BIKIRA YA BIBI HARUSI (75)

SEHEMU YA SABINI NA TANO (75)

ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA NNE (74) Makamanda naaskari waliokuwepo nje, ambao walikuwa wame tega masikio yao, kusikiliza au vijana wakimalizia kuwa uwa majambazi kama watakuwa wame jeruhiwa, basi walitarajia kusikia “fande tume wapata”nikweli wakasikia “chumbani hakuna mtu…” sauti hiyo ilifwatiwa na kishindo cha mtu akianguka toka ndani ya chumba hicho namba kumi na saba, alafu sekunde kama mbili mbele ikasikika “pah! pah! pah!” tOka ndani ya chumba hicho hicho, namba kumi na saba, alafu vishindo vya watu wakianguka, hapo makamanda wote wakatazama, kwa mshangao, ENDELEA…………
Huku Wengine wakianza kutafuta pakujificha, wakati huo wakamwona askari mmoja anatokeza kwenye malango wa kile chumba, wote wakatabasamu, wakijuwa kuwa tayari madui zao wamesha uwawa, lakini ile kutaamaki wakamwona anaanguka chini puuuh!, akifikia kifudifudi, yani aliangukia tumbo, huku akijipigiza kichwa chini kwanguvu, akionyesha mtu huyu, akuwa na uwezo tena wakijimiliki, (contorl) na hapo ndipo walipo pata nafasi ya kuona damu nyingi zikiwa mgongoni mwake, “huyu mtu hatarisana, lazima atakuwa na mafunzo ya juu ya kivita” alisema RPC Iringa, kwa mshangao, “honyo lamwisho, mnatakiwa mjisalimishe wenyewe kabla atuja ingia hatua ya pili” alisema OC FFU kwa sauti ya juu, lakini safari hii, wakasikia jibu, toka ndani ya chumba namba kumi na saba, ambacho kwa sasa kilisha kuwa chakavu, “sisi siyo majambazi, kama mnavyosema” ilikuwa sauti ya Edgar mwenyewe, “kwanini sasa unakataa kujisalimisha” aliuliza RPC Iringa, akitokea mbali kidogo, “hakuna mpumbavu anae weza kujitokez mbele ya watu wanao taka kumuuwa” kwa jibu hili wawili hawa walitazamana, wakiukubari ukweli huo, “tutaongeza nguvu zaidi kama utaki kuji salimisha” alisema OC FFU, nina SMG, na magazine nne” alijibu Edgar, tokea ndani,
Kumbe basi, muda ule baada ya Edgar kuwashonarisasi wakina Kibabu, na kumchukuwa Monalisa, waliungamlango kwa ndani nakukimbilia bafuni, wakichukuwa begi la Monalisa lenye mkanda wa video wenye ushahidi, nikama walijuwa maana wakasikia milindimo mingi ya risasi, ambayo aikuwazuru, maana walikuwa bafuni wakikingwa na kuta imara za jengo hili, na ndipo walipo ina askari wanne kukagua chumba kile, ambao baada ya kuangalia pale chumbani na kuona hakuna kitu, mmoja akawa ana elekea bafuni, huku mwenzie anatoa repoti kuwa hakukuwa na mtu, ndipo Edgar alipo mchapa risasi yule alie ingia bafuni na kuichukuwa SMG yake, na wakati wale wengine wana gutuka na kutaka kushambulia tayari walisha chelewa, maana wali tandikwa risasi moja moja, huku huyu mwingine akidondosha silaha yake na kujaribu kuokoa maisha yake, kwa kutoka nje, akiwa amesha lambwa lishasi ambayo ilipenya mgongoni na kwenda kuchezea maini,
“atuitaji utani wako, sisi tuna taka ujisalimishe” alisisitiza OC FFU, maana yake maongezi yaliendelea, “hakuna anae tania mbele yakifo” alijibu Edgar, huku watu wote wakisikiliza, “tuna kuakikishia hakuna atakae kushambulia endapo utajisalimisha mwenyewe” safari hii alisema RPC mwenyewe, hapo Edgar alicheka kidogo, kiasi cha RPC kuchukia, maana aliona kuwa huyu kijana anamfanya yeye mpumbavu, “na juwa shida yenu ni hii video, mkiipata mtuuwe, lakini na waambie ukweli, akika sito iacha mpaka niakikishe naifikisha sehemu usika, na kila kitu kinakuwa wazi” kauli hii iliwastua ma kuwa shangaza watu wote waliokuwepo mahali pale, awakujuwa kuwa Edgar ana tazama jinsi ya kupanda kwenyedirisha ladogo lla bafuni, lililozibwakwa vioo, pasipo kuwa na nondo, ili watoroke,
Kati yawalio stuka ni kingarame, yeye alistuka kuliko mtu yoyote pale, koridoni “askari wote lindeni mlango, mmoja alete mambomu ya moshi wa kulevya, kikisheni atoki mtu hapo, akitoa pua tu, tandika risasi” yalikuwa ni maneno yaliyo ambatana na sauti kari yenye kilo nyingi za hasira, toka kwa Kingarame, huku wenzie wakitafakali maneno ya Edgar,
“Inamaana wakina Edgar ndio walilala humo jana?” alijiuliza Erasto, alie kuwa chumbani kwake, amesha jikojolea zaidi ya mla mbili, na ilibakia kidogo asushe kubwa, kufwatia misuzi aliyomkuwa anaitoa mfululizo, “na zile kelele za …….., mama yangu tayari amesha mnaniii.” Erasto alijikuta na tamani kuangua kilio, hayo yalikuwa ni mambo ya ndani ya chumba namba kumi na sita, kwa bwana Erasto Misago.
Wakati huo huku koridoni, askari mmoja alinekana akijiandaa kurusha bomu ndani ya chumba namba kumi na saba, huku makamnda wa kuu wakinong’ona wakijadiliana juu ya maneno ya Edgar, kwamba wao wanataka wapate video, ndipo wamuuwe, “rusha haraka hili bomu, unangoja nini wewe” alipaza sauti Kingarame, akimkoromea yule askari, aliseshika bomu, kwamba alikuwa anafanya taratibu, “stooooop” ilisikika sauti kali ya kikamanda, toka upande wa mapokezi, wote waka geuka haraka, na kutazamanyuma, tani upande wamapokezi, wakishangaa nani alie sema stop, wakati wakuu wa jeshi hili wapo hapa, “we kanal, unazuwia ukiwa kama nani, wakati kuna wakuu wako hapa” alisema Kingarame kwa hasira, akimkazia macho Kisona, ambae alionekana akija mbio mbio na kujipenyeza kwenye kundi la askari polisi akifwatiwa na askari wake, wa tatu, wa jeshi la ulinzi walio shika silaha zao mikononi, wakionekana wapo tayari kwa lolote litakalo takiwa kufanyika, “naomba uwe mpole Kingarame, ilijambo limesha fikia mwisho, yiyo inabidi tuwate utaratibu wa kuwakamata hao waalifu, au ume sahau kuwa yupo na mateka, humo ndani” alisema Kisona, kisha akamgeukia RPC, lakini kabla hajaonge neno lolote, ikasikika sauti ya mama Monalisa, “tusaidie baba wamewashambulia kwa risasi nyingi sana” alisema mama Monalisa akimwambia Kisona, ambae aliingia nae humu ndani wakati anaingia, akiongozana mume wake, na wenzao wakina Misago, “kanal unajuwa kama nikosa kuzuwia utendaji wapolisi?” aliuliz RPC Iringa, kwa sauti kali ya mkwala, “ilo lipo wazi, lakini unajuwa kuwa, ni kosa kuwashambulia watu wasio na hatia?” aliuliza Kisona kwa sauti kavu, tofauti na RPC aivyo mzowea mtu huyu, “nani anathibitisha huyu jambazi kuwa hana hatia, na watu alio wauwa, hiyo siyo hatia?” alisema RPC kwasauti ya juu na kali sana, “RPC alikuwa anajilinda, pia syo kwamba yeye ndie alie uwa askari wote, nilikuambia usipo mjuwa jambazi unae mtafuta, utaapoteza wengi” alisema Kisona kwa sauti ile ile kavu, “thibitisha Kanal vinginevyo unaingia hataiani kwa kushilikiana na majambazi” safari hii alisema OC FFU, na Kisona akacheka kidogo, “jana umeshuhudia mashambulizi mangapi hapa mjini, na wame uwawa watu wangapi, sasa muda wotewa mashambulizi awa vijana walikuwepo humu ndani, je ninani aliefanya mauwaji jana usiku?” aliuliza Kisona huku akimtazama OC FFU, ambae alikosa jibu, akabaki anatazamana na wenzake, “najuwa yupo mwenye jibu kati yenu, lakini hawezi kujibu sasa hivi” safari hii Kisona aliwatazama mmoja baada yamwingine, wote wakawa kimya, “baba na mwanangu yupo ndani” alisema mama Monalisa, huku akimgusa gusa Kisona begani, maana aliona kuwa huyu ndie mkombozi pekeewabinti yake, kutoka kwa hawa wanyagati, “onasasa, mki muuwa na binti aliepo humo ndani, alafu baadae mseme kuwa ameuwawa na majambazi” alisema Kisona, huku akimtazama RPC, unajuwa kwanini Kisona alikuwa anaongea sana, ni sababu alikuwa ana vuta dakakika gari lapili la askari wa jeshi la ulinzi, liingie na ndipo wakina mapombeka wataingia mle ndani, ili kuwashinikiza makamanda awa wasitishhe zoezi la kuwashambulia wakina Edgar, mana gari hilo waliliacha mbali sana, kutokana na mwendo kasi waliotembea wakina baba Edgar, na ukizingatia nguvu kubwa ya askari wake ilikuwa bado aija ingia.
Huko ndani Edgar na Monalisa, walikuwa wanasikia kila kitu, na kujuwa kuwa msaada umesha fika, “unaongea upuuzi gani Kisona, unajuwa kuwa sisi tupo kazini?” alisema RPC Ruvuma kwa hasira, na wakati huo huo Kingarame akadakia, “afande huyu anal eta mchezo” alisema Kingarame, kisa akamgeukia yule askari mwenye bomu, “we costable ebu warushie ilo bomu” alisema Kingarame akimwambie yule askri mwenye bomu mkononi, “we! constable usijaribu kurusha ilo bomu” alisema Kisona kwa sauti ya juu na ya ukali, kihasi cha kuwashangaza ata wale makamanda, na kuwa jaza hasira, Kisona akatabasamu kidogo, nikama aliona kitu flani kizuri mbele yake, “hivi Kanal unajiona wewe ndio nani sisi tume shuhudiaaskari watano wanauwawa hapahapa, alafu wewe unasema tuhache, sasa naongea kama RPC, na mkuu wa zoezi hili, constable…” kabla hajamalizia kisona akadakia, RPC, hatua mojaatakayoifanya huyu askari, italeta mahafa makubwa mahali hapa, kabla auja funga maisha kusaidia ujambazi wa askari wako” ilikuwa kauri ya ukali toka kwa kisona, makamanda wakabi midomo wazi, wakisngaa huyu jamaa jeuri anaitoa wapi, “Kisona, ondoka hapa kabla sija amulu askari wangu wakukamte” alisema RPC Iringa kwa sauti ya jazba iliyo ambatana na kitetemeshi, “nikiondoka hapa nikwaachaawa vijana na ushaidi walionao, nitakuwa nimeshindwa kutkeleza amri ya kazi niliyopewa na wakuu wangu” hapo RPC Iringa aka inua uso wake kutazama mbele zaidi, akaona askari kazaa wa jeshi la ulinzi, wakiwa wame shika vyema silaha zao, akageuka nyuma akaona hivyo hivyo, hapo aka shusha pumzi ndefu, “haya bwana kanal unataka kutuambia nini?” aliuliza RPC Iringa, kwa sauti ya kukubari matokeo, “afande analolote huyu anataka kumlinda huyu jambazi” alipayuka Kingarame, lakini RPC aka akamtuliza, “ebu tumsikilize kwanza” maneno haya ya RPC, yalimfanya Kingarame, aone kuwa karibu mwisho wake unawadia, “kisona tuna kusikiliza wewe, kama hauna lolote, tuhache sisi tuendelee na kazi yetu” alisema alisema RPC huku kimtazama Kisona, “kwanza kabisa hawa vijana siyo majambazi, japo wamesha sabishabahadhi ya vifo vya askari kadhaa, hiyo ilikuwa ni kujilinda, wasi uwawe, hukuvifo vingi vikifanywana askari wako ambao siyo waadilifu, ambao walitaka kuwauwa awa vijana nakuchukuwa ushaidi wa mkanda wavideo ambao walipewa na marehemu Lukas, ambae nae alitajwa kuwa ni jambazi, kumbe ni mpiga picha alie shuhudia tukio la ujambzai la pale NMC songea” mpaka hapo makamanda na askari walikuwa wanatazamana, kwamshangao, uku Kingarame akitazama huku na huku, akitazama uwezekano wa kuondoka “una uakika Kisona, au unataka kutupotezea muda” aliuliza RPC songea, kwa mshangao, “ndio nina uakika, tena ata jana usiku kuna askari wenu mmoja anaitwa Mike, alitaka kuuwawa na hao askari walio shiriki ujambazi NMC, wakiofia kuwa ata fichua siri, babaada yake mimi nilimwokoa, na alie taka kumuuwa ni koplo Lusinde, ambae alijeluiwa na askari mlinzi wa benk, ambae alishambuliwa na polisi wenzenu” alisema Kisona na hapo hapo Kingarame akadakia Kingarame, “tena huyu unae mtaja ndie jambazi mkubwa” hapo hapo wakasikia sauti toka nyuma yao upande wa mapokezi, “hapana afande, wewe ndie nausika na haya yote” hapo askari na makamanda wote wakageuka kutazama kule ilikotokea sauti hii, wakamwona Mike, akiwa anatembelea gongo, taratibu akiwasongelea, pale walipo, na nyuma yake wakionekana mapombeka na wenzake watatu, na bwana mandevu yani Ngigo, ambae alikuwa anapingu mikononi mwake, RPC Ruvuma na OC FFU wake wakamtambua mala moja, huku wazazi wa Monalisa wana gundua kuwa kweli kijana Edgar alifanya kazi ngumu kumlinda binti yao , mpaka leo hii wapo hapa, na kwamba akuwa ame mteka
Mpaka hapo Kingarame akajuwa hakuwa na pakutokea, akatazama kushoto na kulia, akiwaza amteke mmoja wao ili aweze kuondoka mahali pale, akajuwa akimteka askari, anaweza kumzidi mahalifa na kumgeuka, hivyo aka ona kimbilio lake ni mama Monalisa, hapo kngarame aka mshika mkono mama Monalisa na kumfutia kwake akimkaba kabari moja matata, huku akimwekea bastola kichwani, “wekeni silaha zenu chini haraka vinginevyo nita mfyetua huyu mwanamke

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!