
SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA : aliuliza Denis kwa sauti ya chini, akimtazama mkewake kwa umakini huku akili yake ikikataa kuwa mke wake ndie ametekeleza mauwaji hayo ambayo yamelitikisa jiji la dar kwa miaka mingi, “ndio tunakuja huko mume wangu, wala husiwe na haraka” alijibu Jackline kwa sauti laini na tulivu, kisha Jackline Michael Nyati akaendelea, “nazani unakumbuka sikuile tulipo kutana pale pale manzese?” alisema Jack na Denis akakubali kwa kichwa, endelea…
Mwaka 2004 mwezi wa saba, saa nne asubuhi mitaa ya manzese, Denis na rafiki yake Mahadhi walikuwa wanawai supu kwenye mgahawa wakaribu na jengo la ofisi yao, iliyopo kwenye jengo la ghorofa nane, linalojulikana kama Mazao building, ambalo limepangishwa na wafanya biashara wengi wengi, ambao waliweka ofisi zao, wakati Denis na Mahadhi wanaingia pale mgahawani, walipishana na watu wengi sana, waliokuwa wanatoka ndani ya mgahawa wakiwawamesha pata kufungua kinywa, “bwana heee! kwa hiyo sehemeji akamaind” aliuliza Denis, wakati wanatembea kuelekea kwenye mgahawa, “moto uliwaka si kidogo, yani leo nataka nirudi mapema kidogo” aliongea Mahadhi akijaribu kuonyesha jinsi gani mke wake alichukia sana usiku uliopita, “tatizo siyo kuchelewa kurudi, tatizo uzinzi” alisema Denis akimsema rafiki yake Mahadhi, lakini ile kutahamaki, Denis alijikuta mkono wake ukigongwa na kitu kizito, nakigumu kama chuma, aligeuka na kutazama kitu hicho kilicho mgonga, hakuona kitu zaidi ya kwamba alikuwa amengonga kibegi kidogo cheusi, kilicho bebwa na mwanamke mmoja, ambae alimwona tokea mgongoni, ambae alitembea atuwa chache kisha yule mwanamke akageuza sura yake na kumtazama kidogo kisha akaendelea nasafari yake, alikuwa ni mzuri wa kuvutia, huku kwenye mkono wake mmoja, yule mwanamke alikuwa amebeba sahani moja iliyo funikwa, alionekana wazi kuwa anafanya kazi kwa mama bupe, huyo mama nimsimamizi wa ule mgahawa, ambao wakina Denis walikuwa wanaenda kupata chochote, Denis alitumia dakika chache kumtazama yule mwanamke, licha ya kumwangalia mgongoni akiwa katika mavazi la kimama ntilie, gauni refu na kanga chakavu aliyo jifunga kiunoni, lakini umbo lake lilionekana wazi jinsi alivyo kaa vizuri, Denis alibaki akimtazama yule dada, akipandisha kwenye jengo ambalo lina gorofa nane la Mazao building, humo ndani wamekodisha watu mbalimbali, ikiwemo ofisi ya kina Denis, inayo jiusisha na utengenezaji wa ramani za majengo na usimamizi wa ujenzi wa majengo makubwa, “hoyaa vipi tena” aliita Mahadhi baada ya kuona mwenzie ameganda,
Muda mfupi baadae, walikuwa wame inamia bakuri zao za supu yakuku, wakifakamia, ukumaongezi yakiendelea, “bola mimi kuliko wewe, yani una penda pombe sijuwi zina faida gani kwako” alijitetea Mahadhi kutoka kwenye msimango ya Denis, “mh! bola uzinzi, wakati na pombe una kunywa, alafu nilisahau, basi jana nili piga mtungi mbaya, ile nafika home, si nika lala ndani ya gari” walicheka kwa pamoja wakisaidiwa na watu walio kaa nao karibu, ambao bahadhi yao wana wafahammu sana vjana awa marafiki, “ngoja pate mke, utabadirika tu!” aliongea Mahadhi akimalizia kicheko “Mahadhi hee! kwani wewe ugongi mtungi, tena shemji akiijuwa ile nyumba ndogo yako ya pale jirani yako, sijuwi utambebaje, unabahati simu nimeisahau kwenye gari, ninge kurecord uavyo bwabwaja alfu nimpelekee” wakati wanaendelea kuongea, mala wakasikia ving’ola vya police vikija upande wao, na kupitiliza kwenye jengo la pili, jirani na lile la kwao, kwa umbali wamita mia moja tu!, linaloitwa Kamanga Plaza, kwa mtaa hule palikuwa na majengo mawili tu! marefu, watu walitimua mbio kuelekea kule ambako magari ya polisi yalipoelekea, huku wakipiga kelele, Denis na Mahadhi walimaliza supu zao na kukimbilia kule walikoelekea wenzao, walijichanganya kwenye makundi ya watu ambao walizuiliwa na polisi wasizidi kusogea,
Yalikuwa ni mauaji yametokea, mchungaji maarufu Chilumba ameuwawa kwa risasi, ambayo inasadikiwa imepigwa na mdunguwaji, wazungu wanaita sniper, utumia silaha ya kulengea mbari, inayotumiwa na waduguaji wa kijeshi wenye mafunzo maalumu, polisi wakagundua pengine risasi imetokea upande wa kushoto wajengo lile inamaana kwenye gorofa lenye ofisi za kina Denis, sababu mzee Chilumba alipigwa kupitia dirisha la upende wa kulia wa jengo la KAMANGA PLAZA,
Wakiwa wanaendelea kushangaa juu ya tukio hilo geni kutokea katika jiji la Dar es salaam, Denis na Mahadhi wakamshuhudia polisi mmoja akiongea kwenye redio call “ hallow charle tango, akikisheni kila mtu anaetoka kwenye hilo jengo la Mazao, anasachiwa, na polisi wengine waingie nadani ya jengo, wafanye msako wa nguvu, umenipata over” kisha ikasikika sauti toka kwenye redio call yake “hallow charle papaa, nimekupata, na sasa askari wamesha zuwia mlango mkuu wakutokea, na wengine wameingia ndani wanaedelea na msako, over” kisha yule polisi akaongea tena, “Charle Tango, target ni silaha kubwa yakijeshi, umenipata over?” hapo ikasikika tena sauti toka kwenye redio, “nimekupata vizuri kabisa over” hapo Denis akakumbuka kitu, “mahadhi, ngoja niende kwenye gari nikachukuwe simu yangu, tutafute pozi nitoe lock, maana ofisini apaingiliki tena” aliongea Denis na kuelekea lilipo jengo la Mazao ambalo lina ofisi yao, huku moyoni mwake afurahia tukio hilo, maana atakuwa amepata mda wa kwenda kunywa pombe, Denis alipo lisogelea jengo lile, aliona mlango mkubwa wakuingilia, ukiwa umezungukwa na polisi wengi sana, yeye akaelekea kwenye gari lake kisha akazunguka upande wa siti ya abiria wambele, na kufungua mlango, alafu aka ingiza mkono kwenye mfuko ambao ulikuwepo kwenye ile siti, akaibuka na bia moja ya kopo, akatazamakushoto na kulia bila kuona mtu , akaifungua na kuanza kuinywa ile bia, kwa kuigugumia, yani gudu gudu, alitumia kama sekunde tano hivi mpaka kuishusha ile bia ikiwa nusu, akatazama tena kushoto na kulia akuona mtu, akaiweka tena bia ake mdomoni lakini safari hii kabala ajapiga ata funda mbili, akasikia “paaaaa” ikifwatia na sauti ya vioo kudondoka chini, hapo Denis akastuka na kutazama upande wa kulia wa gari lake, hapo Denis alimwona yule dada mzuri mwenye umbo lakuvutia, mama ntilie akiwa anaishangaa side mirror ya gari lake, (kioo cha kutazamia nyuma) ambacho kilikuwa kimevunjika, na yeye akiwa ndie mvunjaji, na alikivunja bahati mbaya, baada ya kugonga na lile begi lake jeusi , Denis aliuma meno kwa hasira, huku akishika kichwa “samahani ni bahati mbaya” aliongea yule dada mama ntilie kwa sauti nzuri ya upole, lakini Denis alibaki ameduwaa kama aliepigwa na butwaha, “ nibahati mbaya kaka yangu, ni bei gani nikulipe?“ aliongea yule dada akionyesha mwenye wasiwasi sana, lakini kiukweli akufanana na uwezo wakulipa ile side mirror “we! nenda tu dada, si umeshasema ni bahati mbaya” Denis aliongea kwa sauti ya upole sana, bia yake mkononi, huku anazunguka kwenda kutazama palipo vunjika, alikuta kioo chote kipo chini, kanamba kimegongwa na kitu kizito sana, hapo Denis akashangaa na kuinia ,acho kumtazama yule dada, kitu cha kushangaza akumwona tena yule dada mama ntilie.
Denis akajaribu kusunguka huku nahuku mahali pale lakini akumwona, akarudi kwenye gari lake akachukuwa simu yake na kumtafuta rafiki yake Mahadhi, kisha akamsimulia juu ya yule dada mrembo mama ntilie mwenye begi dogo jeusi, jinsi alivyo mgonga pale mgahawani na alivyo vunja side mirror, dakika chache zilizopita “yani kaka nimeshindwa la kufanya, ni mtoto wa nguvu, sijawai kuona mama ntilie mzuri kama yule” alimwaga sifa Denis “hahahahaha kweli hicho kitakuwa chombo, mpaka wewe umesema hivyo?, ebu nika kione” aliongea Mahadhi kwa kejeri “ametoweka ghafla, nambaya zaidi sijawai kumwona siku za nyuma” Denis aliongea akionyesha kuchachawa na huyo mwanamke “labda atakuwa mgeni pale kwamama bupe” kweli twende tuka mwangalie mgahawani” waliongea hayo wakiwa wamesimama mbele ya jengo lao, pamoja na wananchi wengine wakishangaa juu ya mauwaji yaliyo tokea, ambapo polisi hawakupata chochote, muuwaji alisha toroka, licha yakuangaika kwa masaa manne wakikagua kila mtu aliekuwepo mle ndani, lilikuja gari la wagonjwa nakubeba mwili wa marehemu, likisindikizwa na magari ya polisi, ** Yule dada mama ntilie alikuwa amesimama kwenye duka moja pembeni ya mgahawa, akijiunga nawatu wengine wengi, walio kuwa wamekaa pale akishangaa tukio la kuuwawa kwa mchungaji maharufu Chilumba, akiwa anatazama polisi wakiondoka eneo lile, mala akamwona kijana alie mvunjia kioo cha gari lake akiwa na mwenzie wakija upande aliopo, huku wakiongea jambo flani kwa msisitizo, wakaingia kwenye mgahawa, awakukaa muda mrefu wakatoka, wakaangalia huku nahuku, kisha waka sogea pale dukani wakasimama kwenye kundi lawatu, jirani kabisa na huyu dada mama ntilie lakini awakumwona, sababu alipowaona wakimsogelea akajificha akijibanza kwa watu wengine, walio kuwa wamesimama eneo lile, na aliwasikia kwa ukaribu wale vijana wawili wamkizungumzia, “ni kitu cha ukweli kaka” aliongea yule aliemvunjia kioo chagari, mwenzie akamwuliza “sasa unamtafuta wanini au unataka akulipe side mirror yako?” “hapana yani ata akitaka gari lote nitampatia, nimzuri huyo mwanamke sija pata kuona” aliongea mwenye kuvunjiwa kioo akifwatiwa nakicheko cha yule mwenzie, “manemno ya yule kijana yalimstua dada mama n’tilie, japo alisha wai kusikia vijana wengi wakitoa ahadi kama zile, juu yake lakini huyu alizidisha, na mbaya zaidi alionekana kuwa yupo makini na anacho kisema, kwamba akuwa na utani “yani wewe kweli pimbi, yule Jen wa ofisini amejipendekeza weeee, umemwacha, alafu eti una angaika kwa mama ntilie, usie mjuwa” waliongea wale vijana wakianza kuondoka eneo lile kuelekea ofisini ambako walitoka masaa manne yaliyopita wakienda kwenye chai, ndipo yule dada mama n’tilie alipo achia tabasamu dogo, huku nayeye akiondoka zake na kuvuka barabara kuelekea upande wa pili, huku moyoni mwake akiwaza tabia yake ya kuchukia wanaume wanaodai kuwa wanampenda, na siku zote yeye aliamini kuwa mwanaume anae mwambia anampenda ndie adui yake wakwanza, itaendelea
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU