
SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA: yule jamaa mtu mzima akatoa kofia kichwani kwake, aikuwa sura ngeni sana kwa Denis, ni kama kuna sehemu alishawaai kumwona, akufanana na jinsi Denis alivyokuwa akiwaza, juu ya baba yake Jackline “naitwa Michael Fransis Nyati, au baba Jackline, au babu yake France” aliongea yule jamaa kwa sauti tulivu sana, na yaupole, ENDELEA ….. Denis akamtazama jamaa usoni, nikweli anafanana kiasi kikubwa na mke wake, Jackline, lakini akuwa mzee na maskini kama alivyozani siku zote, na wala akuwa na dalili ya kutokea kijijini kama alivyoambiwa na mkewake Jackline, lakini ni mtu mzima, aliekaa kimazoezi, alivalia nazifu kama wazee wengine wenye uwezo wao kifedha, “usijiulize maswali mengi Denis, utafahamu kila kitu muda ukifika” aliongea mzee huyu, baada ya hapo alichokifanya mzee Michael Fransis Nyati, alimkabidhi Denis vitu viwili, kimoja ni kifaha kidogo kama kishikizo cha nguo, chenye kushika kwenye nguo, kutokana na aina yakitambaa kilicho tengenezewa, kinge weza kunasa kwenye kitambaa chochote, pia alipewa kipaketi kidogo sana kama punje moja ya karanga, chenye unga mweusi, “jitahidi umkabidhi Jackline, pasipo mtu yoyote kuona, ukitoka nipigie simu, nazani utakuwa na jibu lakunipa juu ya huko uendako” aliongea mzee Nyati na kuonyesha ishara, kuwa Denis apaki gari pembeni, kwenye kituo cha dala dala, wakati huo nyuma yao likapark Toyota GX jeusi, ambalo muda mrefu, aliliona likiwafwata nyuma yao, lakini akulitilia maanani, mzee Nyati akashuka na kwenda kuingia kwenye GX kisha likaondoka likimpita pale alipo simama, hapo Denis aliweza kumwona dereva wa gari ilo, alikuwa ni mwanamke alie valia vizuri na kukoleza urembo wake, japo alikuwa ni mtu mzima, lakini uzuri wake ulonekana vyema kabisa, yule mwanamke alimpungia mkono, nayeye akapunga, GX likapotea machoni kwake, maswali mengi yakazidi kichwani kwa Denis, nini kinacho endelea, “Toyota Gx masikini kuja dar usiku, kukamatwa mke wangu, mh! nitajuwa ukweli” aliwaza Denis huku akiingiza gari barabarani pasipo kuangalia, akalikosa daladala na mwendesha pikipiki (Bodaboda) wanaoishia kushusha mitusi mizito, Denis akujari akaendelea na safari yake, Saa moja na robo Denis alikuwa anapark gari lake kwenye maegesho ya magari kituo kikuu cha polisi, kilichopo kaliakoo, askari walikuwa wametapakaa eneo hili, wakiwa vikundi vikundi, Denis aliwasikia wale askari wapolisi wakisimuliana ya liyotokea jana usiku, jinsi mwana dada alivyo fanya mauwaji, na kuwasumbua polisi muda mrefu, sasa amekamatwa, Denis akiwa amembeba mwanae, alipitiliza mpaka ndani kabisa mapokezi, huku akijuwa kabisa kuwa anae zungumziwa ni mke wake, jambo amalo akuliamini kabisa, pale mapokezi alimkuta polisi mwanamke, akajitambulisha na kuomba kuonana na mtuhumiwa alie kamatwa jana, jina lake Jackline, ukweli inspector yule wajana akuwepo pale kituoni, alikuja mala moja na kuelekea hospital, kumwona mmoja wa majeluihi alie jeluhiwa jana, akinusulika kuuwawa jana usiku, lakini kama angekuwepo pale kituoni, akutaka mtu yoyote aruhusiwe kuongea na Jackline, japo maagizo ya mwanzo kabisa, yalisema kuwa anaye luhusiwa kumwona Jackline ni mume wake tu, basi yule polisi mwanamke alimruhusu Denis kuingia kumwona mke wake, kwa sharti moja, la kumwacha mtoto pale mapokezi, aikuwa tatizo kwa Denisi wala France, maana mtoto hyu akuwa mliaji sana, dakika chache baadae Denis alikuwa ndani ya ukumbi mmoja mkubwa, amekaa kwenye kiti akitazamana na mke wake mama France, akiwa amefungwa pingu, mikononi na miguuni, jackline akuonyesha wasiwasi wala kujutia lolote, walishakuwa wame kumbatiana akambusu kidogo, kabla ya kukaa pamoja, kwa kutazamana, pamoja nawatu wawili watatu nao wakiongea na mahabusu wao, wengiwao wakiwa ni wanasheria, “vipi baba umekutana naye?” aliuliza Jackline huku akitabasamu, hapo Denis akakumbuka jambo, “inamaana ata wewe una juwa kuwa baba yako amekuja dar, alafu…” Jackline alimkatiza mumewake kuongea kwa kumfanyia “shiiiiiiiiiiii” kwa sauti ya chini “tulia Denis,utakiwi kuendelea kushangaa, kuballi ana na unacho kiona, si’umeshafika, nitakueleza kila kitu mume wangu” hapo Jackiline, akatazama kushoto na kulia, akaona polisi wapo mbali kidogo, akamtazama Denis, akaachia tabasamu, “Denis nikweli mimi nimeuwa watu wengi sana, zaidi ya ishirini, wakiwepo viongozi wa dini na wafanya biashara wakubwa” hapo Denis alistuka kidogo, kama anataka kusimama na kukimbia, lakini Jackline alikuwa amemshika na kumbana mikono, “labda nikueleze kwanini, nilifanya hivyo, naimani utaelewa tu!, hawa wote nilio wauwa, walikuwa watu wabaya sana, tofauti na watu wanavyozani” Jackline aliongea, huku Denis akiwa katulia, akajitaidi kuondoa wasiwasi, yakuwa alikuwa akilala kitanda kimoja na muuaji, ambae alikuwa akitafutwa na vyombo vya dola zaidi ya miaka miwili, licha yakuwa mke wake ni mwanamke mrembo pia alimwonyesha upendo wa hali ya juu sana, “naona nianze kuku elezea tokea mwanzo ili unielewe, aliongea Jackline akiachia tabasamu laini lililo muweka sawa Denis, Tabasamu ambalo, aliliona kwa mala ya kwanza, miaka miwili na nusu iliyopita, **
Mwaka 1988 feb, askari saba wa jeshi la ulinzi, kikundi mahalumu cha wadunguaji (sniper) toka Tanzania, kilikuwa ndani ya msitu mnene, nyuma ya mlima wa nyilagongo, nchini congo DRC, baada ya kumaliza mission yao ya kuteketeza kambi dogo la waasi, lilozuwia njia ya kuelekea mji mmoja mdogo wa rubelo, kaskazini yay a jimbo la kivu ya kaskazini, ili kuwawezesha wafanya kazi wa umoja wamataifa kufikisha huduma za kijamii mji huo wa rubelo,sasa walikuwa wakisubiri usafiri wa Helicopter, ambayo ilitakiwa iwapeleke, moja kwamoja mpaka kigoma Tanzania, ambako wangekuta gari linawasubiri, kuwapeleka dar es salaam, kila mmoja wao alikuwa amevalia sare za kijeshi zitumikazo kwenye vita kofia nyekundu damu ya mzee, pia vifuani kwao walikuwa wamme valia vazi maalumu la kuzuwia risasi, burret proof, pia kila mmoja alikuwa amebeba silaha yake aina ya magnum sniper rifle, ikiwa imewekwa kwenye mfuko wake maalumu, pia kila mmoja wao alikuwa ana begi lake la vifaa binafsi, huku vinoni mao wame ninginiza bastora, visu, na kamba, wanajeshi awa ambao walikuwa wamesha maliza jukumu lao, lililowaleta nchini humu, walikuwa ni marafiki wakubwa sana, kutokana na kuhudhuria mission mbali mbali wakiwa pamoja, muda wote walikuwa wenye furaha kubwa sana, kutokana na kumaliza salama mission yao,
Kumbe basi, askari mwenzao mmoja, ambae ni Michael Nyati, mwenye cheo cha private, akiwa ndie skari mdogo kuliko wote kwa cheo, na kwa umri, wakati walipo kuwa katika mapambano, yaliyodumu kwa masaa machache yaliyopita, aliokota begi dogo jeusi la ngozi, likiwa na almas nyingi ndani yake, zilizo kuwa zikiandaliwa kwenda kubadirishana na container zilizo sheheni silaha, tka nchini urusi, Michael alillificha lile begi kwenye begi lake kubwa kwa malengo kuwa akifika nyumbani Tanzania, ange uza na kjipatia fedha nyingi sana ya kuendesha maisha yake, lakini baada ya kuwaza sana, akaoa aitakuwa vizuri kama atawanyima wenzake, hivyo aligawa kidogo, zilizobaki ndani ya begi dogo jeusi, akaziweka kwenye begi lake kubwa la kijeshi, kisha akawaambia wenzake kuwa ameokota Almasi, akawaonyesha, vilikuwa vipande saba, vyenye ukubwa wa kidole gumba cha mguuni cha mtu mzima, hivyo aliitaji kuwa patia moja moja kila mmoja, maana kwa ukubwa wa kipande kimoja cha almas hizo, ungeweza kuthaminishwa na fedha nyingi sana ambayo mtu angeweza kuuza kwa fedha ambayo, angeitumia miaka mingi sana, pasipo kuangaika na kitu kingine, lakini basi, pasipo kujuwa kuwa vile vipande vya almas vilienea kwa idadi ya wote saba, na kwamba kipande kimoja kingetosha kuwapatia utajiri mkubwa, Michael Nyati alishuhudia wakubwa wake hao wakazi, wakigombania zile almasi, waligombana sana, adi mkubwa wao kabisa, major Elenest Masinde alipotumia dakika tatu kuwatuliza askari wake, na walipotulia yule afande major Masinde, akamgeukia kijana mdogo Michael “private Nyati ebu! Tuambie nyingine zipo wapi?” Masinde wakati anauliza swali hilo alikuwa amekunja uso, akionyesha akuwa na masihara wakati hule, alimsogelea Edgar taratibu huku akichomoa bastora, kiukweli Michael alijuwa asipo towa zile almas, mwisho wake umefika, maana kwa jinsi alivyo mwona Masinde amekunja sura, akajuwa kuwa hakuwa na utani, basi taratibu akafungua beg lake na kutoa kile kibeg kidogo cheusi, wakati huo, mfuko wa silaha kubwa ya kudugulia mbali, Magnum sniper rifle, ukiwa begani, ilipomalizia kutoa kile kibegi chenye almas, kabla ata ajampatia ule mfuko afande wake Masinde, Michael akahisi kitu kizito kiki mgonga kifuani kwanguvu sana, na kumsukuma nyuma, ikimrusha juu, huku akisikia mlupuko wa risasi toka kwenye bastora iliyopo mkononi kwa afande wake Masinde, michael akiwa ameng’a ng’ania kile kifuko cha almas, japo almasi chache zilidondoka chini, huku akiliachia begi lake kubwa la vifaa binafsi, wakati huo silaha kubwa hipo begani, bastora na kisu kiunoni, Edgar alitupwa hewani, akielekea kwenye korongo kubwa sana lakutisha,
NAAM KWANINI JACKLINE AMEWAUWA VIONGOZI WADINI NAWAFANYA BIASHARA, KIONGOZI HUYU WAKIJESHI ANAMPIGA RISASI ASKARI MDOGO, KWALENGO LA KUMNYANG’ANYA ALMASI ZOTE ALIZOZIPATA, JE? MICHAEL ALIFANYAJE KUJIOKOA, AWA WANAJESHI WENGINE NI WAKINA NANI?
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU