
SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA SEHEMU YA KUMI SITA : akimlazimisha aseme Denis yupo wapi, yule binti alilia sana maana muuza mchele alikuwa bounce, yani anamwii mkubwa, wakati yule muuza mchele akiendelea kumpiga Johari, kutahamaki baba wa yule binti akaingia na timu yake, hapo ndipo kilipotokea kitu mbacho, tokea siku ile Denis akuwai kijiingiza katika mapenzi wala kutamani kufanya hivyo, mpaka alipo mwona huyu mama ntilie, endelea ……
Maana ndani ya dakika tano, Denis aliweza kumwona yule jamaa muuza mchele, akipatwa na dhahama ya kuchalangwa na visuvikari ambavyo wakina mzee Mapande, uvitumia buchani, na mwisho wake wakimuacha muuza mchele alikuwa amelala kwenye kijito cha damu, mwili wote utazani mbuzi yupo machinjioni, mzee Mapande akamchukuwa mwanae, aikiwa na wale watu wake wakaondoka zao, baada ya kuona hivyo Denis alipita juu kwa juu na kutokea upande wapili, yani chumba kingine, nakuondoka zake, tokea hapo licha ya kuwa Denis ni kijana mtanashati, na mwenye kuvutia mbele ya wanawake wengi, wa nyumbani na kazini, ambao walijilengesha sana, wakiwepo wasichana wadogo na wake za watu, ambao walikuwa wakitamani kuwa naye, lakini Denis aliwa mwaga, akuonyesha kuangaika nao, kuna kipindi wakamkashifu, kuwa dudu yake mbovu aiwezi kula kitumbua, lakini yeye akujari, na mengine akuyasikia sababu hakuwa na mazowea na watu wa pale mtaani, ambapo alikuwa ameamia miezi mitatu nyuma ** Magari ya police ya lisimama nje ya mapambano bar, insp Johnso David alishuka nakuingia ndani ya bar hiyo, akaulizia kuhusu muhudumu wakike alie shuhudia yale mauwaji ya wale vijana watutu, kwenye chumba kilicho pangwa na mwanamke toka kijijini, akaambiwa kuwa, baada ya tukio la mauwaji, ile bar aija funguliwa tena, na wafanya kazi wote wapo makwao, kuhusu yule binti, inasemekana yupo mbezi kwa dada yake, lakini akuna anaye pafahamu, na simu yake, alikuwa ameuza baada ya kukosa fedha za kusafirishia mizigo yake, kwenda mbezi, insp Johnson akuwa na ujanja, akarudi kwenye gari na kutoa uelekeo mpya wa kigamboni kwa mzee Soud, brigedia mstaafu, gari zikaanza kuondoka huku akichukuwa simu yake na kuiweka sikioni, akipiga kwa brg msataafu, Soud, ** Saa nane mchana, insp Johnson alikuwa nyumbani kwa brg msaafu, Suod Hassan masoud, nje ya jiji la Dar es salaam, kitongoji cha mji mwema wilaya ya temeke (kipindi hicho) jimbo la kigamboni, Insp Jonhson David alikuwa ametulia akimsikiliza mzee Soud, ambae alikuwa akimsimulia juu ya wanajeshi saba ambao walisafiri kwenda nchi Congo, ambapo walirudi, sita mmoja wao akiwa amepote kwenye mission, mzee Soud alienda mbali zaidi na kuelezea wasiwasi wake juu ya kupotea kwa Michael Nyati, ni kwamba, mpaka yeye anastaafu kazi, wazazi na ndugu wakaribu wa mtu huyu, awajawai kuja kumtafuta ndugu yao, na bado anahesabika mtoro kazini, “katika kumbu kumbu zangu, niliwai kupokea simu moja tu, ya mtu akiulizia juu ya Michael Nyati, sasa ndiyo Napata picha kamili, yule alikuwa Michael mwenyewe, sababu aliulizia watu wote walio enda Congo kipindi kile” akaelezea pia mashaka yake juu ya watu sita walio rudi, toka Congo, ni kuhacha kazi mala tu baada ya kumaliza likizo yao ya mwezi mmoja, ambayo walipewa baada ya kurudi toka kwenye kazi nzito, “na baada ya miaka michache mbele tukaanza kuwaona wakiwa na maisha mazuri, wengine wakaanzisha makanisa wengine ni wafanya biashara wakubwa, mpaka sasa” aliongea mzee soud akionyesha umakini juu ya swala hili, kama kuna kitu alianza kukihisi insp Johnson “samahani mzee Soud, unakumbukumbu yoyote ya hao watu walio safari kwenda Congo?” aliuliza insp akimtazama mzee Soud, ambaye aliinuka na kuelekea chumbani kwake, baada ya dakika chache akarudi akiwa na kitabu cha picha mkononi (photo album) kubwa akaiweka mezani, akafunua kurasa chache, kisha akamgeuzia bwana Jonhson akionyesha kwa kidole picha moja, “ni hawa hapa, hii picha nilipiga nao siku wanaondoka kuelekea Congo, na huyo alie chuchumaa kushoto ni Michael Nyati,” aliongea mzee Soud, huku insp Johnson akiwa ana itazama ile picha kwa umakini mkubwa ulio changanyika na mshangao, ni kama akuamini alichokiona, “unataka kuniambia, kuwa hawa wote walienda congo?” aliuliza insp Johnson, akionyesha kuwa kama kuna kitu aja kiamini katika ile picha “hapo kasoro mimi tu! sikwenda, lakini hao wote unao waona walienda, na huyo bwana mdogo alie chuchumaa hakufanikiwa kurudi” alijibu mzee Soud akijiamini kuwa anachoeleza ndicho kilichopo, “kwani kuna maelezo zaidi waliyatoa juu ya kilicho mtokea mwenzao?” aliuliza insp akiwa ameikazia macho ile picha, “mpaka sasa hakuna anaye ujuwa kweli, zaidi ya hapo wanne waliobakia” alijib mzee Soud Hassan, akimtazama Johnson kwa umakini, “mzee naona nikuache, wacha nika endelee kulishugulikia swala hili” aliongea insp Johnson huku akiinuka toka kenye kochi alilo kalia, akionyesha wazi kuvurugwa na kitu katika ile picha, “kijana mbona imekuwa ghafla hivyo?” mzee Soud alisha gundua mabadiliko ya usoni kwa insp Johnson, na alitegemea kutokea kwa kitu kama hicho “mzee wangu majukumu yamenibana sana, wacha niwai nika pambane” aliongea Johnson, nakuanza kutoka nje, akisaau kuwaaga wengine waliompokea, na sasa walikuwa jikoni wakiandaa chakula, mzee Soud alimtazama sana insp Johnson, adi alipo fika mlangoni aka mwita,”Johnson kuna kitu ni muhimu kuzingatia , unapo mtafuta Michael Nyati, lazima uwe makini sana, maana nimtu hatari sana, husi jaribu kuladhimisha hisia zako, ukikwama nitafute” Johnson alisikiliza kisha akakubariana na mzee Soud, lakini kiukweli mawazo yake hayakuwepo mahali pale, kunakitu kili mvuruga, ** saa kumi jioni mzee Masinde alikuwa msibani kwa mchungaji Kileo, ni baada ya kutoka kwenye msiba nyumbani kwa mchungaji Chilumba, ndipo alipo pokea simu yake ya mkononi, iliyo kuw ikitoa mlio ikiashiria kuna simu ilikuwa ina ingia, “hallow…. Ndiyo…” aliongea mzee Masinde huku anainuka nakusogea pembeni kidogo, nasasa alionekana akiongea na simu pasipo kusika upande wapili, “vipi mbona akuna ata salamu ….. ok! nipo msibani …. njoo nyumbani saa mbili usiku … usijari tutaongea vizuri” alimaliza mzee Masinde nakukata simu, akarudi alipo kaa mwanzo, akachukuwa simu yake na kuandika messeji kisha akisend kwa kudi ( yani kwa namba zaidi ya moja) kisha akairudisha simu mfukoni, huku uso wake ukianza kuonyesha mashaka na wasiwasi ** mida ilikuwa imesogea giza la saa moja lilishaanza kutanda, Michael Nyati alikuwa ametulia na mke wake Anitha juu ya kochi moja la watu wawili, wakikata mvinyo taratibu, macho kwenye TV, walifanyiana michezo ya kimapenzi, nikawaida yao siku zote, walisha zowea siku zote za maisha yao, ata mbele ya Jackline, wao walicheza kama watoto, “vipi umesha wasiliana na jambazi wako?” aliuliza Anitha au mama Jackline, “nilikuwa nasubiri anipigie, lakini naona kimya” alijibu baba Jackline, huku akiinua simu yake toka mezani akacheki muda, ilikuwa saa mojaza usiku, inakaribia na nusu, “wacha nimpigie bwana, kama yupo na huyo mlevi, shauri zake atajuwa cha kufanya” alisema baba Jack na kuanza kupiga simu, mwanae Jackline “hahahah mlevi anamcheka mwenzie” alicheka sana mama Jackline, *** Saa mbili na dakika tano, mzee Masinde alikuwa ametulia nyumbani kwake akamsubiri mwanae ambae alimwambia aje hapo nyumbani mida hii ilionyesha alikuwa ana kitu muhimu anataka waongee, mala mlango uka gongwa “fungua tu! hupo wazi” mlango ukafunguliwa akaingia Insp Johnson akiwa amevalia mavazi ya kiraia, tofauti na aliivyokuwa mchana, itaendelea …….
All Rights Reserved © | Simulizi TAMU