
SEHEMU YA SABINI NA MOJA(7I)
ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI (70) “siyo kukujeruhi, ni kuku uwa kabisa” alisema Lusinde, huku ana inua silaha yake na kuielekeza pale alipo lala yeye Mike, tayari kufyetua risasi, lakini hapo hapo ikasikika “pah!” Mike akijkuwa tayari amesha tandikwa risasi, “mamaaaa!” zilikuwa kelele za koplo Lusinde, alie tandikwa risasi ya bega, bahati alikuwa ame uvaa mkanda wa kubebea bunduki, (siling lifre) vinginevyo ingesha mdondoka silaha yake, ikasikika Risasi nyingine ambayoilimkosa kidogo, hapo Koplo Lusinde akatoka mbio, kuwa chochoro ambayo, mwanzo Mike alikuwa anaiwai, endelea ……
Huku risasi kama tatu hivi zikimfwata, na moja ikimjeluhi tumboni, koplo Lusinde ambae aliwai ule uchochoro, na kuishika bunduki yake, japo kwatabu Lusinde akaanza kujibu mashambulizi, kwa huyu mnoko ambae ameingilia mpango wake wakumpoteza askari mwenzie PC Mike,
Huyu mnoko alikuwa ni PC Daud, ambae sakika chache zilizo pita, baada ya kuachana na PC Mike alieomba aonyeshwe kituo cha polisi Njombe, alitembea kurudi kwenye lindo lake, alokowaacha wenzie, yani kwenye benk ya wakulima, lakini kabla ajaika mbali akastukla kusikia mlio wa risasi, kwanza aka tafuta maficho, akizania kuwa ndio wale majambazi wamesha vamia, kabla aja kaasawa akasikiarisasi ya pili, na hapo ndipo alipo pata bahati ya kuona ilipotokea, baada ya kuona mwale wa moto, yani kutu kama flash, ya mwanga wa camera, kule aliko tokea, ikifwatia kumwona mtu anatokea uchochoroni na kuuka barabara, huku akimwona yule askari alie jitambulisha kwajina Mike, akiwa chini ana galagala, hapo PC Daud akaona msaada wake unitajika, ili kuyaokoa maisha ya askari mwenzie, hivyo akaumia bunduki yake kumshambulia yule mtu alie kuwa ana mshambulia Mike, ambae sasa aliweza kumwona kuwa amevaa sale za jeshi la polisi, japo aliweza kumtandika risasi ya bega, lakini alimwona akikimbilia kwenye uchochoro wa nyumba zilizopo pembeni ya barabara, na kisha akaanza kujibu mashambulizi kwa kumshambulia na silaha yake, hapo ikaanza piga ni kupige, japo PC Daud aliona wazi kuwa adui yake alikosa uwezo wa kushambulia, sababu alisha mjeruhi, hivyo anashindwa kuimiliki vizuri siulaha yake, maana alionajinsi anavyo piga ovyo risasi, PC Daudi akaona kuwa huo ndio wakati wa kumshinda adui yake akaongeza mashambulizi, huku anasogelea pale alipo anguka PC Mike, akafanikiwa kumfikia, na kumuta kumsogeza sehemu salama, huku akijibu mashambulizi, kabla silaha yake aijagoma kupiga risasi, mwanzo akujuwa tatizo la silaha yake, lakini baadae akagundua kuwa risasi zime kwisha, kwenye magazine yake.
“Tutafanyaje Mike, nimishiwa risasi” alisema PC Daud, ambae alikuwa amepiga goti moja, pembeni ya Mike alie kuwa amelala chini, na maumivu makali ya begani na pajani, huku wakiendelea kusikilizia milindomo ya risasi toka kwa adaui yao, bahati nzuri Mike, bado alikuwa na mikebe miwili, ya risasi za akiba, aka chomoa mmoja na kumpatia Daud, ambae alibadirisha haraka na kujibu mapigo.***
Kumbe basi, wakina Kingarame tayari walisha sikia majibizano ya risasi, kwa hakiri ya haraka Kingarame akajuwa kuwa koplo Lusinde ame kutana na kikwazo kwa Mike, hivyo ni vyema kwenda kumsaidia, vinginevyo siri itafichuka na wao kuingia matatizoni, mala moja wali timua mbio kukimbilia kule walikohisi milipuko ya risasi ina tokea.
Nikweli, kwa dakika chache walizo tumia waliweza kulisogelea eneo la tukio, na kumwona PC Daud akijibu mashambulizi, aliyo yaelekezea gizani, kutokana na mwanga uliokuwa una mmulika askari huyu wajeshi la polisi, walimtambua mala moja, kuwa siyo Lusinde, na wala siyo Mike, “atakuwa nani yule mshenzi?” aliuliza Kingarame kwa kwa mshangao na tahadhari, huku yeye pamoja na askari wake wana kodoa macho kumtazama yule askari anaepambana, kukabiliana na mashambulizi afifu toka kwa Lusinde.
Kingarame alistuka zaidi, baada ya kumwona yule askari akiinuka pale alipo piga goti, huku akiwa ame mshika askari mwenzie, na kuanza kuelekea nae kwenye chochoro ya upande wakwanza ukiacha ile aliyo kuwa anashambulia, “anamsaidia Mike,” alinong’ona Kingarame, kisha akawageukia askari wake, “mnasiubiri nini nyie washenzi, shambauliaaaaa” hapo nikama alifungulia mbwa, maana ilifwattiamilipuko ya risasin iliyo miminwa kwa fujo, kuelekea kwa kina PC Daud na PC Mike, ambapo alionekana PC daud akianguka chini kama gunia, hukuMike akiwai chochoro yaupande wapili, “waini kabla ajafika mbali” ali[iga kelele Kingarame, hapo askari polisi awa wakaanza kukimbia kufwata kule alikoelekea Mike.
Na baada ya kuangaika kwa dakika kadhaa awakuona chochote, zaidi ya Koplo Lusinde, ambae walimkuta akiwa katika hali mbaya, kutokana na kujeluhiwa na risasi ya bega na tumbo, “mwaisheni hospital haraka” **
Wakati huo wale askari wawili waliobakia pale benk, matumbo yalikuwa yana watetemeaka kwa uoga, wakishindwa kujuwa wafanyeje, maana walijuwa wazi kuwa, mwenzao Daud na yule askari alie kuja kuomba msaada tayari wapo kwenye matatizo, waliamini kuwa majambazi wanao sumbua mjini huu wa Njombe wameshawavamia wenzao, wakati wanajadiliana la kufanya, mala wakaona magari ya polisi wenzao yanakuja, na kusimama usawa wabenk, wakashuka makanda toka kwenye magari hayo, ambao nao waliwatambua kutokana na vyeo vyao, unajuwa kwanini makamanda walisimama hapa, maana walijuwa wazi kuwa, benk uwa zina lindwa na polisi, hivyo ni vyema waka wauliza polisi hao, sehemu panapo tokea mapigano, “ni hapo mbele tu afande, ni mwenzetu alienda kumsindikiza askari mmoja hivi, alikuwa ajuwi kilipo kituo, sasa tu asikia mapigano” alisema askari mmoja, akielezea zaidi toka ujio wa Mike na kujitambulisha kwake, ndipo walipo mpatia mwenzao amsindikize, hapo makamandaawakut
aka kupoteza muda, waliingia kwenye magari yao na kusonga mbele, kuelekea eneo la tukio.
Sekunde chache ziliwatosha, makamanda awa kufika eneo la tukio, ambapo walimkuta SSP Kingarame akiwa na askari wake, wanalipekua eneo ambalo waliamini kuwa PC Mike atakuwa amejificha, “vipi kingarame nipe report” alisema RPC Ruvuma, kabla ajaona mwili waskari alie lala pale chini, “kwakweli afande leo nime amini kuwa kuna wenzetu wanausika na ujambazi huu” alisema Kingarame, kwa sauti ya masikitiko, na kuweka kituo kidogo, wakati huo sajent Kibabu alirudi haraka sehemu ile, na kumtazama Kingarame, ambae alikuwa anazungusha macho yake kutazama askari walio kuwepo eneo lile, mpaka maco yake yalipo kutana na macho ya Kibabu, ambae alimwonyesha ishala flani ya mafanikio, maana ali chezesha kichwa chake, taratibu juu chini, kama vile vile anaitikia,
“inamaana, huyu askari ame uwawa pia?” aliuliza RPC Iringa, kwa mshangao mala baada ya kuuona mwili wa PC Mike alie kuwa amelala pale chini, “siyo huyu peke yake, kuna mwingine amekufa sasa hivi, wakati tuna jiandaa kumkimbiza Hospital, anaitwa Koplo Lusinde” hapo atawaleaskari wenginewalio kuwepo toka mwanzo wakashangaa, sababu kwhali aliyo ondokanayo Lusinde inakuwaje afe, wakati alikuwa katika hali nzuri tu, siri kubwa alikuwa nayo Kibabu, ambae alishirikiana na askari wake wawili, kumnyonga Lusinde, kama alivyo agiza Kingarame, “mungu wangu” ilimtoka RPC Ruvuma, kwa sauti ya mshangao, huku wote wakigeuka na kutazama nyumba yao, yaninupande wabarabarani, ambako waliwaona askari wawili wakiwa wamebeba mwili wa koplo Lusinde, ambae alikuwa ametumbua macho na kutoa ulimi nje, “kama msipo mjuwa jambazi halisi, tegemeeni kushuhudiavifo zaidi” RPC Iringa alikumbuka maneno hayo, ya kanal Kisona.
“Unaona afande, yani PC Mike, amemshambulia huyu askari, na pia ame muuwa koplo Lusinde alafuamekimbia” alisema Kingarame kwamachungu makubwa, huku anajuwa wazi kuwa Mike atakuwa mzima,na lazima atafutwe ili auwawemala moja kabla ajatoa siri.
“Ok! miili ya askari ya ipelekwe Hopsital kuifadhiwa, na msako uendelee, akikisheni mntampata Mike, akiwa mzima” alisema RPC Iringa kwa sauti yenye machungu makubwa, “ila basikwa yoyote anae jijuwa kuwa anausika, na hili, ajisalimishe mapema, kabla atuja mng’amua sisi, akika lazima utajulikana tu” kwakeli yalikuwa ni maneno yaliyo ambatana na sauti yenye hasira kali sana, toka kwa RPC Iringa, “mpuuzi, utampata nani” aliwaza Kingarame, huku akitabasamulia pembeni.
Hapo Kingarame na askari wake wakatawanyika na kuelekea ndani ya chochoro za mitaa hii, ya mjini wa Njombe, huku makamanda nao, wana elekea hotelini, kila mmoja akiumiza kichwa jisni mambo yalivyo kuwa yanaenda.**
“Nimshenzi sana huyu Malaya, yani anajifana kujishana na mimi” alisema Erasto kwa sauti ya hasira, huku akivua nguo zake zote, na kupanda kitandani, na kufwatiwa na mpenzi wake mpya, dada mhudumu, ambae alisha liua ile taulo, na kuwa mtupu kabisa, “tatizo mpenzi wangu una hasira sana, subiri asubuhi, nitamweleza kuwa alicho kifanya siyo kizuri” alisema dada mhdumu kwa sauti ya kubembeleza, “kesho na mwambia meneja wenu, kama kazi yenu kutukana wateja, tutajuwa hapo hapo” aliendelea kuongea Erasto, kwasauti ya juu.
Sauti ambayo ilifika chumba chapili, yani chumba namba kumi na saba, chumba ambacho Edgar alikuwa ndani yake amekaa kwenye kiti, ana mtazama Monalisa alie kuwa amelala kitandani, na usingizi umesha mpitia, na kutokana na uchovu aliokuwa nao, alikuwa anakoroma vibaya sana, Edgar alitabasamu kidogo, na kukigeuzia kiti upande wa dirishani huku akifuniua panzia, akiweza kuona nje kama kulivyo, Dakika tano baadae Edgar kiwa ame kaa pale kwenyekiti, akajikuta anaanza kusinzia, hii nikutokna na usingizi wa siku tano.
Wakati huo huo, chumbani kwa kina mama na baba Mona, wanandoa awa walikuwa bado awaja lala, “umeona sasa, kumbe Mona alisha mjuwa huyu kijana, kuwa siyo mstaharabu, ndio maana alikuwa anamkataa” alisema baba Monalisa, wakatiwakiwa kitandani yeye na mke wake, “yani kuna umuhimu w kuwasikiliza watoto kile wanacho kisema, pengine Mona alisha shuhudia uchafu mwingi wa huyu mshenzi, sijuwi kesho watatutazamaje awa watu” alisema mama Monalisa huku akimaliia kwa kicheko, “yani mimi nashukuru kuwa, wamesha juwa kuwa tunajuwa” alisema baba Monalisa, na mke wake akauliza “kama wame juwa?” “si wata kuwa kuwa hakuna cha pete wala uchumba?” alisema baba Mona kwa kujiamini, “hiiwewe nawajuwa wwatu wabaya wasivyo na haya, siku zote, wepesi wakuomba msamaha, utayaona kesho yanavyo kuja na kujiliza liza” alisema mama Monalisa, akionyesha kuwachukia rafiki zake na mipango yake ya kumwozesha mwanae kwa Erasto.
Uwezi amini upande wapili, yani chumba cha baba na mama Erasto, wao walisha pitiwa na usingizi, wkiaminikuwa kesho wata yaweka sawa bila wasi wasi wowote, , mi naona tuachane na wanandoa hawa familia rafiki, twende zetu nje ya hotel.***
Kisona na watu wake bado walikwepo eneo hili, linalotumika kwa vyakula na vinywaji, sasa akuna alie kuwa anakunywa wala kula, watu walisha ondoka wote, nazani ni baada ya kusikika milipuko ya risasi, ya mala ya mwisho, “ni uhimu kama tuta pata jibu, la hii milipuko ya risasi” alisema baba Edgar huku akimtazama Kisona, “nikweli ndio maana tupo hapa, tuna subiri jibu” alisema Kisona, ambae wakati huo huo nikama alikumbuka kitu, “Mbogo, ebu nenda kapige simu kwa mkeo, uliza kama ameonge na Edgar” lisema Kisona na hapo nikama mzee huyu alikumbuka kuwa akuwa ameongea na mke wake kwa siku hile, hapo wote wawili wakainuka na kuelekea mapokezi, “nyie nendeni mkapumzike, kesho mapema sana tukutane nje” alisema Kisona, akiwa anaelekea mapokezi mzee Mbogo akiwa mbele, nandie wakwanza kuanza kuitumia simu.
Wakati huo huo, waka sikia muungurumo wa magari ya polisi, yakiingia na maeneo yale ya Hotel, “safi mke wangu, za huko?” alisikika baba Edgar akiongea, pasipo kusikika upande wapili, “mh! mbonaunaonekana una furaha sana leo?” aliuliza bab Edgar, akionyesha kuwa kubadirika sura yake, na kuwa yenye tabasamu la furaha, “hapana ajaniambia” alisema mzee Mbogo, huku akimtazama dada mhudumu, ambae mida hii walimkuta ana jiandaa kupumzika, “ok! ….kwa hiyo ajasema wapowapi?…. dah!…tatizo polisi wana wasakavibaya sana, na pia Njombe ni ndogo” aliongea baba Edgar safari hii akimtazama Kisona, ambae alikuwa anafwatilia maongezi na kuya kadilia maneno ya mama Edgar, “sawa … sasa akipiga simu mwulize yupo sehemu gani na mwambie asiondoke atusubiri, na sisi tunaendelea kumtafuta” alimalizia baba Edgar, na kukata simu, wakati huo makamanda wapolisi walikuwa wanakatiza pale mapokezina kuelekea juu, yani ghorofa ya tatu, “eti! dada kuma mama alipiga simu hapa kuulizia mzee Mbogo?” aliuliza baba Edgar, huku wote wawili yani yeye na Kisona, wakimtazama mhudumu wa mapokezi, “samahanibaba yangu, nikweli zilipigwa simu mbili, moja ya mama mmoja hivi, na nyngine ya kwako, linichnganya mlevi mmoja, mpaka nika sahau kukuambia” alisema dada wa mapokezi, “kwa hiyo mama anasemaje?” aliuliza Kisona, baada yakuona kuwa akuna jibu litakalo wasaidia, kutoka kwa huyu dada, “anatasema kuwa ameongea na Eddy, ame mwambia kuwa, wapo hapa Njombe, na walikuwa wanatafuta sehemu ya kupumzika” alijibu baba Edgar, wakati huo Kiosna alikuwa ana anza kubonyeza simu, akidikanamba za nyumbani kwake ili aongee na mke wake, “ok! we nenda kapumzike, mimi naongea na mwanao, maana najuwa atakuwa bado aja lala anasubiri simu kuroka kwangu” aliongea Kisona akimaanisha kuwa, anataka kuongea na mke wake, ambae ni sdoctor Elizabeth Leonard, na mmiliki wa hospital kubwa sana mkoani Ruvuma na kanda mzima kusini, BETHALEE HOPSITAL.
Mzee Mbogo akaondoka kuelekea chumbani kwake, akimwacha kanal Kisona akiongea na mke wake, ambae akutumia mudamwingi sana, kutokana na kuwa muda ulisha kwenda sana, na kuwa usiku mwingi.
“eti dada ule ugomvi ulikuwa wanini asa?” aliulizaKisonabaada ya kumaliza kuongea na simu, “yani we kka angu haha tu, miulevi hii” alisema yule dada, na kuaza kusimulia jinsi ilivyo kuwa, “kunabinti mmojamzuri mzuri hivi amechukuwa chumba, nazani kipindi kile mme kimbilia juu, maana kuna mama aliongea na simu kisha akatoka mbio mbio, yule binti alisema yupo na mpenzi wake, sijuwi huyu mlevi alimwona yule binti akamtamani, na wakati mwenzie yupo na mpenzi wake, maana alikuja hapa amefura kwa hasira, eti wanavyofanya mapenzi wanapiga kelele” alisema yule dada wa mapokezi, na wote wakacheka kidogo, “atawewe una mjuwa mwanamke mzuri?” aliuliza Kisona kwa utani, “unazani kaka huyu dada ni mrembo, japo ajavaa nguo nzurisana, lakini mzuri, na sijawai kumwona hapa Njombe” alisema dada mhudumu, huku ana funua kitabu cha wageni, “huyu hapaanaitwaaaa.
.. Monalisa.. sijuwi nani maana jinalake la mbele lakizungu, utamwona kesho akichelewa kutoka” alisema yule dada huku akishidwa kulisoma jina la mbele la mtejawa chumbanamba kumi na saba, ok! mdau endelea kutembelea hapa hapa,
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU