BINTI MDUNGUAJI (03)

SEHEMU YA TATU


ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI: Michael akahisi kitu kizito kiki mgonga kifuani kwanguvu sana, na kumsukuma nyuma, ikimrusha juu, huku akisikia mlupuko wa risasi toka kwenye bastora iliyopo mkononi kwa afande wake Masinde, michael akiwa ameng’a ng’ania kile kifuko cha almas, japo almasi chache zilidondoka chini, huku akiliachia begi lake kubwa la vifaa binafsi, wakati huo silaha kubwa hipo begani, bastora na kisu kiunoni, Edgar alitupwa hewani, akielekea kwenye korongo kubwa sana lakutisha, ENDELEA……
Major Masinde na wanajeshi wenzake walishuhudia Michael, akitupwa hewani kwanguvu ya risasi iliyochomoka toka kwenye bastora yeye, major Masinde, na kugonga kwenye kifua cha Michael na kukutana na bullet proof, huku bahadhi ya vipande vya almas vikitawanyika nakudondoka pembeni, private Michael anadondokea kwenye maporomoko marefu, yenye miti na nyasi nyingi sana, major Mainde na askari wenzake, wanajaribu kuchungulia kule bondeni, lakini awamwoni kijana huyu mdogo, kutokana na umbali wa korongo alilo angukia, na kuzuiwa na nyasi ndefu zilizo zungukwa na miti mikubwa, na kusababisha giza nene kiasi cha kushindwa kuona kule chini, wakina Masinde waliokota zile almas na kugawana sawa kwa sawa, wakionyesha kufurahi na kuunga mkono tukio lile, maana walijuwa kuwa wakifanikiwa kufika tanzania wange kuwa matajiri wakubwa, kwa vipande vile vya Almas, wakakubaliana kutoa taarifa ya kutoweka kwa askari, private Michael Nyati, kwamba ametowe katika mapigano na awajuwi alikoelekea, wakiamini kuwa private Michael amesha poteza maisha, muda mchache baadae helicopter ilifika, na askari wote sita waliobakia, wakiongozwa na mkuu wao Major Masinde, walipanda helcoptel kwa kutumia kamba maalumu ,wakiliacha begi lamwenzao pale mstuni maana awakutaka ushahidi, wakatoweka angani kuitafuta Tanzania, wakiamini kuwa mwenzao private Michael amesha kufa,
Walisafiri kwa muda wasaa moja, mpaka kutua kigoma, nchini Tanzania kwenye kambi dogo la jeshi, saa kum jioni, wakaingia kwenye magari aina ya land lover 110, (Defender) mbili wakigawana watatu watatu, nakuondoka kuelekea dar es salaam, ambapo walitumia siku moja na nusu kufika dar es laam, waliingia saa tatu asubui, naku report kwenye kitengo cha operation za siri, wakatoa taharifa yao, mission kuwa ilifanikiwa, ila mmoja wao amepotea katika msitu wa Nyilagongo, mkuu wakitengo brigade gen Soud Hasssan alipokea tahalifa zile, kwa masikitiko makubwa, maana licha ya kuwa kijana yule alikuwa mchapa kazi wa kutegemewa, na mtu aliekuwa anatumia akili za zada kusaidia kuwaokoa wenzake na kufanikisha mipango yote wanayo tumwa na kikazi, pia alikuwa ni kijana mdogo sana, mwenye umri wa miaka ishirini na mbili, akiwa namiaka miwili tu! kazini, baada ya kutoa report yao, wakina Masinde na wenzake watano, waka ruhusiwa na kupewa mapumziko ya mwezi mmoja, huku jeshi likipanga kuficha siri hii mpaka watakapo pata ukweli kamili au kuiokota maiti ya askari Michael Nyati, na endapo akipatikana mzima, ashitakiwe katika mahakama ya kijeshi kwa utoro * Michael shuhudia akirushwa kwa nguvu pasipo balance yoyote, akuwa na pakujishikia zaidi ya kibegi kidogo cheusi na beg lenye siraha yake kubwa, magnum sniper rifle, alisukumwa na risasi na kumtupa pembeni, akajiona kielekea kwenye korongongo refu, aliambaa hewani akijigonga kwenye miti na mawe makubwa, kijana huyu alitumia sekunde kadhaa, akielekea chini pasipo kujuwa kule bondeni kupoje, ghafla alijigonga kwanguvu kwenye jiwe kubwa maeneo yakifua kifua, ambacho kilikingwa na vazi la kuzuwia risasi (bullet proof), akasikia maumivu makali na pumzi zikagoma, akaona mwili ukilegea na kukosa nguvu, huku giza nene likitanda usoni mwake, akaanza kusikia ubaridi kwenye paji lake la uso, kajaribu kujiinua iliaweze kukimbia maana alijuwa wakina Masinde lazima wamfwate kule chini na kumtwanga risasi, lakini akashindwa kwani alihisi maumivu makali sana, maeneo yakifua chake, wakati huo akasikia kitu kile cha ubaridi kwenye paji lake la uso, likigeuka na kuwa kama maji kabisa, huku mwili wake ukiwa tofauti kabisa kama akuwa ame vaa nguo kabisa, basi taratibu akajaribu kufungua macho, naam akakutana na sura ya mschana mrembo sana, akitabasamu, huku akitoa kitambaa kilicholowa maji kwenye paji lake la uso, Michael alijawa na uoga, akutegemea kitendo cha kufumba na kufumbua, akutane na sura ya mschana mrembo, wakati muda mfupi alikuwa akiporomoka kwenye korongo ndani ya msitu mnene, akamtazama vizuri yule mschana mdogo kisi ambae alikuwa maevalia nguo zilizo chakaa, ambazo azikuweza kuuficha uzuri wake,akamwona bado akiwa anatabasamu, hapo Michael akajaribu tena kuinuka, lakini maumivu makali kifuani kwake yakamzidia nakumfanya arudi chini, huku akijishika kifuani kwa maumivu makari, akagundua bullet proof haipo mwilini mwake, siyo hivyo pekee anagunduwa kuwa akuwa na nguo atamoja mwilini, zaidi ya shuka yake ya kijeshi, kilicho mshangza ni kwamba shuka hiyo aliiacha kwenye beg kule juu wakati akiporomoka, sasa alikuwa amefunikiwa “mtanzania! una lamuka sasa” Kiswahili chenye rafudhi ya congo, aliongea yule binti kwa sauti taratibu sana, iliyo ambatana na tabasamu la furaha na matumaini, michaeli alimwona yule mschana, akiinuka na kutoka nje mbio mbio, Michael akapata nafasi ya kujichungulia, kweli akuwa na nguo ata moja ndani, akajaribu kugeuza macho huku na kule mle ndani, akaona ni kibanda kidogo kilichojengwa kwa miti na nyasi, mfano wa vibanda ambavyo alivishuhudia kwenye kambi moja ya wahasi ambao walitoka kuwashambuli,
Mlendani mlikuwa navitu vichache, nguo zilizo tundikwa kwenye kamba, zikiwemo na nguo zake za kijeshi, vyombo vya kupikia, nguo chakavu za kike na mabegi yake yote matatu, yani lile kubwa alilo liacha kule juu na lile la salaha, hapo akashangaa kidogo, beg kubwa la mgongoni aliliacha juu kabisa kule walipo wakina masinde a wenzake, sasa huku limefikaje, na haya mambo yamefanyika muda gani, mbona nikufumba na kufumbua, wakati ana jiuliza maswali hayo mala akarudi yule binti mrembo, sana akiwa ameongozana na watu watatu mwanaume mmoja akiwa na bunduki aina ya smg mkononi, pia wanawake wawili mmoja mama wamakamo akiwa na sufuria mkononi lilionyesha linatoka jikoni, maana lilikuwa linafuka moshi, pia mdada ambae ni kijana sawa na huyu mwanaume, naye alikuwa na smg mkononi, hapo Michael akajuwa ameingia choo chakike, maana watu awa walioneka wazi kuwa ni wahasi, aliendelea kusimulia Jackline huku mume wake enis akimsikiliza kwa umakini mkubwa sana,JE, INAWEZEKANA MICHAEL AMEINGIA KWENYE MIKONO YA WAHASI?

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!