufa, nauzunika kwa watakao endelea kufa” alisema Kisona, na kuwafanya wale makamanda wamshangae tena, “inamaana kanal unahisi vijana wataendelea kufa, wakati tumeongeza nguvu ya kumnasa huyu mshenzi na wenzake,?” aliongea RPC Iringa kwa mshangao, na hamaki, “kuna kitu bado amjakijuwa, katika huu msako wenu, mmesema polisi wengi wame uwawa wakiwa wana pambana na Edgar, ambae amechoma gari likiwa na watu ndani yake, sindivyo?” nikama Kisona aliuliza, “ndio au ukusikia wakati mkuu anasimulia?” aliuliza OC FFU WA Ruvuma, “ok! kwa hiyo huyu jambazi alikuwa mmoja, zidi ya polisi wengi?” aliuliza tena Kisona, na hapo awa makamanda wakacheka kwa hasira, “uwa nasikia huko kwenye mafunzo ya jeshi uwa wanachanganyiwa bangi kwenye chakula” alisema RPC Ruvuma, na wote wakacheka tena, kasoro RPC Iringa peke yake, “ebu tumsikie kwanza, uwa anaongeaga point za maana sana” alisema RPC Iringa, kisha akamgeukia kisona, “ndio bwana Kisona, report inasema alikuwa peke yake, na ameonekana akimkimbiza yule binti” alisema RPC, “hapo nikukumbushe jambo moja ulilo niambia, ulisema kuwa amewachoma watu kwenye gari, sindia bwana RPC?” aliuliza Kisona, na hapo wote walikuwa kimya, kufwatia amri ya kiongozi wao, “ndio, tena ni watu kama nane hivi, wamefia ndani” alisistiza RPC Iringa, Kisona akatabasamu kidogo, “kuna kitu sijuwi kama walikuambia, kuwa gari lile lilikuwa lina tatizo la tairi?” aliuliza Kisona, na hapo OC FFU akadakia, “lakini siyo sababu ya kumfanya Edgar ashiindwe kulilipua gari,” hapo Kisona akacheka kidogo, kicheko cha utulivu, “ni vyema ukajibu kama uliambiwa au huku ambiwa, maana kama hilo una lijuwa nazani utakjuwa una juwa juu ya damu iliyo tap-akaa nje ya gari, na maganda ya risasi yaliyo washambulia watu hao nje yagari” hapo makamanda wakatazmana kwa mshangao, “inamaana tuamini nini, hawa majambzi wwalikuwa wengi au …….?” alishindwa kumalizia swali RPC Ruvuma, siyo hilitu mna maswali mengi ya kujiuliza, maana gari mpaka liungue moto, lazima risasi nyingi zilipigwa kwenye tank, je wakati huo polisi walikuwa wapi, wakati Edgar ameacha kuwashambulia na kulimiminia risasi gari?” itaendelea…….. Hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!