: BIKIRA YA BIBI HARUSI (62)

SEHEMU YA SITINI NA MBILI (62)

ILIPOISHIA SEHEMU YA SITINI NAMOJA (61) , “ebu punguza mwendo” alisema Kingarame na Hokololo aka fanya hivyo, mpaka magari ya wenzao yalipo wakuta, na kuwapa iishara ya kusimama, kiisha SSP Kingarame akaitwa na wakuu wenzake, wakijitenga pembeni na kuanza kikao kifupi pembeni ya barabara, “SSP Kingarame unaweza kutuambia kwenye kiwanda cha chai ulifwata nini” aliuliza RPC Ruvuma kwa sauti kavu na ya chini, awakutaka wale askari wadogo wasikie maongezi yao, endelea ……….
Nikama Kingarame Alisha andaa jibu, “nilipata taharifa ya kuwepo kwa jambazi Edgar kule kiwandani, vipi kwani kuna tatizo?” aliuliza Kingarame akijifanya kushangaa jinsi RPC Iringa alivyo hoji juu ya utendaji wake, “iliitaji kiasi gani cha fedha, kutujulisha?” aliuliza RPC Ruvuma kwa sauti ile ile ya chini, “ilikuwa lazima nifanye hivyo, sababu nimeona kuwepo dalili za askari weu bahadhi kufichua siri zetu kwa majambazi, hivyo nikaamua kufanya shambulio la kushtukiza” lilikuwa jibu zuri la kueleweka toka kwa Kingarame, makamanda wakatazamana, na kukubaliana kwa kichwa, kabla RPC Iringa ajauliza swali, “na huko kiwandani mme kutaje?” hapo Kingarame akaona itakuwa vyema akitoa jibu la kueleweka, maana akuwa na ujanja, ilikupata msaada wa kumsaka Edgar na mwenzake, pale mjini, “tena hizi mbio nilikuwa nawai kuja kuwapa taharifa hii, sababu tukichelewa tu majambazi wanahama mji, sababu wame toroka kule porini na gari la mizigo” aliongea Kingarame, wakati huo huo Kisona na wenzake walikuwa wana katiza eneo lile na kusimamisha gari lao baada ya kuwaona makamanda wapolisi, na kuwasalimia kwa mbali, kisha wakaondoka zao.
Kwa taharifa ya Kingarame, makamanda wakasahaau kuuliza kuhusu Elisha, wakakimbilia kwenye magari yao, huku wakiwa wamegawana maeneo, OC FFU wa iringa alibakia na upande wa kaskazini, yani upende wa makambako, huku OC FFU Ruvuma akienda kuzuwia upande wa kusini yani njia ya kwenda songea, RCO Iringa alibakia kati kati kati ya mjini akifanya patrol kwenye barabara kuu, huku OC CID Iringa, akitembea chochoroni, karibu na stand, wakati OC CID, wa Ruvuma akijiunga na makamanda wakuu yani ma RPC wote wawili na RCO Kingarame kulitafuta gari walilopanda wakina Edgar, yani lile la kiwanda cha chai, kila kamanda akiwa na askari wakutosha, huku Kibabu akiwa na OC CID Iringa, na koplo Lusinde alikuwa na RCO Iringa, kila mmoja pamoja na askari wengine walio fahamu umuhimu wa kuwapata wakina Edgar, na kuchukuwa ushaidi kabla auja mfikia mtu mwingine, walikuwa wamejichanganya katika amakundi mbali mbali, ili kuakikisha wakina Edgar wana poteza maisha mala tu, wanapoonekana, na ushaidi wa video tape, unapatikana haraka sana, kabla aujawafikia wenzao, ambao wana weza kusababisha mtafaluku na wao kuingia jela.
Zilitumika dakika kumi kila mmoja kukaa katika anafasi yake, huku wakina Kingarame wakifika kwenye ghara kuu la kiwanda cha majani ya chai, ambapo walikuta gari walilo lifkilia lime wabeba wakina Edgar likiwa limesha ingia ndani, lakini aikuwa sababu ya wao kushindwa kujuwa chochote, maana walifanikiwa kuona nyayo za watu, walio onekana wameshuka toka kwenye gari moja ya magari hayo mawili yaliyotoka kiwandani, japo maeneja na wafanyakazi walikataa kuwaona watu hao.
Sasa basi wakiwa na uakika kuwa wawili awa wapo hapa mjini, makamanda walitawanyika na askari wao wakiingia mtaani kuwasaka watu awa walioamini kuwa ni majambazi, ***
Huku nako Serena Hotel , mama Monalisa akiwa pamoja na wenzake, wanaendelea kunywa pombe, alijitaidi kuizuwia hasira na chuki aliyo ijaza Moyoni mwake, juu ya mkwe mtarajiwa, kijana Erasto, ambae alisha mgundua kuwa kijana huyu ni mwingi wa habari, akika mume wake baba Mona alifanya kazi ngumu sana ya kumtuliza mke wake.
Lakini kama vile aitoshi, wakamwona kijana Erasto anainuka na kuelekea ndani ya jingo la hotel akitanguliwa na dada mhudumu, sijuwi kwaajili ya pombe, wazazi wa Erasto walionekana waki tazama na kukonyezana, wakimalizia na kicheko cha chini chini, na kuzidi kumjazama hasira mama Monalisa, ambae awakujuwa kuwa wamesha gundua mchezo wao mchafu, na kijana wao, akika uvumilivu ulimsinda mama Monalisa, amba ile anataka kuanza kuongeea la rohoni tu! Mala wakasikia, “samahani jamani eti kati yenu kuna mtu anaitwa mama Mona?” wote waka stuka na kumtazama mwongeaji, alikuwa ni mhudumu wa pale mapokezi, “ni mimi hapa kuna nini?” alijitambulisha mama Mona huku anamkodolea macho ya ulevi Yule dada mhudumu wa mapokezi, “kunasimu yako toka songea” alisema Yule mhudumu na hapo nikama alijuwa alicho itiwa, kwenyesimu, maana alichomoka mbio mbio, akifwatiwa na mume wake, wakiwaacha baba na mama Erasto na dereva wakiwasindikiza kwa mcho, wakikimbia mpaka mapokezi, ambako walikuta mkono wa simu bado ume wekwa pembeni, mama Mona ndio wakwanza kuinyakuwa na kuiweka sikioni, “hallow nani Mona?” aliuliza mama Monalisa, kwa shahuku ya kilevi, “hapana mama ni mimi, eti mama dada Mona amepiga simu, anasema hivi, yupo Njombe…” akika nikama huyu mama alishijkwa na waazimu, maana alikurupuka na kumtazama mume wake huku akiuacha mkono wa simu mezani, kisha aka mrukia mume wake kwa kumkumbatia, “Mona amepiga simu, twendeeee tuka mchukue” alisema mama Mona kwa sauti kubwa sana, sauti ambayo iliwashangaza karibu watu wote eneo lile, sauti iliyo mtumbulisha macho mume wake, kisha baba Mona akammwona mke wake anatoka nje mbio mbio, nay eye akaliunga kumfwata mke mke wake huko wanakoenda kumchukuwa Monalisa, ata walipopita eneo la vinywaji wakawaona wakina Misago wakiliunga na kuwafwata mbio mbio, “vipi baba Mona kuna nini?” aliuliza Misago huku yeye dereva a mke wake, wakijiunga na wawili awa ambao walikuwa wanaongoza kuelekea upande wa barabarani, “Mona amepiga simu, tuna mfwata” alijibu mzee Anderson huku wana zidi kupandisha kuelekea barabara kuu, na wakati huo huo wakapishana na gari la jeshi ambalo lilikuwa lina shuka kuelekea Hotelini, “mbogo ebu simamisha gari awa ni wazazi wa Yule binti, pengine wana taharifa muhimu” alisema Kisona, ambae aliweza kuwatambua licha ya kuwepo giza , na hapo hapo mzee Mbogo akaliweka gari pembeni, nusu awagonge watu wawili walio kuwa wanatelemka kuelekea kule serena hotel, huku wameshikana mikono, mala tu baada ya kusimamisha gari Wote wakashuka, huku wakiilock milango ya gari lao, na kuwakimbilia wakina baba Monalisa, ambao walipofika barabarani wakasimama, nikama walikuwa wanamtafuta mtu, au kitu, maana walionekana wakitazama, huku na huku, “Mona mwenyewe , yupo wapi?” hapo ndipo wakina kisona walipo gundua kilicho, waleta wanafamilia hawa huku barabarani, “mbogo uliwaona wale watu tuliopishana nao pale chini” aliuliza Kisona huku anageuka harakla kutazama chini, yani walikotoka,
“Sijuwi wana kimbilia nini mpaka wanataka kutugonga na gugari gwao?” aliuliza mmoja kati ya wale watu wawili walio nusulika kugongwa na gari la jeshi, ambaae alikuwa ni wakike, “lakini lile ni gari la jeshi na wale walioshuka ni wanajeshi wanawakimbilia wale raia, sijuwi wana nini?” alijibu Yule mwingine lakini kwa sauti ya kiume, huku wana kata kona kuingia kwenye eneo la serena hotel, wakipita “sikia Mona, wewe nenda kachukue chumba, alafu mimi nazunguka kwa nyuma” alisema alisema Yule kijana mmoja mwenye sauti ya kiume, kisha Yule Monalisa aka ongoza ndani ya jinge kubwa la hotel, akiwapita watu waliokuwa katika mijadala, ambayo binti huyu akuizingatia, akaingia moja kwa moja ndani ya Hotel na kulipia chumba, **
Wakati polisi wakiwa katika pilika pilika za kumsaka Edgar, mala kundi la RCO iringa, lililo kuwa lina fanya patrol barabara kuu, wakawaona wanchi kadhaa wakiwa pale barabarani, wakasogeza magari yao haraka sana karibu na wale wanachi waliokuwa wanashangaa shangaa bara barani, “wana shangaa shangaa, “mna fanya nini hapa” aliuliza askari mmoja ambae, aliruka toka kwenye gari na kutua karibu na mke wa Anderson, “kanal Kisona hapa nani mwenzangu?” tayari kisona Alisha mshika Yule askari mwenye sifa, na kumftua miguu, akipola silaha kabla ya kufika chini, kabisa aka msimisha na kuwa amesha mpiga namba saba, yani kabari, (roba) kwenye shingo ya Yule askari alie onekana kuwa na kimbele mbele, “hgrrr! Nai .. nitwa……..naitwa Mike” alijibu yule askari huku akiangaka kujipapatua toka kwa Kisona,…. Yaleo kweli fupi… ila itaendelea…… hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!