BIKIRA YA BIBI HARUSI (77)

SEHEMU YA SABINI NA SITA (77)


ILIPOISHIA SEHEMU YA SABINI NA TANO (76) yaliyo sabaishwa na Erasto ambae hakuwa anajuwa kuwa, alicho kifanya jana usiku, kilionwa na wakwe zake watarajiwa,”namimi naenda” alisema Erasto huku akiingia kwenye gari na kufunga mlango, hapo hapo kila mmoja akaziba pua yake, kwa harufu ya mikojo yapombe, mbayo kijana huyu alijikojolea wakati wa milindimo ya risasi, endelea …….
Hakuna ambae akujuwa ile harufu ilipotokea, ila iliwabidi wakae kimya, sababu kuna mambo yamsingi yaliyo kuwa mbele yao ila kwa wazazi wa Erasto ilikuwa ni aibu kwao, awakuchelewa sana derea wa mzee Anderson akaondoa gari, aina ya nissan patrol, kuifwata barabara kuu, ambayo aliifikia maa moja na kukata kushoto kufwata uelekeo wa songea, kule magari mengine yaliko elekea, , mbele yao wakaliona gari la jeshi aina ya land rover mia na kumi, likiwa linatembe kwa mwendo wa kawaida tu, “hivi huyu kijana mbona anaonekana kama ataki kuwai kumwokoa mkea wangu?” alisema baba mona kwa sauti ya kukata tamaha, huku derev wao anakanyaga mafuta kwangu akibadiri gia , na kuzidi kukimbia kwanguvu, kiasi cha kulisogelea lile gari la jeshi, “au mzee Mbogo ndio ane mshawishi wasi mwokoe mama Mona?” alisema Erasto, “kwanini amshawishi hivyo?” aliuliza Dereva kwamshangao, “si, anamchukia mama Mona, toka alipoikamatabaru ya mtoto wao” alisema Erasto kwa sauti iliyo jaa chuki, pasipo kujuwa kuwa, na yeye amesha likoroga jana usiku, wakati huo walisha lisogelea kabisa lile gari la jeshi.
Wakati wanaongea hayo huku safari ikiendelea, mala wakaona lile gari la jeshi lina aanza kuongeza mwendo, dereva wao akaongeza mwendo pia, akiuwata mwendo wa mia na kumi land rover, lakini kila dakika ilivyoenda, ndipo walipo liona lile gari mbele yao, likizidi kuwaacha, zilikuwa nita ishilini zikawa hamsini, mala mita mia, kisha wakawa wanalionea mbali zaidi, huku likiwapote kwenye kona kadhaa, mwisho wake hawakuliona tena, “heee! lile ni gari au ndege?” aliuliza dereva, “huyu bwana namfahamu sana, anaendesha gari kama ameiba benk” alisema baba Monalisa, nawao wakiwa katika mwendo wa kasi **
Wakati hu mbele kabisa, kilomita kama tano, msafara wa magari sita ya polisi, yalikuwa yana sugua lami kulifukuzia gari, mbalo aliondoka nalo kamanda mwenzao wjeshi lapolisi, kitego muhimu cha upelelezi wa makosa yajinai mkoa wa Ruvuma, ambe wame baini kuwa, ni mhusika mkuu wa ujambazi uliofanyikasongea siku chche zilizo pita, pamoja na mauwaji ya raia na askari wao, ikionekana wazi kuwa sajent Kibabu na PC Hokololo, ni kati ya askari wanaoshirikiana na SSP Kingarame, sababu ukiahilia ukaribu wao ambao umedumu mpaka sasa, pia Kibabu ndie alie waingiza wakina Edgar katika tuhuma za ujambazi iliwaweze kufanya chochote, bila kuulizwa, maana ingeonekana kuwa, wanawasakama jambazi, ikiwa pamoja na kuleta majambazi wengine wawasaidie “sasa naelewa kwanini huyu Kisona, amepewa cho kikubwa kuliko umli wake” alisema RPC Iringa ambae gari lake lilikuwa lapilli, katika msafara huu, ulio tanguliwa na OC FFU wa Ruvuma, na nyuma yake alikuwepo, RPC Ruvuma, ambe alifwatiwa na OC FFU wa Iringa, OC CID Iringa na mwisho kabisa alikuwepo RCO Iringa, huku kila gari likiwa na askari wasio pungua watano wenye silaha zao mikoni, wakisikilizia mwendo mkali wa gari waliyo yapanda, wakiofia kupatahajari na kupoteza maisha yao, kabla ata awajampata wanae mfwata,
“tutampa kweli huyu, mbona mbele hakuna dalili ya uwepo wake?” aliuliza RPC Iringa, wakti huo walikuwa wamesha tembea kwa muda wa zaidi ya nusu saa, pasipo kuona dalili ya gari la Kingarame, “aande ahapa tunatembea mwendo wa kilomitamiana ishilini kwa saa, nimwendo mkali sana, nashauri tukikuta kijiji hapo mbele tuulize kwanza, pengine wamepita njia nyingine, alishauri dereva wa gari la RPC Iringa, na wakati huo walikuwa wame bakiza kilomita mbili, kuingia kitongoji cha Kifanya, na ndio wakati walipo shtuka wakipitwa na gari moja aina ya land rover mia na kumi, lenye rangi ya kijani, na namba za jeshi la ulinzi, ambalo awakupata shida kulitambua kuwa ni gali walilo kuwanalo wakina Kisona, “huyoooo! na yeye anaukuzia” alisema RPC Iringa, huku wakilishuhudia gari lile, liki zidi kuwaacha kamavile wao wamesimama, “hivi unatembea mwendo gani huo?” alisema RPC kw sauti ya kufoka, huku ana chungulia mwenye speed meter, akimwona pengine dereva wake ni mzembe, lakini RPC aliona mshale ulikuwa ume lala kati kati ya mia ishilini na mia halobaini, “he! huyu mzee ndio anaendesha gari namna hii?” aliuliza RPC kwa mshangao, “hakuna haja ya kusimama ebu ongeza mwendo nayule wambele ataongeza tu!” alisistiza RPC, na dereva wake akajaribu kuongeza mwendo, na yule wambelenae alipoona gari la nyuma lina mkaribia nae akaongeza, na wale wanyuma ya RPC nao wakaongeza mwendo, “kweli sijuwi ata nisemeje, huyu mshenzi ametutiaaibu sana, yaniSSP mzima anafanya ujambazi?” alisema RPC Iringa kwa masikitiko, na hayo ndio yalikuwa mawazo yaliyo mtesa RPC Ruvuma, “ukisikia kuaribiana ndio huku, maana lazima wata hisi kuwa, na mimi najuwa huu mchezo wa Kinrame” aliwaza RPC Ruvuma, sasa linamteka mama wawatu, ngoja akutane na huyu mshenzi mwenzie Kisona, amnyooshe” maneno hayo aliongea kwasauti RPC Iringa, na kumfanya dereva wakeacheke kidogo, wakati wao wana waza juu ya hayo, awakujuwa kuwa kuna bahadhi ya askari kwenye magari yao walikuwa wanawaza, jinsi ya kumsaidia Kingarame, ili awagawie mari alizo iba NMC, kama alivyo wahaidi jana usiku, ***
Wakati huo huyo Kingarame waliekuwa wanamzungumzia, alikuwa amesha pita Kifanya na sasa anazidi kuchanja mbuga, Hokololo, akikanyaga mafuta kwa nguvu zake zote, huyu ni kati ya madereva waliokuwa na sifa kubwa yaudereva wa mwendo kasi, katika madereva wapolisi wa mkoa wa Ruvuma, “tuta kuwatume waacha mbali sana” alisema Kingarame amba alikuwa amekaa upande wa mlangoni, huku mama Mona akiwa kati kati, sanjet Kibabu akiwa nyuma ya gari hili, japo alikuwa na jelaha kubwa la lisasi kweny bega lake la kushoto, alakini akuiacha silaha yake, “baba naombauniache, mume wanguan fedha nyingi, ata kupatia kihasi chochote utakacho itaji” lisema mama Monalisa, ambae alijona mwenye bahati mbaya, huku ana tetemeka kwa uoga, kwanza kabisa Kingarame akacheka kwa dharau, “usiwe mjinga we mwanamke, siwezi kukuacha mpaka niakikiishe nimefika sehemu salama” alisema Kigarame huku Hokololo akizidi kukanyaga mafuta, ilikuwa wakimbia wenzao, akiamini kuwa kwa speed aliyo kuwa anaenda, pasinge kuwana gari la kulikuta, “lakini kwanini wewe polisi mkubwa kabisa unakuwa jambazi?” alisema mama Monalisa, na kusababisha Kingarame amkate jicho la hasira, “ukiongea neno jingine, akika hao wanao tufwata, watakukuta katikati ya barabara, umesha kufa” alisema Kingarame kwa sauti ya kuogofya.
Baada ya kutembea kwa nusu saa nyingine, wakiwa katika mwendo mkali, wakawa wameshaingia lukumbulu,na kuanza kupambana na kona, wakiwa katika mwendo wa kasi, “tukifika MADABA, ebu ingia pale kanisani tuombe simu tuongee na Bosso, aamishe mzigo, kabla awaja izunguka nyumba yangu ya mahenge, tumkute barabara ya tunduru” alisema Kingalame, akiamini kuwa hakuna mtu wala gari litakalo wakuta, “tuwe makini sana, maana wanazaweza kurudi Njombe, kwenda kupiga simu songea, iliwatuzuwie” alisema Kingarame, huku safari hiki endelea, “ni orukatwe, na unyongwe, uoni ata aibu, umewasingizia watoto kuwa ni majambazi, na sasa umesha bainika” alisema mama Mona kimalizia na kiishindo cha kiofi lililo tuwa mgongoni kwake, “pumbavu nitakuuwa wemwanamke” alisema Kingarame kwa hasira, huku akimkazia mama Monalisa, alie jikunja kwa maumivu ya mgindo, ambao akuweza hata kujikuna, sababu mkono aukuweza kufikia mahali hapo,
Lakini wakati wanaendelea na safari yao, sijuwi kitu gani kili mtuma Hokololo atazame kwenye side mirror, maana ilekutazama, kwenye kioo cha pembeni cha kutazamia nyuma, kwambali kabisa juu ya kilima kioja, akaliona gari la jeshi, lil linalo milikiwa na Kisona na askari wake, likiwa kilomita kama mbili nyuma yao, likija kwa speed, mala lika zamakwenye mtelemko na kuibuka tena, japo lilikuwa mbali lakini Hokololo aliweza kugundua kuwa lile gari lilikuwa katika mwendo mkali sana, pengie ni mia themanini kwa saa, “afande yule mwanajeshi anatufwata” alisema Hokololo, huku anaongeza mafuta , “shenzi kabisa ebu tuwafanyie kituambacho, watajuta kuzaliwa” alisema Kingarame, huku anatazama kushoto na kulia, “ebu tafuta sehemu ya kuingilia polisi yenye maficho mazuri” alisema Kingarame, na Hokololo akafanya hivyo.
Mita mia na nusu mbele, wakaona njia afifu, iliyo ingia upande wa kushoto wa barabara kuu, pasipo kujari melemko uliopo sehemu ile, Hokololo aka punguza mendo kidogo na kukata kona kushoto, akiwa katikaspeed kali kidogo, kisha akaingia porini kama mita sabini hivi, kisha wakageuza gari na kutazama waliko toka, kisha wakazima gari, baada hapo wakagawana majukumu, wakti sajent Kibabu akimlinda mama Monalis, Kingarame na Hokololo, wakashuka toka kwenye gari wakiwa na SMG zo mikononi, na kujiteg tayari kwa lolote,**
Kumbe basi, wakati wakina kisona wakiwa nyuma ya wakina Kingarame, kwa kilomita mbili, katika mwendo mkali sana, mala ………wakti storyhii inaelekea mwisho jiandae kwa story nyingine tamu zaidi toka hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!