
SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO : “yap! natakatuanze safari siku tatu zijazo” hapo Anitha akapiga magoti karibu na ngozi yake ya kulalia, akaifunua akatoa ubao, akifuatia silaha yake SMG, na mwisho akatoa lile beg la ngozi akaliweka juu, kisha akafungua, ndani “ona hii Michael, utapenda twende nayo Tanzania?” aliongea Anitha huku akiwa amelitanuwa lile begi, Michael akachungulia ndani ya beg, alichokiona ndani ya begi nusu Michael azimie : endelea…
kwa mshangao wa furaha, ya likuwa madini ya almas na dhahabu nyingi sana, ni mala dufu ya zile za kwake, tofauti ni kwamba, hizi zilikuwa ni vipande vidogo vidogo, kama punje za maindi, * kumbe baba yake Anitha alikuwa na uwezo mkubwa kifedha, akiishi mitaa ya vilunga nyuma ya soko kuu la mjini Goma, shuguli zake zilikuwa ni kununua madini nakwenda kuyauza nchi Rwanda, siku waliyopoteana na mwanae Anitha, ilikuwa ni kutokana na vita, anitha alikuwa ametoka shule, akuwakuta ndugu zake nyumbani, kuanzia baba mama na wadogo zake, ata mda mfupi baadae mapigano ya lipoanza, alichukua ilo begi na kuweka nguo zake chache, pasipo kujuwa kuna madini ndani yake, alitembea nalo mpaka alipo fika huku porini ndipo alipo gunduwa uwepo way ale mawe kwenye begi lake, akuwaambia wenzake juu yay ale mawe ya kyng’aa, sababu akujuwa yale mawe yakung’aa yana maana gani, ila alishawai kusikia hadithi yamawe yenye thamani, ndipo alipo chimba shimo ndani ya kibanda chake alicho jengewa na wenzake, na kuliweka beg lake na silaha yake, huku juu yake akifanya kuwa ni sehemu ya kulala, alibaki na sir yake mpaka akaja kutambua umuhimu wake, siku alipo yaona yakitaka kusababisha kifo cha Michael, kule juu alipo pigwa risasi na watanzania wenzake, ***
Michael alimkumbatia Anitha na kumbusu mdomoni, kisha akamwambia “tutaishi maisha mazuri sana tukifika Tanzania, naimani wazazi wako na ndugu zako utawaona tena, na kuwasaidia, ama ulivyo panga” hapo Anitha alifurahi kusikia vile, * siku yatatu Michael na Anitha walikuwa wamesha jiandaa tayari kwa safari, walibeba chakula, nyama porini ya swala iliyo banikwa na kukauka vizuri, pia maji ya kunywa ya kutosha, Anitha aliwaaga wale watoto wamama mtu mzima pamoja na mama yao, pia akawaaga wale dada zake ambao walimsaidia kufika kule porini, akiwa ahidi kurudi kuwasaidia pindi maisha yake yakiwa mazuri, Michael pia alifanya hivyo, wakiwa wamezifungua silaha zao, na kuzitenganisha vipande vipande, na kuzi weka kwenye begi kubwa, Michael na Anitha waliazimwa Smg na wale wanawake waliobaki, kwa ajiri ya kutembelea msituni kipindi wakitafuta mji ulipo, wao wakibaki na smg moja safari ikaanza wakisindikizwa na wale vijana watatu, ambao wangerudi na siraha, walitembea usiku kucha, wakiwa wamevaa nguo zilizo chakaa Michael ili kufanana na wakzi wa maeneo wanayo pita, alipewa na wenyeji wake, alfajili walitokea kwenye kitongoji cha kanyaluchina, kupitia mirima ya Muja, walikuta vita ikiendelea, upande wa goma mjini, kuanzia bhilele kuelekea Tsake na m’bambilo, na kusababisha upande huu wa kanaluchina kujae watu wanao kimbia vita, wakielekea lutchuru mpaka bunagana, kuingia Rwanda au Uganda, pia wapo walioishia kibumba na kuingia Rwanda, wakitumia usafiri wa magari makubwa ya mizigo ila wengi wao wakitembea kwa miguu au baiskeri za miti, maharufu kama chukudu, lakini walisema mpaka wa Rwanda kutokea kibumba ni vigumu kupita kutokana na vikundi vidogo vya wahasi wa maimai, kukalia maeneo hayo, Michael na Anitha waliagana na wale jamaa zao, huku Michael akiwapatia faranga elfu ishirini wanunue mahitaji yao yakule porini kwenye maduka machache yaliyokuwa wazi pale kanaluchina, wale jamaa walishukuru sana wakiwasisitiza Anitha na Michael, kuwakumbuka pindi watakapo kuwa wamefika na kutulia Tanzania, atimae wakatengana wakiwakabidhi silaha zao, huku wakina Michael wakijichanganya kwenye makundi ya wakimbizi, waliokuwa wamebeba mizigo mikubwa, huku wengine wakiwa na mifugo yao, na safari ikaanza. **
Jioni ya kwanza iliwakuta kibumba, wakipita kibhati Kilima nyoka na minara mitatu, wakapumzika kwa masaa matatu saa nne usiku walibadiri nguo zao na kuvaa nguo za kijeshi, ambazo Michael alikuwa nazo pea mbili, moja akampatia Anitha ambae zilimtosha vyema chini akamvalisha rubber, nazo zilimtosha, wakaanza safari awamu ya pili, tofauti na mchana usiku huu awakutumia barabara, walipitia porini kwa msaada wa ramani waliyokuwanayo, walitembea adi juwa lilipo chomoza wakabadiri nguo tena, na kuvaa zile chakavu kisha wakatokea barabarani na kujiunga na makundi ya wakimbizi, walitembe kwa masaa mawili, wakawa wamefika lutchuru, wakaihacha njia ya kuelekea mbuga ya virunga mpaka ruwindi na butembo, wakaingia kulia kuelekea bunagana, hapo walitumia masaa mawili, kuingia bunagana na kusogea kwenye mpaka wa congo na uganda, hapo wakakuta makundi mengi ya wakimbizi, wakijaribu kuvuka mpaka, ukaguzi ulikuwa mkari, askari wajeshi na polisi wa uganda, walisimamia kuakikisha watu awavuki na silaha au kitu chochote kibaya, wakati mwingine askari hao uwapola vitu vyao vya thamani, hapo Michael akatumia akiri ya kuzaliwa nayo, kwanza akajitoa kwenye kwenye kundi kubwa la wakimbizi yeye na Anitha, akaya fwata magari ya umoja wa mataifa yaliyo kuwa yamepaki pembeni, mengine yakisubiri kuvuka na mengine yakishusha wakimbizi au misaada ya chakula na mavazi, akaongea na dereva wa gari moja ambalo lilikuwa lina taka kuvuka, likirudi toka kupeleka misaada ya chakula na dawa, **
Nusu saa baadae walivuka wakiwa ndani ya gari la umoja wa mataifa yani UN, na sale za kijeshi, lile gari lili wapeleka mpaka kampala, ambapo walinunua nguo nzuri za kiraia na kuzivaa, wakamlipa yule jamaa wa UN fendha walizo kubaliana kisha yule jamaa akaondoka na gari lake, na wao wakaenda barabara kuu iendayo Kenya mpaka Tanzania, jioni walifanikiwa kupata gari kubwa la mizigo linaloenda bandari ya dar es salaam kuchukuwa mizigo ya misaada ya wakimbizi, siku hiyo walilala mpakani mwa Uganda na Kenya, siku yapili walilala Arusha Tanzania, wakiachana na lile gari kubwa la mizigo, siku hiyo walillala usingizi mzito mzito nusu kifo, kwenye hotel moja ya kawaida tu, siku ya pili wakapanda basi kuelekea dar es salaam, walitumia masaa kumi kufika dar es salaam (enzi hizo barabara haikuwa nzuri sana) moja kwamoja walishukia kimara na kutafuta nyumba ya wageni, wakachukua chumba na kupumzika, japo mida flani walienda kukaa sehemu ya chakula na vinywaji, walipo maliza kula waliagiza vinywaji, Michael akiagiza pombe, na kuanza kunywa huu wakioonyesha uchangamfu, kwa furaha walizokuwa nazo, ni baada ya miezi sita ya kunusulika kifo, akanywa bia, huku Anitha na ye akijarbu kunywa, ambae muda wote alikuwa akitabasamu kama kawaida yake, japo alionekana kuwa mchovu, kutokana na safari yao ngumu yasiku kadhaa, Anitha alishangaa kuona jinsi watanzania wanavyoishi kwa amani na furaha, kule kwao pengine ata siku ya siku kuu usingeona watu wakikaa kwenye bar mpaka saa mbili, usiku
Pombe ilisha mchukua Anitha, japo alikuwa amekunywa kidogo sana, ilikuwa ni mala yake ya kwanza, usiku ule waliutumia vizuri sana kuburudisha miili yao, maana jana yake awakuweza kufanya mapenzi kutokana na uchovu wasafari, * Asubuhi siku yapili, Michael alimwacha Anitha pale nyumba ya wageni akaanza kuwasaka wabaya wake wakina Masinde, alianzia kwenye kikosi maalumu cha kazi za siri, akaenda na kukaa kwenye mgahawa ulipo jirani na kambi hilo akiangalia wanaoingia na kutoka, pengine angemuona ata mmoja wa askari, ambao alikuwa nao nchini Congo, wakati huo Michael alikuwa amebeba kisu chake kikali cha kijeshi, akiamini kingetosha kutekeleza mauaji, aliyokusudia kwa wabaya wake, kwani alijuwa kati ya adui zake, hakuna ambae angeweza kumzidi uwezo wa kimapigano, Michael alikaa hapo kwa masaa matatu, adi ilipo timia saa nne za asubuhi, lakini hakumwona mtu yoyote kati ya maadui zake, aliogopa kwenda ofisini kwani akujuwa ametolewa taalifa gani na wale wenzake, akapitisha uamuzi wa kwenda kutafuta kibanda cha simu, alipiga simu ikapokelewa “hallow brigade gen Soud hapa, nikusaidie tafadhari” Michael aliitambua sauti ya mkuu wake Soud Hassan, lakini akasita kujitambulisha, “naitwa Sam na mwulizia rafiki yangu Michael Nyati” alidanganya Michael ilikujuwa kama wanafahamu nini juu yake, bahati nzuri brg Soud alifunguka mwanzo mwisho, akimweleza pasipo kujuwa kuwa anaongea na Michael, kuwa Michael ameandikwa kama mtoro jeshini, sababu amewakimbia wenzake wakiwa kwenye kazi nje ya nchi, hivyo akipatikana atoe taharifa ili akakamatwe, pia Michael akaulizia juu ya wale maadui zake akaambiwa walihacha kazi baada tu! ya kurudi toka likizo waliyo pewa baada ya kumaliza mission huko congo, Mchael akarudi hotelini akiwa amejawa na mawazo, ya kuwakosa maadui zake, lakini akuwa na jinsi,** baada ya kukata simu ambayo alikuwa akiongea na mtu asiye mfahamu aliye jitambulisha kuwa ni rafiki wa kijana mpotevu Michael Fransis Nyati, brig Gen Soud Hassan, alistuka kidogo na kufikilia jambo, kakumbuka jambo moja kuwa ile sauti ya mtu ambae ametoka kuongea nae, ni sauti inayofanana kabisa na sauti ya askari wake Michael Nyati, hapo mzee soudy akagunduwa kuwa kunajambo zito nyuma ya panzia, ambalo lingeleta mahafa kwa siku za hivi karibuni, na kwa jinsi anavyo mjuwa kijana Michael, ni mtu mwenye kutumia akili nyingi sana kwenye mambo yake, hapo bwan Soud akapiga simu nyumbani kwa bwana Masinde ndie pekee ambae alikuwa na namba zake za simu yake ya nyumbani, simu ile ilipokelewa na mtoto wa bwana Masinde, “hallow shikamoo,” ilikuwa ni sauti a mtoto Johnson, mwenemiaka mine, “malahaba John, mpe simu baba niongee nae,” bwana Soud alimfahau sana huyu mtoto, kwakuwa siku zote anavyo piga simu lazima apokee kwanza ndipo ampatie baba yake, ni kweli baada ya sekunde chache bwana masinde akawa amesha shika simu, brg Gen Soud akaongea na bwana Masinde akimsimulia kile alicho kihisi kuwa, ni ni kuongea na kijana ni Michael Nyati, akamwuliza kama kuna jambo lolote lililo jificha juu ya kupotea kwa kijana huyo nchini congo, lakini bwana Masinde ambae kwa sasa, maisha yake yalikuwa mazuri zaidi ya kipindi akiwa mwanajeshi, alikataa kabisa kutokea jamb lolote zaidi ya kijana huyo kutoweka katika namna ya kushangaza, baada ya kukosa alicho tarajia bwana Soud alikata simu na kubaki akivuta picha yakile kitakacho tokea siku za usoni, mwasho wasiku brig gen Soudy akajikuta akitabasamu, huku akijisemea peke yake, “sasa watavuna walicho panda” ** huku nako Michael na Anitha walifaya mipango ya kuuza vipande viwili vya almas, ambapo walijipatia milioni mia tatu, kwa kipindi hicho, nifedha nyingi sana, ambazo ungefananisha na billion tatu kwa sasa, akanunua gari moja aina ya land rover 110 wagon, na vitu vingi sana vya kuwasaidia huko wanakoenda, pia wakanunua pamoja na mavazi yao, safari ya songea kwa wazazi wa Michael ikaanza, wazazi wa Michael awakuwai kupata tahalifa ya kupotea kwa Michael, hivyo awakushangaa kumuona Michael akirudi nyumbani, kilicho wastua nikuja na mwanamke mwenye rafudhi ya congo pia mandevu na nywele nyingi sana, mwisho aliwaambia kuwa, ameamua kuhacha kazi yajeshi, huku akiwataka wazazi wake wasimwambie mtu yoyote, uwepo wake pale songea, wakiulizwa waambiwe awajuwi,
Michaeli alinunua eneo kubwa sana nje yamji, na kujenga nyumba moja kubwa sana yenye gorofa mbili, akiuacha msitu mkubwa ukizunguka nyumba hiyo, alifungua kiwanda cha kutegeneza wine itokanayo na matunda yaasiri, akawaajiri watu, waifanye kazi hiyo, akaongeza magari mengine matatu na trector mbili kwaajili yakilimo akaweka mifugo mingi sana yakila aina, ndani yamiakamiwili alikuwa amesha wasaidia wale rafikizake wacongo, ambao aliwasafirisha kwenda Kinshasa kutoka kule porini nakuwawezesha fedha nyingi zakufanyia bihashara, pia alifanikiwa kuipata familia ya akina Anitha waliyoikuta kwenye kambi ya waimbizi ya ngara Tanzania wakawatoa nakuwasafirisha afrika ya kusini wakimpatia mzee madini baadhi na fedha za kuanzia, wote waliahidi kumtembelea wapatapo nafasi , ***Ilikuwa imesha pita miaka miwili toka tukio la kupigwa risasi Michael kwenye misitu ya congo litokee, ilikuwa ni mwaka 1990 mwezi wa sita, Anitha alijifungua mtoto wakwanza wakike, siku hiyo Michael alikuwa kwenye bechi la hospital ya mkoa wa Ruvuma akijaribu kusoma gazeti la mzalendo, lakini mawazo ayakuwepo pale kabisa, aliwaza jinsi atakavyo mshika mwanae wa kwanza baada ya kutoka chumba cha kujifungulia, Michael akuweza kulisoma lile gazeti kabisa, akalikunja na kulishika mkononi, muda mchache baadae walikuwa wamemaliza taratibu za hospital na kuanza kuelekea nyumbani, tabia yake ya kutabasamu kila mala, bado alikuwa nayo Anitha, ambaye uzuri wake ulizidi mala dufu, na kiswahili chake kilianza kuwa safi, japo kuna maeno bado aliyatamka kwa rafudhi ya ki congo,
Walianza maisha mapya wakiwa baba na mama Jackline, zilisha pita siku saba toka Anitha ajifungue, siku hiyo Michael akiwa anaweka vitu vyake sawa kwenye gari lake 110, akaliona lile gazeti la mzalendo, ambalo alishindwa kulisoma siku ile, ambayo mke wake alikuwa anajifungua, akalichukuwa na kulitazama, macho yake yaligonga kwenye picha moja juu ya ukurasa wa kwanza kabisa wa gazeti hilo, akalishika na kulikunjua vizuri, maana alivutiwa na picha ile, Michael Nyati au baba Jack aliona picha moja ya mchungaji wakanisa flani, akiwa amezungukwa na waumini, sura ya yule mchungaji ndiyo iliyo mvutia Michael, kichwa cha habari kiliandikwa “mch Chilumba kuanza kuponya wagonjwa” Michael akatabasamu, nitabasamu la uchungu, na kuufanya uso wake ufanane na simba anayepiga muhayo, akalichukua gazeti na kuinganalo ndani ya nyumba na kukaa sebuleni, sambamaba na mke wake Anitha, ambae alikuwa amemlaza mtoto kwenye kochi, akaanza kuisoma ile habari kwa kina, aligundua kuwa mteule daraja la pili Chilumba, ambae ni moja kati ya wale askari walio mwacha mstni congo, baada ya kuhacha kazi ameamua kufungua kanisa, maeneo ya buguruni rozana, hapo Michael akamtazama mwanae ambae Jackline alikuwa
amelazwa juu ya kochi, pembeni ya mama yake, akatikisa kichwa kuafiki jambo flani, huku akiachia tabasamu lake kama lile la nje, lililo mshangaza Anitha, “wewe mbona unatabasamu hivyo” aliuliza Anitha kwamshangao, maana akuwai kumwona mume wake akiwa katika hali kama hiyo “wamekwisha, washenzi, atimae nimewakamata” aliongea Michael akimwonyesha picha gazetini, * “nazani mpaka hapo umeanza kuelewa Denis?” aliliza Jaclene Michael Nyati, ambae ndie mama Fransis, mke wa kijana Denis, huku uso wake ukiwa umetawalliwa na tabasamu, “nimeanza kuelewa, lakini ilikuwaje uwe mama ntilie, wakati baba yako ni mtu mwenye fedha nyingi kiasi hiki?” aliuliza Denis kwa sauti ya chini, akimtazama mkewake kwa umakini huku akili yake ikikataa kuwa mke wake ndie ametekeleza mauwaji hayo ambayo yamelitikisa jiji la dar kwa miaka mingi, “ndio tunakuja huko mume wangu, wala husiwe na haraka” alijibu Jackline kwa sauti laini na tulivu, kisha Jackline Michael Nyati akaendelea, “nazani unakumbuka sikuile tulipo kutana pale pale manzese?” alisema Jack na Denis akakubali kwa kichwa, HAYA MDAU, JACKLINE ANAZIDI KUSIMULIA KISA CHA YEYE KUUWA WATUWNGI KIASI HICHO, ENDELEA KUFWATILIA MKASA
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU