: BIKIRA YA BIBI HARUSI (59)

SEHEMU YA HAMSINI NA TISA (59)
 
ILIPOISHIA SEHEMU YA HAMSINI NA NANE (58) “nita furahi sana, Mona akirudi salama, tena nita mvisha pete mala moja, yani hapo hapo” hivi mama Mona atajibu nini?, ebu tembelea kuanzia saa nne kamili. hapa hapa kwa. ENDELEA……….
alisema Erasto, pasipo kujuwa maana ya maneno ya wakwe zake, ambao tayari walisha gundua uchafu anao ufanya, ilibakia kidogo mama Mona apaliwe na pombe aliyo kuwa anainywa, akaishia kukooa kidogo, “na wewe bwana, ebu kunywa taratibu” alisema baba Mona huku akimpokea mke wake grass, na kuiweka mezani, meza ya tatu kutoka pale walipo kaa wao, alionekana dada mhudumu akiwa ameka na chupa kubwa ya pombe ikiwa mezani, na mikononi mwake alikuwa anahesabu fedha.
“Vipi Salma Mbona una mtazama huyo dada?” aliuliza mama Salma huku yeye na mue wake mzee Mohamed waki mtazama binti yao, ambaealiicheka kidogo, “hapana nashanga kuona mwanamke ana kunywa pombe kihasi kile” hapo wote wakacheka, “hii ndio inaitwa tembea uone” alisema mzee Mohamed, kisha akageuka upande waliokaa wakina baba Monalisa, “ebu waone wale” hapo Salma na mama yke wakageuka na kutazama kule kwenye meza ya wakina mzee Anderson, “sijuwi wana sherehe flani au wana sumbuliwa na kitu” alisema mama Salma akionyesha mshngao wake juu ya unywaji wa watu wale, na wakaati huo huo wakasikia miungurumo ya magari ikiingia pale hotelini, na baada ya sunde chache baadae, waka waona makamanda wa polisi wanapita kuelekea ndani ya jengo kubwa la polisi, “afadhari kumbe wame fikia hapa hapa, itakuwa lahisi kuongea na RPC mwenyewe” alisema mzee Mohamed. ***
Tayari ilisha timi saa mbili na robo, Edgar na Monalisa waliisha ingia kwenye eneo la kiwanda cha kukaushia majani ya chai, na wakalikodolea macho gari flani kubwa lililokuwa lina maliziw kupakizwa marobota ya majani ya chai, yaliyo fungwa kwenye mafurushi makubwa ya vitambaa vya magunia, “nyie wakinani na mfwata nini hapa” ilisikika sauti toka nyuma yao, pasipo wao kutarajia, wakaguka ghafla na kumtazama alie wasemesha, wakamwona jamaa mmoja alie valia koti kubwa l baridi na silaha yake ya kuwindia, (gobole) akilining’iniza begani kwake, “sisi ni wanafunzi tume tokea chuo, tunaitaji msaada wako” alijibu Edgar, kwa sauti ya kirafiki, huku atabasamu, “wanafunzi gani nyie wakati mme beba bunduki, au majambazi?” aliuliza yuke mlinzi, kwa sauti ya mkwala.
Hapo Edgar aka simulia mkasa wao kama ulivyo kuwa, na kusisitiza kuwa wanaitaji msaada wa sehemu ya kulala, ikiwezekana wapate na chakula, “ok! ebu kani nyuma ya hicho kibanda, nakuja” aliosema yule mlinzi, ambae alionyesha kuwaelewa na kukubari kuwapa msaada walio uitaji, akishwa kufanya lolote zaidi, maana alihisi kuwa watu wale ni zaidi ya hatari, akizingatia wana smg, mlinzi aliwaacha wakina Edgar wakizunguka nyuma ya kile kibanda walicho onyesha, kikawaida akikuwa kibanda kama kibanda, ila ni chumba imara kilicho jengwa madhubuti.
