
: BIKIRA YA BIBI HARUSI (58)

SEHEMU YA HAMSINI NA NANE (58)
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA SABA (57): “hapana….. ha… ha…hapana, ajafika mtu hapa, nyie ndio wakwanza” alijibu mlinzi , lakini kisona alisha soma kitu kwenye hakiri ya mlinzi, na kumfanya Kisona acheke kidogo, kisha aka mtazama mzee mbogo, “na huyu ni mmoja wao, ato kaa alione juwa la kesho,”endelea……
Siyo kwamba mlinzi akusikia maneno yale, lakini hakuyaelewa yana maana gani, Kisona aka tazama ardhi ya eneo lile, nikama kuna kitu alikuwa anakitafuta, alipo kiona aka tabasamu kidogo, “ok! tuna kutakia kazi nje, lakini kuwa makini kwa kazi mpya uliyo pewa, maana malipo yakeayatakuwa mazuri atakidogo, ifanikiwe hisi fanikiwe” hayo yalikuwa maneno ya kisona, sekunde chache kabla awajaondoka zao, kuelekea Makambako.
Kagiza kalisha ingia na kumfanya mzee Mbogo, kuwasha taa za gari hili la kijeshi, “Kingarame alishafika huku, na amshaongea na huyu mlinzi” alisema kisona, ambae alishaona alama za matairi ya gari, na kuyatambua ni matairi ya gari aina ya Toyota land cruzer, “sasa si itakuwa hatari kwa wakina Edgar endapo wata kuja hapa?” aliuliza baba Edgar, huku akikanyaga mafuta kupandisha mlima mkubwa kidogo, baada ya kulivuka dalaja moja kubwa la mbao, lililo ufunika mto ambao uliokuwa unatililisha maji, kuelekea mashariki, kilomita mbili toka kwenye kiwanda cha majani ya chai, “inamaana bado uja juwa chakufanya?, sasa kazi yetu ni kuchunguza nyendo za kina Kingarame tu!, maana lazima watapewa taharifa, mala tu Edgar na Monaisa watakapo fika hapa, na wao watatoka haraka kuwai mahali hapa, hivyo Makambako atutakiwi kukaa sana, ***
Ndani ya msitu huu mnene sana, Safari ya Edgar na Monalisa iliendelea kimya kimya, akuna alie weza kumsemeshamwenzie, kila mmoja alionekana kuwaza jambo lake, wakati Edgar akionekana kuumia moyoni mwake, juu ya taharifa ya Monalisa kuwa na mchumba, Edgar bola angeambiwa na mtu mwingine, lakini siyo Monalisa mwenyewe, na kilicho muumiza zaidi ni kwamba, mchumba mwenyewe ni Erasto, kijana alie msababishia ugomvi mkubwa sana na wazazi wa binti huyu, uogomvi ambao umekuwa ni wakifamialia, na uliovunja urafiki mkubwa kati ya familia zao mbili.
Wakati Edgar anawaza hayo Monalisa nae alikuwa anawaza yakwake,Mnalisa aliwaza jinsi Edgar alivyo ipokea taharifa ya yeye kuwa na mchumba, atamhivyo akuacha kupambana kwaajili yake na kuwashinda maadui, “bola nisinge mwambia mapema, inaonekana ameumia roho” akika Monalisa alijutia ulopokaji wake, “lakini ngoja, nitajuwa lakufanya” alijiwazia Monalisa, huku akimtazama Edgar aliekuwa ameushikilia mkono wake, akamwona bado akiwa kimya, kama kuna jambo anawaza, na wakati huo huo, mbele yao umambali kama wa mita kama mbia nne hivi, waliona mwanga wagari, likipandisha mlima, “gari lileeee” alisema Monalisa kwa sauti iliyo changamka kidogo, huku akiwa bado ameushikilia mkono wa Edgar, “lakini inabidi tuwe makani, inaweza kuwa ni karibu na mjini, au magari ya polisi” alisema Edgar, kwa sauti tulivu, huku wana badiri uelekeo, na kuelekea kule waliko liona gari linapita.
Walitembea taratibu wakikatiza kwenye vichaka vilefu vyanyasi, mpaka walipo ifikia barabara ya vumbi, aikuwa tofauti sana na ile ya kwenda mbugani, yani inayopita kwenye mashamba ya wale wakulima, na ndipo walipo anza kuziona taa nyingi, upande wao wa kushoto, umbali kama wa kilomita kama mbili hivi, kwa makadilio wa haraka haraka, ikionyesha kwamba kulikuwa naa makazi ya watu, na wao wakaanza kutembea barabarani, kimya kimya, kufwata uelekeo wa zile taa, “Edgar samahani” alisema Monalisa, kwasauti yaupole na nyembamba, akiwa bado ameushikilia mkoni wa Edgar, daima huo ndio ulikuwa mtindo wao wa kutembea, “samahani ya nini Mona?” aliuliza Edgar kwa mshangao, huku akisimama na kumtazama Monalisa, “naona ume chukia nilivyo kuambia kuwa nina mchumba” lisema Monalisa kwa sauti ile ile ya upole, huku akikwepesha macho yake, yasikutane na macho ya Edgar, ambae alitabasamu kidogo, “hapana Monalisa, wala usiwe na wasi wasi, sija chukia kama unavyo zania” alisema Edgr kwa sauti tulivu, kisha wakaendeleakutembea, “sasa mbona hupo hivyo?” aliuliza Monalisa, huku akimtazama Edgar, “univigumu sana kujizuwia kuonyesha ninavyo jisikia” alisema Edgar huku akitabasamu, Monalisa nae akatabasamu, “kwa hiyo Eddy unanupendda hen” aliuliza Monalisa, huku ana tabasamu, “sijawai kuacha kukupenda Mona, aijilishi yote ya;liyo tokea na yanayoendelea kutokea, nitaendedlea kukupenda” alisema Edgar sijuwi alikuwa anamanish nini, maana maneno haya yliugusa moyo wa Monalisa, ambae halihisi kauchungu mfali kaliko yatekenya machozi kule yanako kuwaga, na kuanza kuchuruzika kwenye macho yake, akayavuta sambamba na kuvuta kamasi nyepesi, kitendo kilicho mjulisha Edgar kinacho endelea kwa binti huyu, “lakini simpendi Erasto, nime lazimishwa na mama, sijawai kufanya nae chochote” alisema Monalisa na hapo Edgar akasimama na kumgeukia Monalisa, akamtazamakwa sekunde kadhaa, kisha akashindwa kusema neno, alafu akageuka nakuendelea na safari kimy kimya, wakizidi kuzisogelea taa, ambazo zilizidi kuwa nyingi kila walipo zisoglea, “sijuwi ple ni wapi inabidi tupate mtu wa kumwuliza, kama nisehemu salma tulale hapa hapa” alisema Edgar huku wanendelea kutembea.***
“Afande, mpaka sasa nimeshapata majina yaaskar wote navikundi vyao, pamoja na askari tulio nao kwenye magari, lakini inasemekana PC Isaya na PC Elisha, awakulala huku porini, na awakuonekana huku ata mala moja, mpaka tulivyo wakuta wame uwawa” alisema OC FFU toka Ruvuma, wakati aka wakilisha report ya kazi aliyopewa, “maana yake nini, ndio tumeshindwa kutambua awa wawili walikuwa na nani?” aliuliza RPC Iringa kwa sauti ya ukari, “hapana Afande, bado tunaendelea na uchunguzi, nazani tuta juwa walikuwa na nini mala ya mwisho” alisema OC FFU, kwa kujiaminisha kwa RPC, “ok! nazani huu ni muda wa kuelekea mjini, kila mmoja awe makini na askari wake anaoendanao mjini” alisema RPC Iringa kisha wote wakaelekea kwenye magari yao.
Safari ika anza kuelekea mjini Njombe, safari hii yalikuwa magari nane, yakiongezeka magari, mawili yani gari la RCO Ruvuma, namaanisha SSP Manase Kingarame, na gari la OCD Njombe, tayari iliisha timia saa mbili kasolo za usiku, alafu kuna habari ya wale askari walio lazwa kule Makambako sijuwi wanaendeleaje, inabidi kesho tuwai tukawaone, kabla ya kuwenda porini” alisema RPC Iringa, akiwa na dereva wake ndani yagari.***
Haya sasa huku Serena Hotel, mambo yalikuwa bam bam, mama yake Monalisa alisha kuwa anaendelea kukandamiza pombe kwa fujo zote, kiasi cha kuwashangaza baba na mama Erasto, ambao walihisi kuwa hii ni sababu ya kuto kumwona binti yake, lakini ilikuwa tofauti, kwa mume wake, ambae alionekana kujawa na furaha, na uchangamfu, “nahisi mwanangu karibu atapatikana” alisema baba Monalisa, huku ana mimina pombe kwenye grass, “kwanini unasema hivyo, bwana Anderson, maan hiyo ndiyo furaha yetu” alisema Misago na wakati huo Erasto alikuwa anakaa kwnye meza yake, akitokea chumbani kwake, wote waka mtazama, kwa sura mbali mbali, wakati mama na baba Erasto wana tabasamu, huku mzee Anderson alikuwa katika hali ya kawaida, akimtazama Erasto na kumtazama mke wake, ambae alimtazama kijana huyu kwa macho makali yaliyo jaa chuki, bahati nzuri ni baba Mona na derevapeke yao ndio walio ona macho ya mama Mona, “naamini kuwa Mona karibu anapatikana, kwasababu ilijambo limetokeakwa maana yake” alisema baba Monalisa, na mke wake aka unga mkono, “nikweli ata mimi nimeamini kuwa, kila jambo linatokea kwa sababu zake” kauli ile ili onysha kuwafurahisha wakina misgo na familia yake, “nita furahi sana, Mona akirudi salama, tena nita mvisha pete mala moja, yani hapo hapo”

