BINTI MDUNGUAJI (16)

SEHEMU YA KUMI NA SITA

ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI TANO : zikiwepo za kawaida na bikini, aina ya chupi ambazo akuwai kuzitumia, katika maisha yake, pia kulikuwepo na tight saba za rangi tifauti, “huyu ananitania ngoja arudi atanitambua” alijisemea Jackline na kuvirudisha vile vitu ndani ya begi, kisha akalifunga na kulipeleka chumbani endelea ……
Wakati huo Kule hospital insp Johnson aliomba vipimo vya alama za vidole vya marehemu Kileo na walinzi wake, akaletewa kopi kimi na moja, “insp tumekuletea na hivi hapa vingine nane, ukiachilia wale vijana vijana walio uwawa, juzi usiku kule Jambo Pub, pia kuna wengine watano wameuwawa jana buguruni ”aliongea doctor wenye cheo cha luten, ambae aliletwa kwaajili ya kazi hiyo ya kupima alama za vidole toka kituo kikuu, “vya nini hivi vyote, wakati naitaji vya awa watatu tu!?” aliuliza Insp Johnson, akichukua kopi ya mchungaji kileo “afande nime gunduwa kuwa alama za vidole zilizo patikana kwa wote kumi na moja, ni zamtu mmoja, kuanzia kisu kilicho tumika na aina ya upigaji” jibu hilo lilimstua insp Johnson, akazichukua zile copy na kuzikaguwa haraka, kweli anagunduwa zina fanana, “inamaana huyu muuwaji ni mwanamke?” kitu ambacho insp Ernest akutaka kuamini, “hapana sasa hawa walio uwawa bar, wanauhusiano gani na hawa askari wastaafu?” aliuliza yule doctor, “juzi usiku tuliambiwa kuwa awavijana wa hapa bar, walikuuwawa ndani ya chmba cha mwanamke, na yule mwanamke alimshambulia mhudumu na kuondoka zake, hapo Insp akatoka haraka na kuamuru magari ya elekee manzese, mapambano bar and guest house, ** ilisha timia saa tano asubuhi Denis na Maadhi baada ya kumaliza kunywa soup kwa mama bupe, wakaelekea Jambo pub wakapata bia mbilimbili za kuanzia, kisha Mahadhi aka lipa deni la Denis la carton moja ya bia, baada ya hapo kila mmoja akashika njia yake, wakati Mahadhi akiwa anaelekea kaliakoo Denis alielekea sinza, alienda moja kwamoja mpaka kwenye duka la urembo, lenye poster card na midori ya urembo alitumia nusu saa kuchagua mdori mzuri mkubwa size ya kati, ambae alivalishwa kinguo kilicho andikwa “only you can show me, what love is … ” japo alijiuliza sana kuhusu uelewa wa mgeni wake juu ya ile lugha ya kigeni, maana aliamini kwa mwanamke mama ntilie, kuwa amesoma na kupata uelewa wa kusoma na kuielewa lugha ya English, lakini Denis akuwa na namana, aliona bora aanze kutumia ujanja ku fikisha ujumbe kwa mwenyeji wake, pengine anaweza kumwelewa, huu ni ujana alioupata toka kwa Mahadhi, anapo taka kumbembeleza mkewake, akafikilia kitu kingine ambacho kita msaidia kwenye kumlainisha yule mwanamke kule nyumbani, maana swala la kutongoza kwake lilikuwa kazi ngumu sana, Denis akiwa bado anaumiza kichwa, aliendesha gari akirudi alikotoka, na kwenda adi njia panda ya mabibo, pasipo kupatajibu, akapuuzia mawazo yake, na kusimamisha gari kwenye soko la mahakama ya ndizi, akashuka kwenye gari nakuanza kununua mazaga muimu ya chakula, zikiwemo ndizi viazi kuku wakienyeji ambao walichinjwa na kunyonyolewa, wawili, kisha akanunua nyanya na vitu vingi sana, ambavyo viliitajika nyumbani, alibeba kwa wingi sana, wasinge weza kumaliza watu wawili ata kwa mwezi mzima, “awa mama ntlie wanapenda sana kujipikilisha,” saa sita na robo akaanza safari ya kurudi nyumbani, njiani akifunua kopo moja baada ya jingine la bia na kulitandika taratibu, huku akiwaza, endapo mwenye jiwake atakuwa aelewi kusoma English ataanzaje kutafsilia, baada ya kuwaza kwa muda kidogo, akapata jibu, akatabasamu, nibaada ya kuiona bar moja kubwa njiani mtaa wa luguruni, akakata kona ya ghfla kulia, akiikosa kuigonga pikipiki iliyokuwa inapita kwa mwendo wakasi, Denis akaingia na kupaki gari lake pale bar, ikiwa ni karibu na kufika mtaani kwake, akaziacha bia zake ndani yagari, ambazo bado zilikuwa nyingi kwenye gari, akafunga gari na kutafuta sehemu nzuri ya kukaa, kwanza akaagiza chakula, nusu saa baadae aakiwa amesha maliza kula, akaanza kunywa bia, “baada ya hapa ata nikianza kuongea nae, tuta enda sawa, yani mtoto mzuri mpaka namwogopa” alijisemea Denis, aimalizia kwa kicheko, ** huyu ndie Denis mwenyewe kabisa toka akiwa mdogo, nimwoga sana wa wanawake, licha ya kuwa mwoga kukataliwa, pia ilisha waikutokea safari moja, akiwa kidato cha tatu, kuna binti mmoja Johari, alikuwa ni mwanafunzi mwenzake, mtoto wa mzee Mapande, jina alilopewa kutokana na kazi yake ya kuuza bucha la nyama ya ng’ombe, Johari alijilegesha mwenyewe kwa Denis, akitumia mtego wa vizawadi na vi offer vingi vingi, mpaka Denis alipoingia mtego na kuanza nae mausiano, kweli Johari alimteka Denis kwa fedha na zawadi nyingi tofauti kila siku, na yeye akalipa fadhira kwa kumpatia penzi moto moto Johari, kiasi cha kusababisha, habari yao isambae kama moto kwenye nyasi kavu, baada ya mda kidogo likatokea tatizo, kumbe yule binti Johari mtoto wa mzee Mapande, alikuwa anatembe na kijana mmoja muuza mchele huko sokoni, ndie ambae alikuwa akimhudumia Fedha pamoja vitu vingi sana, nandie aliempatia jeuri ya fedha ya kumkamatia Denis, lakini kutokana na kukolea kwa Denis, Johari akajikuta akishindwa kumpatia penzi kijana muuza mchele, huku akimpiga kalenda ya kumpatia kitumbua kila kukicha, yule muuza mchele aliona mabadiriko, katika penzi lake na Johari mtoto wa mzee Mapande, baadea ya kwaza sana akaona achunguze ni kitu gani kinacho sababisha mapenzi yao yaporomoke, mwishoe aka gundua kuwa, kuna mwanafunzi mwenzake na Johari, ndie anae mzuzua mpenzi wake, hivyo akaamua kuunda mtego wa kumnasa Denis, akipania kumfanyia kitu mbaya, iwapo atamkamta akiwa na binti huyo, wakati huo huo, mzee Mapande nayeye alisha sikia tetesi za kuwa, kuna kijana muuza mchele anatoka na mwanae, kumbe siku ya fumanizi, ndiyo siku ambayo baba wa yule binti, alipanga kufanya fumanizi la mwanae na muuza mchele, na muda alio ambiwa kuwa, mwanae anaye msomesha kwatabu, ameonekana anaingia guest house, muda huo alikuwa buchani, baba wa yule binti akaambatana na njemba zipatazo sita, wote wakiwa na zana za kazi zitumikazo buchani, wakaelekea kule guest house, wakati huo huo kule guest, baada ya Denis kusikia mlango wa chumba cha guest, unagongwa kwa nguvu, ikionyesha ishara kuwa anafumaniwa, haraka sana akapanda juu ya dali, akipitia kwenye seheu mahalumu ya kuingilia dalini endapo mafundi wa umeme wanaitaji kufanya marekebisho, kisha akajibanza kimya kabisa, akawa anachungulia mle chumbani kwa kutumia pale alipo ingilia, aliweza kumwona muuza mchele anaingia mle chumbani, na kuanza kupiga yule Johari, akimlazimisha aseme Denis yupo wapi, yule binti alilia sana maana muuza mchele alikuwa bounce, yani anamwii mkubwa, wakati yule muuza mchele akiendelea kumpiga Johari, kutahamaki baba wa yule binti akaingia na timu yake, hapo ndipo kilipotokea kitu mbacho, tokea siku ile Denis akuwai kijiingiza katika mapenzi wala kutamani kufanya hivyo, mpaka alipo mwona huyu mama ntilie, itaendelea ……..

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

error: Content is protected !!