Nikweli yule mlinzi lienda moja kwa moja mpaka jikoni, na kukuta hakula kilicho bakia, baada ya wafanyakazi kumaliza kula, ulikuwa ni wali na maharage, aka uweka kweny doo akichanganya vyote kwa pamoja, kisha aka toka na ile ndoo mpaka kwenye kibanda alicho waacha wakina Edgar na Monalisa, akazunguka na kuwapa ile ndoo ya chakula, subirini niwletee maji ya kunawa, alisema yule mlinzi mwema kwawakina Edgar, huku anaondoka, kumbe safari hii yule mlinzi akuelekea kule jikoni mbako kuna bomba, alienda moja kwa moja kwenye kibanda kingine kidogo sana, na kuingia ndani humo kulikuwa na meza moja kubwa yenye simu juu yake, hivyo mlinzi haraka sana akatoa kikaratasi na kuanza kubonyeza namba za simu akizitazama kwenye klile kikaratasi aliicho pewa na Kingarame, ***
Tayari Kisona na timu yake waliisha kuwa wame maliza mizunguko yao kule Makambako, na sasa walikuwa njiani wakielekea Njombe, wakiwaacha wagonjwa wakiwa wame fumbua macho, japo walionekana kuwa katika amumivu makali sana, pia mke wa Mapombeka nae alikuwa katika hali nzuri yeye na mwanae Joseph, pia walimwacha ngigo, akiwa mahabusu ya kijeshi, amepondeka pondeka kwa kipigo cha mala kwa mala, “unajuwa yule jamaa ni mjinga sana, kwahiyo ameona afadhari apelekwe polisi, kuliko kubakia pale?” alisema baba Edgar, na wote wakacheka, sana, “maana mala tu Ngigo alipo waona akaanza kulia, kidai anataka apelekwe polisi, “unazani yule anamaanisha nini, anajuwa kuwa Kingarame ata mtoa mala moja, baada ya kumpeleka kule” alifafanua Kisona, na wakati huo walikuwa wana kata kona kuingia njia ya kuingilia Serena Hotel, ambako sekunde chache baadae walikuwa wana simamisha gari, kwenye mahegesho ya hotel hii, “jamani leo tuta kuwa kama polisi, akuna kubadiri nguo, akuna kunywa pombe, mpaka tutakapo tangaziana, maana tukizubaa tu! tume wapoteza wakina Edgar, alisema Kisona kabla awaja shuka, na kuwasalimia sakari polisi waliokuwa nyuma ya magari haya yapolisi, wakisubiri amri ya wkuu wao kuwa wakapumzike au wendelee kuwasubiri.
Hapo hapo Sereana hotel, kuna mambo mengine mawili yalikuwa yana endelea, moja ni kwamba kuna askari mmoja, toka Iringa alie kuwa kwenye gari la OC CID, Ruvuma, alimfwata dereva wa RPC Iringa na kumnongoneza kuwa, anaomba ampeleke kwa mkuu wao huyo,yani RPC Iringa, akidai kuwa kunajambo anataka amweleze, kabla awajaondoka kwenda kulala kule kituoni, pasipo kujiuliza anataka kuoongea nae nini, dereva wa RPC akakubari kuongozana na yule askari, jamani ngoja nika mwulize mkuu kama tuondoke au tusubiri,” alisema dereva wa RPC, huku akiondoka na mwenzie kuelekea kwenye jengo kubwa la hotel, wakiwa nyuma ya askari wa jeshi la ulinzi, ambao waliachiana kama mita tano tu!, sasa basi wakati wanakatiza mapokezi ili watawanyike, Kisona na baba Edgar, wakaitaji kutumia simu ya hotel, kuwasiliana na familia zao, lakini wakakuta mkonga wasimu ume wekwa pembeni, “samahani kaka, kuna simu ya mtu hewani, labda baadae kidogo” aisema dada mhudumu wa mapokezi, hapo mzee Mbogo na Kisona, waka pandisha ngazi kueleka juu.
Lakini sasa, wakati wakina Kisona wana pandisha ngazi za pili, yani za kwenda ghorofa ya tatu, mala mbele yao wakamwona Kingarame anashuka gazi, kuja chini, anapishana na askari polisi wawili, waliokuwa wanapandisha juu, nikama Kinmgarame aliwashangaa sana wale askari ambao licha ya kupishana nao, ilionekana mmoja wao akigeuka mala mala na kusabisha macho yao, yakutane mala kwamala na Kingarame, ambae alikuwa anageuka geuka kuwatazama wale askari polisi, yani dereva wa RPCC Iringa, na yule anae taka kwenda kuongea na RPC, ilibakia kidogo awapamie wakina Kisona, “mungu wangu, huyu mzimu amefwata nini hapa” alijiuliza Kingarame ambae, alipishana na wakina Kisona, bila kusemeshana, zaidi ya kuwakodolea macho kwa mahangao, kbla aja geuka nakutazama mbele, kisha kuzifwata ngazi za kushukia chini, huku wakina Kisonawakiendelea kuoandiuisha ngazi kueleka juu, kama vile awakumjari Kingarame.
Lakini aikuwa kweli, mala baada ya kufika ghorofa ya tatu yani ya juu kabisa, Kisona aka mtazama mzee Mbogo, “tayari mchezo umekamilika, ebu kaa kama dakika tano hivi kiisha shuka chini, wapitie wakina Katembo, tukutane kwenye gari” alisema Kisona huku akiingia chumbani kwake, na kumwacha mzee Mbogo ana shangaa, “sasa sindio tuna mwachia nafasi ya kufanya anacho kusudia” alisema baba Edgar lakini akujibiwa namtu yoyote,hapo baba Edgar akaona bola atimize majukumu aliyopangiwa, akatazama saa,yake na kuanza kuhesabu dakika tano, iliashuke chini.
Kumbe Kisona alipo ingia ndani ya chumba akupoteza ata dakika, na pasipo kuwasha taa, aka fungua dirisha la kioo, ambalo likuwa na msaada wa nondo, nazani ni kutokana nakuwa juu sana, mjenzi au mmiliki wa jengo hiliakuona ulazima wa kuweka nondo kwenye jengo hili, la tatu juu ya majengo mengine mawili, hapo kisona aka chungulia kushoo na kulia kisha akapanda kwenye dirisha na kulirukia bomba lamaji machafu lililo toka bafuni, na kkuanza kutelezanalo mpaka chini, ambako akuzubaha sana aka tembea haraka sana na kwenda kujibanza karibu na sehemu ya mahegesho ya magari, ambapo bado yalionekana magari ya polisi na askari wakiwa bado eneo lile, Kisona akatulia na kusubiri alicho tarajia kita tokea.
Nikweli dakika chache baadae, akamwona Kingarame anakujambio mbio, na kumwambia dereva wake aingie kwenye gari, hapo siyo Hokololo peke yake, alie ingia kwenye gari, ata askari walio kuwa na gari la RCO Ruvuma nao walidandia gari haraka sana, kisha likaondoka kwa speed, wakiwaacha wenzao wana wasangaa, dakika chache baadae wakatoka wakina mzee Mbogo na askari wote, wajeshi la ulinzi, wakaingia kwenye gari na kisona, na kuondoka zao, wakielekea kule alikoelekea Kingarame na askari wake.
Huku wakiacha mambo mazito kule Hotelini, maana baada yadereva kumgongea mlango, boss wake RPC, na kumweleza kuwa kuna mtu anaitajikuongea nae, “ok! we nenda mimi niongee na huyu askari” alisema RPC, na yule dereva aka wapisha, “ok! niambie kunalolote la kusaidia operation hii?” aliuliza RPC, akimkazia macho yule askari, “afande nimeona mna angaika kujuwa kuwa yule askari marehemu Elisha, alikuwa kundi gani, ukweli nikwamba, yule askari pamoja na wenzake, jana usiku walikuja na SSP Kingarame, pale kituoni, akalala pale, na leo mapema sana, yeye pamoja wenzake, walikuja kuchukuliwa na gari la SSP Kingarame”**
kule kiwandani mambo yalikuwa hivi, yule mlinzi aliifanikiwa kuppiga simu na kujitambuliisha kwa mwanamke alie pokea ile simu, akijitaja kuwa ni mlinzi wa kiwanda cha chai, na kueleza shida yake kuwa anataka kuongea na kamnda Kingarame wa chumba anamba tisa, akaambiwa asubiri kidogo, na baada ya dakika chache, akasikia sauti toko kwenye simu, “SSP Kingarame hapa nani mwenzangu” hapo ndipo mlinzi alipojitambulisha kwa mala ya pili na kuleza kuwa tayari wakina Edgar wapo hapa kiwandani, “sikia akikisha awa ondoki hapo, mpaka sisi tutapofika, kumbuka ukifanikiwa utafurahi mwenyewe, lakini, kosa dogo, gharama yake ni kubwa sana” alisema Kingarame na kukata simu, hapo mlinzi akapata wazo moja la haraka, ni kuwafungia wakina Edgar kwenye chumba, ili iwe lahisi kwake kuwakabidhi wakina Kingarame, hivyo mlinzi haraka sana akarudi pale alipo waacha wakina Edgar, “sikia bwana mdogo, ebu ingieni humu ndani, maana mkubwa wangu karibu atapita na gari kwenda mjini, anawza kuwaona ikaniletea matatizo,” alisema yule mlinzi huku akiwasaidia kubeba ndoo ya wali ndondo,(maharage) huku wakina Edgar wakifwata nyuma na kuingia ndani ya kile chumba ambacho, zaidi ya meza ndoogo, kulikuwa na kitanda chenye godoro chakavu na blangeti, “nisubirini humu” alisema yule mlinzi huku anazima taa yandani na kutoka nje akiurudisha mlango, wakati huo likasikika lile gari kubwa likiondoka pale kwenye ghara na kuikamata uelekeo wa mjini, lakini alikuondoka kabisa, likasimama karibu na kile kibanda ambacho kilikuwa mita kama kumi hivi toka lilipo gari, “jamani meneja yupo wapi, tuna chelewa?” alisema mmoja wa watu waliokuwa ndani ya gari wote walikuwa wame kaa kwenye cabin (mbele ya gari) “ngoja nika waitie” alisema mlinzi, huku anakimbilia kule kwenye jengo la meneja, lakini akufika mbali akamwona meneja anaingia kwenye gari, hivyo yeye aka elekea kwenye kile chumba kidogo chenye simu, na kuitoa kuuri kwenye lock ya mlango wa kile chumba kisha aka tulia kidogo magari yaondoke, ili atakapo waungia wakina Edgar, ata kama wakipiga kelele zisisikike kwa mtu yoyote,
Nikweli gari la meneja lilitangulia mbele ya gari kubwa la mizigo lililobeba marobta ya majani ya chai, na safari ikaanza, hapo hapo mlinzi hakupoteza muda aka kimbilia pale kwenye kibanda kisha kwatahadhari kubwa aka choomeka komeo kwenye tundu lake na kuvesha kufuri taratibu, alafu akalibanakisha akaondoka kwa nyata, na kwenda kukaa mita kama hamsini hivi toka kwenye kibanda, “ngoja nisubiri mshiko wangu, nyie mtajijuwa wenyewe” aliwaza mlinzi, ambae alisha kifunga kile chumba alicho waacha wakina Edgar. itaendelea…… hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata