BINTI MDUNGUAJI (12)

SEHEMU YA KUMI NA MBILI

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI MOJA : huku akisikiliza zile habari zikisomwa kwa kifupi, habari moja ilimvutia sana bwana Michael, iliyosema kuwa viongozi wa dini watoa tamko juu ya mauwaji ya mchungaji Chilumba, habari hii iliambatana na picha ya watu watatu wakiwa wamesimama, alichoweza kuona ni jina la gazeti kisha ile habari ikapita, alitaka kujilidhisha na ukweli wa alichokiona kwenye picha, akaagizia gazeti mjini haraka sana, endelea …….
Wakati huo Denis naye alikuwa anapark gari lake kwenye maegesho ya kazini kwao manzese, nje ya jengo la Mazao, akaliangalia gari la rafiki yake Mahadhi kama alikuwa ameshafika, akuliona alikuwa bado ajafika, akashuka kwenye gari, akiwa na makopo mawili matu ya bia, alizo kuwa amezinywa njiani, akafunga vizuri Milano ya gari lake aina ya Toyota Noah, kisha akapitia kwenye debe maalumu la kutupia taka taka, (garbeg bin) akayapupa yale makopo, na kuelekea ndani ya jengo, muda wote alikuwa akimuwaza yule dada mama ntilie alie mwacha nyumbani kwake, huku mpango wake ukiwa ni kwenda kutoa udhuru ofisini, ili akakae namgeni wake, ikiwezekana ajaribu kumweleza jinsi anavyo jisikia moyoni mwake, maana jana akuweza kuongea nae vizuri, baada ya kupitiwa na usingizi, na ukichukulia kutongoza kwake ilikuwa kazi ngumu sana, maana toka alipo tongoza kipindi yupo shuleni, na siyo kwamba alitongoza ni kwamba mwanamke alijilengesha mwenyewe, Denis akiwa bado anapandisha ngazi, akasikia sauti ya Mahadhi akimwita toka nyuma yake “vipi kaka inamaana ukuniona wakati napark gari?” aliongea Mahadhi huku akipandisha ngazi haraka haraka, nusu ya kukimbia, “haa! nimeangalia gari lako sijaliona, nikajuwa bado ujafika” aliongea Denis hulu akisimama kumsubiri mwenzie, “basi ile wewe una toka tu! hapo park, na mimi naingia, nikajuwa umeniona ila una muwai Janeth” wote wakacheka, Janethi ni secretary wa boss wao, waliongea mengi sana huku wakipandisha ngazi “ujuwe leo sijisikii vizuri, nataka nimwambie bosi naenda yumbani kupumzika” aliongea Denis, akimdanganya Mahadhi alihisi akimwambia ukweli juu ya mama ntilie, angemtania sana, na kudadisi mambo mengi tena pengine ange taka waende wote akamwone, kwa sababu Mahadhi akumwona yule mdada jinsi alivyo mzuri, “mh! au mtungi wajana ulikuzidi, tena hapo ulipo una arufu ya pombe, kama umetoka kuongezea sasa hivi” aliongea Mahadhi kwa sauti ya chini, maana ndio walikuwa wakiingia kwenye ofisi yao “ho! Wanaume ndio mnaingia kazini” walipokelewa na Janeth secretary wa boss wao, alie kaa kwenye kiti chake cha kuzunguka, mbele ya meza kubwa, yenye computer na makablasha kadhaa, huku TV, kubwa ikiwa kwenye kona moja ya chumba kile kikubwa cha mapokezi, “leo kijana wako amewai hen?” alichombweza Mahadhi, sababu anajuwa kuwa siku zote amekuwa akimshobokea Denis, lakini Denis akuwa tayari kusawazisha, “nimeona, tena leo Denis kapendeza sana, nitampa offer ya lunch mkirudi” alibwabwaja Janeth akiendelea kuweka vitu vyake sawa , tayari kwa kazi, “tukirudi?, tukirudi Kutokawapi?” aliuliza Denis kwa hamaki, na mshangao, wakati mwenzie Mahadhi, alishangaa kimya kimya, maana awakuwa na safari yoyote ya kikazi leo, “boss ameniagiza kwamba, mkifika tu! nendeni kwa mhasibu, mkachukue fedha kwa ajiri ya mafuta ya gari, kisha muende kisalawe, kuna wahindi wanataka kujenga gholofa, mkaiangalie site, malipo ya ziada mtayapata huko huko” Janeth aliwakabidhi na namba za simu, za hao wahindi, kiukweli Denis hakuwa na namana ilibidi aifanye hiyo kazi, maana licha ya kuwa na ujuzi zaidi ya mahadhi wa kuset majengo ya kuyasanifu, pia ilipo tokea kazi kama hiyo uwa wana ipwa fedha nyingi sana, wakaondoka mala moja wakitumia gari la mahadhi, wakiofia kutumia la Denis kutokana na kukosa side morror * saa mbili asubuhi, Jackline alikuwa amemaliza shuguli zake, sasa alikuwa ametulia kwenye kochi amewasha TV akiangalia habari za matukio na michezo, alikuwa amesha fahamu jina la yule kijana mlevi, ni baada ya kupekua na kuchunguza chumbani kwa yule kijana mlevi, alikuwa anaitwa Denis Edgar Mbogo, akajuwa kuhusu kazi yake, kuwa ni msanifu wa majengo na mbunifu wa ramani za majengo ya aina zote, kingine alicho gunduwa, ni kwamba mle ndani ya nyumba hapakuwa na dalili ya kuwa kuna mwanamke aliwai kuishi, Jackline akiwa anaangalia TV, mala akastushwa namlio wasimu yake, akaitazama kwenye kioo, “baba, hooo! shit!” alikuwa amesahau kumpa report ya asubuhi kama alivyo agizwa kufanya kila asubuhi “hallow! shikamoo baba” aliongea kwa utulivu Jackline, mala tu baada ya kupokea simu, “malahaba mwanangu, naona leo umelala sana ugenini, vipi hupo peke yako?” tofauti na alivyo tegemea, baba yake aliongea taratibu na kwa upole “ameenda kazini, nimebaki mwenyewe” aliongea Jackline, wa sauti tulivu huku anainuka na kuchungulia nje ya dirisha, “ok! sikiliza maelekezo, kuna target imeonekana, inabidi uifwatilie” baba mtu aliongea na kuanza kutoa maelekezo ** Saa mbili nanusu Ndani ya kituo kikuu cha cha polisi, Inspector Johnson David alikuwa amesimama mbele ya askari kumi, wakiwa na vyeo mbalimbali, wakiwa wamejipanga mistari miwili, walio valia mavazi ya utayari kimapambano, na bunduki zao aina ya SMG, zikiwa mabegani mwao, Inspector Johnson David alipewa report na askari mwenye cheo cha sajenti, kuwa wote wapo na wapo tayari kwa kazi, akaamuru waingie kwenye magari kisha uelekeo asubuhi ile ni kule manzese ya lipo tokea mauwaji ya mchungaji Chilumba, kwenye jengo la Kamanga Plaza, kumbe baada ya kuwaza sana Inspector Johnson David, akakumbuka kuangalia security camera za jengo la pembeni na Kamanga Plaza, linalojulikana kama Mazao Building, ambalo muuwaji alitumia kumdungua mchungaji, safari ikaanza kuelekea manzese, ** saa tatu kasolo Jackline alikuwa njiani, kwenye kituo cha daladala cha kibamba njia panda ya shule, akisubiri mabasi aina ya Toyota coster, yatokayo nje ya mji kibaha chalinze mpaka msata na mkata, akiacha hiace ambazo utumia muda mrefu kufika mjini, kabla ya kuingia kwenye basi alinunua gazeti moja, kwenye meza za wauza magazeti, walipo eneo hilo la kituo cha daladala, leo alikuwa amevaa gauni moja kubwa kama la jana, lakini hili lilikuwa jipya kidogo lililo shonwa kwakutumia kitenge, pia begani alitundika upande wa kitenge, na mwingine akiwa ameufunga kiunoni, kichwani mwake akiwa amejifunga kilemba kibwa cha upande mzima wa kanga, nakumfanya azidi kuonekana mzuri zaidi, leo Jackline, akuwa na begi jeusi, ila kama kawaida yake, ndani ya gauni lake la kitenge, alivaa kikaptula chake cha jinsi, akiwa amenig’iniza bastora yenye silence baller na upande mwingine, kisu kikali cha kijeshi, aikuwa lahisi basi kustukia kutokana kuzibwa na ukuwa wa hipsi na makalio yake ya kuvutia, gari lilifika na Jackine akapanda, akiwa na gazeti mkononi, alifwata seat iliyo kuwa wazi, na kukaa, kisha aka geuza gazeti lake, ukurasa wambele kabisa, kulikuwa na picha ya watu watatu, na kichwa cha habari ya picha hiyo kilisema, viogozi wadini watoa tamko kifo cha mchungaji Chilumba, akasoma maandishi chini ya picha, ni kweli ya liwatambulisha wale watu wa kwenye picha, Jackline hakuwajari wale wengine, yeye alimjari wakatikati, maana wakulia tayari alisha kufa ni mchungaji Chilumba, wa kushoto msaidizi wa mchungaji Kileo, ambae ndie alie mkusudia katika ilepicha, japo maelezo ya baba yake ni kwamba, aende akamfwatilie apajuwe anapoishi, kisha ajuwe watu atakao kutana nao, pengine ange wajuwa wengine zaidi, kisha baada ya hapo ndie awe wapili baada ya mchungaji Chilumba, ** Denis na Mahadhi tayari walikuwa kisalawe, kwenye site wakiseti jengo ambalo ina bidi lijengwe hapo, namna jengo litakavyo kaa, ili wakaichagulie ramani moja wapo kati ya nyingi zilizopo ofisini kwao, awakutumia muda mrefu sana mahali hapo, wakakubariana na wateja wao, ambao waliwaelekeza waende upanga (mtaa) ambako zipo ofisi za wateja wao, kwa ajili ya malipo ya ziada, wakaingia kwenye gari na kuanza safari, walitumia gari la Mahadhi gari la Denis walilihacha ofisini kwa kuwa alina side mirror moja, ambayo Denis alipanga akisha toka upanga achukuwe gari lake akatafute side mirror kwenye maduka ya spare za magari, kisha aelekee nyumbani kumuwai mgeni wake, ambae jana usiku alishindwa kuongea naye kutokana na kupitiwa na usingizi, ‘hivi Denis unajuwa kuwa jana yame tokea mauwaji mengine, mitaa ya ile karibu na bar tuliyo kuwa tume kaa jana usiku?” alongea mahadhi lakini Denis akustuka, “mbona mimi sikuona, au nilikuwa tungi sana?” aliliza Denis huku akitamani kumaliaza mizunguko mapema apate chakula na bia ata mbili hivi, “mimi mwenyewe nimesikia asubuhi hii, wengine wana sema kuna demu sijuwi ni jinni, lime uwa watu watatu, yani midume kabisa, na mapanga yao” hapo Denis akacheka sana, kiasi cha ku shangaza Mahadhi, “ina maana mimi naongea upuudhi?” aliuliza Mahadhi kwa hamaki akionekana kukasilishwa na kitendo cha Denis kucheka namana hile, “hilo ni kwanyinyi wazinzi, weunazani jinni lina mpenda mlevi?” hapo wote wakacheka, huku safari ikiendelea, ** Inspector Johnson David alikuwa mbele ya computer za chumba cha usalama, cha jengo la Mazao, akiwaangalia sana watu walioingia na kutoka ndani ya jengo ilo jana, muda ambao mauwaji yalitokea, baada ya kupitia HDD za computer zinazoendesha camera za usalama kwenye lile jengo, kwamuda mrefu sana, akuna alichokiona zaidi ya mschana mmoja alievalia gauni cha kavu, huku amebeba sahani mbili za chakula, na begi dogo jeusi kwa pani, lakini awakujua alikoelekea zaidi ya kumwona akirudi nje akiwa na sahani tupu, hapo Inspector akatia shaka kidogo, juu ya yule dada, maana alificha sura isionekane kwenye camera, unge zani ni mtu ambae alijuwa uwepo wa camera zile ndani ya jengo lile, ila mwonekano wa yule dada wakifukara, ukamfanya apotezee yale mawazo yake ya kumtilia shaka, akaona bora aende hospital ya muhimbili, ambako mwili wa marehemu Chilumba na wale vijana watatu ilihifadhiwa, japo miili ya wale vijana wabakaji aikuwa mihimu kwake, ilihifadhiwa hapo kwaajiri ya uchunguzi zaidi na kusubiri mazishi, na yeye aliamua kwenda kupata report ya madaktari, maalumu, toka kwenye jeshi la polisi, baadea ya kushuka toka kwenye dala dala, kituo cha buguruni rozana, jackline akaanza kutembea kuelekea msibani, kwenye kanisa la mch Chilumba, akatoa simu yake, na kumpigia baba yake, ambae alimweleza kuwa ameshalipata gazeti na sasa anaelekea msibani, hile kutaamaki akashangaa simu yake imekwapuliwa na kijana mmoja, ambae litimua mbio na kutimua mbio, kilikuwa kitendo cha ghafla, kama kipanga anavyo pitia vifaranga vya kuku, huku yule kijana aifwatiwa na mwenzie, na sasa wakawa wawili, hapo Jackline akatabasamu, pasipo kupiga kelele za mwizi, kama wafanyavyo watu wengine wanapoibiwa, akatazama kusoto na kulia, akaona watu wachache tu! wakimtazama bila msaada wowote, hapo Jacklini akainama na kushikilia gauni lake kwa chini, akainua gauni lake na kulishikia kwa juu, na kuanza kuwa kimbilia wale wezi, kwani aliangalia mbio za wale vijana, akaona zipo ndani ya uwezo wake, , “weee dada usuwafwate weweeee” zilisikia sauti za watu kimtahadharisha Jackline kuwa asiwafate wale vijana, ambao walikimbia mbio nakuingia kwenye vichororo vya hapa buguruni, upande wa kwa mzee malapa, wakidai itakuwa hatari sana kwake ** vijana awa wenye mwonekano wa kudhoofu, kwa matumizi ya mihadarati, walikimbia na kwenda kutokea kwenye uzio wanyumba moja, ambayo ilikuwa chakavu, na hapo waliingia kwa fujo na kuwastua wezao watatu, walikuwa wanatumia dawa za kulevya, wengine wakijichoma kwa sindano wengine walikuwa wanamisokoto ya bangi mdomoni, “hoya wana vipiiii, mnakata stimuuuu?, mnakuja mbiiiiooo” aliongea mmoja kwa sauti ya kilevi, akiwalaumu wenzake, kwa kumwaribia starehe yake, lakini alipowaona wakiwa wameshika simu nzuri, akachanua tabasamu la kilegevu, utazani anausingizi, “hoyaaa wapi tena, meutoa uo mzigo mpya kabisa” aliuliza yule alie walahumu wenzake mwanzo, ndie alionekana kuwa mbabe wao pale, huku akinyoosha mkono ili apewe ile simu, “kuna demu mmoja hivi alikuwa na mbwela mbwela, hapo mtaa ya katat…” akuwai kumalizia maneno yake yule alie shika simu, akastulliwa na sauti toka nyuma yake, “mimi hapa” wote wakageuka kwa mstuko, baada ya kusikia sauti ya kike nyololo, hapo wote watano wakatabasamu, wakiamini wamepata kitu chabuleee, “hoyo, sikilizeni wanangu, hapa mimi mwenyewe na kuwa wakwanza, alafu ebu msachini kwanza,” maneno hayo Jackline aliyasikia, na kuzidi kumtia hasira, wale vijana ambao kwa sasa walisha fikia idadi watano, walishuhudia yule dada mrembo sana, akifunua gauni lake, na wao kuliona paja lake laini lililo nona na kuwa fanya dudu zao zisisimke, na kuanza kusimama tayari kwa kazi ya kutafuna kitumbua, kwa kitendo kile, vijana walizani, mschana mrembo ameamua kuwapa kitumbua kwa iyali yake, lakini walishangaa kuona akiibuka na kisu,”wasalimieni kuzimu” ilikuw nisauti moja ya kutisha, toka kwa mrembo huyu, ** kumbe tukio lile la yule dada kuonekana kuwa ana wakimbilia wale wezi lilionekana kwa watu pale mitaa ya rozana, kuna bahadha ya wananchi wakaonelea waende kufatilia lile tukio, lakini kutokana na sifa zakutisha za wale vijana, wakashidwa kwenda kufwatilia, watu wakiwa wame jikusanya kikundi, bado wana jadiliana la kufwanya mala waka mwona mmoja kati ya vibaka maarufu wa lile chimbo, akija maali walipo simama wao, huku ame jishika tumboni kwa mikono miwili, iliyo lowa damu, wakamshangaa akizidi kuwasogelea, kwa mwendo wa kidhaifu sana, akionyesha kuwa amezidiwa na maumivu makari sana, lakini alipo wakaribia wakamwona akiziwa na maumivu na kujibwaga chini, huku akiacia mikono yake aliyo kuwa ame jishikilia tumboni, hapo watu wakapiga kelele za uoga na kutawanika, wakiwaacha watu wachache wenye roho ngumu, wakishuhudia tumbo la yule kibaka mteja, likiwa wazi kabisa na kuruhusu utumbo wa kijana huyu, kutawanyika kama mbuzi alie pasuliwa, dakika chaahe baadae polisi walifika mahali pale, na kuuliiza kilicho tokea, wakaelezwa jinsi tukio lilivyo kuwa, mala moja polisi waka elekea kule aliko tokea yule kibaka, kwa kufwata michilizi ya damu, wakiamini wata mkuta huyo mwanamke aliekuwa anawakimbiza, huku wakionganisha na tukio la mauwaji ya jana usiku manzese, lakini walipo fika eneo la tukio, walistaajabu walicho kikuta, walikuta miili ya vibaka wanne ikiwa imelala kwenye madimbwi ya damu, huku majalaha makubwa shingoni mwao yakione kana kwa uwazi kabisa, tayari walikuwa wamesha kufa, na muuwaji akuonekana, itaendelea ……

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!