BINTI MDUNGUAJI (14)

 

SEHEMU YA KUMI NA NNE

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NA TATU : lakini alipigwa ngumi ya shingo, iliyo tuwa kwenye koo lake, iliyomfanya ashindwe ata kuvuta pumzi kwa sekunde kadhaa, huku akiongezewa ngumi ya shavu na kujibwaga chini kama mzigo, kilikuwa ni kitendo cha haraka sana, kilicho tumia sekunde kama sita mpaka saba, yule mlinzi mwingine aliona tukio zima, la kushangaza, kwa mwanamke mrembo kama huyu, kupiga ngumi nzito za kijambazi kama hizi, endelea …….
Akaona bora akamsaidie mwenzie, ambae alikuwa amelala chini akijishika kooni kwake, lakini Jackline akusubiri mpaka yule mlinzi wa pili asogee kabisa, aliruka juu na kumtwisha kifuti cha kifuani, sambamba na kiwiko cha usoni, kilicho mchana pua yake, na kusababisha damu kutapakaa usoni kwa yule mlinzi wa pili, ambae alipepesuka huku akijishika puani, wakati akishangaa damu zake mwenyewe,alistuka akiongezewa ngumi tatu mfululizo za uzoni, zenye uzito mkubwa, kwa speed ya umeme, akimaliziwa na teke mzunguko la kichwani, lililo mrusha mpaka ukutani, na kujibamiza kisogo, kisha akatuwa chini kama furushi, hapo hapo yule mlinzi wapili akapoteza maisha, kisha Jackline akarudi alipolala yule mlinzi wa kwanza ambae bado alikuwa amelala chini, akishindwa kuinuka kutokana na mamivu ya kuvunika mbavu, huku amejishika kooni, akikaza misuri ya shingo akionekana kukosa pumzi, “unakumbuka nilikuambia nini pale msibani” aliuliza Jackline baada ya kuchuchumaa pale chini alipo lala yule jamaa “sa…sa..…” alikoroma yule mlinzi wa kwanza akijaribu kusema samahani, kwa sauti ambayo Jackline alijuwa kuwa, ingeweza kumfikia mchungaji Kileo kule ndani ya choo, hapo Jackline akachomoa kisu kwenye usawa wa paja leke, na kukididimiza shingoni kwenye koo la yule jamaa, ambae alipoteza maisha pale pale, kule chooni mchungaji Kileo alishasikia vishindo vya vurugu, nje ya choo, akajuwa kuwa walinzi wake wanazuwia watu kuingia mle chooni, lakini wakati anajiandaa kutoka, akiwa ameshamaliza kujisaidia akasikia sauti ya kike ikiongea kwa kunong’ona, huku mlinzi wake moja akikoroma, akahisi kuna tatizo, lakini alipo kuwa ameisikia ile sauti yakike, akaona kuwa hakuna tatizo yaweza kuwa ni binti mmoja amepotea choo, maana tokea alipo gunduwa kuwa muuwaji wa mchungaji mwenzie alitumia silaha aina ya Magnum Sniper Rifle, yeye na wenzie walitilia mashaka uwepo wa Michael Fransis Nyati, askari ambae walimpiga risasi wakiwa mission za kivita huko nchini Congo, nasiyo mwanamke kama alivyo sikia nje ya choo, mchungaji kileo akafungua mlango na kutoka nje, cha kwanza kuona ni mwili wa yule mlinzi alie mpatia simu, akiwa amelala chini, damu zimemtapakaa usoni na kisogoni, mlinzi wa pili na yeye kama mwenzake alikuwa amelala chini damu zimetapakaa, hukuzinyine zikiendelea kutokaa kwenye jelaha shingoni kwake, wakati anashamngaa tukio lile, mchungaji akagundua kuwa mle ndani ayupo, peke yake, kuna mwanamke, tena alishakuwa amemsogelea karibu kabisa na kisu mkononi, tena bado kikiwa kinavuja damu, kitendo bila kuchelewa, mch Kileo alirusha ngumi ya maana, kumpiga yule dada, ambae aiikwepa kwa kusogea pembeni kidogo, na kufanya ile ngumi ya mchungaji, ipite hewani kama anafukuza nzi na kugonga ukutani, karibu na nguzo ya mlango, lakini Kileo akusikilizia maumivu, akarusha mateke matatu mfurulizo, yote ya kapita pahewa, yule dada aliyakwepa, Kileo akaona kuwa akifanya mchezo ya tamkuta yaliyo wakuta walinzi wake, muda mchache uliopita, akaona wacha ajikumbushe umaili wake wa kipindi yupo jeshini, “ mzee Kileo, leo auna ujanja” ilikuwa sauti tamu ya Jackline ambae muda huu alikuwa ameachia tabasamu baya sana, na kufanya ashindwe kujulikana kama anacheka au amekasirika, “unataka nini kwangu we! mwanamke” aliuliza Kileo huku akionyesha kuzidiwa na uoga, baada ya mashambulizi yake kushindwa kufanya kazi, “umesaau mlicho kifanya mwaka 1988 misitu ya Kanaluchina nchini Congo” aliuliza Jackline kwa sauti ya chini “lakini alikuwa ni major Masinde, sisi wengine unatuonea tu!” aliongea Kileo akijiandaa kuchomoa bastora kwenye mfuko wa ndani wakoti lake la suit, kitendo kilicho onekana wazi machoni kwa Jackline, Kileo alimshuhudia yule mwanamke akiwa hewani ametanguliza magoti yote mawili kisu mkononi, alishindwa kumkwepa, magoti yakatuwa kifuani kwake, ikifwatiwa na kisu kuzama shingoni kwake, mchungaji akaanguka chini kama gunia lililo tupwa toka begani kwa kuli, Jackline akifwatia juu yake, magoti ameyatanguliza kifuani kwa mchungaji, jackline alichomoa kisu shingoni kwa mzee Kileo, akimwacha mchungaji akiwa katika atua za kukata roho, Jackline aliendea sink la kunawia mikono, akaafungua bomba la maji taratibu, kama yupo nyumbani kwake, kisha akanawa vizuri ili iwe rahisi kwake kupita nje bila kustukiwa na mtu yoyote, ** Nje nako inspector Johnson David baada ya kumaliza uchunguzi wake, akatoka na kukutana na kundi kubwa la waombolezaji, waliokuwa wakimsubiri amalize uchunguzi wake, na wao wakamwone mpendwa wao, inspector Johnson David alikuwa ameshajulishwa uwepo wa watu awa nje, kilichomvutia ni uwepo wa rafiki mkubwa wa marehemu, ambae ni mchungaji Kileo, licha ya kuwa maarufu samna sana mzee huyu pia anamfahamu toka siku nyingi sana, akaambiwa mch Kileo yupo chooni, akaona aitakuwa vibaya akamsubiri, maana ukiachilia kufahamiana kwao, pia ange weza kuoji mambo mawili matatu, yatakayo msaidia wenye uchunguzi wake, inspector Johnson David alisimama pamoja na waombolezaji, macho yake kule kilipo choo alichoingia mchungaji Kileo, ulipita mda mrefu pasipo kumwona mchungaji akitoka chooni, wala kuona mtu mwingine akielekea huko, maana ilisemekana walinzi walizuwia watu wasiingie kule chooni, tofauti ni kwamba walionekana wakina mama pekee wakienda na kurudi toka chooni, inspector Johnson David na askari wake wakiwa na kundi la waombolezaji walisubiri sana pale nje, pasipo kumwona mchungaji, akitoka, ilisha pita nusu saa toka inspector Johnson David, akae pale nje pamoja na waombolezaji, “kwani aliingia saa ngapi huko chooni?” aliuliza inspector Johnson David, macho akiyaelekeza chooni, wakati huo akamwona mtu mmoja anaelekea kule chooni, kwenye vyoo vya kiume, akumjari akamgeukia yule mtoa matangazo, akiashiria anataka jibu “nikama nusu saa hivi, imepita” alijibu yule mtowa matangazo, wakati wanaendelea kuulizana juu ya kuchelewa kwa mchungaji Kileo kutoka chooni, mala wakasikia kelele toka upande wa chooni, zikifwatiwa na yule jamaa alieingia muda mfupi uliopita, kule chooni, akitokea chooni huku akikimbia, “mauwaji!…. jamani..mauwaji ..kuna watu wame kufa chooni” aliongea yule mtu mwanamume, akiwa amejawa na kiwewe cha hali ya juu, hapo kengere ya hatari ikagonga kichwani kwa inspector Johnson David, akatowa amri kwa askari kulizunguka eneo zima la hospital pasipo kuruhusu mtu kutoka, na wengine kuziwia watu kutoka na kuingia chooni, huku yeye na wazee wachache pamoja na yule askari wake mwenye cheo cha Sgt, wakielekea chooni, walipoingia chooni walikuta wale vijana wawili walinzi wa kileo, wakiwa wamesha kata roho, lakini mchungaji kileo likuwa bado ameshikilia shingoni, damu ziki churuzika kwa wingi huku akitapatapa, “mnyanyueni tumwaishe ndani, anaweza kupona bado mzima huyu” alisema inspector Johnson David, kitendo cha haraka sana, walimnyanyua juu juu mchungaji Kileo, wakiongozwa na inspector Johnson David, wakaanza kuelekea ndani kwenye chumba cha emergence, lakini wakiwa njiani wamembeba mchungaji kileo, inspector Johnson David aliona kama mchungaji Kileo alikuwa anataka kusema neno flani, lakini akashinda kutokana na maumivu aliyo ya pata kooni, pamoja na mwili wake kuzidi kuishiwa nguvu, kuli sekunde, inspector Johnson David akazidi kusogeza sikio lake karibu na Kileo, pengine ange ambulia chochote, huku safari inaendelea “nya.. nya.. nya.. nyathiii” ndilo neno pekee aliloweza kutamka kileo, lika sikika masikioni kwa inspector Johnson David baada ya hapo Kileo akatupa mikono huku na huko, kisha akatulia kabisa, atawalipo mfikisha ndani, tayari alikuwa amesha fariki, inspector Johnson David aliuma meno kwa uchungu, na kupiga ngumi ukutani kwa hasira, maana licha ya kuwa mch Kileo alikuwa ni mtu anae mfahamu sana, lakini pia alikuwa mtu muhimu, katika uchunguzi ule ukizingatia ndie alie onana na muuwaji uso kwa uso, inspector Johnson David, akakumbuka kitu, hapo hapo akapiga simu kituo kikuu, kuomba msaada wa askari ishirini kwa ajiri ya kuzunguka eneo la hospital, hii kubwa ya muhimbili, ili waweze kumkamata mwuaji, ambae aliamini kuwa bado alikuwepo eneo lile, wkati huo askar polisi walio kuwepo walikuwa wametawanyika mle ndani ya eneo la hospital wakizuwia mageti ypte ya kuingilia na kutokea, hakna kuingia hakuna kutoka, ** kumbe baada ya kumaliza kazi yake, Jackline alinawa vizuri na kutoka nje pasipo kuwa na arama yoyote ya damu, wala sura ya mbuzi kama ilivyokuwa mle ndani, wakati akiwashugulikia wakina Kileo, akapita upande wapili wa jengo akiwa kwepa waombolezaji wenzake, na kutokea kwenye chuo cha sayansi na tiba, kisha akajipenyeza kwenye majengo ya chuo adi kwenye hostel za chuo, akaona uchochoro mwingine mbele yake, alipo uchungulia akagundua mbele ya uchochoro ule kuna bar, hivyo akaenda na kutokea kwenye choo cha bar hiyo, hapo akaingia chooni na kijifanya kama mteja aliepo pale bar, alizuga kwa sekunde chache kule chooni, kabla ya kutoka na kuelekea upande wa bar, ile Bar ilikuwa na watu wengi kiasi, wakipata soup na wengine wakipata vinywaji mbalimbali, ila wachache wakinywa pombe, Jackline akiwa anapita kati kati ya ile bar, alikuwa makini sana, huku akiangalia kama kuna mtu anaye mtilia mashaka, aka waona vijana wawili pembeni kidogo ya ukimbi wa bar, mmoja amegeukia upande wake na mwingine amemgeuzia mgongo, wakiwa wame kaa meza moja kule pembeni ya ukumbi wa bar, mezani kwao kulikuwa kuna chupa ya maji na chupa mbili za bia, moja ikiwa imesha kwisha, na nyigine ina bia nusu, kilichomvutia kwenye ile meza, ni nguo aliyoivaa yule kijana ambae alikuwa amemgeuzia mgongo, ilikuwa ina fanana na aliyo vaa mwenyeji wake Denis asubuhi, na sasa alimwona yule kijana alievaa nguo kama ya mwenyeji wake mlevi, ambae amesha mjuwa jina anaitwa Denis, akiinua chupa ya bia na kuiweka mdomoni, anaigugumia kisha anaiweka chini ikiwa robo, wakati anaendelea kumwangalia yule kijana vizuri akagongana macho na yule aliegeuikia upande wake, akamtambua kuwa ni yule aliekuwa na Denis jana yake, pale Mazao building, wakati Denis akimtafuta yeye, Jackline akageuza shingo mbele, ili yule kijana aliekuwa na Denis, asije akamkalili, muda wote alikuwa akitembea kulifwata geti la kutokea nje ya bar, alipo jaribu kuangalia tena ile meza, sasa alimwona vizuri Denis, wakiwa wamesimama na yule mwenzie huku Denis akigugumia chupa ya bia, na yule mwenzie akijaribu kumwonye kitu kule upande alipo yeye Jackline, akuna mwingine aliye onyeshwa ni yeye Jackline, hapo moyo wa Jackline ukalipuka kwa hofu, akijuwa kuwa mwenyejiwake anaweza kumwona, na endapo Denis akimwona lazima amuuwe, maana lazima ataambatanisha matukio, Jackline akageuka tena kuangalia mbele na kuongeza mwendo, akawai kutoka nje ya geti, akiwa na uwakika kuwa Denis ajamwona, Pale nje alishuhudia magari manne ya polisi, yaliyo beba askari wengi, ya kiwa katika mwendo wa kasi sana, huku ya kipiga ving’ora ya kielekea hospital, Jackline akatabasamu huku anaelekea kituo kidogo cha daladala, na kujichanganya na Abiria wanao subiri magari yaendayo sehemu mbalimbali, japo aliyakuta magari mawili ya endayo mbezi, lakini alitulia kwanza kuona kama wale vijana wawili watatoka, na kama wakitoka je watamfwatilia?, akiwa pale kituoni aliweza kuwaona Denis na rafki yake wakitoka bar na kuanza kuangalia huku na huku, kisha wakaingia kwenye gari Toyota IST nakuondoka zao, wakaingia barabarani, wakielekea upande alipo yeye ilikuikamata barabara ya fire, Jackline akusubiri tena akaingia kwenye gari lililo andikwa mbezi muhimbili, akatafuta seat na kukaa, akiliona gari la kina Denis likipotelea upande wa fire ** Nikweli Mahadhi alimwona Jackline, lakini akuwa akimfahamu, alimwambia Denis amwangalie yule mwanamke, jinsi alivyo na umbo na sura nzuri, lakini Denis alikuwa busy na chupa yake ya bia, ata alipo geuka na kumtazama akuweza kumwona, adi walipo gutushwa na ving’ora vya polisi, muda huo walikuwa wamesha pata soup na kupumzika kidogo pale bar, huku Denis akinywa bia mbili akidai na towa lock, baada ya kusikia ving’ora vya polisi, walisimama na kutoka nje, baada ya kuangalia kama wangemwona yule dada, ambae Mahadhi ana msifia kuwa mzuri sana,lakini awakumwona, walipo mkosa wakaamua kuingia kwenye gari na kuondoka zao, wakiikamata barabara ya fire, kisha morogoro road kuelekea upande wa magomeni,** inspector Johnson David alikuwa anawapanga askari walio ongezeka kutoka kituo kikuu, wakati huo alikuwa akijaribu kulipambanua lile neno, alilo kuwa akijaribu kulitamka chungaji Kileo, waandishi wa habari walisha anza kusogea eneo la tukio wakapewa utaratibu wakuingia, pale hospital, msako mkari uliendelea ndani ya eneo lote la hospital, “nyathi, anamaanisha nini?” alijikuta akiongea kwa sauti kidogo, kiasi cha yule askari wake mwenye cheo cha SGT aliye simama pembeni yake akasikia, “vipi afande, umeongea na mimi?” aliuliza yule, SGT, inspector Johnson David akamsimulia yale maneno ya mwisho ya mchungaji Kileo, kisha wakajadiriana mambo machache, inspector Johnson David, alikuwa anafahamu kuwa, awa marehemu wawili, kabla ya kuwa wachungaji walikuwa wanajeshi wajeshi la ulinzi, na kitengo chao kiliusika na nakazi za siri, ndani na nje ya nchi, na walikuwa wadunguwaji, pia ni muuwaji katka kitengi hicho cha siri, ambao walikuwa ni wataalamu wa kutumia silaha ya kudungua toka mbali, na ndiyo silaha iliyotumika kumuuwa mchungaji Chilumba, baada ya hapo walipata jibu, waende kikosi kikuu cha mission za siri, ambacho wakina Kileo walikuwepo wakifanyia kazi, kabla ya kuhacha jeshi, kutokana na muda kuwa umekwenda sana, la zima wausika wanao kusudia kuwaona ofisini, watakuwa wamesha ondoka, wakapanga waende kesho mapema, hivyo inspector Johnson David akatoaa maagizo kwa doctor mchunguzi, akisema kuwa kesho atapitia pale kupata majibu ya vipimo vya kileo na walinzi wake, maana masaa yalisha tembea sana pasipo kumpata muusika wa mauwaji, zaidi ya kukamata watu waliokuja kutazama wagonjwa wao na kutibiwa, * Ilisha timia saa mbili usiku, akiwa ame valia gauni lake refu ndani kikaptula cha jinsi chenye zana za kazi, Jackline alikuwa amesha maliza kupika na kuwasiliana na baba yake, na kumpa report ya kazi aliyo mtuma, japo alisha pitiliza malengo, na kumuuwa kabisa mchungaji Kileo, sasa Jackline alikuwa amejilaza kwenye kochi kubwa akitazama tv, ambayo ilikuwa na onyesha taharifa ya habari, na tukio lililo onyeshwa muda mrefu, ni la mauwaji ya mchungaji kileo, ikiwa ni mauwaji mfurulizo ya wachungaji wawii, ambao ni marafiki, chakula kikiwa mezani karibu na kochi dogo la mtu mmoja, licha ya kuwepo na sebule ya chakula, lakini Jackline aliamua kuweka hapo, kwa ajiri ya mwenyeji wake, sababu alijuwa lazima angekaa kwenye makochi na siyo kwenye viti vya ukumbi wa chakula, wakati anaendelea kutaazama TV, mala akasikia sauti ya muungurumo wa gari, nje ya nyumba, moja kwa moja akajuwa ni mwenyeji wake mlevi, baada ya dakika chache alimwona Denis akiingia ndani, huku akiburuza begi kubwa, kwa mkono mmoja, huku mkono mwingine amebeba mifuko mitatu, midogo meusi, inayonukia nyamaza kuku na chips, akiyumba yumba kwa kuzidiwa na pombe, mwanzo Jackline alizani kuwa Denis alikuja na mgeni, kengere ya tahadhari ikagonga kichwani kwake, sababu akutaka mtu mwingine aongezeke mle ndani, ingekuwa ni hatari kwake, kwani ange bainika mapema sana, akabaki amemtazama huyu kijana mlevi, akimwona akiingia peke yake ndani na kuweka beg chini, kisha akamkabidhi Jackline vile vimifuko vya chips na kuku, “ume..umeee..shindaje hapa nyumbani?” alisalimia Denis kwa sauti ya kilevi huku anakaa kwenye kochi tofauti na lile la chakula, Jackline akacheka kimya kimya, akimtazama mwenyeji wake jinsi alivyolewa “salama kabisa, umeniacha peke yangu, yani leo umechelewa sana kurudi” aliongea Jackline akijifanya kudeka, kumzuga mwenyeji wake, huku akifungua vile vimfuko alivyo kuja navyo Denis, akakuta kuna vyakula, akashangaa akamtazama mwenyeji wake, kwa mtazamo wa pekee, huyu kijana mlevi, kuwa anaonekana kumjari sana, Jack akaenda mbari zaidi na kuwaza labda anamtega ili ampende, “mh! kaka kwa nini umenibebea chakula” aliuliza Jackline akimtazama Denis, ambae sasa alikuwa akilegeza tai shingoni kwake “kwani .. wewe.. ni robot? Siiiiiii….. nimekuuuu ..bebea ili ule” aliongea Denis kwa sauti ya kilevi, akimalizia kuitoa tai shingoni, “si ulihacha ela ya chakula, mimi nimesha kupikia chakula hiki hapa” aliongea Jackline akiwa anasogeza chakula alicho kiandaa kwa ajiri ya mwenyeji wake, Denis ana stuka na kumwangalia Jackline usoni, macho yao yana gongana, nikama Denis amekumbuka kitu “hoooo! Kweri nimekumbukaaaaa..” jinsi alivyo mtazama na maneno aliyoongea ya limstua Jackline akamkazia macho Denis, “umekumbuka nini kaka yangu” aliongea Jackline akimsogelea Denis karibu, mkono wake wa kulia akiwa ameshika gauni, na kuanza kulipandisha juu taratibu, mpaka usawa wapaja, bado kumalizia kidogo afikie kwenye zana za kazi (kisu), macho ya Denis yalituwa kwenye paja la Jackline, likamchanganya, “duu! Ndiyo maana mimi naamini kabisa yani, daah! hujuwe ukiambiwa kwa haraka haraka uwezi kuamini wala kusadiki” aliongea Denis kwa sauti ya kilevi akijaribu kukwepesha macho yake, ya sitazame paja la mgeni wake, ambalo aliamini kuwa ameinua ile nguo kwa bahati mbaya, huku mapigo ya moyo ya Jackline ya kizidisha speed, alikuwa bado amesimama karibu ya mwenyeji wake mkono bado nchi chache kukamata kisu na kumwaga damu, “mbona sikuelewi kaka kunanini?” aliuliza Jackline, akizuwia asionekane kama yupo kwenye hali gani, “Mahadhi aliniambia lakini sikuamini, daah! sasa nimeamini” alitulia kidogo Denis akavuta pumzi kidogo ile ya kilevi levi, huku akifunua chakula, hapo Jackline alikumbuka kuwa wakwanza kumwona pale bar, alikuwa ni rafiki yake ambae atajana walikuwa pamoja, akahisi ndie mahadhi, hapo akaona akuna namna tena, zaidi ya kupoteza roho ya mwenye jiwake. kisha atafute sehemu ya kwenda kuishi,
HAPO SASA MKONO WA JACKLINE UMEKARIBIA KISU, NA VIPI INSPECTOR JOHNSON DEVID, ATAFANIKIWA KUMJUWA MUUWAJI HIYO KESHO

 

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata