
SEHEMU YA KUMI
ILIPOISHIA SEHEMU YA TISA : hapo Jackline akatabasamu kidogo “karibuni kuzimu,” ilisikika sauti tulivu ya Jackline masikioni mwa wale vijana, ambao waliduwaa wasimwelewe kabisa anacho maanisha huyu dada,ambae bado alikuwepo juu ya kitanda, zaidi walishangaa huyu mwanamke akuonyesha dalili yoyote ya uoga au wasiwasi usoni kwake, hapo walishuhudia tabasamu la hajabu sana, usoni kwa huyu dada, endelea …..
Wakatazamana usoni, kwa mshangao, kila mmoja akizani labda yule dada ni jinni, kutokana na kujiamini kwa kutoa ile kauli, ya karibu kuzimu, ** wakati huo ilisha timia saa tatu za usiku, magari yalikuwa yameanza kupungua barabarani, asa barabar kuu iendayo morogoro, Denis na Mahadhi walikuwa kwenye bar, ya Jambo pub, wakiendelea kunywa pombe, bar hiyo ipo pembeni ya barabara ya morogoro upande wapili, ikitazamana na jengo la ofisi yao (Mazao building) “we! Chapombe muda wakuondoka umewadia” aliongea Mahadhi huku anasimama na kujipapasa mfukoni, akatoa funguo ya gari, “poa kaka, wewe nenda, wacha mimi nimalizie hii ya mwisho, tutaonana kesho” aliongea Denis kwa sauti iliyozidiwa na ulevi, Mahadhi akaanza kuondoka, akielekea kwenye maegesho ya magari, akimwacha rafiki yake akiwa anakata maji, ** yule mhudumu wa vyumba baada ya kuwafungulia wale vijana watatu, mlango wa chumba cha Jackline alirudi mapokezi na kusikilizia, akijuwa kabisa kuwa mwanamke mwenzie ana bakwa na midume mitatu, alivuta picha jinsi tukio la mle ndani linavyotokea, aliona kuwa yule dada mshamba atakuwa ame kamatwa miguu na mikono, akiingiliwa huku analia kimya kimya, baada ya kutishiwa kisu, lakini aikuwa hivyo, maana azikupita ata dakika mbili, aliona ule mlango wachumba cha yule mdada ukifunguliwa, kitendo ambacho akutegemea, alimwona yule dada akitoka akiwa na mabegi yake mawili kama alivyokuja jana jioni, yule dada mhudumu akuelewa kilichotokea, alimwona yole dada akija upande wake, alitamani kukimbia lakini kilichompa moyo nitabasamu usoni kwa yule dada, ambae alipofika pale mapokezi, akamsogelea kabisa, wakawa uso kwa uso wakitenganishwa na meza, “nenda kawafunike mabwana zako” ni kauri iliyo ambatana na kitendo cha ghafla cha mkono mmoja wa yule dada, kumkamata mhudumu wa vyumba na kumvuta kwake, akimtandika kichwa cha nguvu,kilicho lenga katikati ya uso wa wa mhudumu, kilichompeleka chini yule mhudumu, na kumfanya ajishikilie sehemu ya pua iliyoshikwa na maumuvu makali sana, huku akianza kuisi maj maji ya moto yaki mchuruzika sehemu hiyo, alipo jiangalia alikuwa anatoka damu, yule mhudumu akajiinua haraka sana, alipoinuka akumwona tena yule dada, kwa kitendo kile, dada muhudumu akajuwa fika kuwa wale jamaa ndani hawapo salama, akatoka pale mapokezi huku akijishika kwenye pua yake, akizuwia damu, na kwenda kutazama kule chumbani, “kwanini wale jamaa wamemwachilia yule mwanamke”, aliwa za dada mhudumu, wakati akiingia ndani ya chumba kwa fujo, nusu ajikwae kwenye miili ya wale vijana watatu, ikiwa imelala kwenye dimbwi la damu, huku shingo zao zikiwa na majeraha makubwa ya kisu, yule dada mhudumu akapiga kelele zilizo wafanya watu wote walio kuwepo pale bar, wakimbilie kule chumbani, ** Denis alikuwa ameshamaliza bia yake, aliyosema kuwa ni ya mwisho, akanunua katon moja ya bia za kopo na soda nne aina ya cola nazo za kopo, na kuelekea kwenye gari, huku anayumba yumba, ghafla akakoswa koswa na gari la polisi lililokuwa speed, huku likipiga king’ora, Denis akatazama lile gari la polisi likiingia kwenye chochoro za mitaa, akasonya kilevi, na kuendelea na safari yake ya kulifwata gari lake, alipolifikia akazibana kwapani zile soda zilizo kuwa chache kwenye mfuko, huku mkono wa kushoto hukiwa umeshikilia bia, akaanza kufungua mlango wa gari, lake aina ya noah, akiwa anaangaika kulenga tundu la ufunguo kutokana na urevi, ghafla akasukumwa na mtu aliekuwa anapita njia, Denis aliyumba kidogo, huku soda zikimdondoka, yule mtu ambae alikuwa amebeba mabegi mawili, alionyesha busara, akasimama kisha akainama kumsaidia kuokota zile soda, akamkabidhi Denis, “samahani kaka yangu ni bahati mbaya” ilikuwa sauti tamu ya kike, muda wote Denis alikuwa ameganda akimshangaa yule dada, kumbe alisha mtambua, toka akiwa anaokota zile soda za kopo baada ya kuliona lile begi dogo jeusi, ni yule dada mama ntilie, Jackline naye akaduwaa, akamkumbuka huyu kijana “huyu tena” alisema kwa sauti ya kunong’ona ** wakati huo polisi walisha fika eneo la tukio, pale Mapambano bar and guest house, kwanza walizunguka eneo lote, na kuanza kukagua eneo zima ndani na nje, huku wakiwazuwia watu kutoka na kuingia eneo hilo, waliwaita wahudumu, kwa ajili ya kuwachukua maelezo, walipo muhoji yule dada mhudumu wavyumba, aliwaambia kuwa muuwajia ni mwanamke, akiwaeleza jinsi alivyo na mavazi yake, na mizigi aliyobeba, “yani ametoka sasa hivi”, haraka sana polisi waligawana, wengine wakabaki pale mapambano bar na wengine wakatoka nje wakijaribu kufwatilia huyo mwanamke alikoelekea, wakiwa kwa miguu, walielekea kule aliko elekea Jackline, njiani waliangalia kwa umakini kla waliepisha nae, wakifwata maelekezo ya dada mhudumu. *** Jackline Michael Nyati alimtazama kwa umakini, yule kijana aliemvunjia kioo cha gari mchana wa siku ile, huku mapigo yake ya moyo, yakienda mbio, akamwona yule mkaka akiyumba yumba kwa ulevi, “we.. we! Mwanamke mbona ninabahati sana nawewe,” Jackline alitamani kucheka lakini akajizuwia “ebu.. ebu.. nisaidie kufungua mlango wagari, maana mikono yangu imelegea ghafla baada ya kukuona” aliongea kilevi yule kijana, akimnyooshea funguo zagari Jackline, hapo Jackline akaona huyu kijana analeta mazowea, akataka amtwange japo kichwa kisha aondoke zake, lakini wakati anajiandaa, aliwaona polisi wanne wakija upande wake huku wakiangalia kila mtu wanae pishana nae, akakumbuka alipishana na polisi wakati anatoka Mapambano bar, lakini sasa wapo kwa mguu tena atua chache toka pale alipo, hapo Jackline akaidaka funguo ya gari toka kwenye mikono ya yule kaka, na kufungua mlango wadereva, kisha aka fungua mlango wa dereva kabla hajazunguka na kufungua mlango wanyuma na kuingia haraka sana na kisha kuufunga, akimwacha yule kijana mlevi Denis akimshangaa, Jackline akaomba sana huyu mlevi asilopoke neno lolote “kumbe unataka rift” alionge Denis kwa sauti ya kilevi, huku anazirushia bia na soda kwenye kiti cha jirani yani cha abiria wa mbele, wakatihuo wale police walikuwa wanakatiza pale walipo, wakiwa makini na silaha zao mikononi, yule kijana mlevi aliingia kwenye gari, kisha akakaa kwenye kiti cha dereva, akawasha gari na kuingiza gia ya kuondokea, akaikamata barabara kuu ya morogoro, safari ya kuelekea nje ya mji ikaanza, “sasa.. we!..mdada una elekea wapi?” Denis alikumbuka kama yupo na mtu mle ndani ya gari, “niondoe maeneo haya, maana mama ninaye kaa naye, amewatuma watu wanataka wanibake” aliongea Jackline kwa sauti ya uoga wa kuigiza, iliyo changanyika na wasiwasi ya kweli, maana aliofia mwendo mkali wa gari lile, na jinsi dereva mwenyewe alivyokuwa amelewa “mh! huyo mama ni ndugu yako?” aliuliza Denis akionyesha dailili ya huruma, lakini katika hali ya ulevi “hapana mimi nimekuja juzi toka Songea, nimekuja kutafuta maisha, ndo nimefikia kwake” Jackline alicheza na akili ya Denis “loooh! Kwa hiyo sasa hivi, auna pakukaa?” aliuliza Denis huku akizidi kukanyaga mafuta, wakati huo alikuwa akipita ubungo mataa “ndiyo sina pakukaa, ila usijari nita pata tu!” aliongea Jackline huku wasiwasi ikizidi, kutokana na mwendo wa kijana huyu mlevi “dada yangu usijari, utafikia kwangu utakaa kama kwako” maneno hayo yaliupasua moyo wa Jackline, hapo haraka sana mawazo mawili yakamjia kichwani, moja ni kwamba, huyu kijana amesha mtamani, kwake mwanamume anaye mtamani ni adui yake, pili huyu kijana amememuokoa kwa polisi, pia anaweza kuwa msaada kwake, kwa sababu amesha fanya amuwaji nyumba ya kulala wageni, hivyo polisi wanaweza kuanzisha msako mkubwa kwenye nyumba zote za wageni, ikawa rahisi kumstukia au kukamatwa kabisa, hivyo akikaa kwa huyu mlevi itakuwa nafuu kwake, lakini itakuwaje endapo atataka kitumbua, “mkeo je?, si’ataniuwa?” aliongea Jackline akimtega Denis ambae bado alikuwa amjuwi jina, “haaa wapi? mkeee atoke wapi?” aliongea Denis kwasauti kubwa ya kilevi, iliyomfanya Jackline acheke kwa sauti ya chini, sasa wasiwasi wakufika salama ulipungua baada ya kuona yule kijana mlevi yupo makini sana na uendeshaji wa gari lake, sasa walikuwa anaingia mbezi mwisho, ndipo Denis akatafuta sehemu nzuri karibu na bar, akaparki gari, Jackline akamtazama kwa umakini sana, akujuwa yule kijana mlevi anataka kufanya nini, Denis akamgeukia Jackline, ambae alikuwa amekaa seat ya nyuma, huku akiachia tabasamu lake la kilevi, hapo Jackline akaona kuna dalili ya kujeruhi mtu au kuuwa kabisa, maana alihisi kuwa huyu kijana mlevi ameingiwa na tamaa ya kimwili, itaendelea…………
JE? DENIS ANATAKA KUFANYA NINI,
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU