
SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI MBILI : kwa kufwata michilizi ya damu, wakiamini wata mkuta huyo mwanamke aliekuwa anawakimbiza, huku wakionganisha na tukio la mauwaji ya jana usiku manzese, lakini walipo fika eneo la tukio, walistaajabu walicho kikuta, walikuta miili ya vibaka wanne ikiwa imelala kwenye madimbwi ya damu, huku majalaha makubwa shingoni mwao yakione kana kwa uwazi kabisa, tayari walikuwa wamesha kufa, na muuwaji akuonekana, endelea…….
* wakati wao wana wana shangaa kule kwa vibaka, Jackline alikuwa ameshafika msibani, kanisani kwa malehemu mch Chilumba, na kujichanganya na waombolezaji, akikaa upande wa wakinamama, huku macho yake ya kiwa kule walikokaa wanaume, akijaribu kufananisha sura aliyoiona kwenye gazeti, yani ya mchungaji Kileo, pale msibani zilisikika sauti za musiki kwenye maspeeker makubwa, zikipiga nyimbo za maombolezo, na matangazo ya hapa na pale, Jackline akatazama sana sehemu walipokaa wanaume, asa wenye umri mkubwa, alishuhudia waandishi wa habari mbalimbali, pamoja na vituo vya redio na tv, wakiwahoji wazee waliokuwa eneo hilo, aliweza kuwaona wazee wengi sana, lakini akuiona ile ya sura ya kwenye gazeti, ya mchungaji Kileo, muda mfupi baadae, yaliingia magari matatu, mawili yakiwa madogo meusi aina ya Range Rover, na moja basi dogo aina Toyota Coster likiwa na dereva peke yake, ubavuni limeandikwa na jina la kanisa moja lakilokole Daraja la uokovu, (jina la kubuni) walishuka watu watatu kwenye gari la pili, aina ya Range Rover, wakiwa wame valia suit nyeusi, mmoja akiwa ni mzee wa makamo, na wawili vijana walio jengeka kimazoezi, wakionekana ni walinzi wa huyu mzee wa makamo, moyo wa Jackline ulichanua kwa furaha na tabasamu la matumaini, ni baada ya macho yake kutua usoni kwa yule mzee wamakamo alie shuka kwenye gari, ambae alikuwa amevalia mewani nyeusi ya jua, alikuwa ni mwanajeshi mstaafu sajenti Kileo, ambae sasa anaitwa mchungaji Fredrick Kileo, Jackline alimwona mchungaji Kileo akielekea walipokaa wazee wenzake, ambao nao walionekana kuwa ni watu wenye uwezo wa kifedha, mchungaji Kileo akasalimiana nao, kwa kushikana mikono na kila mmoja, huku wakipeana pole, mwisho akakaa jirani na wazee mmoja alie valia suit kama yeye na miwa ni nyeusi, lakini yeye alivalia na kufia kubwa nyeusi ya duara, Jackline akawaona wakinong’onezana jambo, na dakika chache baadae Jackline alimuona mchungaji Kileo, akiinuka pamoja na yule mzee mrefu mweusi alie valia kofia kubwa ya duara, wakasogea pembeni, huku wale vijana wawili shupavu, wakiwa sogelea kidogo na kusimama pembeni yao wakiwaachia atuwa chache, ili waongee bila wao kusikia walikuwa wakiongea nini, inaonyesha ni walinzi makini wa mchungaji Kileo, Jackline aliwaona wale wazee wawili wakiongea kwa muda mrefu, wakijadiriana jambo, Jackline akaona atumie muda huo kusogea eneo hilo, pengine angesikia na kugundua jambo ambalo lingemsaidia katika kazi yake, ya kuwa saka na kuwa maliza wabaya wa baba yake, Jackline aliinuka na kuelekea pale walipo simama wale wazee wawili, akijifanya kama anatafuta kitu flani, lakini wakati anawakaribia, ghafla alishangaa amesukumwa kwa nguvu sana, nusu ya kuanguka chini, alisaidiwa na wepesi wake kutokana mazoezi aliyo kuwanayo na uimara, kujizuwia kuanguka, aligeuka haraka na kumtazama yule aliemsukuma, alikuwa ni kijana mlinzi wa mchungaji Kileo, “usisogee huko, pita kule” ilikuwa sauti kavu yakuchukiza toka kwa yule kijana shupavu, huku wale wazee wawili, pamoja na watu wengine wengi pale msibani, waliona tukio lile, waombolezaji wengi walisikitika sana,kwa tukio ile ambalo walilichukulia kama ni tukio la kinyanyasaji, “namana vijana walio jengeka kimazoezi, wakijichukulia ujiko, mbele ya bossi wao, kwa kumnyanyasa mwanamke dhaifu, aliejitolea kuja kwenye msiba wa mchunagaji Chilumba” hayo yalikuwa ni mawazo ya waombolezaji walio wengi pale msibani, ilawale wazee wawili akiwepo mchungaji Kileo, waliangalia kisha wakatabasamu, alafu wakaendelea na maongezi, Jackline alishikwa na hasira kali sana, ikamjia hamu ya kuuwa, japo akupanga kufanya hivyo mapema kiasi hiki, kama alivyo elekezwa na baba yake, maana ilikuwa ni mapema sana toka ya fanyike mauwaji ya mchungaji Chilumba, siku moja iliyo pita, yani jana, ndio maana leo aliiacha silaha yake kubwa, aliwatazama wale wazee akawaona wakiendelea na story zao, akawatazama wale vijana wawili, ambao nao walikuwa wakimtazama, nakufanya macho yao yagongane, Jackline akaachia tabasamu baya sana, ambalo tena adimu kulitoa, linapooneka ilo tabasamu uwa ni ishara mbaya sana, ata baba yake akiionaga ilo tabasamu uwa makini sana mda huo, maana kuna kitu kinaweza kutokea, ni tabasamu lililo wastua wale vijana, walinzi wa mchungaji kileo, kisha Jacklin akamwambia yule alie msukuma, alikuwa bado yupo karibu yake, kwa sauti ya chini sana “kaa tayari kaka” kisha Jackline akakunja sura na kuirudisha ile ya upole, akageuka na kuanza kurudi alikokuwa amekaa mwanzo, na kumtazama Mchungaji Kileo, ambae ndie wakatika katika ile picha kwenye gazeti, na ndie aliekusudiwa kuwa anaefwatia kufa, baada ya mchungaji Chilumba, maongezi ya wazee awa wawili hayakutumia mda mrefu sana wakarudi walipo kuwa wamekaa mwanzo, kisha wakamwita mmoja kati ya walinzi na kumpa maagizo flani, nayeye akaenda kwa mzee mmoja ambae alionekana kuwa ni muusika kwenye ule msiba, akamnong’oneza jambo, kisha yule mlinzi akarudi sehemu yake, karibu na mwenzie wakisimama nyuma ya kocho alilo kalia mchungaji kileo, dakika chache baadae likasikia tangazo, toka kwenye maspika makubwa ambayo yalitumika kupigia nyimboza maombolezo “yeyote anaetaka kwenda hasptal ya Muhimbili, anaweza kungia kwenye coster, tuungane na mchungaji kileo, ambae anaenda kuuangaia mwili wa mchungaji Chilumba” hapo Jackline aliachia tabasamu, huku akiwa mmoja kati ya watu wachache walio inuka na kuelekea kwenye basi dogo aina ya Toyota coster, “lazima kieleweke, nikipata mwanya mdogo tu! nita wafundisha adabu awa vijana” aliwaza Jackline muda mfupi tu! baada ya kuingia kwenye basi, na kukaa kwenye seat, ** inspector Johnson David aliinia ndani ya Ofisi ya kitengoo cha uchunguzi, kinacho simamiwa na madoctor toka jeshi la polisi, ambao wali mpatia majibu ya uchunguzi katika mwili wa malehemu Chilumba, “malehemu ameuwawa kwa kupigwa na risasi, aina ya hE exprosive, 7.62 mm, ya silaha aina ya sniper mugnum rifle, toka ussr, toka umbari wa mita mia mbili na hamsini, alama za vidole hakuna” aliongea Doctor wa polisi, ambae alikuwa aisoma kwenye karatasi, kisha akafunga lile karatasi na kuchukuwa jingine, “kuna hii report ya miili ya wale vijana watatu, kama ungependa kujuwa majibu yake,” alisema yule daktari, akimtazama Inspector usoni, “ni vyema ningefahamu pia” alijibu inspector Johnson David, na yule Doctor akaendelea kusoma, “vipimo vinaonyesha kuwa muuwaji alikuwa mmoja tu, alietumia kisu kikari chenye upana zero mills mpaka tatu, na meno kama ya msumeno yenye urefu wa cmm moja, ni visu ambavyo viliwai kutumika nchini, miaka ya 1985 mpaka 1990, na askari maalumu wa jeshi la ulinzi, vilivyo tengenezwa nchini islael, mwaka 1978, pia kuna arama za vidole bahadhi ya sehemu zao za miili, lakini hazija fnana na mtu yoyote ambae arama zake zimesha wai kupatikana, licha ya hivyo kuna alama za upigwa na vitu vizito, ambavyo vina mwoekano wa ngumi lakini uzito ambao umetumika ni wa nyundo ya chuma, iliyo sukumwa kwa uzito wa kilo mia moja” alimaliza yule Doctor wa polisi, report hii ya pili ndi iliyo mstua inspector Johnson David, kuliko ile ya kwanza, maana ile report, ili onyesha kuwa muuwaji wa wale vijana wabakaji, alikuwa ni zaidi ya hatari, ambae yeye alifahamu kuwa ni mwanamke toka shamba, ndie alie toka pale Mapambano guest and bar, eti ngumi yenye msukumo wa kilo mia moja, “naweza kwenda kuona miili ya hao marehemu?” aliuliza inspector Johnson David, “bila shaka afande, tuna weza kuongozana” alijibu Doctor, wakainuka na kwenda kwenye sehemu ya kuifazia miili ya marehemu, dakika chache baadae walikuwa wamesha fika eneo la mutual, ambalo lipo kwenye ya bara bara kuu mle ndani ya hospital, hapo shughuli zote zika sitishwa, wakimpisha inspector Johnson David, aikague miili ya marehemu, ** saa tano na nusu magari matatu yalikuwa yanaingia ndani ya hospital kuu ya taifa, yakiwa ni mawili madogo aina ya Range Rover, moja likiwa mbele moja kati kati ya coster lenye watu wengi sana ndani yake, liliuwepo nyuma, kati ya magari hayo matatu, yalienda moja kwa moja na kusimama kwenye maegesho ya pale mutual, kisha watuwengi wakaanza kushuka kwenye magari yale, wakati Jackline na waombolezaji wengine wakishuka toka kwenye basi dogo, mchungaji Kileo na walinzi wake walishuka toka kwenye Range Rover Jeusi, akaelekea mapokezi pale pale mutual, akiongozana na wazee wawili watu walio onyesha kuwa ni wazee wenye busara zao, wakaomba kuingia ndani kwaajili ya kuuona mwili wa mpendwa wao, laini wakaambiwa kuwa wasubiri kidogo, maana kuna inspector Johnson David ndani ya sehemu hiyo, akikamirisha mambo ya kikazi, mch Kileo akuwa na ujana akarudi kwa waumini wenzake, na kutulia akisubiri inspector atoke ili na yeye aingie akamwone Rafiki yake bwana Chilumba, huku mmoja kati ya wazee aliongozana nao mapokezi, akiwa tangazia waombolezaji kuwa, wasubiri kidogo polisi wamaize kazi zao wao pia wata ruhusiwa kuingia, pale alipo kuwa ame kaa bwana Kileo aliwaza mengi sana, juu ya kifo cha mchungaji mwenzie, “inamaana alikuwa ana ugomvi na watu flani” yalikuwa ni mawazo ya mchungaji Kileo, kabla aja banwa na mkojo, na kuwaomba walinzi wake wamsindikize kwenye choo cha jumuia kilichopo umbari wa mita miamoja toka pale walipo kuwepo, hapo walinzi wa mchungaji kileo, waliwai kwenye mlango wa choo na kuzuwia mtu yeyote hasiingie mle ndani, huku wakiwaondoa watu walio kuwepo mle ndani ya choo, baada ya kuingia ndani ya choo, mchungaji kileo alimkabidhi simu zake zote mbili, mlinzi wake mmoja, na kuingia kwenye choo kimoja, kati ya vingi vilivyomo mle ndani, ya jengo kubwa la vyoo, akiwaacha walinzi wawili nje wakiangalia usalama wake, huku nako Jackline akiwa amejitanda kanga zake vizuri kabisa aliwafata nyuma, mpaka alipo waona wakiingia chooni ndipo na yeye alipoongeza mwendo na kuingia choo cha kiume,** baada ya kumalizana na matajiri wao wa kihindi, maeneo ya upanga karibu na ofisi za wizara ya ulinzi, Denis na Mahadhi wakaonelea watafute sehemu nzuri ya kupata chakula kidogo wachangamshe matumbo, “unajuwa toka asubuhi hatuja pata chochote” aliongea Mahadhi huku akiendesha gari taratibu, akifwata bara bara ya diamond jubilee, uelekeo wa muhimbili, “umeona hen, sema atuna haraka sanaaaaa! mimi nita gonga ata bia mbili ksha ukaniache ofisini” alisema Denis ambae alikwa anatamani sana bia, huku moyoni akipania kwenda kumweleza yule mwanamke alie mwacha nyumbani kuwa anampenda, ikiwezekana awe mke wake, jambo hilo alilifanya kuwa siri moyoni mwake, “ina maana leo atunywi pamoja?” aliuliza Mahadhi huku anakata kona, na kuifwata bara bara ya fire, “leo na wai home kidogo” aliongea Edgar, akionyesha kuto taka maswali zaidi, Mahadhi hakuoji lolote zaidi alikata kona upande wa kulia kuelekea tena muhimbili, kisha akasimamisha gari nje ya bar moja kubwa sana, ijulikanayo kama hoster, karibu kabisa na hoster za chuo cha madoctor wa muhimbili, ** moja wale walinzi wa mchungaji Kileo, walishangaa kumwona mtu anaingia kule chooni, wakati wao walisha zuwia watu wasiingie kule chooni mpaka boss wao atakavyo maliza haja zake, kilicho washangaza zaidi ni kwamba mtu mwenyewe alikuwa ni mwanamke, tena kwenye vyoo vya kiume, walipo mtazama vizuri, ni yule mwanamke wa liemzuwia kusogea eneo alilosimama mchungaji Kileo, “we mwanamke ume tuchokoza tena?” aliongea mmoja wa wale walinzi, yule alie msukuma kule msibani, safali hii walimwona, alikuwa anawasogelea kwa mwendo wa haraka sana, huku akishika gauni lake na kulinyanyua kwa juu, na kuyahachia mapaja yake manene kuonekana, yule mlinzi aliepewa simu na mchungaji ashike, alimwona mlinzi mwenzie ambae ata kule msibani ndie alie msukuma huyu dada, akimfwata tena yule dada kwenda kumzuwia, huku akiwa ametanua mikono yake, na kuandaa ngumi kwa ajili ya kumtandika yule dada, ambae mda wote walizani kwamba, huyu mwanamke amepotea njia na kungia choo cha kiume, “leo utakuwa mfano kwa wajiga wenzako” alisikika yule mlinzi, ambae alimchukulia Jackline kuwa ni dhahifu, ilikuwa tofauti, wote walishangaa kumwona yule dada, bado alikuwa akija kwa speed ile ile, akiwa amekunja sura kwa hasira, lakini alizidi kuwa mzuri, muonekano wa mwanamke huyu uliwafanya walinzi awa watambue kuwa huyu dada safari hii, akuwa na utani atakidogo, na wala ajapotea mlango kama wa livyozani, alikusudia kuingia kule chooni, hapo yule mlinzi aliinua mkono wake na kurusha kofi kumwendea yule dada ambae ni Jackline Michael Nyati, yule mlinzi alishangaa mkono wake ukidakwa na kubanwa kwa nguvu ikifwatiwa na ngumi kali iliyochomoka kwa mkono wa kushoto wa Jackline, na kutuwa sawia kwenye mbavu changa za yule mlinzi, akifwatia sauti kama ya kuvunjika kwa kijiti kikavu, kisha ya kafwatia maumivu makari ya kuvunjika kwa mbavu zake akataka kupiga kelele za maumivu, lakini alipigwa ngumi ya shingo, iliyo tuwa kwenye koo lake, iliyomfanya ashindwe ata kuvuta pumzi kwa sekunde kadhaa, huku akiongezewa ngumi ya shavu na kujibwaga chini kama mzigo, kilikuwa ni kitendo cha haraka sana, kilicho tumia sekunde kama sita mpaka saba, yule mlinzi mwingine aliona tukio zima, la kushangaza, kwa mwanamke mrembo kama huyu, kupiga ngumi nzito za kijambazi kama hizi, itaendelea …………
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU