BIKIRA YA BIBI HARUSI (82)

SEHEMU YA THEMANINI NA MBILI (82)

ILIPOISHIA SEHEMU YA THEMANINI NA MOJA (81) ambae alibinya jicho moja, wote wakatabasamu, tabasamu ambalo lilonyesha pengo la SSP Kingarame, na wakati huo askari wengine pamoja na makamanda, wakaingia kwenye magari na kuondoka zao, huku OC CID akiingia kwenye gari la RPC Iringa, gari lake lilibeba watuhumiwa, likitanguliwa na polisi mmoja mwenye cheo cha koplo, wa kutoka iringa, alie ambiwa na RPC Iringa, endelea………
Mita mia moja mbele msafala huu uliwapita wakina Kisona, waliokuwa wanatembea kwa mguu, wakiwata uelekeo wa Njombe, RPC Iringa aliekuwa gari la tatu kukutoka nyuma, yani pamoja na lile gari walilo kuwa wanalivuta, ambalo ndani yake alikuwepo OC FFU wa Ruvuma, aka mtazama Kisona, wakati huo kanal mwenye umri dogo Kisona, alikuwa ana mtazama Kisona, alie kuwa ndani ya gari, macho yao yakagongana, kisha Kisona akatikisa kichwa taratibu juu na chini, kama vile alikubari jambo flani kuwa linaenda sawa, mwendo ulikuwa wa wastani kutokana na yalemagari yaliyo kuwa yanavutwa, maanamengi yao matairi yalitobolewa, “afande kwanini umeshindw kuelewanana yule kanal, unajuwa kuwa jamaa ana uelewa mkubwa wa mapigano, na uwa ana mtazamo wa mbali sana” alisema OC CID wa Iringa, kwa sauti yenye tahadhari kubwa, RPC akatabasamu kidogo, “ukitaka umjuwe adui yako, jifanye chizi kidogo” ilindilo jibu la RPC kwenda kwa OC CID, na OC CID, akuelewa kitu, wakati huo huo wakashangaa kuona magari yana simama, walipotazama vizuri, wakakumbuka kuwa mahali hapa, nipale walipo lipita gari la jeshi la ulinzi, yani lile la wakina Kisona, maana waliwaona bahadhi ya askari, yule mama alietekwa na mume wake, binti yao, pia walimeona Edgar na mzee Mbogo, dereva ambae uendeshaji wake wa gari uliwashangaza wengi sana.
Ikabidi washuke ili kuona kuna kitu gani, kilicho simamisha msafara, makamanda na askari wote, wakaduwaha kuuona mwili wa sajent Idd Kibabu ukiwa ume lala kwenye kijito cha damu, pembeni ya barabara, “hoofff! huu ndio mwisho wa udharimu” alisema RPC Ruvuma, kabla OC FFU ajaongezea neno, “haya pakizeni kwegari haraka” amri hii ilitekelezwa haraka sana, mwili wa sajent Kibabu ukapakizwa kwenye gari ambalo lilibeba miili ya wale askari wengine, walio poteza maisha.
kwaupande wa Kingarame alistuka na kujawa na hofu kubwa, kwa jinsi askari wake alivyo fanywa, maana aukiachilia yeye kufanya mauwaji mengi ya kikatili, lakini hili la Kibabu lilikuwa kiboko, ukiachilia sehemu ya tumbo, iliyoonyesha kufujwa damu nyingi, lakini shingoni, palionesha wazi kuwa pame pitishwa kisu maana jelaha kubwa sana lilionekana, likiwa na damu mbichi kabisa, huku kichwa kikining’inia, kama mbuzi ane enda kuchunwa ngozi.
“pumbavu umekutana na wanaume” alining’ona RPC iringa, huku wanarudi kwenye magari yao na kuendelea nafari pasipo kuwaongelesha chochote, wale walio wakuta sehemu ile, yani mzee mbogo, mzee misago dereva, Edgar na Monalisa, na askari wawili wa jeshi la ulinzi, na wakati huo huo wakina kisona walikuwa wana tokezea eneo hilo. ***
Makao makuu ya jeshi la polisi, palikuwa pame zizima, maana ilishitushwa na habari hii ya kingarame kushiriki ujambazi na kusingizia wananchi, yani raia wema, mkuu wa jeshi hilo la polisi yani nspector general, alisha pokea pokea simu tatu, yakwanza kabisa ilikuwa inatoka kwa waziri wa mambo yandani, yapili toka kwa waziri mkuu, yatatu toka kwa rais mwenyewe, wote walikuwa wanaitaji maelezo kamaili na hatima ya operation hii, yani kama hao polisi walio usika kwenye tukio la ujambazi wamesha akamatwa, au kuthibitiwa kivyovyote vile, jibu ilikuwa moja tu, “bado atujapata ahalifa kamili, na sisituna jiandaa kwenda Njombe, tukifika tutatoa taharifa kamili” nikweli IGP, wakipindi hicho alikuwa anaelekea kwenye uwanja mdogo wa helcopter, uliopo mle ndani ya eneo la makao makuu ya jeshi lao, la polisi, akiongozana na mkuu wa upelelezi wajeshi la polisi, Tanzania nzima, na mkuu wa FFU Tanzania, pamoja na askari wao walioshika silaha zao.***
Ilikuwa tofauti kidogo kwa jeshi la ulinzi, wakati Chief Of Deffence, Force, na wamadhimu wake, wanajiuliza jeshi la Ulinzi limeingiaje ndani ya operation hii ya polisi, mala wakapokea simu toka ikulu, ikiwataka kuongeza nguu katika operation hiyo sababu nguvu ya wale polisi wasaliti aikuwa imejulikana, lengo ni kuwa thibiti na kuwa kamata, mala moja, pasipo watu hao kutoroka au kiuleta madhara zaidi, ndipo mkuu wa opretion za ndani ya nchi, katika jeshi la ulinzi akapiga simu, briged ya kusini akimtaka briged kamanda kuongeza nguvu Njombe, yani aongeze askari na silaha, huku mkuu wa majeshi yani CDF, na mkuu wa mafunzo na utendaji kivita jeshini, pamoja na mkuuwa uchunguzi na utambuzi jeshini,wkaelek
ea kwenye kambi la askari wa hanga yani air force, kwenda kupanda helicopter ya kivita, gun ship callier, tayari kwa safari ya kuelekea Njombe, maana akukuwa na muda wa kupumzika, kama ilivyo kawaida ya majeshi yote duniani, inapotolewa amri kama hii, mala moja utekelezwa kwa haraka, na ukizingatia ime tolewa narais mwenyewe.
Hivyo mala moja brigedia Fransis Haule akamjulisha mkuu wa mafunzo na utendaji kivita, katika briged yake, kuwa aandae helicopter mojakwaajili yao, na pia amwagize commanding office wa Njombe, yani mkuu wa kambi apelike kombania moja ya mapigano Njombe, kwenye eneo la tukio, kombania moja uchukua watu mpaka mia na kumi au ishilini, inategemea na uwezo wa jeshi na vifaha walivyo navyo.
Wakati maandalizi yanafanyika huku BrigediHaule, akiwa na uakika kuwa wanaenda kwa ushaidi, na kufwata amri ya CDF, yani mkuu wa jeshi la ulinzi, maana Kisona atakuwa amesha maliza kazi, ndipo brig Hule alipo kumbuka kuwa mzee Mbogo yupo, na mke wake atakuwa kati hali ya wasi wasi sana juu ya mtoto wao, hivyo ni vyema kama wataenda nae, ili akaungane na familia yake.
Bado makamanda awa walikuwa wana mkumbuka sana mzee Mbogo, na kuthamini mchango wake, katika jeshi la ulinzi, na pia walikuwa wana mfaamu vuzuri kijana Edgar, kwamchango wake katika timu yao briged ya mpira wa kikapu, akika nikijana mwenye juhudi na kipenzi cha watu wengi sana, kwakifupi brigedia Haulealiona umuhimu wa kuondoka na mama Edgar, nae akatulize moyo wake, baada ya kuiona familia yake ikiwa salama.
Akiwa na uhakika na anacho kifanya, brigedia Fransice Haule, ambae alisha pokea report zote za Njombe, kuhusu Edgar na baba yake, toka kwa askari walio warudiasha wakina Mampombeka, alitumadereva wake akimbie seed farm kumchukuwa mama Edgar ili waelekee Njombe,
Nusu saa baadae tayari, walikuwa hewani, ndani ya Helcopter kuelekea Njombe, huku mama huyu akionja usafiri huu kwa mala yakwanza, “asante mungu kwakunipa hiki kidume, leo nimepanda helicopter, kwa aajili yake” alijisemea mama Edgar, akiwa hewani ana tazama uzuri wa Tanzania ya kusini, muda alionekana kuwa mwenye furaha.***
Turudi Lukumbulu, pale walipo kuwepo wakina Kisona, ambao waliushuhudia msafari wa polisi ukiondoka, huku nyuma kabisa wakiliona gari la polisi’ lililobeba waharifu, waliolindwa na askari kama sita hivi, wenye silaha zao mikononi, “asante Edgar, ume mwokoa na mama yako pia” alisema baba Monalisa, aliekuw ame mshika mkono mke wake, ambe ne alikuwa amemshika mkono Monalisa, huku baba Monalisa alie mshika mke wake kwa mkono wa kushoto, anampa Edgar, mkono wa kulia, Edgar akautazama mkono wake, ulikuwa ume chafuka kwa damu, baba Monalisa akagundua Edgar alimaanisha nini, akamwachia mke wAke na kumkumbatia Edgar, huku mama Monalisa bado akimtazama Edgar kwa macho ya uoga na tahadhari, “Edgar huu sio wakati wa kupongezana, kuna kazi inatusubiri huko mbele” alisema Kisona huku akieleka kwenye gari, wakifwatiaaskari wake na mzee Mbogo, alie ingia kwa dereva kama kawaida yake, Edgar nae akakimbilia gari, huku Monalisa akichomoka mbio kumwai Edgar, we mona ebu njoo huku tupande gari letu” alipiga kelele mama Monalisa, huku akimkimbilia Monalisa, “nyie pandeni kwani tume kuja wote?” lilikuwa jibu la kitoto lakini liliwhekesha karibu wotepale, kasolo mama Mona peke yake, ambae aliduwaha, “Mbogo ebu subiri kwanza,nime pata wazo” alisema Kisona, huku nako baba Monalisa alikuwa ana mtuliza mke wake, “mwachetu akae na mwenzie” alisema baba Mona huku ana shangaa kumwona Kisona anashuka toka kwenye gari, na kumsogeleamzee Anderson, “mzee kuna jambo nataka tuongee kiidogo, nazani halitokuwa gumu kwako” alisema Kisona, huku akimshika mkono baba Mona na kusogea pembeni***
Naam Helcopter tatu ilikuwa hewani, magari sita makubwa ya kijeshi sambamba na madogo matatu, moja wapo likimbeba mkuu wa kambi la jeshi la Makambako, yalikuwa barabarani yakitokea Makambako, kuelekea Njombe, msafara mkubwa wa polisi ukiwa una maliza kona za lukumbulu kuelekea kijiji cha Kifanya, msaara huo pekee ulikuwa na sura tofauti na wakati unakuja, ulikuwa na mhanganyiko wa magari mazima na mabovu, mambovu matatu pamoja na lile la kina kingarame, yalivutwa na magari mengine matatu, huku moja tu likiwa peke yake bila kuvutwa, nilile walilo panda wakina Kingarame, chini ya ulinzi mkali,
RPC Ruvuma alikuwa gari la mbele ya RPC Iringa, mala kwa mala alikuwa anageuza shingo yake kutazama nyuma, na kulichungulia gari lililo wabeba wakina Kingarame, “sijuwi huyu bwana anamaana gani, yani kagombana na yule kanal, alafu ana waweka wale majambazi wakae gari la nyuma kabisa” alilalamika RPC Ruvuma, huku mala kwa mala akiangalia nyuma.
Kingarame akiwa amekalishwa chini ya sakafu yagari hili la polisi, kama wakaavyo waharifu wengine, aliowai kuwakata siku za nyuma, huku amefungwa pingu mkononi, kama wenzie saba walivyo fanywa, “tupo wapi hapa” aliuliza Kingarame akiwa amekaa chini, akuwa na uwezo wa kuona vizuri nje, “tupo Kifanya afande” alijibu mmoja wa askari polisi walinzi akijibu kwa nidhamu ya hali ya juu, usingesema kuwa ni mwalifu, kihasi kwamba ata wale wengine, yani waharifu wakainua shingo zao na kuwatazama askari wanao walinda, waka gundua kuwa wote walikuwa ni wenzao waliowai kushirikiana na Kingarame katika matukio mbali mbali ya uajambazi, na atajana usiku walikuwa pamoja kwenye msako, na ndio alio wpa ahadi ya kuwagawiamali nyingi sana, endapo watafanikisha mipango yao, askari wote ndani yagari hili, walijikuta wakitabasamu, tena tabasamu la ushindi, ote wakatzama mbele kupitia nyuma ya kioo cha gari hili wakawaona dereva na yule koplo wakiwa wana tazama mbele, awana ata wasi wasi, yule askari alie toa jibu la mahali walipo aka ingiza mkono mfukoni na kutoa kipande kirefu cha waya, na kuukunjwa kwa namna flani, kisha aka anza kuifungua pingu ya Kingarame, ambae baadata kumfungua tu, aka mkabidhi bastola, kisha aka wafungua wengine wawili alafu akawakabidhi waya ili wafunguane, huku safari inaendelea.
Wakati wanaendelea kufunguana na pingu, huku wanakaribia kukicha kijiji cha Kifanya, ghafla wakaliona gari la jeshi lilile lakisona, likiwa overtake, (likiwapita) kwa speed kali kweli kweli, hapo Kingarame akatabasamu, “nilimsahau huyu mshenzi, sasa tuna weza kuondoka bila wasiwasi, mpaka waje wageuke, watakuwa wamesha chelewa” alisema Kingarame, na mwingine akadakia, tena ukizingatia wame kolofishana na RPC, ndio kabisaaa, mpaka wapatane na kufanya kazi pamoja tutakuwa tumesha fika songea”.
“Ingekuwa ametokea songea, ningesema yupo mpango mmoja na Kingarame” alisema RPC Ruvuma akiendelea kumlahumu mwenzie wa kutoka Iringa, ghafla wakasikia mlio wa risasi ukitokea nyuma ya msafara wao, RPC Ruvuma akageuka kutazama nyuma, alicho kiona kilimstua RPC Ruvuma, “aya ndio aliyo yataka huyu mpuuzi” alisema RPC Ruvuma, huku anashuhudia lile gari lanyuma kabisa,………. itaendelea hapa hapa

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!