
SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI NNE : alitulia kidogo Denis akavuta pumzi kidogo ile ya kilevi levi, huku akifunua chakula, hapo Jackline alikumbuka kuwa wakwanza kumwona pale bar, alikuwa ni rafiki yake ambae atajana walikuwa pamoja, akahisi ndie mahadhi, hapo akaona akuna namna tena, zaidi ya kupoteza roho ya mwenyeji wake, kisha atafute sehemu ya kwenda kuishi, endelea…….
“kweli…. kabisaaaaaaa …ni …nimeamini, mkiwa wawili… ndani yaaaa… yaaaaa, ya nyumba, yani ata maisha…… yanakuwa safi sanaaaaaaaa, mimi nilijuwa niiiiiii maneno yake ya kizinzi tu! kumbe yana ukweli ndani yake” aliongea Denis kwa sauti ya kilevi, hapo Jackline alishusha pumzi kwa nguvu, kama mtu alie kuwa amebeba mzigo mzito, “yani .. yani leo nimekuta.. chakula kizuriii..alafu…ala.. ahhhh” alibabaika Denis, huku macho yake yakiwa yameganda kwenye paja zuri, lilo jaa vizuri la Jackline mgeni wake, hapo Jackline akagunduwa kuwa bado alikuwa amepandisha gauni lake, akaliachia haraka, “ho! Samahani.. siku.. siku kusudia kuangalia” aliongea Denis kwa sauti yake ya kilevi huku akigeuza kichwa chake na kutazama mezani, Jackline akamtazama Denis, kisha akatabasamu, kidogo huku moyoni akijisemea “una bahati, ungekuwa umesha chinjwa” aliwaza hayo akimwangalia Denis, ambae alikuwa akifunua hot pot la chakula, akamwoana mwenyeji wake, Denis anataka kuchota chakula kwenye hot pot, iliaweke kwenye sahani, anasita kidogo “henheee!, nimekumbuka chukua funguo nenda kwenye gari nimesaau mzigo wangu…. pale kwenye seat ya pembeni kwa dereva” aliongea Denis kwa msisitizo wa kilevi, huku akimpatia Jackline funguo za gari, Jackline alizipokea funguo kisha akatoka nje, huko nje aliwaza sana juu ya tukio alilotaka kulifanya dakika chache zilizopita, ni tukio la kutaka kumchinja mwenyeji wake, tukio zima lilipita kichwani kwake adi tukio la Denis kushangaa paja lake, hapo aliinua gauni lake nakuangalia paja lake, kisha akacheka kidogo, “inabidi niwe makini na huyu mlevi, maana naweza kumchinja bila sababu” Jackline aliwaza hayo, huku akifungua mlango wa gari upande wa seat ya abiria, akakutana na carton ya bia za kopo, na soda nne za kopo kwenye mfuko, akaduwaa akatikisa kichwa kama anasikitika, huku tabasamu likichanua mdomoni kwake, “baba anakunywa pombe, lakini huyu kazidi, zile za jana bado zipo leo kabeba nyingine” alijisemaea Jackline huku akichukua lile carton la bia na soda, na kufunga mlango wa gari, kisha akarudi ndani, “hivi kaka unaitwa nani alafu kwanini unakaa peke yako?” aliuliza Jackline kwa sauti tamu sana, huku akifunga mlango kwa ufunguo, akizuga kuwa amjuwi jina yule kijana mlevi mwenyeji wake, lakini akujibiwa kitu, zaidi alisikia sauti ya mkoromo, akageuka kumtazama mwenyeji wake, alikuwa ameegemea kochi amesha lala, Jackline akatabasamu kidogo, akitikisa kichwa kwa masikitiko, akasogea kwenye meza na kuziweka bia mezani, na soda akaziweka kwenye friji, akamtazama tena mwenyeji wake alikuwa amesha lala kabisa, chakula mezani kikiwa wazi, akija guswa kabisa “mgeni siku yapili, analala sebuleni” alijisemea Jackline, kisha akazima Tv na taa za ndani alafu akajilaza kwenye kochi kubwa, alichelewa sana kupata usingizi, akiwaza hili na lile, kuhusu watu wanne waliobakia kuuwawa, pia aliwaza atakuwa amewauwa watu wangapi mpaka atakapo maliza kuwauwa wausika wanne waliobakia, maana mpaka sasa amesha uwa watu wenginekumi, tofauti na wausika walio kusudiwa, Jackline aliwaza sana mpaka akapitiwa na usingizi, ilisha timia saa tano na nusu za usiku, ** Usiku saa tano, ikiwa inaelekea saa sita kasoro, ndani ya nyumba moja kubwa ya kifahari mitaa ya kinyelezi mwisho, walionekana wazee wanne wakiwa katika mjadara mkubwa sana, “sikiliza Alex ninacho kueleza niukweli huyu siyo mwingine ni private Michael Nyati” aliongea lieutenant (luteni) Kaijage, akimwambia capten Alex Mwasaga, ambaye akuamini kabisa kuwa Michael atakuwa bado mzima, wazee awa wau wazima, ni major Dvid Johson Masinde, na wenzake, wakina capten Alex mwasaga, luten James Kaijage, na sajint taji Mathayo GK, “jamani mimi naona tujadiriane, tumpate adui wa kweli, maana tukisema tumfikirie mtu ambae tumeshuhudia akipigwa risasi na kuporomoka, kwenye makorongo, tutakuwa tuna poteza muda” aliongea kwa msisitizo capten Alex, “mh! Alex umesaau kitu kuhusu swala la risasi, kumbuka kuwa wote tulikuwa tumevaa body amour (bullet proof), alafu risasi yenyewe ilikuwa ya bastora” alikumbusha major David Masinde, na wote wakatulia na kuvuta kumbukumbu, kisha wakaanza kukubari ukweli huo wa major Masinde, kwa kutikisa kichwa juu chini, kasolo Alex yeye akuamini kabisa, kwamba Michael Nyati atakuwa hai, “lakini kama ni yeye, kwanini alikaa kimya mda mrefu, leo hii imepita miaka ishilini na kitu, ndiyo aanze kututafuta?” Alex kiukweli bado alikuwa haamini kabisa, kama kweli vifo vya wakina Chilumba na Kileo, vinausiana na tukio walilo lifanya mwaka 1988 huko nchini congo, “labda Alex umesaau kuwa private Michael Nyati, ni mtu ambae anatumia akili nyingi sana kwenye mambo yake” aliwakumbusha ssgt Mathayo, akiwasimulia baadhi ya matukio na mipango aliyowai kuisuka Michael, akiwa askari mdogo, wa cheo na umri, na kuwaokoa kwenye matukio mbari mbari ya hatari, na kutoa mipango iliyo wasaidia wafanikishe mission, “jamani mimi naona tuwe makini kuanzia sasa, tujuwe kabisa kuwa tunawindwa, na pengine tukaitwa na kuhojiwa na polisi au vyombo vya habari, kwa hiyo tuwe makini na majibu yetu, maana endapo tutakubari kuwa muuwaji ni Michael, lazima tutaje sababu ya yeye kufanya hivyo, kwa hiyo hapo swala ni kukataa tu, kwamba atujuwi lolote, zaidi ya kwamba Michael alitoweka tukiwa mission (missing in action) Congo, huku tukiendelea kujilinda sisi wenyewe” aliongea major Masinde, akionyesha umakini mkubwa sana na kikao kilifungwa, wote wakatawanyika, alibakia Major Masinde ambae alikuwa mwenyeji wao, walichagua hapo kwa major Masinde, kwa sababu, kwanza nyumba ilikuwa sehemu ambayo aina msongamano wa nyumba, hivyo maongezi yao ya singe sikilizwa na mtu yoyote wa jirani, pili wenzake wangeweza kufika kwa ulahisi kutokana na kuwa, wawili kati yao wanakaa mbezi na kimara, mmoja alikuwa ana kaa mbezi beach, hivyo wangetumia barabara ya malamba mawili, la mwisho kabisa, mke wa major Masinde alikuwa amesafiri kwenda kwao musoma, kusalimia ndugu, na watoto wa masinde wote ni wakubwa wanamaisha yao, hivyo pale nyumbani alibaki yeye mwenyewe ** Asubuhi na mapema siku ya pili, ilikuwa ijumaa, kama ilivyokuwa jana yake, Jackline alikuwa amejilaza kwenye kochi akijifanya amelala, aliweza kumshuhudia mwenyeji wake akijiandaa kwenda kazini, leo alivalia shati la blue na tai nyekundu, ya kipepeo na suruali nyeusi na viatu vyeusi, “mh! huyu kaka ni mlevi, lakini anajipenda sana” aliwaza Jackline, huku amejifanya kulala, ikwa ni mala ya kwanza katika maisha yake, Jackline kuona kuwa mwanaume kapendeza, akuwai kuona mwanaume anavaa alafu akaona eti! amevaa vizuri, alichukia sana wanaume, pasipo sababu ya wazi, zaidi ya kuambiwa na baba yake awachukie wanaume, akiwa amejilaza juu ya kochi Jackline alimwona mwenyeji wake, ambae siku ya pili leo anamlaza sebuleni, sababu ya ulevi, akiingia chumbani, baada ya dakika chache akatoka akiwa amebeba shuka jingine, siyo lile la jana, Jackline alimwona mwenyeji wake akija moja kwa moja mpaka alipo lala, akamfunika vyema kabisa, kisha huyo, cha pombe akaelekea kwenye friji akafungua na kuchukua kopo moja la soda ya baridi aina ya cola, akalifungua na kuligugumia mpaka alipo maliza, akachukua jingine, kisha akafunga mlango wafriji, akaenda mezani akachukua makopo mawili ya bia, kisha atowa fedha mfukoni mwake kiasi cha elfu selathin, na kuziweka mezani akika ndamizia na kopo moja labia kati ya yale yaliyopo mezani kisha huyo, akaelekea nje, Jackline akasikia muungurumo wa gari, likiwashwa na baada ya dakika chache likaondoka, na kutokomea, Jackline baada ya kuakikisha gari limesha ondoka akanyanyuka toka juu ya kochi, akavua gauni lake na kubaki na kikaptula cha jinsi na tishert akaanza kwa kufanya mazoezi, ni kwaida yake siku zote za maisha yake, ** Asubui ya leo ilimkuta insp Johnson David akiwa mwenye mwazo mengi sana, nahii yote nikutokana na mauwaji yanayo endelea kutokea mfurulizo, usiku kucha alikuwa akiwaza juu ya kesi hii nzito, ambayo amekabidhiwa yeye, kati ya mambo aliyo ya waza, ni neno alilo tamka marehemu Kileo, “nyathi” alikuwa anamaanisha nini, “nitapata jibu nikienda kuwaona watu wa MSM, (Military Secret Mission),” alijisemea Johnson akiinuka toka kitandani na kumwacha mke wake na mwanae mdogo, wakiendelea kuuchapa usingizi, akaanza kujiandaa kwa ajiri ya kwenda kazini, ** Saa moja na robo, Denis ndio alikuwa anaingia kazini, akaegesha gari lake kwenye maegesho mbele ya Mazao Building, kabla ajashuka akakamata kopo la bia, akalifungua na kulimiminia mdomoni kama mtu mwenye kiu kali ya maji, alifanya hvyo kwa kurudia rudia, mpaka alipo maliza, kisha aka iliweka lile kopo pamoja na makopo mengine tupu ya bia na soda mle ndani ya gari, akatulia kidogo ndani ya gari akijisonya sonya kila mala, alijilaumu sana kwa kushindwa kuongea na mgeni wake, kumweleza kwa anampenda “leo lazima nitaongea naye, lakini mbona jana kama niliongea nae kidogo, ata sikumbuki niliongea naye nini, haaa! niujinga, kwani na yeye mwenyewe ajuwi…. ” mawazo ya Denis yalikatishwa ghafla, baada ya kufunguliwa kwa mlango wa gari lake, upande wa abiria, “kaka vipi na kuona umefika alafu umeganda kwenye gari” alikuwa Mahadhi, ambaye alisimama nje ya gari akishindwa kuingia ndani ya gari kutokana na makopo matupu ya bia na soda kujaa pale chini ya siti ya abiria, akacheka kidogo, kisha akaenda kwenye gari lake na kuchukua mfuko wa Rambo, na kuyaweka yale makopo, kisha wakatoka na kuongozana, kuelekea ndani ya jengo wakiyaacha yale makopo kwenye dust bin, “Denis, leo ni melikologa mbaya” aliongea Mahadhi wakati wana pandisha ngazi, kuelekea ofisini kwao, “nini tena mwanangu” aliuliza Denis wakati wanapandisha ngazi kuelekea ofisini kwao, wakasimama kidogo na Mahadhi kuanza kusimulia “ndugu yangu jana si nime litoba, baada yakutoka hapa, nika pita buguruni, yule demu wangu wa chama alinistua, ni kakaa pale mpaka saa saba usiku, ndio nikaenda home, nikamkuta wife kavimba, nikajaribu kujichekesha wapi, nika mdanganya kuwa niliku sindikiza wewe nyumbani, sababu ulizidisha pombe ukazima, hapo kidogo akaelwa, lakini amepanga kukupigia simu akuulize” alimaliza Mahadhi kusimulia, “pumbavu, ngoja apige usikie nitavyo kukataa, ukuwa na sababu nyingine, zaidi ya kuni taja mimi kuwa mlevi?” aliongea Denis akianza kupandisha ngazi, akionyesha kuto kupendezwa na kitendo kile, “sikia Denis, mimi na wewe tuta malizana pale Jambo, nakurusha na carton moja la bia” alisema Mahadhi huku akiendelea kuongea “nikitoka hapo naenda kumnunulia wife mdori wenye maandishi mazuriiiii, lazima atulie” ilo neno lamwisho likamvutia Denis, “umesema mdori inamana shemeji anapenda midori?” aliuliza Denis kwa shahuku “tena na mauwa pembeni, hapo umemaliza, ata kama alinunaje, atapoa tu!” aliongea Mahadhi kibabe, Denis akatabasamu, ** Magari mawili ya polisi, ya likuwa ya mesimama nje ya jengo moja kubwa la ghorofa mbili, ndani ya kambi moja kubwa la Jeshi, akashuka insp Johnson, akapokelewa na askari mmoja wajeshi la ulinzi mwenye cheo cha kopro, na kumuongoza mpaka kwa kwa mkuu wakitengo cha mission za siri jeshini, baada tu ya kuingia ndani ya ofisi hile, Insp Johnson akapiga saruti kwa mkuu wakitengo hicho, mwenye cheo cha brigedie, na kwenye shati lake kifuani upande wakulia, alikuwa amevaa kidari cha jina kimeandikwa Rodrick DM, “karibu insp… nani vilie” aliongea yule Brig akimpa mkono Insp Johnson, “Johnson David” aliongea insp Johnson David akimtajia jina yule mkubwa wajeshi, “ndiyo bwana Johnson, karibu sana, nilipo julishwa ujio wako nikaona bora nikusubiri, vinginevyo usinge nikuta, ninge kuwa nimesha ingia kwenye kikao” alisema yule mkubwa, huku anajiweka sawa kwenye kiti chake, “afande nimekuja kukuona, juu ya awa askari wastaafu walio uwawa mfurulizo, kama labda kuna lolote mnalo lijuwa ambalo linaweza kutusaidia kumpata muuwaji, au chanzo cha mauwaji” aliongea Insp Johnson kwa nidhamu ya hali ya juu iliyo mvutia yule mkubwa wajeshi, “bwana insp ilo swala ata sisi linatuhumiza vichwa sana, maana ata silaha ina yotumika ni ya kijeshi, lakini atuja pata kumjuwa muuwaji ni nani, na sababu ya kufanya hivyo ni nini” aliongea yule mkubwa akionyesha masikitiko, “kwani silaha hizo zipo jeshi zima?” aliuliza insp Jonhson, “mh! hapana zaidi ya ikuru na hapa kwetu, akuna sehemu nyingine zilipo hizi silaha” alijibu yule kamanda akijitaidi kuvuta kumbukumbu, “kwani afande kuna upotevu wa silaha ulishawai kutokea wa silaha kama hiyo,” aliuliza insp Johnson, “ilo ndilo swala ambalo nilikuwa najaribu kukumbuka,” Brigedia Rodrick akamsimulia Insp Erenest kuwa silaha ya aina hiyo ya Magnum Sniper Rifle ilipotea mwaka 1988 nchini Congo ikiwa mokononi mwa Private Michael Nyati, ambae toka kipindi hichi mkuu wa kitengo akiwa brigedia Suod, ambae amestaafu miaka mitatu baada ya tukio hilo, private Michael akuwai kuonekana tena, na Jeshi lina amini alipoteza maisha, insp Johnson alisikiliza kwa umakini sana story ya brigedia Rodrick, huku akiandika kwenye note book yake, insp Johnson akasikia jina la Nyati, aka jumlisha na Nyathiii, akatowa damu mdomoni na maumivu makali ya mchungaji Kileo, akapata “Nyati” akajikuta akiongea mwenyewe huku brigadia Rodrick akimsikia, “vipi ulishawai kupata habari zake huyu mtu” aliuliza brig Rod, “samahani afande, nilijaribu kuunganisha uwezekano wa huyu Nyati, kuusika na mauwaji ya wenzake, labda uelewano wao ulikuwaje kabla ya kupotezana huko porini” aliongea insp Johnson David, “sidhani kama kuauwezekano wa kutambua maelewano yao kwa ipindi hicho, maana ata mimi nilikuwa askari mdogo sana,” alijibu Rodrick, “labda kuna kumbukumbu zozote za watu walio shiriki hiyo operation ya mwaka 1988,” hapo brg Rodrick aliwaza kidogo kisha aka sema, “sidhani kama hiyo kumbukumbu itakuwepo, maana kuna kipindi tuli pokuwa tunaamishia nyraka kwenye computer toka kwenye mafire ya kawaida, nyalaka nyingi zilipotea, ila kwa kukusaidia, chukua alama za vidole za Michael Nyati, tutakupatia toka kwenye file lake la uajili, kisha nenda kwenye matokeo yako ya vipimo vya hao marehemu, uangalie kama vinaendana, ukipata jibu tujulishe na sisi,” aliongea Brg Rod huku akitoa namba zake za simu na kumpatia insp Johnson, kisha akamwita yule kopro, akamweleza ampatie insp Johnson finger print za Michael Nyati, zilizopo kwenye file lake, kisha yule Brg akaondoka zake, walipo baki wawili yule Kopro alimwelezea insp Johnson David juu ya usumbufu uliotokea kwa siku zile mbili, za mauwaji ya askari wale wa staafu, kitu ambacho wanashindwa kuamini nikwamba kwa umri ambao sasa atakuwa nao Michael, kama bado yupo hai ni miaka hamsini kasoro, na mauwaji ya jana yamethibitisha kuwa huyu muuwaji ni kijana mwenye nguvu sana, na siyo mzee, sababu amepambana na wanaume watatu, “ila kama unataka maelezo zaidi mtafute brg mstaafu Soud, yeye alifanya kazi na kikundi hicho kwa ukaribu sana,” alimaliza yule kopro akimpatia nakala ya alama za vidole vya Michael na akamwelekeza maeneo anayokaa mzee Suod, huko kigamboni mji mwema, Insp Johnson akaingia kwenye gari lake pamoja na askari wake, wakaondoka zao na kunyoosha muhimbili, kucheki alama za vidole vya muuwaji, afananishe na za Michael Nyati,* Jackline alikuwa amesha maliza shuguli zake zote, ikiwa na kuongea na baba yake, ambae alimsisitiza kusitisha mauaji mpaka polisi wajisahau, huku mzee Nyati akiendelea kutafuta habari za wabaya wake wengine, pia Jackline alikuwa amesha maliza kunywa chai na viazi mviringo, na sasa alikuwa ametulia juu ya kochi akiangalia Tv, na soda aina cola, ni moja kati ya soda za mwenyeji wake mlevi zilizopo kwenye friji, ikiwa mkononi, alikuwa amevalia kikaptula kifupi cha jinsi na tishert nyeupe, nguo nyingine pamoja na za mwenyeji wake alikuwa amezifua kwa kutumia mashine ya kufuria, kasoro gauni lake moja lefu chakavu aliyoiweka kwa zarula, muda wote Jackline alikuwa akikumbuka jana jioni, alipo taka kumtowa roho mwenyeji wake, akajikuta anatabasamu, wakati akiendelea kukumbuka matukio hayo, akakumbuka kuwa mwenyeji wake alikuja na beg jana usiku, akanyanyuka na kulifwata chumbani, maana alisha lipeleka huko, sasa alisha kizowea chumba hicho, maana ata kuoga aliogea huko, na nguo alibadirishia huko, nikutokana na mwenyeji wake kuto mwonyesha chumba cha wageni, akalibeba lile begi, na kuja nalo sebuleni, akaliweka juu ya meza, na kulifungua, alichokiona ndani ya begi hilo alijikuta akipatwa na hasira kilicho amatana na kicheko kwa wakati mmoja, zilikuwa ni nguo na viatu vya kike, akatoa kigauni kimoja chepesi “mh! kizuri sana” alinong’ona Jackline, huku anajipimisha kile kigauni, kikamtosha vizuri sana kikiishia kwenye mapaja, “ni chakulalia, sijuwi anamwanamke wake?” alijisemea Jack, kitu kama wivu kili mtaka kumwingia huku akianza kutoa kitu kimoja baada ya kikingine, licha ya kuwa na nguo nzuri za kila aina, lakini Jackline kwake yeye suluwali ndilo vazi analolipenda zaidi, na mle ndani ya begi zilikuwapo mbili za jinsi, zilizobana “nzuri sana, kumbe ana mwanamke huyu” alijisemea Jackline huku akijipimisha, nazo zilimkaa vizuri, “mbona kama ameninunulia mimi” pia magauni na viatu vizuri, per tatu lakini kilicho mfanya atabasamu na kushindwa kumwelewa huyu mlevi, ni nguo za ndani, yani chupi saba za aina mbari mbari, na rangi tofauti, zikiwepo za kawaida na bikini, aina ya chupi ambazo akuwai kuzitumia, katika maisha yake, pia kulikuwepo na tight saba za rangi tifauti, “huyu ananitania ngoja arudi atanitambua” alijisemea Jackline na kuvirudisha vile vitu ndani ya begi, kisha akalifunga na kulipeleka chumbani itaaendelea……
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU